Wanaume kuvaa Mkufu na bangili za m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Wanaume kuvaa Mkufu na bangili za mkono

Question

Ni ipi hukumu ya wanaume kuvaa mkufu na bangili za mkono?

Answer

Imethibitishwa katika Sharia ya Kiislamu kwamba ni haramu kwa wanaume kuvaa dhahabu, ama wanaume kuvaa mikufu ya fedha kwa ajili ya mapambo na kujifananisha na wanawake, hili pia ni haramu, kwa sababu mila na desturi zinaelekeza kwamba mikufu ni aina ya pambo maalumu kwa wanawake na si kwa wanaume. Sharia ya Kiislamu inawakataza wanaume kuiga wanawake na kinyume chake. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas (R.A) amesema: "Mtume (S.A.W) amewalaani wanaume wanaojifananiza za wanawake na wanawake wanaojofannaniza na  wanaume."

Hata hivyo, ikiwa kuvaa mkufu wa fedha kwa haja au dharura, kama vile kwa ajili ya kuwatambua wanajeshi jeshini kwa njia ya nambari ya kijeshi iliyo nakishiwa kwenye mkufu unaovaliwa shingoni mwao, basi hakuna ubaya wowote kulingana na Sharia ya Kiislamu,  Kwa hakika, inakuwa ni lazima katika hali hii ikiwa amri ya kijeshi itatolewa kwa lengo hilo.

Ama kuvaa bangili kwa nia kwamba inataleta baraka na kuzuia shari, hili limeharamishwa katika Uislamu, kwani Mtume (S.A.W) amesema: "Yeyote anayevaa hirizi, Mwenyezi Mungu hatatimiza ombi lake, na yeyote anayevaa kinga ya uchawi, Mwenyezi Mungu hatatimiza ombi lake." Maana yake: yeyote anayevaa vitu hivi vinavyoaminika kuleta heri na kuzuia shari hatatimizia lengo lake.

Maelezo

Imethibitishwa kisharia kwamba ni haramu kwa wanaume kuvaa dhahabu kwa aina yoyote, iwe ni pete, bangili, mikufu, na kadhalika. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ari kwamba Mtume (S.A.W)  amesema: ((Kuvaa hariri na dhahabu kumeharamishwa kwa wanaume wa ummah wangu na kumeruhusiwa kwa wanawake zao)).

Ama wanaume kuvaa fedha: Wanazuoni wamesema kuwa inaruhusiwa kwa wanaume kuvaa pete za fedha, wakitoa Hadithi ya Abdullah bin Umar (R.A.) ambaye amesema: (Mtume S(.A.W.) alikuwa na pete ya fedha, ambayo ilikuwa mkononi mwake, kisha ikawa mkononi mwa Abu Bakr, kisha ikawa mikononi mwa Umar, Kisha ikawa katika mikono ya wa Uthman, hadi ilipoanguka katika kisima cha Aris, ikiwa na maandishi: Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu”.

Haijaruhusiwa kwa wanaume kuvaa mikufu: Iwe umetengenezwa kwa fedha au madini mengine, kwa sababu hii ni kama kujifananiza na wanawake, na Sharia ya Kiislamu inawakataza wanaume kuiga wanawake na kinyume chake. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas (R.A) amesema: (Mtume (S.A.W). amewalaani wanaume wanaojifananiza za wanawake na wanawake wanaojofannaniza na  wanaume).

Mila na desturi zimefanya kuvaa mikufu, bangili za mkono, hereni, na aina nyingine za vito kuwa jambo mahususi kwa wanawake na si kwa wanaume. Imekatazwa kwa wanaume kuvaa mikufu ya fedha kwa kuiga wanawake, kama ilivyopokelewa kwa Abu Huraira (R.A) amesema: ((Mtume (S.A.W0. amemlaani mwanamume anayevaa nguo za wanawake na mwanamke anayevaa nguo za wanaume.))

Hata hivyo, ikiwa wanaume watavaa mikufu ya fedha kwa sababu ya haja au uhitaji, na si kwa ajili ya mapambo, kama vile kuwatambua wanajeshi waliouawa vitani kwa nambari ya kijeshi zilizonakishiwa kwenye mkufu unaovaliwa shingoni mwao, na yanayofanana na hayo, basi hii linaruhusiwa kulingana na Sharia ya Kiislamu na hakuna ubaya wowote, bali, inakuwa ni lazima ikiwa ni amri ya kijeshi.

Ama kuvaa bangili kwa nia ya kupata riziki na bahati nzuri, au kuzuia madhara, hii imeharamishwa katika Uislamu, kwani Mwenyezi Mungu pekee ndiye ananufaisha na kudhuru. Muumini lazima achukue hatua zinazohitajika na kuweka imani yake kwa Mwenyezi Mungu. Hizi bangili ambazo baadhi ya watu huvaa ni kama yale ambayo wachawi na wadanganyifu hufanya wanapowapa watu hirizi ili kuwakinga na madhara au kuwapatia baraka, hii ni mojawapo ya mila za kijinga ambazo Uislamu umeziharamisha. Imepokewa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir kwamba alimsikia Mtume (S.A.W)  akisema: "Yeyote anayevaa hirizi, Mwenyezi Mungu hatamkamilishia lengo lake, na yeyote anayevaa hirizi, Mwenyezi Mungu hatamlinda."

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Ni Haramu kwa wanaume kuvaa mikufu ya dhahabu.

 Pia ni Haramu kwa wanaume kuvaa mikufu ya fedha kwa ajili ya mapambo na kuiga wanawake, kwa sababu Sharia ya Kiislamu inaharamisha wanaume kujifananisha na wanawake.

 Ikiwa kuvaa mkufu wa fedha ni lazima au kwa haja, kama vile kwa ajili ya kuwatambua wanajeshi jeshini kwa njia ya nambari ya kijeshi inayonakishiwa kwenye mkufu unaovaliwa shingoni mwao, basi hakuna madhara yoyote kulingana na Sharia ya Kiislamu. Kwa hakika, kuvaa mkufu katika hali hii kunakuwa ni wajibu ikiwa ni amri ya kijeshi.

 Kuvaa bangili kwa imani kwamba huleta bahati na kuondoa shari kumeharamishwa katika Uislamu, na ni mojawapo ya desturi za kijinga ambazo Uislamu umeziharamisha.

Share this:

Related Fatwas