Kutoa Zaka kulingana na mwaka wa ku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Zaka kulingana na mwaka wa kuzaliwa Yesu

Question

Ninamiliki shirika la kibiashara, na ni vigumu kwangu kulipa Zaka kulingana na mwaka wa Hijiria, kwani bajeti ya shirika hilo inafungamana na mwaka wa kuzaliwa Yesu. Je, inajuzu kwangu kuihesabu kwa kuzingatia mwaka wa jua?

Answer

Inayozingatiwa katika kutoa Zaka ya pesa ni kupitiwa na  mwaka wa Hijiria - mwaka wa Hijria - na kiasi cha Zaka ni robo ya kumi (2.5%). Iwapo ni vigumu kwa mtu anayewajibika kuhesabu Zaka yake kwa mujibu wa mwaka wa Hijri kwa sababu kiasi cha fedha zake hakiko wazi isipokuwa kwa kuhesabu bajeti ya taasisi yake, ambayo ni kwa mujibu wa mwaka wa kuzaliwa Yesu, basi hakuna ubaya katika sharia ya Kiislamu kuihesabu kwa mujibu wa mwaka wa kuzaliwa Yesu, isipokuwa kwamba katika suala hili asilimia imeongezwa kuwa (2.575%). Badala ya (2.50%)

Maelezo

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Sharia ya Kiislamu imezingatia haki za masikini, na imefafanua upana hukumu za utoaji wa Zaka kwake – kuanzia kiwango cha chini kinacholazimisha kutolewa, aina ya mali inayopaswa kutolewa, na wakati unaopaswa kutolewa – ili haja ya masikini isitegemee matakwa au matamanio ya tajiri, ikizingatiwa hulka ya nafsi ya binadamu yenye ubakhili na kupenda mali.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa} [Al Hashri 9], na Mweynyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi} [Al Fajr 20].

Ama kuhusu kupita mwaka ni kupita mwaka mzima kwa mtu anayewajibika kuilipa, na mali yake imefikia kiwango cha Nisabu, kutokana na kauli ya Mtume (S.A.W.) “Hakuna zaka katika mali hadi ufikie mwaka”. Imesimuliwa na Abu Dawud, Al-Tirmidhiy, na Ibn Majah katika “Al-Sunan.

Na ameripoti makubaliano juu ya mahitaji ya mwaka, zaidi ya mwanachuoni mmoja kama vile; "Makubaliano ya Ibn Al-Mundhir." "Al Huul" kwa ujumla hutumika kumaanisha mwaka.

Inayomaanishwa kwa kupita mwaka katika asili yake ya kisharia ni mwaka wa Hijiria na sio mwaka wa kuzaliwa Yesu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: {Wanakuuliza khabari ya miezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hija} [Al Baqarah 189], na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua} [Yunus 5]. Basi miezi inayozingatiwa katika Sharia inatokana na mwandamo wa mwezi, na mwaka unaozingatiwa katika Sharia ni mwaka wa mwandamo.

Na inabainika kutokana na hilo, kwamba hukumu za kisharia –miongoni mwake ni sharti la mwaka kwa ajili ya kuwajibika Zaka- kimsingi zinahusiana na mwaka wa mwandamo, sio mwaka wa jua. Na kutokana na hayo, zimefikiana matini za Wanachuoni wa Fiqhi wa Imamu Hanafi, Maliki, Shafi na Hanbali. [1]

Lakini ikiwe ni vigumu kwa mtu aliyewajibika kutoa Zaka katika kuzingatia mwaka wa mwandamo, kama vile kuunganisha bajeti ya kampuni au taasisi yake - kama ilivyo suala letu - na mwaka wa jua, basi inajuzu kwake katika hali hiyo kutegemea mwaka wa jua katika kuhesabu na kutoa zaka yake. Lakini wakati huo, anawajibika kuongeza asilimia ya Zaka kutoka 2.5% iliyoainishwa na Sharia kwa mwaka wa Hijiria, hadi asilimia ya idadi ya siku ambazo mwaka wa jua unazidi mwaka wa mwandamo. Hiyo kwani, mwaka wa jua una siku kumi na moja (11) takriban zaidi ya mwaka wa mwandamo. Siku za mwaka wa "kuzaliwa Yesu" wa jua ni takriban (365), wakati siku za mwaka wa "mwezi" wa Hijiria ni takriban (354). Hiyo inasababisha kukatwa kwa mwaka kutoka kwa Zaka ya mtu anayelazimika takriban kila miaka thelathini na tatu.

Kwa hiyo, hiyo inaweza kurekebishwa na mtu anayelazimika kulipa (2.577%). Asilimia hii hupatikana kutokana na kuzidisha robo ya kumi (2.5%) kwa idadi ya siku katika mwaka wa (kuzaliwa Yesu) (365) ikigawanywa na idadi ya siku katika mwaka wa Hijri (354), yaani: (2.5 x 365 ÷ 354 = 2.577%).

Hili linaungwa mkono kutoka maoni ya Wanazuoni wa Madhehbu ya Malik katika kuzingatia mwaka wa jua unapaswa kwa ajili ya Zaka ya mifugo, ambayo inakusanywa mwanzoni mwa majira ya joto, ambao ni msimu mingoni mwa misimu ya mwaka wa jua. Hiyo ni kwa ajili ya kuhakikisha faida kubwa zaidi na kupunguza ugumu na shida inayowakabili wamiliki wa mifugo na wakusanyaji Zaka wakati wa kuzingatia mwaka wa mwandamo. [Dhuu’ Ash Shumu’ Sharhu Al Majmou’].

Basi iwapo ni vigumu kwa mtu anayewajibika kuhesabu Zaka yake kwa mujibu wa mwaka wa Hijiria kwa sababu kiasi cha fedha zake hakiko wazi isipokuwa kwa kuhesabu bajeti ya taasisi yake, ambayo ni kwa mujibu wa mwaka wa kuzaliwa Yesu, basi hakuna pingamizi kutoka kwa Sharia kuihesabu kwa mujibu wa mwaka wa kuzaliwa Yesu, lakini inazingatiwa katika suala hili asilimia hiyo imeongezwa na kuwa (2.527%).

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

kushurutisha mwaka unaohitajika kwa Zaka linatokana na mwaka wa mwandamo, sio mwaka wa jua.

Inajuzu kutegemea mwaka wa jua, pamoja na kuzingatia tofauti baina ya miaka miwili.

Tofauti baina ya miaka miwili inakokotolewa kwa kutoa 2.577% kutoka mwaka wa jua badala ya 2.5%.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Z aidi

 

[1] - “Al-Bahr Al-Ra’iq” cha mwanachuoni Mkuu Ibn Nujaym Al-Hanafi (2/219, chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy), “ Sharhu Al-Kharashi’s  juu ya  Mukhtasar Khalil” (2/162, chapa ya Dar Al-Fikr), “Fatawa Al-Subki, Dar’s Al-Maarifah’), “Al-Lubab” cha mwanachuoni Mkuu Ibn Adil Al-Hanbali (3/334, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah).

Share this:

Related Fatwas