Kulala na Kupitwa na Swala ya Alfaj...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulala na Kupitwa na Swala ya Alfajiri

Question

Ni ipi hukumu ya mtu aliyelala na kupitwa na Swala ya Alfajiri?

Answer

Swala inapendekezwa kisharia (Mustahabb) kwa Muislamu kuharakisha kutekeleza katika wakati wake wa kwanza.  Kutoka kwa Abdullah bin Mas'ud  (R.A). amesema: Nilimuuliza Mtume (S.A.W).: ((Ni amali gani inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Akasema: Swala katika wakati wake).

Ama kwa yule aliyepitwa na moja ya Swala katika wakati wake kwa udhuru kama vile kulala, kusahau na mfano wa hayo, ni wajibu kwake kuharakisha kuilipa Sala hiyo.

Mtume (S.A.W). amesema: (Mwenye kusahau Swala, au akalala na ikampita, basi kafara yake ni kuiswali pindi aikumbukapo).

Ikiwa mtu atalala na kupitwa na Swala ya Alfajiri mpaka jua likachomoza, bila kukusudia kuikosa, na hakuamka kutokana na uchovu mwingi, basi ni wajibu kwake kuilipa anapoamka.

Katika Hadithi ya Safwan bin Al-Mu'attal (R.A.) amesema: (Hatukuwa tukiamka mpaka jua linachomoza, Mtume (S.A.W.) akamwambia: Basi ukiamka sali).

Maelezo

Imethibitika kisheria kuwa Swala ni nguzo ya Uislamu na ni nguzo ya pili baada ya Shahada mbili.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na simamisheni Swala, na toeni Zaka, na rukuuni pamoja na wanaorukuu}[Al-Baqarah: 43].

Pia Anasema: {Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu}[An-Nisaa: 103].

Kutoka kwa Abdullah bin Umar (R.A.) amesema: Mtume (S.A.W). amesema: (Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Shuhuda ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Sala, kutoa Zaka, Hija, na kufunga Ramadhani)[1].

Inapendekezwa kisheria kwa Muislamu kuharakisha kutekeleza Sala katika wakati wake wa kwanza na kujiandaa kwa ajili yake.

Imepokewa Katika Hadithi ya Ibn Mas'ud,amesema:  nilimuuliza Mtume (S.A.W). ibada gani inayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: Swala katika wakati wake, akasema: kisha ibada gani? Akasema: Kuwatendea wema wazazi wawili. akasema: kisha ibada gani? Akasema: jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu”[2].

Faida inayopatikana  kutokana na Hadithi hii kuwa kutekeleza Swala katika wakati wake wa kwanza ni miongoni mwa amali bora na zinazopendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kwa yule anayepitwa na wakati wa moja ya Swala tano za Faradhi (Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, na Isha) na hakuziswali, hukumu yake ni: Ni wajibu kwake kulipa Swala hizo zilizompita.

Hadithi ya Anas bin Malik (R.A). inasisitiza kuwa kulala au kusahau ni sababu zinazomfanya mtu alipe Swala pindi anapokumbuka[3].  Hadithi inatoa ushahidi kwamba alipitwa na Swala ya Faradhi kwa sababu ya kulala au kusahau na mfano wa hilo; basi ni wajibu kwake kulipa Swala hiyo.

Vilevile, ikiwa mtu atalala na kupitwa na Alfajiri mpaka jua kuchomoza bila kukusudia, iwe ni kwa sababu ya uchovu mwingi au kukosa wa kumuamsha, hapati dhambi. Na niwajibu kwake kufanya haraka kuilipa atakapoamka; imepokewa kutoka kwa Abu Saeed Alkhudry Katika kisa cha Safwan bin Al-Mu'attal, ndani ya kisa hiki alimwambia  Mtume (S.A.W). “... Mimi siswali mpaka kuchomoza jua, sisi watu wa nyumbani tumezoea hivyo, hatuamki mpaka kuchomoza jua, akaema: Ukiamka Swali”[4].

Mtume (S.A.W). ametoa udhuru kwa anayeshindwa na usingizi kutokana na mazoea yake ambayo amezoea kiasi kwamba hawezi kuamka isipokuwa baada ya jua kuchomoza.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kusali Swala tano za Faradhi katika wakati wake wa kwanza ni jambo linalopendekezwa kisharia, na ni miongoni mwa amali bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu.

Mwenye kupitwa na Swala ya Faradhi kwa udhuru wa kulala au kusahau, ni wajibu kwake kuharakisha kuilipa.

Ni katika rehema za Mwenyezi Mungu kwamba amejalia kutokuamka kwa ajili ya Swala ya Alfajiri katika wakati wake wa kwanza kutokana na kuzidiwa na usingizi au uchovu mwingi kuwa ni udhuru unaomruhusu mhusika kuilipa Swala hiyo baada ya kuamka bila ya kuwa na dhambi.

 

[1] Imepolkelwea na Al Bukhary.

[2] Imepokelewa na Al Bukhary

[3] Imepokelewa na Muslim.

[4] Imepokewa na Abou Dawoud.

Share this:

Related Fatwas