Maana ya uwezo katika Hija na Umra

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya uwezo katika Hija na Umra

Question

Ni nini maana ya uwezo katika Hija na Umra

Answer

Uwezo ni sharti ili Hija iwe wajibu, uwezo unapatikana kwa mwili kuwa na nguvu, na kuhimili ugumu wa safari na kutekeleza ibada ya Hija,  njia kuwa salama, na kumiliki gaharama zake miongoni mwa chakula, vinywaji na malazi, na gharama za usafiri ambazo zinamfiksha mji mtukufu na kumrudisha katika mji wake pasi na kujinyima au ubadhirifu, na kuwa haya matumizi ni ziada ya mahitaji yake ya msingi na mahitaji ya wanaomtegemea kipindi cha kukosekana kwake nyumbani, miongoni mwa malazi, mavazi, samani, chakula cha familia yake na mavazi yao na kulipa madeni yake.

Maelezo

 

Hija na Umra ni miongoni mwa alama na ibada kuu za Uislamu. Zinaunganisha maana za aina zote za ibada, kwa kuwa zinajumuisha ibada ya kimwili na ya mali. Hivyo basi, anayetekeleza Hija au Umra ni kama vile amefunga, ameswali, amekaa Itikafu, ametoa Zaka, na amejitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu hiyo, Sharia ya Kiislamu imezithibitishia fadhila kubwa na thawabu nyingi. Imepokewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema:
“Umra moja hadi Umra nyingine ni kafara ya madhambi yaliyo kati yake, na Hija iliyokubaliwa haina malipo ila Pepo.”

Amepokea An-Nasaaiy na At-Tirmdhy katika Sunan zao kutoka kwa Abdullah bin Masoud R.A. amesem: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.): “Fuatilizieni kati ya Hija na Umra kwani hivyo vinaondoa umasikini na madhambi kama mpuliza chuma anavyoondoa uchafu wa chuma, dhahabu na fedha, na Hija njema malipo yake ni pepo”.

Wanazuoni wa Madhebebu manne ya Fiqhi wamekubaliana kwamba uwezo ni sharti la kupasa Hija, hakuna Hija kwa asie na uwezo, Imamu Shafi na Hanafi wanaeleza kuwa hilo ni sharti la kupasa Umra pia; kwa sababu Umra kwao ni wajibu, ama Imamu Hanafi na Malik Umra kwao ni Sunna ya yenye kuhimizwa. [1] Na wemetoa ushahidi kwamba uwezo ni sharti ya kupasa Hija na Umra kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea)[Aal-Imran: 97].

Na uwezo kisharia wametofautiana Wanazuoni wa Fiqhi katika tafsiri yake, Madhehebu ya Imamu Hanafi wanasema kwamba uwezo wa maandalizi na kipando, kuwa vimezidi katika mahitaji yake ya msingi, na mahitaji ya yule ambaye anamtegemea yeye kipindi ya kutokuwepo kwake na usalama wa njia.

Madhehebu ya Malik wanaeleza kuwa uwezo ni uwezo wa kufika Makka, na maeneo ya Ibada ya Hija hata kama kwa kutembea pasi na uzito mkubwa, pamoja na usalama wa njia, roho na mali, uwezo kwao haushii katika maandalizi na kipando.

Madhehebu ya Imamu Shafi wanaeleza kuwa uwezo upo aina mbili: Uwezo unahusiana na nafsi, na uwezo unapatikana kutoka kwa mtu mwingine. Ama uwezo unaohusiana na nafsi unafikiwa kwa sharti: ikiwemo kuwepo maandalizi, vyombo vyake, chakula chake wakati wa kwenda na kurudi, na kupatikana mnyama kwa mtu ambae yupo mbali na Makkah, ama aliye karibu na Makkah, basi kutamlazimu kuhiji akiwa na nguvu ya kutembea  kwakutokuwa na uzito, yeye hazingatiwi kupatikana mnyama, akiwa hawezi kutembea kwa uzee au alaipatwa na madhara ya wazi basi anazingatiwa kama mtu wa mbali. Na kunashartiza kuwa maandalizi na mnyama kuwa ni ziada ya deni lake na chakula chake na chakula cha wale wanaomtegemea kipindi chote cha safari yake kwenda na kurudi na mahitaji yake ya asili, pamoja njia kuwa salama.

Madhehebu ya Imamu Hanbali wanaona kwamba uwezo ni uwezo wa maandalizi na mnyama anayeendana na hali yake, na kuwa ni ziada ya mahitaji yake ya msingi na mahitaji ya wanaomtegemea kipindi cha kukosekana kwake, na ni miongoni mwa sharti za kupasa Hija katika Madhehebu yao ni njia kuwa salama usalama wa rorho na mali na heshima([2]).

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kwamba uwezo ni sharti ya kupasa Hija unafikiwa kwa mwili kuwa na nguvu, kuvumilia ugumu wa safari na kutekeleza ibada ya Hija, na usalamawa njia, na kumiliki matumizi na maandalizi, na kuwa hayo matumizi ni ziada ya mahitaji yake ya Msingi na mahitaji ya wanaomtegemea kipindi cha kukosekena kwake.

 

([1]) Hashiyat Ibu Abdeen 2/472. Ash-Sharh As-Sagheer, 2/4

([2]) Ar- Rawda Al-Muree, uk.247.

Share this:

Related Fatwas