Tofauti kati ya kupita kiasi katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti kati ya kupita kiasi katika dini na kuchukua tahadhari

Question

Je, kuchukua tahadhari wakati wote kufuatana na kauli za wanvyuoni ni kupita kiasi katika dini au la? Na kama siyo, basi tofauti gani kati ya mambo hayo mawili?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sheria ya Uislamu imekuja kwa uvumilivu, huruma na uongozi wa njia iliyonyooka, na miongoni mwa madhumuni yake yaliyo muhimu zaidi yalikuwa ni kuondoa ugumu wa maisha na uzito kwa watu. Mwenyezi Mungu anasema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote}[ AL ANBYAA: 107], na Mwenyezi Mungu anasema: {Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanayemkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anayewaamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao} [AL ARAAF: 157], Mwenyezi Mungu alisema: {Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.} [AL MAIDAH.6], na kwa hivyo kupita kiasi katika dini ni jambo baya; kwa sababu ni kinyume na madhumuni ya sheria yenye kusamehe na pia ni kinyume na yaliyokuja katika matini ambayo ni wazi kwamba zungukio la jukumu ni uwepesishaji, upunguzaji uzito, na mjongeleano kwa kiasi anachokiweza mtu mzima.
Imepokelewa na Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Abu Huraira, kwamba Mtume, S.A.W.. amesema: “majukumu ya dini ni rahisi, yeyote atakaeingiza ugumu ndani yake atashindwa. Basi elekeeni na mumkaribie Allah kwa ibada, nanyi furahini kwa Pepo, na kutafuta msaada kwa sala katika wakati wa asubuhi na jioni, na sehemu ya usiku”. Hafidh Ibn Rajab amesema katika {Sharhu Sahihul Bukhari, 1/149-151, Maktabat Al-Ghurbaa Al-Athariyh – Al-Madina Al-Munawara.]: “Maana ya hadithi hii: kukatazwa kupita kiasi katika dini ni wakati mwanadamu anapojaribu kutekeleza ibada kwa kiasi asichokiweza isipokuwa kwa ugumu na uzito mkubwa. Na hivyo ndivyo ilivyokusudiwa kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Yeyote atakaeingiza ugumu ndani yake atashindwa”. Maana yake ni: dini haiwezekani kuchukuliwa kwa mfumo huu wa kupita kiasi, basi yeyote atakayefanya hivyo katika dini atashindwa ... Na kauli ya Mtume S.A.W..: “Basi elekeeni na mkaribie na ibada, nanyi furahini kwa Pepo”. Kuelekea ibada maana yake ni: kuelekea madhumuni yaliyokusudiwa, asili yake ni kama vile kuuelekeza mshale ulipate lengo linalokusudiwa kwa mshale huo bila kulikosa. Kukaribia ni: mtu akaribiane na lengo kama hakulipata; lakini afanye bidii kwa ajili ya kulipata basi analipata mara moja na wakati mwingine anakaribiana nalo, au kukaribia kwa yule ambaye ameshindwa kulipata lengo hilo. kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Basi mcheni Mwenyezi Mungu kadiri mnavyoweza} [AL TAGHABUN: 16], na Mtume akasema S.A.W..: “Kama nikikuagizeni kufanya kitu chochote basi kifanyeni mnavyoweza.”
Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim katika Sahihi zao –na maneno haya ni ya Imam Muslim - kutoka kwa Abu Huraira RA. Amesema: Wakati wahabeshi walipokuwa wanacheza kwa mikuki yao, kando ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.. Omar ibn Al-Khattab akaingia na kuokota mawe madogo na kuwapiga nayo. Mtume S.A.W. akamwambia: “waache Ewe Omar”. Katika hadithi ya Al-Bukhari iliyopoelewa kwa njia nyingine, kwamba wao walikuwa wakicheza katika msikiti. Na Ahmad amepokea katika kitabu chake cha Musnad kutoka kwa mama wa waumini Aisha RA, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema wakati huo: “Mayahudi wajue kwamba kuna mapumziko katika dini yetu, hakika mimi nimetumwa kwa Dini ya al-Hanifiyyah (kuelemea Dini ya haki na kujiepusha na dini potofu) ambayo in usamehevu”. Al-Haafiz Ibn Hajar akaipa hadithi hii daraja ya Hasan katika [Taghliq Al-Taaliq, 2/43, Al-Maktaba Al-Islamiy).
Imamu Abu Jaafar Al-Tahawy Al-Hanafi alitaja katika [Mushkil Al-Athar, 1/269-270, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.] Kwamba kuna anayetia kasoro katika hadithi ya Aisha kuhusu kucheza kwa ujumbe wa wahabeshi msikitini, akisema: “Kama ilivyopokelewa na Aisha kuhusu lipi ni lazima kuachwa na lipi ni lazima kutokubalika; kwa sababu ni kucheza wahabeshi katika msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na hivyo ni miongoni mwa liwazo ambalo halifanyiki katika msikiti wowote, na vipi wavuke mipaka katika msikiti wa Mtume!.” Imamu El-Tahawy alijibu kwa hili kwa kusema: “jibu letu kuhusu jambo hili kwa neema ya Mwenyezi Mungu na msaada wake ni kwamba yaliyotokea katika hadithi ya Aisha kuhusu wahabeshi ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., siyo miongoni mwa liwazo baya, kwa sababu linahitajiwa na watu kama hawa katika vita, basi jambo hili ni zuri na linakubalika katika msikiti na mahali pengine popote.”
Na imepokelewa na Ahmad katika kitabu chake cha Musnad, kutoka kwa Muhjin Ibn Al-Adraa RA. kwamba Mtume, S.A.W. amesema: “Hakika nyinyi ni Umma mmependelewa wepesi” . Al-Haafidh Ibn Hajar katika kitabu chake [Fathul Bari, 1 / 94-95, Dar Al-Marifa- Beirut.] anasema: “Katika hadithi ya Muhjin Ibn Al-Adraa pamoja na Ahmad: “Hamuwezi kulipata jambo hili kwa ushindani na “lililo bora katika dini yenu ni wepesi”. Na huwenda Faida inayopatikana katika hadithi hii ni ishara ya kuitumia ruhusa inayopatikana kisheria, kwa sababu kuwa na lengo katika sehemu ya ruhusa kunakuwa kama vile mtu kuacha kutayamamu anaposhindwa kutumia maji na ikapelekea madhara kwa kuyatumia maji hayo.”
Na kutia uzito wakati ambapo hakuna uzito ni jambo baya sana katika dini, basi mambo ambayo Mwenyezi Mungu aliyoyafanyia wasaa na nafasi ya tofauti kati ya wanavyuoni na mitazamo mingi hairuhusiwa kuwatia watu mazito, kwa hivyo, katika misingi ya kifiqh kwamba: (hairuhusiwi kukataa mambo ambayo wanavyuoni wametofautiana nayo, lakini inaruhusiwa kukataa mambo ambayo wanavyuoni wamekubaliana nayo tu) [Rejea: Al-Ashbahu wal Nadhair kwa Al-Suyuti. p 158, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], Ibn Taymiyyah katika [Al-Fatawa Al-Kubra, 2/92, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] anasema: “Katika Sahih Muslim kwamba Mtume S.A.W. alisema: “Wameangamia wenye kuzidisha” amesema maneno haya mara tatu, yaani: watu ambao wanawatia watu mazito wakati ambapo hakuna haja ya kufanya hivi”.
Abu Dawood katika Sunan yake kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A. alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alikuwa akisema: “Je, msijitie mazito ili Mwenyezi Mungu asiwatieni mazito na hakika kuna watu wamejitia mazito na Mwenyezi Mungu amewatia kwao mazito, basi ni mabaki yao katika maghala na nyumba, Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo”.
Hii ni kukataza kwa kutia mazito katika dini, kwa sababu jambo hili linatafuta ukali wa makalifisho na ukali wa adhabu, Mwenyezi Mungu ameifanya dini rahisi na yenye msamaha, na anayekwenda kinyume cha maazimio ya dini, na anajitia mazito, ni la lazima atashindwa katika mambo ambayo amejilazimisha kutokana na mazito hayo ambayo ameyafikiri kwamba miongoni mwa mambo ya dini, baada ya hivyo anajiona mbali na dini an anafanya mambo kinyume chake na uamuzi wake unapungua na tama yake inadhoofika, na hajui kwamba kujitia mazito kulikuwa mlango wa shetani naye, Mwenyezi Mungu anasema: {Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata} [AL HADEID: 27], na Mtume S.A.W. akasema: “Yeyote ambaye aingize ugumu ndani yake atashindwa”
Mullah Ali Al-Qari katika kitabu cha [Mirqaat Al-Mafatiih Sharhu Mishkaat Al-Masaabiih, 1/266, Dar Al-Fikr- Beirut.] amesema: “Inaonekana kwamba maana ya: (Je, msijitie mazito) kwa kulazimisha mambo ya kuabudu ambayo ni mazito kama ni Nadhri Au kuapa, basi Mwenyezi Mungu atawatieni mazito, yaani atawalazimisheni kama mlivyojilazimisha nafsi zenu, basi hamtaweza kufanya mambo hayo, mtachoka, mtaacha kufanya mambo hayo na mtaadhibiwa, na maana hii ndio inafaa maelezo yake Mtume S.A.W., aliposema: (watu) yaani: miongoni mwa wana wa Israeli. (walijitia mazito juu ya nafsi zenu): kwa matendo ya ibada yaliyo magumu na juhudi kamili. (basi Mwenyezi Mungu atawatia mazito juu yao) kwa kuwalazimisha kufanya mambo hayo barabara kama yalivyo, na imesemekana: walijitia mazito juu ya nafsi zenu wakati ambapo wameamuriwa kumwua ng'ombe wakauliza kuhusu rangi yake, umri wake na sifa zake nyingine, basi Mwenyezi Mungu amewatia mazito juu yao kwa kuwaamuru kumchinja ng'ombe ambaye ana sifa maalum ambazo hazipo isipokuwa katika ng'ombe moja tu, na mwenye ng’ombe huyu hakumwuza isipokuwa kwa kujaza ngozi yake dhahabu.”
Kuchukua tahadhari maana yake katika lugha ni kuwa mwangalifu na kuyachukua mambo yanayoaminika, na imekuja katika kamusi ya [Lisan Al-Arab kwa Ibn Mandhur (kidahizo: tahadhari, 7/279, Dar Sader.] kwamba kuchukua tahadhari ina maana ya kuwa mwangalifu.
Katika [Al-Misbaah Al-Muniir” kwa Al-Fiyumi (kidahizo: tahadhari, 1/156, Al-Maktaba Al-Elmiyah.]: “Kuchukua tahadhari maana yake ni kuomba kuwa mwangalifu.
Ama kuhusu istilahi, kuchukua tahadari maana yake ni kuepuka mambo ambayo yanafanana na yaliyokatazwa.
Al-Jerjani alisema katika kitabu cha [Al-Tarifaat, uk 12, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: kuchukua tahadari katika lugha maana yake ni kuwa mwangalifu, na katika istilahi maana yake ni kujitahadhari kufanya madhambi”.
Imamu Al-Qaraafi aliueleza ucha Mungu kwa maana ambayo inafanana na kuchukua tahadhari, aliposema katika kitabu cha [Al-Furuq, 4/210, Dar Aalam Al-Kutub]: “Na ucha Mungu ni miongoni mwa matendo ya viungo vya mwili, na ni kuacha mambo yasiyo na aibu; kwa ajili ya kuchukua tahadhari na mambo yaliyo na aibu… na jambo hili linapendezwa na kwa kufanya hivi tunaweza kuepuka tofauti kati ya mitazamo ya wanaviyuoni kwa kadiri tunavyoweza”.
Lakini Imamu Al-Izz Ibn Abd Al-Salam hufanya maana ya tahadhari ni kubwa zaidi kuliko ucha Mungu, ambapo aliposema katika kitabu cha [Qawaid Al-Ahkaam, 2 / 18-19, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.]: “Kuchukua tahadhari ni aina mbili: moja: inayopendezwa, na inaelezwa kwa ucha Mungu, kama kunawa mikono mara tatu akiamka kabla ya kuiingiza katika chombo.. aina ya mbili: inayolazimishwa miongoni mwa tahadhari kwa sababu ni kama njia ya kupata mambo ya haramu”.
Matini za Quraani na Sunna zimeonyesha uhalali wa kuchukua tahadhari na kuamuru kwake, miongoni mwa matini hizi ni kauli ya Mwenyezi Mungu, {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi.} [AL HUJURAAT 12], Mwenyezi Mungu ameamuru kuepuka mengi ya dhana tu, na hakuweka mipaka kwa wingi huu, lakini hakuonyesha ili kumwonya mwislamu na kumsisitiza achukue tahadhari na asifanye dhambi kwa kuacha mambo ambayo pengine ni madhambi na kama akiwa hakuthibitika kwamba ni madhambi.
Imamu Ibn Al-Sobki alisema katika kitabu cha [Al-Ashbaah wa Al-Nadhair, 1/110, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.]: “mara moja nimechukua msingi huu kama ni dalili yaani: kuchukua tahadhari, Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi.}, Mwenyezi Mungu ameamuru kuepuka baadhi yasiyo madhambi kwa hofu ya kufanya yaliyo madhambi, na hivyo ni kuchukua tahadhari, nayo ni ufahamu mzuri.”
Katika tafsiri ya Imamu Al-Razi [Mafatihu Al-Ghaiyb, 28/110, Dar Ihiyaa Al-Turath Al-Arabi.]: kauli ya Mwenyezi Mungu: {baadhi ya dhana ni dhambi.}aya hii ni ishara kwa kuchukua tahadhari.”
Sheikh Al-Fadani katika kitabu cha [Al-Fawaid Al-jania, 2/171, Dar Al-Bashair Al-islamiyah-Beirut.] akasema: “Kauli yake: {Dhani nyingi} haionyeshi vizuri kwamba inapaswa kuchukua tahadhari na kuangalia mambo yote yaliyokatazwa.”
Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa al-Nu'man Ibn Bashir, R.A. ameashiria vidole kwa masikio yake akisema nikasikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.. anasema: “Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui. Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu). Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allaah ni makatazo Yake. Na hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote kitakua kizima, kikiharibika kiwiliwili chote huharibika. Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.” Kauli ya Mtume S.A.W.: “yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu” ni ishara ya kuchukua tahadhari; kwa sababu ya anayefanya mambo yenye shaka mara nyingi huanguka katika haramu hata kama ikiwa hakukusudia, au atazoe kutojali, akathubutu kufanya mambo yenye shaka kisha atathubutu kufanya mambo makubwa zaidi yenye shaka halafu mengine nk. mpaka kuanguka katika haramu kwa makusudi, na mambo yenye shaka siyo miongoni mwa halali ambayo iko wazi, ingawa hivyo inapaswa kuchukua tahadhari na mambo hayo kwa ajili ya kutoanguka katika haramu; kwa mujibu wa kauli yake Mtume S.A.W.: “yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake.”
Kuepuka vitu vyenye shaka ni jambo zuri katika dini, kwa sababu yule ambaye amefanya hivyo atakuwa hana hatia na atahifadhi heshima yake kutoka maneno ya watu kuhusu yeye. [Rejea: Sharhu Al-Nawawi ala Sahihi Muslim 11/28, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi.]. Na kuchukua tahadhari na kujisafisha nafsi kwenye dini ni jambo ambalo linatakiwa katika sheria wakati wote. [Rejea: Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Ibn Al-Sobki, 1/112].
Imepokelewa kwa Al-Tirmidhi, Ibn Majah na Al-Hakim katika Al-Mustadrak na imerekebishwa na Atiya Al-Saadi alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.. alisema: “”mja hafikii kuwa miongoni mwa wacha Mungu mpaka aepuke vitu ambavyo visivyo na aibu kwa ajili ya kuchukua tahadhari na vitu ambayo venye aibu. Mtu ambaye anataka kuwa miongoni mwa watu ambao wacha Mungu; anapaswa achukue tahadhari vizuri sana ili asianguke katika dhambi, hata kama hiyo ina maana ya kwamba kuacha baadhi yanayoruhusiwa kwa hofu ya kutolewa kwa makatazo, hadithi hii ina dalili ya kwamba kuchukua tahadhari ni jambo zuri linalipwa thawabu na linakusudiwa na Mwenyezi Mungu.
Mtume S.A.W. amechukua tahadhari na amehukumu kwake katika matukio maarufu, kama vile kwamba iliyopokelewa na masheikh wawili kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A., alisema: Mtume S.A.W., amepita kwanye tende iliyoanguka akasema: “Lau kuwa si miongoni mwa Sadaka bila ya shaka ningeila.”
Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah R.A., kwamba Mtume wa Allah S.A.W, alisema: “Mimi nikigeuka juu familia yangu, nikakuta tende imeanguka katika kitanda changu nikainyanyua kwa ajili ya kuila kisha nikaogopa kuwa sadaka nitaitupa.”
na Al-Bukhari katika Sahih kutoka kwa Al-Harith Ibn Oqba kwamba yeye ameoa binti wa Abu Ihab Ibn Aziz, mwanamke amekuja kwake akasema: Mimi nimemnyonyesha Oqba na ambaye alimuoa, Oqba akasema: sijui kwamba wewe umeninyonyesha wala hukuniambia. akapanda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., katika mji akamwuliza, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. Akasema: “Vipi na imesemekana hivyo” Oqba akamtaliki, na akaolewa na mume mwengine.
Al-Hafidh Ibn Hajar amesema katika [Fathu Al-Bari, 4/293, Dar Al-Maarifa- Beirut.]: “dalili katika kauli yake: “Vipi na imesemekana hivyo.” Ni kwamba yeye anaona kuwa amri yake kumtaliki mke wake, ilikuwa kwa ajili ya mwanamke aliyesema kwamba amewanyonyesha, basi inawezekana anasema kweli basi atafanya haramu, Mtume alimwamuru kumtaliki kwa kuchukua tahadhari kwa mujibu wa kauli ya watu wengi.”
Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah R.A. kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake, asiingize mkono wake ndani ya chombo (chenye maji) mpaka auoshe mara tatu, kwa sababu hajui wapi umelala mkono wake.”
Imamu Al-Nawawi amesema katika [Sharhu Sahihi Muslim, 3/179, Dar Ihiyaa Al-Turath Al-Arabi.]: “Hadithi hii ina dalili ya masuala mengi katika mtazamo wetu na mtazamo wa wengi .. miongoni mwao ni kwamba: kuchukua tahadhari katika mambo ya ibada na mengine ni jambo ambalo linapendezwa kama ikiwa haliendi mbali na mpaka wa tahadhari kwa mpaka wa wasiwasi.”
Imamu Al-Jassas Al- Hanafi anasema katika kitabu cha [Al-Fusuul fi Al-Usuul, 2/110, Wizarat Al-Awqaf Al-Kuwaitiyah.]: “Na kuzingatia kuchukua tahadhari ni msingi mkuu miongoni mwa misingi ya fiqhi, ambao wanavyuoni wote wameutumia.”
Sheikh Ibn Taymiyyah katika [Majmuu Al-Fatawa, 20/262, Mujamaa Al-Malik Fahd Al-Madina Al-Nabawiyah.]: “Wanavyuoni wote walikuwa na mtazamo wenye uzito kuhusu dalili amabayo yenye tahadhari zaidi kuliko dalili inayoruhusisha, wanafiqhi wengi wametafuta dalili ya kuchukua tahadhari katika hukumu nyingi kwa mujibu wa hivyo, ama kuhusu kuchukua tahadhari katika kufanya kitu ni jambo ambalo ni zuri kwa mujibu wa watu wenye busara kwa jumla.”
