Hukumu ya Kutoa Mfuko wa Ramadhani kutoka katika Mali za Zaka
Question
Ni nini Hukumu ya Kutoa Mfuko wa Ramadhani kutoka katika Mali za Zaka?
Answer
Inajuzu kutoa Zaka kwa mahitaji muhimu hayo ambayo masikini wanayahitajia, kama vile chakula na mavazi. Na miongoni mwa hayo kutoa katika mfumo wa mifuko yenye vyakula vya kutumika kukidhi mahitaji yao katika mwezi huu uliobarikiwa. Ifahamike kwamba hiki kiwe ndicho wanachokihitaji na si kile ambacho kinafaradhisha juu yao, na kwamba hiki kiwe kulingana na mahitaji yao. Bidhaa hizi zinapaswa kuwa zinazofaa na zisiwe duni au za ubora wa chini, na zinapaswa kuthaminiwa kwa bei ya kawaida.
Na kwamba hilo lisichukuliwe kuwa ni sababu ya kujifaharisha na kujionesha baina ya watu, na kwamba utoaji wa Zaka kwa fedha taslimu usiwe kwenye vyakula tu au mifuko ya Ramadhani hadi ikawa ni kiandamo cha jumla, kwa sababu hicho kinaweza kuwasababishia wale wanaostahiki Zaka hunyimwa kile wanachokihitaji katika masuala mengine ya matumizi kama vile matibabu, elimu, na kadhalika, yakizingatiwa masharti ya utoaji wa Zaka na kadhalika. bidhaa, kulingana na Fatwa iliyopendekezwa.
Maelezo
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sharia ya Kiislamu imebainisha wanaostahiki Zaka katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu uliofaridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima [At Tawbah 60]
Aliwaweka mafakiri na masikini mbele yake, ili kubainisha kipaumbele chao katika kustahiki Zaka, na kwamba lengo lake la msingi ni kuwatoshea na kudumisha maisha na riziki zao. Na Aya hii imeeleza kwa herufi “lam” ambayo inaashiria umiliki; kwa hiyo, Wanachuoni wa Fiqhi wengi walishartisha umiliki ndani yake, basi wakawajibisha umiliki wake kwa mafakairi au masikini ili waweze kuutumia kwa haja yao, ambayo wao ni wajuzi zaidi kuliko wengine. Hata hivyo, baadhi ya Wanachuoni waliruhusu utolewaji wake kwa namna ya kiasi maalumu cha fedha taslimu, wakati manufaa yanapopatikana kwa kujua haja ya masikini na kukidhi matakwa yao.
Kwa hiyo, Mtume (S.A.W.) amewabainisha katika Hadithi kuhusu kumtuma Muadh R.A. huko Yemen, akisema: “Wakikutii katika hili, basi waambie kwamba Mwenyezi Mungu amewawekea sadaka ichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kuwapa masikini wao”. [Imepokewa na Al-Bukhariy na Muslim katika Sahihi zao, na kitamko imetoka kwa Al-Bukhariy].
Na njia bora zaidi ya kulipa Zaka ya mali ni kuwapa masikini kwa njia ya pesa. Kama ikitolewa kwa njia ya chakula, hitaji la haraka la mtu masikini lazima lizingatiwe. Usinunue bidhaa yeyote duni na kuwapa masikini bila mpangilio, au kununua bidhaa za gharama kubwa ambazo hawahitaji. Haya yote yanaweza kupatikana kwa kuchunguza mahitaji ya masikini ambao chakula kitagawiwa ili kubaini ni bidhaa gani muhimu wanazokosa.
Ama yale wanayofanya baadhi ya watu kuandaa mifuko yenye vyakula vya Zaka ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwapa baadhi ya watu mafakiri na masikini, hiyo inajuzu kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu. Hii ni kwa sababu inatokana na kuzingatia lengo la kutoa Zaka, ambalo ni kukidhi mahitaji ya mafakiri na masikini. Kwa kuzingatia lengo hili, inajuzu kutoa Zaka katika thamani yake kwa mujibu wa Madhehebu ya Hanafi na wale wanaokubaliana nao, na hiyo ndiyo rai inayopendekezwa kwa Fatwa.
