Waislamu kutilia umuhimu elimu za kiakili
Question
Je! Waislamu kutilia umuhimu elimu za kiakili kunahesabiwa ni katika kuacha Qur`ani na Hadithi kama wanavyodai watu wenye itikadi kali?
Answer
Kutilia umuhimu elimu za kiakili ni kutilia umuhimu Qur`ani na Hadithi, kwani kwa akili ndiyo kunafahamika kusihi Qur`ani na Hadithi kama dalili inayozingatiwa, kisha kinafahamika kinachokusudiwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa waja, akili haipingani na nukuu, bali kimoja kinaikamilishe kingine, kama kulivyokuwa na mambo uthibitisho wake haukamiliki kwa dalili za kunukuu au kwa Qur`ani na Hadithi pekee pasi na akili, kama uwepo wa Mwenyezi Mungu, pia kuna mambo akili pekee si njia ya kuyafahamu mambo hayo, kama kuwepo Pepo na Moto, na uhakika wa mizani na Sirat, na Majini na Malaika. Ama hukumu za kifiqhi kama faradhi za Swala, Sunna zake na adabu zake, akili japo si chanzo cha hukumu hizo, lakini imeyafahamu kutoka katika Matini za Qur`ani na Hadithi, na ikaukutanisha na mifano; hivyo basi kutilia umuhimu kuipa akili mafunzo na kudhibiti kanuni zake kuna umuhimu mkubwa, kwani akili ikiharibika, ufahamu unaharabika pia, na kama utaharibika ufahamu, tutakengeuka makusudio ya Mwenyezi Mungu kwetu, hivyo, basi Mwenyezi Mungu Anatuzindua katika hilo katika Aya mbalimbali, Anasema: (Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao tia mambo akilini)[Ar-Raad, 4] .. (Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu)[Al-Anaam, 98].