Tofauti Kati ya Ada na Ibada

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti Kati ya Ada na Ibada

Question

Kuna tofauti gani kati ya ada na ibada kwa mujibu wa mtazamo wa sheria ya Kiislamu? Je, mambo yote ambayo ni wajibu ni lazima yawe miongoni mwa ibada? Au inawezekana baadhi ya mambo ambayo ni wajibu yawe miongoni mwa ada?

Answer

 Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na amani ziwe juu ya Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na juu ya jamaa zake, familia na wafuasi wake, na baada ya hayo ..,
Ibada katika lugha ina maana ya utii na unyenyekevu, kama katika aya hii: {Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana.(92) Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake.} [MARYAM: 92.93], Imamu Ibn Jarir Al-Tabari amesema katika tafsiri yake [JamiiAl-Bayaan 18/261, Muasasat Al-Resala.]: “Mja atakuja kwa Mola wake siku ya kiamamnyonge, mtiifu, akikiri kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu”. Kama katika aya hii: {Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada} [AL FATIHA: 5] yaani tunakutii kwa namna ambayoinatufanya tunanyenyekea. Ibn al-Atheer alisema: “Maana ya ibada katika lugha ni: kutii pamoja na kunyenyekea. Baadhi ya wataalamu walisema: asili ya utumwa ni: udhalili na unyenyekevu. [Taju Al-Arus kwaAl-Zubaidi 8/330, 331 Daru Al-Hidaya], neno la ibada katika lugha inaonesha mwenye kuabudu anayedhalilika kwa Mola wake akioneshaunyenyekevu wake kujisalimisha kwake kwa Mola wake kwakikamilifu,kwa ajili ya kumridhisha, na asili ya kuabudu: udhalili. [Tajiu Al-Arus 8/340].
Ibn Saidah amesema katika kitabu cha [Al-Mukhasas 4/62, DaruIhyaa Al-Turathu Al-Arabi)] “Asili ya ibada katika lugha ni udhalili”.
Maana ya ibada katika istilahi inakaribiana na maana yake katika lugha, inasemekana kwamba ibada ni: yaliyofanywa kwa ajili ya ibada, kwa sharti ya kutia nia na kujua anayeabudiwa. inasemekana kwamba ibada ni: yaliyofanywa na mwislamu kinyume cha matamanio yake kwa ajili ya kumtukuza Mola wake. Rejea: [Al-Hudud Al-Aniqatu kwa Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Ansari uk. 77, Daru Al-Fikru Al-Muaser – Beirut], [Al-Taarifat kwa Al-Jrjana uk. 189, Daru Al-Kitabu Al-Arabi.].
Baadhi ya wanavyuoniwametofautisha kati ya maana tatu nazo ni: kutii,kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu na ibada, Ibn Abidin anataja tofauti kati yao, akinukuu Zakaria Al-Ansari Sheikh Al-Islam akitambua kwamba misingi ya madhehebu ya Hanafi haikupingana na tofauti hii pia alinukuu Al-Hamwiy miongoni mwa wanavyuoni wa madhehebu ya Al-Hanafiy, akisema katika maelezo yake [Radu Al-Muhtar ala Al-Durr Al-Mukhtar 1/106, DaruAl-Kutub Al-elmiyah]: “kutii ni: kufanya mambo yanayolipwa, kama yakitegemea nia au la, kama amefahamika mwenye kuyafanya kwa ajili yake au la. Kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu ni: kufanya mambo yanayolipwa, baada ya kujua nani anayejisogeza kwake, hata kama hayategemei nia. Na ibada ni: kufanya mambo yanayolipwa, kwa kutegemeania. Kama vile; sala tano, kufunga saumu, Zaka, Hija - na hayo mambo yote yanayotegemea nia, nikujisogeza kwa Mwenyezi Mungu, kutii na ibada. Na kuhusu kusoma Quraani na mambo ambayo hayategemei nia- ni kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu na kutii, lakini siyo ibada. Na kuhusu kuzingatia ambapo kunaongoza kwa kumjua Mwenyezi Mungu ni kutii, siyokujisogeza kwa Mwenyezi Mungu wala ibada. Na misingi ya madhehebu yetu haipingani nayo. Al-Hamwi. Lakini kuzingatia hakukuwa kujisogeza kwa Mwenyezi Mungukwa sababu ya kutojua anayejisogeza kwake, kwa sababu kujua kunatokea baadaye na kuzingatia siyo ibada pia kwa sababu hakutegemei nia”.
