Kuomba Dua Wakati wa Kunyesha kwa Mvua
Question
Je, wakati wa kunyesha mvua ni miongoni mwa nyakati ambazo maombi hujibiwa?
Answer
Kuomba dua wakati wa kunyesha mvua ni miongoni mwa nyakati ambazo dua hujibiwa; kwa sababu ni nyakati za karama, fadhila, upole, na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake.
Maelezo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu amechagua baadhi ya sehemu na nyakati, na amezifanya kuwa ni sehemu pa kutazamiwa kujibiwa kwa dua, kama rehema na fadhila kutoka Kwake kwa waja Wake, Na miongoni mwa nyakati hizi ni: kuomba dua wakati wa kunyesha mvua; kwa sababu ni nyakati za karama, fadhila, upole, na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kama ilivyo katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Dawud na Al-Hakim kutoka kwa Sahl Ibn Sa'd (R.A) imeinuliwa kwa Mtume (S.A.W): “Mambo mawili hayarudishwi: dua wakati wa Adhana, na chini ya mvua” Yaani: wakati wa kunyesha kwake; kwa sababu ni wakati wa kushuka kwa rehema.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Umamah (R.A) kutoka kwa Mtume (S.A.W): “Milango ya mbinguni hufunguliwa, na dua hujibiwa katika sehemu nne: wakati wa kukutana kwa safu katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakati wa kunyesha mvua, na wakati wa kusimamisha Swala, na unapoiona Ka'bah” Imepokewa na Al-Bayhaqi katika Al-Ma'rifah, na At-Twabarani katika Al-Kabiir.
Na Imamu Shafii amepokea katika Al-Umm kutoka kwa Abdul Aziz Ibn Omar kutoka kwa Makhul kutoka kwa Mtume (S.A.W) amesema: “Tafuteni kujibiwa dua wakati wa kukutana kwa majeshi, na kusimamisha Swala, na kunyesha mvua”.
Pia wanazuoni wa Fiqhi wametumia athari zinazoonesha upendeleo wa kuomba dua wakati wa kunyesha mvua kuwa ni ushahidi kwamba dua wakati wa kunyesha mvua hujibiwa. Miongoni mwa hayo ni: Hadithi ya Umm Al-Mu'minin Bibi Aisha (R.A): “Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alikuwa akiona mvua anasema: Ee Mwenyezi Mungu, ijaalie iwe mvua yenye manufaa” Imepokewa na Al-Bukhari. Na katika tamko la Abu Dawud kwamba alikuwa akisema:”(Ee Mwenyezi Mungu, ijaalie iwe mvua nzuri, yenye kufurahisha”.
Na Muislamu anaomba kwa anachokitaka kwa Hadithi ya Al-Bayhaqi: “Dua hujibiwa katika sehemu nne: wakati wa kukutana kwa safu, na kunyesha mvua, na kusimamisha Swala, na kuona Ka'bah”, na kwa kile kilichopokewa kwamba Mtume (S.A.W) amesma: “Tafuteni kujibiwa dua wakati wa matatu: wakati wa kukutana kwa majeshi, na kusimamisha Swala, na kunyesha mvua”.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kuomba dua wakati wa kunyesha mvua ni miongoni mwa nyakati ambazo dua hujibiwa; kwa sababu ni nyakati za karama, fadhila, upole, na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake, kama ilivyooneshwa na Sunna Tukufu.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
