Kususia Bidhaa za Wapiganaji Maadui...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kususia Bidhaa za Wapiganaji Maadui.

Question

Nini Hukumu ya kugomea bidhaa za wanaowapiga vita waislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Baadhi ya mataifa -hasa katika kipindi cha vita na migogoro- yanategemea silaha ya uchumi ili kumwathiri adui yake kwa kuwa silaha ya uchumi ina athari inayoonekana katika kuweka utawala wa nchi zenye nguvu kiuchumi dhidi ya nchi maskini, kama vile kuzuia kuuza bidhaa kwa nchi maskini au kutonunua kutoka mataifa maskini, au kuchukua hatua zote mbili, na pengine kuna mzingiro wa kijeshi unazuia kuingia au kutoka bidhaa.

Na kutomwezesha mpiganaji adui ni jambo la kisheria, wenye akili hawahitilafiani nalo, na wanachuoni walizungumzia biashara na watu wa vita, na wengi wao waliojuzisha waliweka sharti ya kutowapa silaha nzito na mfano wake, pia walizungumzia hayo katika mlango wa yanayochukuliwa kutoka biashara yao miongoni mwa mali katika kuwafanyia wepesi katika bidhaa muhimu ambazo tunazihitajia.

Ama hukumu ya kisheria katika kususia ni kujuzu kisheria katika asili yake lakini inaweza kukosolewa na hukumu zingine za kisheria, kama vile waislamu wakipatwa na madhara ya kijeshi au kiuchumi kutokana na mzingiro, basi wakati huo, hukumu itakuwa inazunguka baina ya Makruhu na Haramu kwa mujibu wa hali, na huwenda mzingiro wa kiuchumi ukawa na athari kubwa juu ya wapiganaji maadui, basi kwa wakati huo hukumu itakuwa inazunguka baina ya wajibu na kupendeza, kwa mujibu wa hali.

Na dalili ya hayo ni nyingi, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wakamateni mateka (kama wanavyokufanyieni) na wazungukeni na wakalieni katika kila njia} [AT TAWABA 5].
Al Tabariy alisema: "na wazungukeni" anasema wazuieni kushughulika katika nchi za Uislamu". [Tafseer Al Ttabariy, 143/14, Ch. Muasasat Al Risalah]. Na hayo yanaingia katika kila mzingiro ikiwemo wa kijeshi na wa kiuchumi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamuwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa..} [AL ANFAL 60].

Abu Al Souud alisema: {nguvu kama muwezavyo}, yaani kila aina ya nguvu na silaha vitani. [Tafseer Irshaad Al Aql Al Saleem 32/4, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Haikuwapasia watu wa Madina -na Mabedui wakaao pembeni mwao, kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (wasende vitani). Wala (haiwapasii kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake (Mtume, wakamwacha Mtume kwenda vitani, wao wakasalia na raha zao Madina). Haya ni kwa sababu ya kuwa hakiwapati kiu wala taabu wala njaa katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakanyagi njia iwachukizayo makafiri, wala hawamtii adui hasara yoyote, ila huandikiwa kitendo chema (kabisa) kwa ajili ya hayo. Hakika Mwenyezi Mungu haharibu ujira wa watendao wema} [AT TAWABA 120].

Na ushahidi hapa ni kwamba aya imebainisha kuwa kila kinachowabughudhi makafiri ni jambo la kisheria, na hiyo ina uhusiano na kile kinachoitwa vita vya kisaikolojia, na hakuna shaka kwamba kususia sekta ya kiuchumi kunakusanya upande wa mali na hali wakati mmoja.