Utii maana yake ni kubwa zaidi kuliko kujisogeza na ibada nazo ni chini ya jina lake; kwa sababu ya utii ni: Kazi zote ambazo anayezitenda atalipwa, kama akiwa na nia ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu au hakukumbuka jambo hili wakati alipolifanya hivyo. Ama kuhusu kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu ni: Kazi zote ambazo anayezitenda atalipwa, kwa nia ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu, hata kama niasiyo sharti katika kulipwa kitendo hiki. Ibada ni: kutekeleza amri ambazo Mwenyezi Mungu ameziamuru kwa sharti ya kutia nia ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu ili alipwe.
Kama utii mtupu unagawanywa katika sehemu mbili: (vitendo vinavyolipwa kwa nia - na vitendo vinavyolipwa pasipo na nia); na kama utii unaolipwa kwa nia ukigawanywa katika: (ibada - na kujisogeza); bado sehemu nyingine ya utii mtupu, ambayo ni: (inayolipwa pasipo na nia) na Hakuna shaka kwamba sehemu hii inaingia katika vitendo vya dunia vinavyokusudiwa kufanya maslahi ya watu na mambo mengine ya maisha yao na shughuli zao, navyo wanavyovitenda kutokana na tabia njema na mila na desturi nzuri ambazo wanazo tu, na hadithi ambayo imepokelewa na Al-Tirmidhiy na Ibn Majah na Ahmad kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah inaonesha sehemu hii ya vitendo vya ibada: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: "Mungu amsamehe mtu aliyewatangulieni, alikuwa rahisi kama akiuza, akinunua, na kama akiombwa mali yake".
Na ada katika lugha ni: vitendo vinavyorudishwa, na vinavyojulikana, mila na desturi [Lisan Al-Arab 3/316, Dar Sadir], Katika lugha ya Kiarabu baadhi ya wakati neno la dini linatumika na linakusudiwa maana ya ada na uhusiano ambao kati yao ni kama kwamba mtu anarejea kwayo katika vitendo vyake vyote.Ibn Mandhur mwanachuoni alisema katika [Lisaan Al-Arab 13/169]: “Na dini ni: ada na ushahidi wake ni kama ambavyo Waarabu wanasema: dini yangu iko hivyo, yaani ada yangu”.
Kitu cha kawaida nafsi inakipenda; kwa sababu mwenye kufanya kitu hichoanakirejea mara kwa mara, inasemekana alizoea kitu fulani, yaani alikirejea mara nyingi na akikikariri [Al-Muhkam wa Al-Muhit Al-Aadham 2/321, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.], Mwana wa kibedui aliimba akisema:
Amezoeatabia nzuri nimeona. :mtuanakipenda anachokirejea
Na ada katika istilahi ni kisawe cha desturi, yaani: “Ni jambo ambalo linarudiwarudiwa na linakubaliwa na watu wenye tabianzuri kwa kulikariri mara kwa mara, na neno la ada linafahimika kwamba ni jambo maalum linalokaririwa na limezoeleka kinyume cha jambo ambalo linatokea kwa bahati mara moja au mbili, na watu hawalizoei, basi jambo hili siyo miongoni mwa ada na halitegemei hukumu yoyote, na desturi inakaribiana na ada katika maana”. [Durar Al-Hukaam fi Sharhi Mijallatu Al-Ahkaam 1/44, Ibara ya 36, Dar Al-Jiil].
Na Mwenyezi Mungu anasema kwa Mtume wake katika Qur'an: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili.} [AL AARAAF: 199], Ibn Al-Najaar Al-Futouhiy alisema katika [Sharu Al-Kawkab AlMuniir uk. 599- 600, Matbatu Al-Sunna Al-Muhammadiyah.]: “(na) miongoni mwa dalili za Fiqhipia (kutumika kwa ada) ambayo ndiyo maana ya maneno ya wanavyuoni kwamba: ada inatumiwa kisheria; kutokana na hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Masoud R.A., kwamba: “jambo ambalo waumini waliliona ni bora basi jambo hili ni bora katika dini ya Mwenyezi Mungu”, na kutokana na mtazamo wa Ibn Attia katika aya hiyo: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema,} maana ya mema ni desturi, nayo ni: vitu vyote ambavyo nafsi zimevijua na sheria haivipingi. Ibn Dhafr akasema katika kitabu cha [Al-Yanbuu] kwamba: “desturi nivitu ambavyo wenye busara wamevionani vitu vizuri, na Mwenyezi Mungu amevikubali vitu hivi. Neno la wema linalokaririwa katika Quraani kama alivyosema Mwenyezi Mungu {Na kaeni nao kwa wema} [AN NISAA: 19], neno hili linakusudiwa kutokana na desturi ya watu katika wakati ule kuhusu jambo hilo ... basi hukumu ya kisheria imetegemea mambo yaliyozoeleka kwa watu. Na miongoni mwa mambo hayo ni kauli ya Mtume S.A.W. kwa Hindmke wa Abu Sufyaan "Chukua kwa wema kinachokutosha wewe na mwanao", na miongoni mwa mambo hayo pia ni: hadithi iliyopokelewa na Al-Haram Ibn Mahisah Al-Ansari kwamba, "Kutoka kwa Al-Baraa Ibn Aazib alisema: ngamia wa Al-Baraa aliingia katikabustani akafanya uharibifu, basi Mtume S.A.W. akawahukumu watu wa mabustani wahifadhi mabustani yao wakati wa mchana, na watu wa mifugo wahifadhi mifugo yao wakati wa usiku". Imepokelewa kutoka kwa Abu Daawuud na wanavyuoni wengi wameisahihisha hadithi hii. Na hiyo ni daliliinayothibitisha kutumia ada katika hukumu za sheria; kwa hivyo Mtume S.A.W. ametegemea ada katika hukumu, yaani kila kitendo kina hukumu maalum, ambayo haina msingi katika sheria wala katika lugha kama vile; kulima ardhi ambayo imeharibika, kuweka uzio katika wizi, na kula chakula katika nyumbamiongoni mwa nyumba za marafiki. Na vitu ambavyo vinakabidhiwa, vinaachwa, vinachukuliwa, vinatolewa, zawadi, vinachukuliwa kwa nguvu, kukaa kwa wema, na kufaidika kwa mwenye kulipa kodi kama ilivyozoelewa. Na mifano ya mambo hayo ni mingi sana na haiishi”.
Msingi wa kisheria unasema kwamba: (ada inatumika), na msingi huu ni mmoja kati ya misingi mitano mikuu iliyokubaliwa, na ambayo inasemekana kwamba masuala yote ya kifiqhi katika Uislamu yanarejea kwenye misingi hiyo [Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Al-Suyutiuk. 7, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na maana yake kama ilivyoelezwa katika [Durar Al-Ahkam 1/44]: “Yaani kwamba adaya umma au ya mtu binafsi inatumiwa kama hukumu kwa ajili ya kuthibitisha hukumu za kisheria. Jambo hilo ni msingiuliotajwa katika kitabu cha Al-Ashabah na kitabu cha Al-Majaami, na maana ya msingi ni ule unaorejewa; kwa sababu ni dalili ambayo hukumu inaitegemea”.
Mwanachuoni Al-Suyooti anazungumza kuhusu umuhimu wa kurejea kwa desturi na ada juu ya kujua hukumu za kisheria zinazofaa uhalisia, alisema akisisitiza wingi wa matawi ya kifiqhi ambayo yanayotegemewa juu ya msingi huo [Al-Ashabhwa Al-Nadhairuk.90.]: “Ujuekwambaada na desturi wanavyuoni wamezirejea katika Fiqhi katika masuala siyomengi. Nayo ni kama vile: umri wa hedhi, umri wa kubalekhe, na kutoka manii, na muda wahedhi, nifaasi, usafi, vitendo ambavyo havikubaliwi katika sala, najisi zinazosamehewa, urefu wa muda na ufupi wake katika kutia udhumara nyingikwa ajili ya kusali sala nyingi, hotuba, Ijumaa, kati ya kutoa na kukubali, kuamkia, na majibu yake, ucheleweshaji unaozuia kuzirejeabidhaakwa ajili ya kasoro, katika kunywa na kumwagilia mazao na kuinywesha mifugo kutoka vijito na mito inayomilikiwa, kula matunda yanayoanguka, kutengeneza pesa zilizoibwa…”.
Ada inafanywa kuwa kamahukumu kwa ajili ya kuthibitisha hukumu ya kisheria kama hakuna matini katika Qur-ani na hadithi inayohusu hukumu inayothibitika, lakini kama ikiwa na matini basi inatekelezwa matini hii na hairuhusiwa kuachwa na kufuatwa ada; kwa sababu hairuhusiwi kwa waja kubadilisha matini, na matiniina nguvu zaidi kuliko desturi; kwa sababu desturi pengine inaegemea juu ya upotofu, lakini Qur-ani na hadithi, haziegemei juu yauongo, kwa hiyo hairuhusiwa kuachwa jambo la nguvu kwa ajili ya kuchukuliwa la dhaifu. Imamu Abu Yusuf anasema: Kama matini ikipingana na desturitunafikiria kama matiniikitegemea desturi na ada, au la? Kama matiniikitegemea desturi na adainachukuliwa ada na matini inaachwa. Kama matinihaitegemeidesturi na ada basi matini inachukuliwa na ada inaachwa, hata hivyo, haipaswi kueleweka kwamba Imamu Abu Yusuf anaona kwamba kuachwa kwa matini na kuchukuwa kwa desturi na ada, lakini maoni yake ni kama ya tafsiri ya matini tu. [Durar Al-Ahkamfi Sharhimijalatu Al-Ahkam 1 / 44-45].
Kutokana na hayo, inafikirika kwamba kitendo kinacholazimika ni miongoni mwa ibada, na inafikirikapia kiwe miongoni mwa ada, kama vile: wajibu wa kukaana wanawake kwa wema,basi wajibu hapa hauingii katika masuala ya ibada, baliunaingia katikamasuala ya kiuchumi na maingiliano ya kijamiina ada; kwa sababu ibada inategemea nia, wakati ambapo suala la kukaa na wanawake kwa wema halitegemea nia, kwa hivyo, siyo kila jambo la wajibu ni ibada, na siyo kila utii ni ibada inategemeania. Wanafiqhi wamegawa vitabu vya fiqh na milango yake kwa ibada, miamala n.k. Ingawa sehemu hizi zotezina mambo yanayowajibika na mambo yanayokatazwa.Hii inaonesha kwambaipo dhana maalum ya ibada na kuabudu kwa vitendo maalum, na jambo hilo halizuii kumweleza mfanya biashara, kwa mfano, kwamba yeye ni mtiifu wa Mwenyezi Mungu, kwa vitendo vya biashara, lakini ni utii kwa maana pana, kinyume na anayekaa msikitini, anayesali, na anayefunga, kwa sababu hizi ni ibada kwa maana ya maalum.
Mwanachuoni mkubwa Ibn Abidin katika kitabu chake [Raddu Al-Muhtar 4/499, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.] alisema kwamba: “Masuala ya ibadayanakusudiwa vitendo vinavyomfanya mja kuwa karibu na Mola wake anayeabudiwa, na kupata thawabu na ukarimu, kama vile: nguzo nne n.k., namiamala inakusudiwa maslahi za jamii kama vile; kuuza na udhamini n.k., na kama kwamba kuuza au kununua kunaweza kuwa wajibu lakini bado ni miongoni mwa miamala, na pia sala pamoja na riyaa haitoki nje ya mambo ya ibada”.Alau Al-Ddin Al-Bukhari anasema: [Kashfu Al-Asrar Sharhu Usuulu Al-Bazdawiy 3/394, Dar Al-Kitabu Al-Isalami.]: “Nia ni wajibu katika ibada kwa ajili ya kupambanua kati ya ada na ibada”.
Pia anasema katika kitabu cha [Kashfu Al-Asrar 1/282): “Mwanadamu hawezi kuishi bila ya kula kwa mujibu wa maumbili yake kwa hivyo ni jambo la lazima aainishe kipindi kwa ajili ya kufunga na kipindi kingine kwa ajili ya kula, basi wakati wa mchana ulikuwa kwa ajili ya kufunga; kwa sababu katika wakati ule nafsi inahitaji kula na kunywa, basi kufunga kutakuwa kinyume na matamanio ya nafsi katika kipindi cha mchana, lakini hali ya kufunga usiku inafaa na matamanio ya nafsi, na asili ya ibada iwekinyume na ada na siyo kulingana sawasawa”.
Na katika kitabu cha [Maraqi Al-Falaah Sharhu Nuru Al-Idhaah uk. 351, na juu yake Hashiatu Al-Tahtawi, toleo la Mustafa Al-Halabi.]: “(Na inachukiza kufunga siku zote); kwa sababu humdhoofisha mtu au kunakuwa kama ada, lakini ibada ni tofauti na ada”.
Mwanachuoni Ibn Al-Daqeeq anasema katika kitabu cha [SharhuUmdatu Al-Ahkam 2/52, Matbaatu Al-Sunna.]: “Wanawake wamekatazwa kuvaa nikabu na glavu na hukumu hii inaonesha kuwa ihram ya wanawake inahusu uso wake na mikono yake. Na siri yake, na siri ya kukataza kuvaa mavazi ya kushonwa na mambo mengine miongoni mwa yaliyotajwa – Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi – ni ukiukaji wa ada, na kutoka nje ya mambo yaliyozoeleka kwa ajili ya kuijulisha nafsi mambo mawili: la kwanza: kuwa mbali na ulimwengu, na kukumbuka kuvaa sandana kuacha mavazi yaliyoshonwa. La Pili: kujizindua kuhusu ibada hii kuuisiwe kama ada, na hivyo itakuwa sababu ya kuhifadhi misingi yake, nguzo zake, masharti yake, na adabu zake”.
Ni wazi kuwa kutokana na yaliyotangulia hapo juu kwamba mambo muhimu zaidi ambayo yanapambanua kati ya ibada na ada ni kwamba: ni lazima kutia nia ya kumsogelea Mwenyezi Mungu katika ibada zote kwa kufuata utaratibu wake pamoja nakuonesha unyenyekevu kwake kwa njia isiyo ya mazoea katika maisha ya kijamii ya watu; kwa sababu ibada inategemea ukiukaji wa ada na kuondoa hisia inayozoeleka, na hali hiyo si lazima katika ada, lakini uzuri wake ni kama ilivyoelezwa kwamba ni mambo ya utiifu yanayolipiwa thawabu, lakini wakati mwingine ni lazima turejee kwayo kama hakuna matini kutoka katika Quraani au hadithi ili iwe dalili miongoni mwa dalili za kisheria ambazo zinatambuliwa na Sheria.Kwa hivyo, baadhi ya mambo yanayolazimika yanategemea desturi na ada, na wanachuoni wanaoeleza mambo hayo kuwa ni wajibu, hawasemi kwamba ni miongoni mwaibada.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas