Kujishulisha na kupiga picha wakati wa Ibada ya Hija na Umra
Question
Nilisafiri katika safari pamoja na (kundi) la mahujaji kwenda Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutekeleza faradhi ya Hija. Kila tulipopita katika maeneo matukufu, niliona baadhi ya watu waliokuwa pamoja nasi katika kundi la mahujaji wakizidisha sana upigaji picha kwa simu zao kupita kiasi cha kawaida. Jambo hilo lilikuwa linatuletea ucheleweshaji wa kutekeleza ibada kwa wakati unaotakiwa, na pia liliwasababishia usumbufu baadhi ya wazee na watu wasiojiweza. Kwa hiyo niliwaomba kwa heshima wapunguze wingi wa kupiga picha, lakini mmoja wao alinijibu kuwa yeye anajitahidi kupata picha za kumbukumbu kwa maeneo matukufu. Hata hivyo, waliendelea kufanya hivyo mpaka jambo hilo likamfikia msimamizi wa mpangilio wa safari, naye pia alikasirishwa na kitendo hicho, kwa kuwa kinamkwamisha katika kazi na jukumu lake kutokana na kuchelewa kwa mwendo wetu. Basi, hukumu kwa mujibu wa Sharia ni ipi kuhusu kuzidisha upigaji picha kwa namna hii iliyopitiliza?
Answer
Kupiga picha wakati wa Ibada ya Hija kunajuzu kisharia kwa sharti la kutopelekea kuwachelewesha mahujaji, na kupiga picha kwa kuvuka mipaka kunaweza kusababisha kero, hasa panapkuwa na wazee, pamoja na hayo mtu aliyehirimia anatakiwa kulazimika na utulivu na adabu wakati wa kuwepo katika maenezo matakatifu kama Msikti wa Makkah, kwani Mwenyezi Mungu ameamrisha kuutukuza na kuuheshimu, pia mwenye kuhuji anatakiwa kujishughulisha na unyenyekevu katika kutekeleza ibada ya Hija, ili Mola amlipe dhawabu na malipo, na kuifanya Hija yake ni yenye kukubaliwa.
Maelezo
Uhalisia wa kupiga picha: Ni mtu kutumia kamera ili kuchukua picha ya kumbukumbu.
Picha kwa maana hii katika asili yake inajuzu kisharia, sharti isiwe na yaliyokatazwa; kama kupiga picha mwili uliouchi, au uchi ambao ni wajibu kusitiriwa, na kusababisha madhara kwa watu wengine … n.k.
Na imethibiti kwamba miongoni mwa ibada tukufu zaidi ambazo zinaelezea uchamungu wa moyo na kunyenyekea kwake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuadhimisha Ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: (Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo)[Al-Haj: 32].
Na kutukuza Ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakusanya kuonesha maana za kuheshimu, kutukuza unyenyekevu, na kufuata amri za kutekeleza na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Ibada hizo; kwani kutukuza kwake ni katika kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, imepokewa Hadithi kutoka kwa Abdullah bin Abbas R.A. amesema katika kutafsiri kwake kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu)[Nuh: 13], mna nini hamjui ukweli wa utukufu wake?
Na kwa kuwa Hija ni alama katika alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu; hilo linahitaji kumtukuza kwa kuonesha maana ya juu kabisa ya heshima, kwa adabu, kuhifadhi upole wakati wa ibada, sawasawa hilo lilikuwa wakati wa kutufu pembezoni mwa Al- Kaaba tukufu au katika kukimbia kati ya Swafa na Marwa, kusimama Arafa na wakati wa kutupa mawe, na heshima hii haiji ikiwa Mtu anashughulika na kupiga picha kila sehemu katika sehemu tukufu kwa njia inayovuka mipaka; kwa namna anasababisha kuchelewesha watu katika kutekeleza ibada katika kutufu au kusayi, au hata katika mambo ya mpangilio ya kila kundi katika makundi ambayo watu wanashirikiana kwa pamoja, kama kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kupiga picha kukiwa kutasababisha madhara ya kuchelesha harakati za watu wengine au aina yeyote ya maudhi, kutazingatiwa ni haramu kisharia; kwa kauli ya Mtume (S.A.W): “Usidhuru wala usijidhuru” Hadithi hii imetolewa na Bukhari katika Sunanih.
