Uislamu na Kukubaliana kwake na Eli...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uislamu na Kukubaliana kwake na Elimu ya Kisasa, Kiroho na Kimfumo

Question

Elimu ya kisasa kama tuonavyo hivi sasa inatufichulia siri mbali mbali za ulimwengu ambazo hazijawahi kufikiriwa na mtu yoyote miongoni mwa waliotangulia, na shukrani za haya zinarejea katika mfumo wake ambao elimu hiyo imeufuata, je Uislamu unakubaliana na elimu kiroho na kimfumo? Na nini mwonekano wa makubaliano hayo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

1) Hakika ukitazama kwa mtazamo wa kina -katika kauli ya marehemu profesa Abu Al Wafa Al Ghonemiy Al Taftazaniy mmoja wa wanavyuoni wakubwa wa kisasa wa falsafa ya Kiislamu -, utakuta kwamba elimu katika msingi wake ni jambo lenye thamani, kwani msomi hupata maelezo yake kwa mujibu wa maadili maalumu, yanayojulikana kama misingi ya mfumo wa kielimu, kwa hivyo basi, elimu si maelezo tu bali pia ni njia au mfumo wa kupatia maelezo hayo, nayo kwa zingatio hili, elimu kitu chenye thamani miongoni mwa vitu vya thamani, jamii inapoiamini elimu kama ni njia ya maisha, basi jamii hiyo hufanikisha maendeleo yake ya kiungwana yanayotakiwa, na iwapo jamii haikuiamini thamani hiyo basi watu wake huwa ni wahanga wa ulimwengu wa mawazo na uzushi, na hawatafanikisha lolote katika jamii yao kwa upande wa mali na wa kiroho.

2) Na kwa maana hii, thamani ya elimu ni thamani ya msingi katika Uislamu, kwani hii ndiyo inayofanya pawepo na tofauti ya vyeo kati ya watu katika jamii kwa msingi wake, kwani elimu ni msingi wa kila kazi yenye mafanikio au mwenendo bora, na ucha Mungu - ambao pia ni miongoni mwa misingi ya utofautishaji wa vyeo baina ya watu- nayo inarejeshwa kwenye elimu kwa hukumu za kidini, kwa hivyo basi, ubora kati ya watu kwa hali iliyo wazi, hurejea pia katika elimu; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mwenyezi Mungu atawainua walioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.} [AL MUJADALAH 11]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema pia: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?} [ZUMAR 9].

3- Na Uislamu umewatanabahisha watu kuwa elimu haisiti katika kiwango maalumu, na hapo kale watu walikuwa wakiamini kuwa yaliyothibitika kielimu yako hivyo hivyo kama yalivyo na hayatetereki, mpaka pale wataalamu wa mfumo wa kutafiti walipokuja kuthibitisha kuwa matokeo ya elimu huwa katika hali ya uwezekano na yanaweza kubadilika. Na jambo hili linatufafanulia kuwa maendeleo ya elimu yanasonga mbele, na maana yake ni kuwa hayo yote yamekusanyika katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu.} [TWAHA 114]. Na kisha ikawa ni wajibu kwa mwislamu ajiongezee elimu siku baada ya siku, kwani mwendo wa elimu kamwe hausiti.
4) Na miongoni mwa yaliyo na dalili za kina ni kwamba elimu katika Uislamu ina kiwango cha juu mno cha umuhimu. Hakika ni kwamba jambo la kwanza aliloteremshiwa Mtume S.A.W katika Quraani Tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui}. [AL ALAQ 1-4]. Kwa hiyo tunaona Bwana wetu Mtume S.A.W anajaalia ukombozi wa wanaojua kusoma na kuandika miongoni mwa mateka wa vita vya Badr ni kuwafundisha waislamu kumi walio mjini kusoma na kuandika.

5- Na elimu katika Uislamu sharti iwe na manufaa, Mtume S.A.W alikuwa akiomba kujikinga kutokana na shari ya elimu isiyonufaisha katika dua yake maarufu: "Ewe Mola wangu hakika mimi nakuomba unikinge na moyo usio na ucha Mungu, na dua isiyosikilizwa, na nafsi isiyotosheka, na elimu isiyokuwa na manufaa". Na kinachokusudiwa kwa tamko la “elimu yenye manufaa katika Uislamu yaani ni ile ambayo mtu na jamii wananufaika nayo. Na imepokelewa kutoka kwa khalifa Omar Bin Abdulaziz kwamba alimwaandikia Abu Bakar Bin Hazm akisema: "Angalia kilichokuwa Hadithi ya Mtume S.A.W, na ukiandike, kwani mimi ninachelea kutoweka kwa mafunzo ya elimu (yaani kuondoka athari za elimu) na kutoweka kwa wanazuoni, kwa hivyo waeneze elimu na wakae kwa ajili ya elimu mpaka wafundishe asiyejua, kwani elimu haiangamii mpaka pale inapokuwa siri."

6- Kwa hiyo elimu katika Uislamu ina thamani ya kimsingi, na kuoana kwa elimu na Uislamu kuko wazi, hakuna uwezekano wa kuzungumzia kuwepo kwa ukinzani kati ya elimu na Uislamu, kwa hivyo basi, Uislamu kuwa pamoja na elimu ni uhai na mfumo. Quraani inapoelekeza akili katika ugunduaji wa siri za viumbe hulingania kwa ulinganiaji wa wazi kwa maana ambayo inafahamika katika zama zetu hizi.

7- Na Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Quraani Tukufu: {Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani ya mawingu hayo. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha.}[AR RUUM 48]. Na katika kauli yake: {Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.}[AN NUUR 43].

Kwani Quraani Tukufu kwa aya hizi mbili inatusukumia katika ufikiriaji wa kielimu uliopo kwenye mfungamanisho wa maonekano ya maumbile kwa sababu zake za kweli na zisizokuwa za kufikirika tu, Mawingu, mvua, na radi vinafungamana katika kutokea kwake na visababishi maalumu kama vile joto la jua na maji ya baharini.

8- Na Quraani Tukufu ina aya nyingi zinazohimiza akili ya mtu mwenye ufikiri juu ya kufichua kanuni za maumbile ambayo ni muonekano wa mfuo wa ulimwengu kama ambavyo wakati huo huo, ni dalili za kwamba ulimwengu huu haukuumbwa kimakosa au kipuuzi na kwamba kuna upeo wake.

9- Na Quraani Tukufu haiafikiani na sayansi ya kisasa tu bali imeitangulia sayansi hii. Kwani ndani yake kuna aya nyingi za miujiza ya kisayansi na bado wanavyuoni wangali wakifichua kila wakati siri za miujiza ya kisayansi. Na kuna watafiti wengi waliozungumzia upande huu wa miujiza ya Quraani kwa ufafanuzi zaidi.

Marejeo: Profesa Dkt. Abu Al Wafa Al Ghonemiy Al Taftazaniy (Profesa wa Falsafa ya Kiislamu; Chuo Kikuu cha Kairo), Al-insaanu Walkawnu Fiy Islaam, (Mwanadamu na Ulimwengu katika Uislamu), Kairo, Dar Al Thaqafat Li Nashr wa Al Tawuzee, 1995, (Uk. 21-23/ 60-63).

Share this:

Related Fatwas