Na miongoni mwa hadithi tukufu za Mtume S.A.W. ni kutoka kwa Anas, kwamba Mtume S.A.W alisema: "Piganeni na washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu pamoja na ndimi zenu (lugha zenu) [Imetolewa na Abu Dawuud, Al Nassaiy, Ibn Habaan, Al Haakem na aliisahihisha kwa ya Sharti ya Muslim, na ilitolewa na Al Khatteeb Al Baghdadiy katika Al Faqeeh na Al Mutafaqeh 557/2, Ch. Dar Ibn Al Jawziy], na alisema: akawajibisha mdahalo na washirikina, pia akawajibisha matumizi na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Na ushahidi ni kwamba hadithi imebainisha kuwa jihadi na ubabe hauwi kwa silaha tu, bali kugomea au mzingiro wa kiuchumi ni moja ya aina za jihadi kwa mali kwa sura ya kuacha, kwani kuacha au kuzuia ni kitendo, na mwanadamu huwenda akapata thawabu kama vile kuacha yaliyoharamishwa na yaliyochukizwa, na huwenda akaadhibiwa kama vile kuacha wajibu, kwa hivyo jihadi kwa mali inagawika sehemu mbili; jihadi kwa vitendo vizuri na jihadi kwa vitendo vibaya.
Na hayo yanaungwa mkono na yaliyotajwa kutoka kwa Anas, alisema: "Mtume S.A.W. aliingia Makka kwa ajili ya Umra ya Kadhai, na Ibn Rawaha alikuwa mbele yake akisema:

Kuweni mbali na Mtume enyi kizazi cha makafiri
na leo tunakupigeni kama isemavyo Dini
kipigo kinachotenganisha uso na shingo
na kumsahaulisha mtu na Yule ampendae

Omar R.A alisema: "Ewe Ibn Rawaha! Unasema shairi hili katika msikiti wa Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.? Basi Mtume S.A.W. akasema: "Mwachie, na ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, maneno yake ni makali kwao kuliko kasi ya mikuki." [Imetolewa na Al Tarmaziy, kisahihishwa na Al Nassaiy.].

Na msingi wa mlango huo ni yaliyotajwa katika Sahihi mbili katika kisa cha kusilimu Thumamah Bin Athaal, bwana wa watu wa Alyamamah aliposilimu,: "Mtume S.A.W alimbashiria na akamwamuru kufanya Umra, basi alipofika Makka mtu mmoja alimwambia: umeacha dini yako? Basi akasema: hapana! Lakini nilisilimu pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.. Na Wallahi! Haikujieni chembe ya ngano kutoka Alyamamah isipokuwa kwa idhini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.".
Na pia ilitolewa na Ibn Habaan aliyesema: "Katika maelezo hayo kuna dalili ya kuhalilisha biashara ya waislamu pamoja na nyumba za vita.

Na aliyoyataja Ibn Habaan yanafafanuliwa na riwaya ya Al Baihaqiy katika kitabu cha [Al Daleel] ; "Basi walimkasirisha, akasema: mimi Wallahi sikuacha dini yangu lakini nimesilimu, na nimemwamini Muhammad, na ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Thumamah iko mikononi mwake, haikujieni chembe ya ngano kutoka Alyamamah - ilikuwa ni shamba ya Makka- katika maisha yangu yote, mpaka aruhusu Mtume Muhammad S.A.W., na alirudi katika mji wake, na akazuia mizigo ya chakula kwa Makka hadi makuraishi walichoka, basi walimwandika risala Mtume S.A.W wakimtaka amwandikie Thumamah ili aruhusu mizigo ya chakula kwenda Makka, basi Mtume S.A.W akafanya hivyo.

Na ushahidi hapa ni kwamba kukubali kwa Mtume S.A.W. kitendo cha Thumamah katika kugomea kiuchumi, na kumruhusu baadaye ni dalili kwamba asili yake ni kujuzu.

Na miongoni mwa yanayoingia katika mlango huo pia, ni kitendo cha Nabii Yusuf pamoja na kaka zake, alichokisimulia Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Quraani katika kauli yake: {"Na alipowapatia chakula chao alisema: "(Mkinijia mara ya pili) nijieni na ndugu yenu wa kwa baba. Je! Hamuoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wakaribishao? (Basi nitakukaribisheni nyote kwa uzuri) (59). "Na kama hamtaniletea, basi hamtakuwa na kipimo (cha chakula) chochote kwangu, wala msinikukaribie}[YUSUF 59,60].

Na ushahidi ni kwamba Yusuf amani ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iwe juu yake alitaka kuwanyima chakula kaka zake kama ni mbinu ya kuwalazimisha kumletea ndugu yao.

Na wanachuoni katika hukumu zao walizingatia masilahi na madhara yanayotokana na sheria ambazo nchi inazitumia juu ya wafanyibiashara wa mataifa adui, na wala hawakutoa hukumu hivi hivi, bali walizingatia yanayotokana na miamala, na walijuzisha kubadilisha hukumu kwa ajili ya hayo.

Al Sarkhasiy alisema: "Na ana haki kutoa bidhaa yoyote anayoitakia isipokuwa tulizozitaja, pia mfanyibiasahara mwislamu ana haki kuwachukulia mizigo yoyote ambayo anaitaka kwa ajili ya biashara, na Al Shafiy -rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iwe juu yake- anasema kwamba haifai kwani wanazidisha nguvu kwa mizigo hiyo kama vile, vyakula, mavazi, na silaha. Lakini sisi tunatumia dalili hii : “Mtume S.A.W. alimzawadia Abi Sufiyaan R.A. tende mbivu iliyokandwa alipokuwa Makka hali ya kuwa ni kafiri, na yeye akamwomba Abuu Sufiyaan ampatie ngozi, na aliwapelekea watu wa Makka dinari mia tano walipokumbwa na ukame ili zigaiwe kwa wanaohitaji."

Na baadhi ya mahitaji ya waislamu kama madawa n.k yanatoka nyumba ya vita (kwa maadui), kwa hivyo tukiwazuia wafanyibiashara waislamu kuwachukulia yasiyokuwa silaha basi na wao watazuia ya kwao, na bila shaka hapa kuna madhara." [Al Mabsuutt 91/10, Ch. Dar El Maarifa.]

Na Al Khatteeb Al Sherbeeniy alisema:"Basi kama kafiri atamuomba imamu ruhusa ya kuingia mji wa Alhijaaz basi atamruhusu kama kuingia kwake ni masilahi kwa waislamu, mfano anapeleka risala, kufunga mkataba wa amani au kubeba chakula au mizigo ambayo tunahitaji sisi waislamu. Na kama kuingia kwake si kwa masilahi ya waislamu basi imamu asitoe idhini ya kuingia, na kama kuingia kwake si kwa ajili ya biashara yenye haja kubwa kama vile manukato basi imamu asimruhusu kuingia Alhijaaz ila kwa sharti ya kuchukua mizigo kutoka kwake. Na kiwango cha sharti kinakadiriwa na imamu, kwa kumwiga Omar R.A. ambaye yeye alikuwa akichukua ushuru (sehemu moja ya kumi) wa bidhaa kama mashuka kutoka kwa wakristo wa Misri wanapofanya biashara mjini Madina, na alikuwa akichukua nusu ya ushuru (nusu ya sehemu moja katika kumi) kutokana na ngano ili kuwahamasisha kuleta bidhaa hiyo ambayo waislamu wanaihitajia.

Na mpiganaji adui aliyeingia nchini kwetu hafanywi kuwa ni mjumbe wala asiruhusiwe kufanya biashara tunayoihitajia. Na iwapo hatuihitajii, imamu anaweza kumruhusu kwa kuchukua ushuru, hata kama utazidi sehemu moja ya kumi au utapungua, na kama atamsamehe ushuru pia inajuzu. [Mughniy Al Muhataaj 67/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elimiyah].

Na kutokana na hayo yaliyotangulia inabainika kuwa kususia na kugomea (katika sekta ya uchumi) bidhaa za mataifa au makundi au mashirika wapiganaji maadui wa waislamu inajuzu kisheria katika asili yake katika hukumu yake ya kisheria, lakini inawezekana kukosolewa na hukumu zingine za kisheria ambazo ni wajibu au Sunna au Makruhu au Haramu, kwa mujibu wa tofauti ya hali na kubadilika kwa vipimo vya masilahi na madhara kwa mujibu anavyokadiria kiongozi wa waislamu na anayesimamia maswala ya mahusiano ya kimataifa na kiuchumi, na namna gani kususia huku kunamwathiri adui, na majibu ya kitendo hiki kwa nchi za waislamu, jamii zao na maisha yao ya kiuchumi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas