Kufunga Saumu bila ya kubainisha mw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufunga Saumu bila ya kubainisha mwaka wa kufidia Saumu

Question

Inabidi nifidie Ramadhani mbili nilizozivunja kwa sababu ya ugonjwa, lakini sikumbuki nilizivunja mwaka gani. Nilifunga kwa nia ya kufidia Ramadhani nilizozikosa, lakini sikubainisha kuwa nilikuwa nafunga mwaka gani. Je, funga yangu inatosha kama kufidia saumu nilizokosa, au kutobainisha mwaka maalumu wa kufidia saumu nilizokosa kunabatilisha funga yangu?

Answer

Saumu kwa nia ya jumla ya kulipa (qadhaa) bila ya kubainisha mwaka wa kulipa ni sahihi na inakamilisha wajibu. Inatosha kuwa na Nia ya kulipa bila ya kulazimika kubainisha mwaka au siku, kwa sababu yote ni aina moja ya Saumu.

Maelezo

Asili ya kulipa Saumu ya faradhi inatokana na kauli ya Allah (S.W): “Na yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa au yuko safarini, basi {Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine.} [Al-Baqarah: 184].

Asili ni kwamba ni sharti katika kulipa saumu ya faradhi, nadhiri, au kafara kuwa na Nia thabiti, kubainisha nia hiyo, na kuiweka kabla ya Alfajiri kwamba kesho atafunga kwa ajili ya Ramadhani, au kwa ajili ya kafara, au kwa ajili ya kulipa.

Kwa msingi huu, swali letu linahusu mtu ambaye anapaswa kulipa saumu za Ramadhani mbili ambazo alizifungua kwa sababu ya ugonjwa, na hajui ni lini wajibu wa kulipa ulianza kwake. Akafunga kwa nia ya kulipa bila ya kubainisha kwamba anafunga kwa ajili ya Ramadhani ya mwaka fulani. Wanavyuoni wa Imamu Hanafi, kwa maoni yao ya sahihi zaidi, wanasema kuwa saumu yake haitakamilisha wajibu wa kulipa Ramadhani.

Lakini Wanavyuoni wa Imamu Shafi wanaona kwamba si sharti kubainisha mwaka wa kulipa, kwa sababu Saumu ya kulipa (qadhaa) yote ni ya aina moja. Kwa hivyo, Saumu ya mtu ambaye ana Nia ya kulipa kwa ujumla bila ya kubainisha mwaka ni sahihi, na saumu yake inakamilisha wajibu wake. Na haya pia ni maoni ya baadhi ya Wanavyuoni wa Imamu Hanafi.

Kwa upande wa Wanavyuoni wa Imamu Maliki na Hanbali, inaeleweka kutoka kwa maneno yao kwamba kubainisha mwaka katika saumu si wajibu, bali inatosha kuwa na Nia ya kulipa. Kwa hivyo, kosa katika kubainisha wakati halihitajiki. [1]

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia;

Si sharti kubainisha mwaka katika Nia ya kufunga Saumu ya qadhaa, bali inatosha Nia ya kufunga Saumu ya wajibu.

Ikiwa mtu alibainisha mwaka na akakosea katika wakati, hili haliathiri, kwa sababu si sharti kuwa na Nia ya kulipa mwaka fulani au siku fulani iliyopita, bali inatosha Nia ya kulipa.

 

[1] “Tabiin Al-Haqaiq” ya Imam Al-Zayla’i Al-Hanafi (6/220), “Al-Fawakih Ad-Dawani” (1/304, Dar Al-Fikr), “Al-Mughni” (3/133, Maktaba ya Kairo), “Fath Al-Qadir” (2/312, Dar Al-Fikr).

Share this:

Related Fatwas