Kuitikia Salamu Wakati wa Kusoma Qur'ani Tukufu
Question
Mtu emekaa msikitini akisoma Qur'ani Tukufu na baadhi ya wanaopita wanamsalimia. Je, inamlazimu kuitikia salamu ya yule anayemsalimia?
Answer
Kuitikia salamu kwa msomaji wa Qur'ani Tukufu kwa yule anayemsalimia kunaruhusiwa , na hitilafu ipo kati ya wajibu au au si wajibu kuitikia, msomaji anaweza kuitikia salamu au asiitikie, bila ya dhambi wala ubaya wowote kwake katika hilo. Lakini ikiwa atajua kwamba kuacha kuitikia kunaweza kusababisha athari mbaya kwa anayemsalimia, basi kuitikia kunakuwa bora zaidi, hata kwa ishara ya mkono, kwa ajili ya kumtia moyo, na kuhifadhi upendo baina yao, na kuimarisha vifungo vya udugu.
Maelezo:
Salamu ni maamkizi ambayo Mwenyezi Mungu amewapa Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema.}[An-Nur: 61]
Na tumeamrishwa kutoa salamu na kuieneza katika jamii kwa ujumla; kwa sababu ya wema na heshima iliyomo ndani yake. Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullah Ibn 'Amru kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (S.A.W): ((Ni upi Uislamu bora? Akasema: Kuwalisha chakula, na kutoa salamu kwa unayemjua na usiyemjua)) Hadithi hii imepokelewa na (Bukhari na Muslim).
Wanachuoni wa Fiqhi wamekubaliana kwamba kutoa salamu na maamkizi ni Sunna inayopendekezwa, na kwamba kuitikia ni wajibu kwa mtu mmoja; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Na mnapoamkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo.}[An-Nisaa: 86] [1]
Na jumhuri ya Wanachuoni wa Fiqhi - miongoni mwa wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi, na baadhi ya Maimamu wa Madhehebu ya Maliki, na pia baadhi ya Maimamu wa Madhehebu ya Shafi kama vile Al-Adhra'iy na Jalal Ad-Din As-Suyuti, na wafuasi wa Madhehebu ya Hanmbali – wameondoa katika wajibu wa kuitikia salamu kwa yule anayeitoa: sehemu ambazo mpokeaji (anayesalimiwa) hawezi kurudisha salamu; kwa kuchunga hali yake aliyonayo ili asiingie katika dhiki. Na miongoni mwa hawa ni msomaji wa Qur'ani Tukufu - kama lilivyo suala letu - hivi kwamba haimlazimu kuitikia salamu kwa yule anayemsalimia, si kwa neno wala kwa ishara. Na Imamu Malik na Shafi katika kauli yao yenye nguvu wamesema kwamba msomaji wa Qur'ani Tukufu ni kama wengine, hivyo inamlazimu kuitikia salamu kwa maneno kwa yule anayeitoa.
Na kundi la Wanachuoni wa Fiqhi - miongoni mwao ni Imamu Al-Wahidi Ash-Shaafi - wamesema kwamba msomaji wa Qur'ani Tukufu anaruhusiwa kuitikia salamu kwa ya anayemsalimia kwa ishara bila ya maneno. Ikiwa atarudisha kwa maneno, basi inambidi aanze tena kusoma kwa istia'adha (kusema A'udhu billahi minash-shaytaanir-rajiim) mara nyingine, kisha arudi kusoma Qur'ani Tukufu. [2]
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Msingi wa suala hili unategemea urahisi, hivyo inaruhusiwa kufanya kazi ndani yake kwa kauli yeyote miongoni mwa kauli za Wanazuoni wa Fiqhi bila ya dhambi kwa anayetekeleza katika hilo wala ubaya.
Jambo linaachwa kwa msomaji wa Qur'ani Tukufu na tathmini yake ya kile ambacho ni bora kufanya kulingana na hali yake, na hali ya anayemsalimia, iwe atahuzunika kwa kuacha kuitikia salamu au la, na kile ambacho desturi ya watu ilivyo kwao, kwa njia inayotimiza kusudi la sharia ambalo ni kueneza urafiki na upendo katika jamii na baina ya watu.
[1] "Ngazi za Makubaliano" (uk. 156, chapa ya Dar Al-Kotob Al-Ilmiyyah).
[2] “Al-Bahr Al-Ra’iq” (2/16, chapa ya Dar Al-Kotob Al-Ilmiyyah), “Asna Al-Mataleb” (4/183, chapa ya Dar Al-Kotob Al-Ilmiyyah), “Kashaf Al- m m Qina’” (2/178, Dar Al-Kotoy-I-Ilmiyyah) Al-Kabir” (1/198, chapa ya Dar Al-Fikr), “Al-Majmu’” (2/167, chapa ya Dar Al-Fikr).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
