Hukumu ya kufanya chat kati ya vija...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kufanya chat kati ya vijana wa kiume na wa kike

Question

Nampenda msichana, na nazungumza naye kwa njia ya simu. Ninajua kuwa hatufanyi maasi yoyote katika mazungumzo yetu – Alhamdulillah. Pia nakumbuka kuwa sikubali kabisa kutoka naye au kukutana naye, ili tusije tukaanguka kwenye kosa, na nataka nipende kwa njia safi. Pia nimemfundisha mengi kuhusu Uislamu na hukumu zake. Hapo awali hakuwa akiswali, alikuwa akizungumza na wavulana na kuwasalimia kwa kupeana mikono, lakini sasa hayo yote ameacha. Hata marafiki zake wamesikia maneno yangu na wameiga mfano wake.

Kile ninachotaka kujua ni mambo mawili:

La kwanza: Je, Mwenyezi Mungu atanilipa thawabu kwa hiki nilichokifanya?

La pili: Je, mazungumzo yangu naye kwa njia ya simu ni haramu au siyo, ikizingatiwa kwamba hatuzungumzi mambo mabaya, na mazungumzo yetu mengi yanahusu Swala, Hijabu na ndoa?

Naomba mnijulishe.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kwanza: Kazi uliyofanya ya kumpa mwenzako nasaha ni jambo jema ambalo linakubalika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atakulipa kwa hilo. Mwenyezi Mungu atalifanya jambo hilo kuwa katika mizani ya mema yako Siku ya Kiyama.

Pili: Mazungumzo kati ya kijana wa kiume na wa kike yanaruhusiwa kisharia ikiwa yapo ndani ya mipaka ya mafundisho ya Kiislamu, yaani kwa adabu, heshima ya pande zote, na kila mmoja awe na dhana nzuri kwa mwenzake. Lakini ni kwa sharti kwamba mazungumzo hayo hayachochei hisia au mapenzi haramu. Na ikiwa unahisi ladha au msisimko kutoka kwa sauti yake, basi haifai kuendelea na mazungumzo hayo.Top of FormBottom of Form

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas