Kumuombea Dua Mtu katika Swala kwa kumtaja jina
Question
Kuna baadhi ya watu wanaonipenda, je, kunajuzu kwangu kuwaombea dua katika Swala kwa kumtaja jina?
Answer
Hakuna ubaya kisharia kwa mwanadamu kumuombea dua katika Swala mtu maalumu katika watu wazuri miongoni mwa jamaa zake kwa kumtaja jina, kama wazazi wake au mwalimu wake, iwe katika Swala ya Faradhi au Sunna.
Maelezo
Kisharia kwa Ushahidi wa Qur`ani Tukufu na Hadithi za Mtume (S.A.W) kunapendeza kuomba Dua, katika Qur`ani Tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka) [Al Baqara:186].
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike ) [Al Ghafir:60].
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka.. ) [Al Aaraf:55].
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo) [Al Israa:110].
Na dalili ya hilo katika Hadithi za Mtume (S.A.W) ni iliyotolewa watu wa Hadithi na Al Hakim kutoka kwa Annuuman bin Bashiri (R.A): Kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Hakika Dua ndio Ibada” kisha akasoma: (Niombeni nitakuitikieni.) [Al Ghafir:60].
Na Hadithi iliyotolewa na Imamu Al Tirmidhy katika Sunanih katika Hadithi za Anas R.A kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Dua ni Ubongo wa Ibada”, na kwa haya wamekubaliana wanazuoni wa Fiqhi na Hadithi katika hili.
Dua katika Swala limeruhusiwa, isipokuwa Wanazuoni wa Fiqhi wa Hanafiy katika riwaya ya wazi wamelifungamanisha hilo kwa kuwa tamko la Dua liwe kutoka katika Qur`ani Tukufu.
Na mapokezi kutoka Madhehebbu ya Hanbali yametofautiana katika kuruhusiwa daua katika Swala, na wamekubaliana kuruhusiwa kwa kile kilichokuja katika Qur`ani Tukufu na Hadithi za Mtume (S.A.W), ama tamko lisilochukuliwa katika Qur`ani Tukufu hakujuzu kuomba kwa tamko hilo, isipokuwa likiwa linaendana na yaliyokuja katika Qur`ani Tukufu na ikakusudiwa Akhera, ama dua inayokusudiwa kupata starehe za Dunia, mapokezi yametofautiana kutoka kwa Imamu Ahmad pia kati ya kujuzu na kutojuzu.
Ama kumuombea Dua Mtu maalumu katika Swala kwa kumtaja jina lake, Wanazuoni wametofautiana katika kuruhusiwa kwake: Madhehebu ya Imamu Malik na Shafi na Hanbali katika Madhehbu sahihi wamejuzisha hilo[1].
Na kauli ya kujuzu ndio iliyochaguliwa; na hii kwa kuwafikiana kwake na yaliyopokewa kutoka katika Hadithi tukufu ambapo Mtume (S.A.W) aliwateua watu maalumu katika kunuti, imetolewa na Al Bukhary na tamko ni la Muslim kutoka kwa Abouhurayra R.A amesema: Mtume (S.A.W) alikuwa kiomba katika kunuti: “Ewe Mola wangu wa Haki muokoe Salma bin Hashim, Ewe Mola wangu wa Haki muokoe Al Walid bin Walid, Ewe Mola wangu wa Haki muokoe Abi rabiia, Ewe Mola wangu wa Haki waokoe wanyonge katika waumini, Ewe Mola wangu wa Haki zidisha adhabu yako kwa Watoto wa familia ya Mudhar, ewe Mola wangu wape ukame kama ukame wa zama za Nabii Yussuf”.
Na sehemu ya dalili: Ni kwamba Mtume (S.A.W) amewataja watu kwa majina yao, na hili limepokewa pia kutoka kwa mtu zaidi ya mmoja katika Masahaba watukufu na Tabiin na wema waliotangulia wote. R.A.
Ni katika yanayotoa dalili ya kuruhusiwa kumuombe Mtu dua kwa kutaja jina lake ni Hadithi iliyotolewa na Imamu Muslim kutoka kwa Abouhurayra, kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Sehemu ambayo mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni katika sijida, basi zidisheni Dua hapo”.
Amri ya kuomba Dua imekua jumuishi, na kanuni inasema kitu jumuishi kinasalia katika ujumuishi wake, na kitu kilichoachiwa moja kwa moja kinapita katika kuachiwa kwake mpaka utakapokuja umahususi/umaalumu au kufunga.
Na katika Hadithi hizi na nyinginezo katika Hadithi sahihi kuna dalili ya waliyokubaliana wanazuoni wa Fiq’hi.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kumuombea dua mtu maalumu katika Swala kwa kutaja jina lake, kunajuzu kisharia.
Amri ya dua imekuha jumuishi, na tamko jumuishi linasalia katika ujumuishi wake mpa litakapokuja tamko mahususi/maalumu au linalofunga.
[1] Al Sharh AL Kabeern 1/251/252. Al Insaaf 2/82.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
