Kuhimili Gharama za Kurudisha Bidha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhimili Gharama za Kurudisha Bidhaa Iliyonunuliwa Mtandaoni

Question

Mwanamume aliuza vitabu kwa mwanamume mwingine. Mauzo yalifanyika kupitia intaneti, na walikubaliana kwamba mnunuzi, baada ya kuvichunguza vitabu, angekuwa na haki ya kuvirudisha na kurejeshewa thamani yake tena ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe ya kuvipokea. Vitabu vilipofika na mnunuzi akavipokea na kuvichunguza, alitaka kuvirudisha. Akaiomba kampuni ya usafirishaji kuvirudisha kwa muuzaji. Ni nani anayepaswa kubeba gharama ya kurudisha?

Answer

Gharama ya kurudisha bidhaa iliyonunuliwa kupitia mauzo "mtandaoni" na kuisafirisha tena kwa muuzaji, katika kipindi kilichokubaliwa kati ya muuzaji na mnunuzi au kilichoelezwa na sheria, inakuwa juu ya mnunuzi. Hili ni isipokuwa wakikubaliana na kuridhiana juu ya vinginevyo. Katika haya yote, masharti na taratibu zinazobainishwa na sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya mtandaoni, ulinzi wa mlaji, na kadhalika, huzingatiwa.

Maelezo

Miamala ya Kifedha katika Sharia ya Kiislamu imewekwa kwa ujumla wake kutimiza maslahi ya viumbe na kukidhi mahitaji yao, ndani ya mfumo wa amri na makatazo ya kisharia yanayofanya kazi ya kufikia usawa katika kila upande kupata manufaa yake kwa kushughulika na upande mwingine. Mwenyezi Mungu amehalalisha mauzo na ununuzi katika asili yake...

Muamala unaoulizwa ni aina ya mauzo ya kielektroniki, mojawapo ya picha za taratibu za kisasa za kimikataba katika mauzo. Kufanya mikataba ya mauzo na ununuzi "mtandaoni: online" kwa njia ya masoko ya kielektroniki, ambapo muuzaji huonyesha maelezo ya bidhaa na jinsi ya kumkabidhi mteja baada ya kukubaliana bei, ni katika kundi la kuuza kitu kisichopo kinachoelezwa.

Mauzo haya ni halali na hakuna kizuizi cha kisharia juu yake, kwa kuzingatia yale ambayo idadi kubwa ya Wanachuoni wa Fiqhi wamekubaliana (kutoka Kwa Imamu Hanafi, Maliki, Shafi, na Hanbali), kwa sababu asili katika miamala ni uhalali isipokuwa kile ambacho sharia ilileta kukiharamisha. Mradi mauzo ya biashara ya mtandaoni yanatimiza vipengele muhimu vya mauzo halali, ikiwa ni pamoja na sheria na masharti yanayohusiana na ofa na kukubalika, wahusika walioingia mkataba, na mada husika, basi yanaruhusiwa kulingana na sharia ya Kiislamu.

Maswahaba watukufu (R.A) walikubaliana kwa kauli moja kuhusu uhalali wa kuuza kitu ambacho hakipo lakini kinaweza kutolewa, bila pingamizi lolote. Makubaliano haya yameripotiwa na wasomi wengi. [1]

Wanachuoni wa Fiqhi wengi wamebainisha uthibitisho wa haki ya kuona (khiyar Al-ru'yah) kwa mnunuzi. Ikiwa atanunua bidhaa lakini hajaiona, anakuwa na hiari (uchaguzi) anapoiona: akitaka achukue kwa bei yake, na akitaka arudishe. Na hayo ni kwa ajili ya dharura inayoita [kufanya hivyo] wakati haiwezekani kuona, ili kuleta manufaa ya haraka kwa muuzaji kwa kuharakisha kupata thamani (bei), na kwa mnunuzi kwa kupata kwa bei rahisi (istarhkas) [2].

Ikiwa makubaliano yamefanyika, bidhaa imemfikia mnunuzi na ameipokea, na anataka kuirudisha baada ya hapo, basi gharama katika hali hii inakuwa juu ya mnunuzi. Hii ni kwa mujibu wa yale yaliyotajwa na Wanachuoni wa Fiqhi wengi (Imamu Hanafi, Shafi, na Hanbali) kwamba mnunuzi akirudi kwenye bidhaa iliyouzwa, basi mzigo wa kurudisha unakuwa juu yake.

Ushahidi wa hilo ni yale yaliyopokewa na Imamu Ahmad katika "Al-Musnad" na Ibn Majah na Nasa'i katika "Al-Sunan" kutoka kwa Samurah (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: ((Jukumu linamuangukia aliyochukua mpaka alipe)). Na neno "Jukumu" (على) katika Hadithi ni neno la lazima. Kwa kuwa mnunuzi amepokea bidhaa, basi utekelezaji (ulipaji/kukamilisha) unakuwa lazima kwake, isipokuwa wakubaliane kwa kuridhiana juu ya vinginevyo. Inaeleweka kutokana na matini ya mafuqaha kwamba gharama ya kurudisha bidhaa iliyouzwa na mzigo wake kimsingi inakuwa juu ya mnunuzi isipokuwa wakikubaliana vinginevyo.

Mweka-Shaeria wa Misri pia ameelekea huku kuhusiana na bidhaa. Amempa fursa mlaji kurudi kwenye bidhaa aliyoinunua kwa mbali (distance selling) ndani ya siku kumi na nne (14) tangu kuipokea. Pia amemlazimisha msambazaji (muuzaji) kurudisha kiasi cha fedha kilicholipwa na mlaji kwa njia ileile ya malipo, ndani ya muda usiozidi siku saba (7) tangu tarehe ya kurudisha bidhaa. Huku akiamua kwamba mzigo wa kurudisha katika hali hii unakuwa juu ya mlaji - yaani mnunuzi - si muuzaji. Yote haya ni isipokuwa wakikubaliana na kuridhiana juu ya vinginevyo, kama ilivyoelezwa na Kifungu (40- aya ya 1, 2) cha Sheria Namba (181) ya mwaka 2018 kuhusu Ulinzi wa Mlaji.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Miamala ya kifedha katika Sharia ya Kiislamu kwa ujumla wake imewekwa ili kufikia manufaa ya viumbe na kukidhi mahitaji yao.

Masoko ya kielektroniki ni katika kundi la kuuza kitu kisichopo kinachoelezwa, na mauzo haya yanajuzu na hakuna kizuizi ndani yake.

Katika hali ya kurudisha bidhaa baada ya mnunuzi kuipokea, basi gharama za kurudisha ziko juu ya mnunuzi.

 

[1] "Nawadir Al-Fuqahaa" (uk. 241, toleo la Dar Al-Qalam).

[2] “Al-Hawi Al-Kabir” (5/19, kilichochapishwa na Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah), “Bidayat Al-Mubtadi” (uk. 133, kilichochapishwa na Muhammad Ali Subaih), “Al-Kafi” (2/678, kilichochapishwa na Maktabat Al-Riyadh Al-Haditha), “Al-Mughan, kilichochapishwa na Makhirata 4/95” (49/495)

Share this:

Related Fatwas