Je, inawajibika kuoga kwa sababu ya Madhii?
Question
Je, inawajibika kuoga baada ya kutoka Madhii?
Answer
Madhii: Ni maji meupe, (mepesi) na yenye ute, yanaotoka kwenye uume au uke wa wakati wa kuchezeaana kwa ajili ya tendo la ndoa au kuliwaza, na pengine asihisi mtu wakati wa kutoka kwake ladha. Hukumu yake: Ni najisi na lazima ioshwe na kutolewa mwilini na nguoni, na yanabatilisha udhu.
Ama Manii ni majimaji mazito, meupe kwa wanaume, na ya manjano kwa wanawake, na si mazito kwake. Hutoka anapofika kileleni na yanapotoka humalizika hamu ya tendo, hukumu ya ni twahara, lakini inapasa kuoga baada ya kutoka kwake.
Wadii: ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa. Hukumu yake ni najisi, na lazima kuoshwa na kutolewa mwilini na nguoni, na hubatilisha udhu.
Na dalili ya kile tulichokitaja ni Hadithi ya Ibn Abbas, R.A., ambapo anasema: “Manii, Wadii, na Madhii. Ama Manii, yanawajibisha josho, Ama Wadii na Madhii, amesema: Osha uume wako au makende yako na tia udhu kama kama udhu kwa ajili ya Swala.”
Lakini kutokwa na uchafu ukeni kwa wanawake ni umajimaji safi, wakati mwingine yanafanana na madhii au jasho, yanayotoka ukeni. Hukumu yake ni Hubatilisha udhu, lakini ni twahara, na si lazima kuosha sehemu ya nguo au mwili inayogusa.
Maelezo
Madhii: Ni maji meupe, (mepesi) na yenye ute, yanaotoka kwenye uume au uke wakati wa kuchezeaana kwa ajili ya tendo la ndoa au kuliwaza, na pengine asihisi mtu wakati wa kutoka kwake ladha.
Hukumu yake: Ni najisi na lazima ioshwe na kutolewa mwilini na nguoni, na inabatilisha udhu. Yaani: Ikiwa mtu aametawadha udhu na Madhii yakimtoka mtu, udhu wake hubatilika.
Na dalili ya hayo ni hadithi ya Ali R.A., ambaye amesema: “Nilikuwa mtu ambaye mwenye Madhii mengi, kwa hivyo nilimwamuru mtu amwulize Mtume (S.A.W) kwa nasaba ya binti yake, Kwa hivyo akauliza, naye akasema: ‘Tawadha na osha uume wako.” Imepokelewa na Al-Bukhariy.
Hadithi inaonyesha kwamba mtu si wajibu kuoga, baada ya kutoa madhii, bali wajibu ni kutawadha na kusafisha mwili na nguo kutokana na athari zake.
Na tofauti baina Madhii, Manii, na Wadii ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Manii ni majimaji mepesi, meupe kwa wanaume, na manjano kwa wanawake, ambayo si mazito kwake, alama yake ni kwamba hutoka wakati wa kufika kileleni, Na hayo ni tofauti na Madhii kama ilivyotangulia.
Hukumu ya manii: Ni twahara, lakini inapasa kuoga baada ya kutoka kwake. Kwa sababu ikiwa Manii yatatoka baada ya kujamiiana au katika ndoto usngizini, mtu huyo anakuwa mwenye janaba, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba -isipokuwa mmo safarini - mpaka mkoge.}[An Nisaa 43].
Na Kutoka kwa Umm Salamah R.A., amesema: “Umm Sulaym alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu haoni haya katika haki. Je, ni wajibu kwa mwanamke kuoga ikiwa anaota ndoto nyevu?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) akasema: ‘Ndiyo, akiona maji.’” Imepokelewa na Al-Bukhariy. Yaani, ikiwa manii yatatoka, basi lazima aoge.
Ya Pili: Wadii: Ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa.
Hukumu ya Wadii ni najisi, na lazima kuyaosha na na kuyaondoa mwilini mwilini, na hubatilisha udhu. mtu akitawadha na akatoka na Wadii, udhu wake hubatilika Na dalili ya Hayo, ni hadithi ya Zur’ah Abi Abd al-Rahman, ambaye amesma: “Nilimsikia Ibn Abbas, R.A.,, akisema: Manii, Wadii, na Madhii. Ama Manii, yanawajibisha josho, Ama Wadii na Madhii, amesema: Osha uume wako au makende yako na tia udhu kama kama udhu kwa ajili ya swala.”[1]
Ikumbukwe kwamba: hukumu kuhusu majimaji ya ukeni, yaani, ute wa uke wa wanawake, na suala tofauti limeelezewa peke yake katika kitabu hiki; kwa hivyo rejea nyuma.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Baada ya maelezo haya ya kina, tunaweza kuhitimisha yafuatayo:
Madhii: Ni maji meupe, meupe (mazito kidogo) na yenye ute, unaotoka kwenye uume au uke wakati wa mawazo ya matamanio au wakati wa kuchezeana na pengine asihisi mtu wakati wa kutoka kwake.
Hukumu yake: Ni najisi na lazima ioshwe na kuyandoshwa mwilini na nguoni, na yanabatilisha udhu.
Manii ni majimaji mzito, meupe kwa wanaume, na wa yanjano kwa wanawake, ambao si mazito kwao. hutoka wakati kufika kileleni, na kutolewa kwake hukomesha hamu ya tendo. Nayo ni tofauti na Madhii kama ilivyotangulia.
Hukumu ya ni twahara, lakini inapasa kuoga baada ya kutoka kwake
Wadii: ni maji meupe mepesi yanayotoka baada ya kukojoa. Hukumu ya Wadii ni najisi, na lazima uoshwe na kuondoshwa mwilini na nguoni, na hubatilisha udhu
[1] - Imepokelewa na Al Baihaqiy katika kitabu cha: “As Sunan Al Kobraa”262/1
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