Hilo pia ni dhihirisho la mshikamano wa kijamii, na malipo ya kutoa sadaka wakati wa Ramadhani huongezeka thawabu maradufu. Kutoa sadaka katika mwezi huo uliobarikiwa ni sawa na ujira wa kutoa sadaka katika miezi mingine. Imepokewa katika Hadithi ya Salman Al-Farsi (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) amesema: “Mwenye kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika mwezi wa Ramadhani kwa kufanya jambo jema lolote atakuwa kama ametoa Faridha wakati wowote mwingine, na anayetoa sadaka ya Faradhi katika Ramadhani, atakuwa kama aliyetoa Faradha sabiini katika wakati wowote mwingine wa Ramadhani.” [Imesimuliwa na Ibn Khuzaymah katika Sahihi yake na Al-Baihaqiy katika Shuab Al-Iman.]
Lakini, ujuzu huo uko chini ya masharti ambayo lazima yazingatiwe yafuatayo:
Kwanza: Usahihi wa utafutaji juu ya masikini na wahitaji, na kutokuwa dhaifu katika kuigawanya na kumpa kila mtu, awe jamaa, majirani na kadhalika, muhimu wawe wanastahiki kweli. Katika hali hiyo, watakuwa na kipaumbele katika kutoa, bila kuwapuuza wengine wanaohitaji, ikiwa wapo.
Pili: Bidhaa au chakula lazima kiwe kile ambacho masikini na wahitaji wanakihitajia wakati huo wa mwaka, sio kile wanacholazimishwa au kile ambacho wanaweza kuhitaji katika siku zijazo, sio sasa. Na hiyo ili jambo lisigeuke kutoka katika kuwanufaisha masikini na kuwajibisha kwa kile wanachopewa katika vitu hivyo, jambo ambalo lingewalazimu kuviuza kwa bei ya chini baada ya kuvichukua, ama kwa sababu hawavihitaji, au kwa sababu wanahitaji kununua vitu vingine zaidi ya vile walivyolazimishwa.
Tatu: Kutotoa vitu vya ubora duni au vya duni miongoni mwao. Bali, ni muhimu kutoa bidhaa zinazofaa - kutoka kwa kile mlipaji Zaka alichomiliki awali - kwa masikini. Jambo hilo ni suala la jamaa ambalo linahitaji kuelewa uhalisi na kufanya kile kinachoitwa "utafiti wa kijamii" kwa wale wanaostahili. Bidhaa hizi lazima ziwe ni kwamba angeridhika nazo ikiwa zingebaki naye na hakuzitoa.
Nne: Inazingatiwa -wakati wa kutathmini bidhaa- bei ya kawaida ambayo itafaa ikiwa mtoa Zaka angemwuzia mtu mwingine bila ya lengo la kupata faida, kwa sababu makusudio ya Zaka ni kuwanufaisha wale wanaostahiki, na sio kujinufaisha.
Tano: Zaka isitolewe kwa pesa taslimu katika mfumo wa vyakula au mifuko ya Ramadhani, ili liwe kimbilio la kiujumla. Hii inaweza kusababisha wale wanaostahiki kupata Zaka kunyimwa njia za kulipia matumizi mengineyo, kama vile matibabu, elimu, na mengineyo. Zaidi ya hayo, kuna wanaostahiki wengine wa Zaka ambao wanapaswa kulipwa na kuzingatiwa, kama vile kundi la wenye madeni na wengine.
Yanaongezwa juu ya hayo, makusudio ya mtoa Zaka yasiwe tu umaarufu, kujulikana, sifa, au kuonesha ukarimu wake kwa masikini, hasa pale baadhi ya watu wanapowakusanya masikini mbele ya nyumba zao na kuwapa mifuko hiyo kwa njia ya kufedhehesha na isiyo ya kibinadamu. Hili linapingana na sharia ya Kiislamu inavyoelekeza, ambayo ni kupeleka pesa za Zaka nyumbani mwa mafakiri au wanaohitaji na kuwaheshimu, sio kuwadhalilisha.
Kwa hivyo, ikiwa hayatafikiwa masharti haya tuliyoyaeleza na masharti yanayofanana na hayo yanayohudumia masilahi ya mafakiri, masikini, na wale wanaostahiki Zaka kutoka katika makundi yake mengine na kuwaletea manufaa, basi wanapewa pesa za Zaka, na wana uhuru wa kuzitoa wanavyoona inafaa kufikia maslahi yao, ambayo wanayajua zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Hii ni kwa sababu ruhusa ya kutoa Zaka kwa pesa taslimu inategemea maslahi ya wale wanaostahiki kuipata.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Ni bora zaidi ya kutoa Zaka na kuwapa masikini taslimu.
Kama ilitakiwa Zaka itatolewa kwa wale wanaostahiki kuipata katika mfumo wa chakula, ni lazima izingatiwe kwa kile ambacho masikini wanakihitajia zaidi na kujua bidhaa gani ni muhimu wanazokosa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