Na madhara yaliyokatazwa katika Hadithi yanajumuisha madogo na makubwa, hili ni neno jumuishi linalokusanya kutodhuru katika mambo yote isipokuwa yale ambayo Sharia imeeleza uhalali wake kwa maslahi ya kisharia.
Hivyo basi kupetuka mpaka katika kupiga picha wakati wa ibada ya Hija ni aina katika aina za maudhi, na kutochunga hali za watu wengine kunakoweza kuwaingiza katika kero zilizokatazwa kisharia, pia hili linazingatiwa ni katika matendo yanayopingana na hali ambayo inatakiwa kwa anayezuru Msikiti wa Makka kuwa nayo, sawa sawa awe amehirimia Hija au laa; hivyo basi haifai kujishughulisha na jambo lingine nje ya ibada kama kupiga picha za kumbukumbu, kwa sababu asili ni kuwa hali yake katika kipindi hiki ni kuachana na upuuzi na matamanio huku moyo wake ukifungamana na Mola wake, akijishughulisha fikra zake kumridhisha Mola wake, akitaraji kukubaliwa Hija yake; ili apate katika hilo malipo arudi kama alivyozaliwa na mama yake hana dhambi wala kosa, Hija yake inakuwa imekubaliwa.
Na kunasisitizwa hili la kukataza kupiga picha kuliopitiliza wakati wa ibada ya Hija kwa mtu aliyeingia Msikiti wa Makka akiwa amehirimia au haja hirimia; kutokana na utukufu wake, haiba yake ambao Mwenyezi Mungu Ameulezea: (Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu)[Aal-Imran: 96-97].
Basi iweje katika eneo tukufu?! Na hali yakuwa Mwenyezi Mungu Ameielezea misikiti kwa ujumla: “Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu Ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni. Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Swala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka)[An-Nur: 36-37].
Imamu Ibn Kathir amesema: “Mwenyezi Mungu Ameamrisha uhifadhiwe na kutwahirishwa na uchafu na upuuzi wa maneno na vitendo ambavyo haviendani na eneo hilo”([1]). Na hapana shaka kwamba kuwaudhi wanaotekeleza ibada ya Hija au Umra na kuwachelewesha kutekeleza ibada zao kunahesabiwa kuwa ni katika matendo ambayo hayaendani na hali ya mtu ambaye anatakikana kuwa nayo anayekusudia sehemu hii yenye baraka.
Na imepokewa kutoka kwa Ayyash bin Abii Rabia Al-Makhzoumy kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Uma huu utaendelea kuwa katika kheri muda wa kuwa wanatukuza Msikiti Mtukufu ukweli wa kutukuza, wakipoteza hilo, wameangamia”. Hadithi hii imetolewa na Ibn Majjah katika Sunanih.
Kuwa na adabu kamili na upole katika nyumba ya Mwenyzi Mungu, kunazingatiwa ni katika kuadhimisha aliyoyatukuza Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Anasema: (Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi)[Al-Haj: 30]. Na vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, eneo la haramu na Msikiti wa Makka, Al- kaaba na mji mtukufu wa Makkah.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kupiga picha kipindi cha ibada ya Hija kunajuzu kisharia kwa sharti ya jambo hilo kutosababisha kuchelesha mahujaji. Na wajibu wa mtu aliyehirimia na asiehirimia kufuata adabu, upole na utulivu wakati wa anapokuwa katika maeneo matakatifu kama Msikiti wa Makka.
Mtu aliye katika ibada ya Hija anatakiwa ashughulike na unyenyekevu katika kutekeleza Ibada, ili alipwe na Mwenyezi Mungu Mtukufu malipo na thawabu, na kufanya Hija yake kuwa ni yenye kupokelewa.
([1]) Tazama: Tafseer Al Qur’aan Al-Adheem, 6/56.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