Kuchukua tahadhari ni jambo ambalo linatakiwa kama mtu aliyesahau sala moja miongoni mwa sala tano za wajib na hajui kwamba amesahau sala ipi analazimishwa kusali sala tano zote; ili achukue tahadhari kwa kufikia sala nne kwa ajili ya kupata sala iliyolazimishwa.
Al-Shalabi alisema katika ufafanuzi wake juu ya [Tabiin Al-Haqaaiq, 1/190, Dar Al-Kitabu Al-Islami]: “Kama akikosa sala katika mchana na usiku na hajui sala ipi hii: anapaswa kusali sala tano kwa ajili ya kuchukua tahadhari.”
Imamu Al-Shirazi alisema katika [Al-Muhadhab, katika Fiqhi ya ya Imamu Al-Shafi'I, 1/106, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.]: “Kama akisahau sala moja na hakujua ni sala ipi, inapaswa asali sala tano zote.” Na hivyo kwa sababu ya wajibu kujisafisha nafsi yake kwa yakini, kila sala miongoni mwa sala tano inawezekana kuwa ndio imesahauliwa, basi hali ya shaka ilikuwa tano, kwa hivyo ni wajibu asali sala tano; ili kutimiza hali zote za shaka, na kuthibitisha kuhusu kujisafisha nafsi yake kutoka faradhi. Kama vile mtu ambaye hajui wapi sehemu ya uchafu katika nguo alitakiwa kusafisha nguo yake nzima.
Imamu Al-Shafei RA, alisema katika kitabu cha [Al-Um, 8/111, Dar Al-maarifa]: “Kama akiwa hajui wapi sehemu ya najisi katika nguo, inapasa kufua ngua nzima na hakuna la kufanya isipokuwa hivyo”. Kujua kwa usafi kunategemea kuchukua tahadhari kwa kuifua nguo nzima, ama kuhusu kufua sehemu nyingi za nguo haizigatiwi usafi; kwa sababu najisi yake haina shaka na kuiondoa ina shaka kwa sababu sehemu ya najisi siyo wazi kabisa, na yakini haiondolewa kwa shaka, basi kama hakuna kwake isipokuwa nguo hii, ni lazima achukue tahadhari kwa kuifua nzima. Na pia kama mtu yeyote akiwa na wasiwasi kuhusu dada yake kwa njia ya kunyonyesha kutoka mwanamke mmoja ni lazima achukue tahadhari na kumtaliki kwa ajili ya kuacha uharamu wa ndoa ya dada.
Inawezekana jambo la kuchukua tahadhari ni linapendezwa kama katika hali ya kuepuka tofauti ya wanavyuoini, Imam Al-Nawawi anasema katika kitabu chake [Rawdhatu Al-Talibiin, 10/219, Al-Maktab Al-Islami-Beirut.]: “Wanavyuoni wanakataa mambo yanayokatazwa nao wote, lakini mambo ambayo hawakukubaliana nayo hayakatazwi; kwa sababu kila mmoja wao anafanya jitihada, anaweza kushinda katika jitihada yake au kushindwa, na aliyeshindwa hana dhambi lolote. Lakini kama akipendekeza kuepuka tofauti hiyo, basi ushauri huu utakuwa mzuri zaidi, lakini kwa upole; kwa sababu wanavyuoni wamekubaliana kwamba kuepuka na tofauti ni jambo ambalo linapendezwa kama hakuna uvunjaji wa Sunna yoyote ambayo ni thabiti au kuanguka katika tofauti nyingine.”
Kutokana na msingi huo yapo masuala mengi yaliyotajwa katika vitabu vya fiqhi kwa mujibu wa kila madhehebu, basi inapendezwa kutia udhu kwa mtu ambye amemgusa mwanamke, kwa mujibu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa kwa ajili ya kuepuka tofauti ya wanavyuoni wengine wanaosema katika hali hii kutia udhu ni la lazima. [Rejea: Hashiyat Ibn Abidin, 1/90, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kwa mujibu wa Imam Malik inapendezwa kusoma Bismillahi mwanzoni mwa Al-Fatiha katika sala kama akikusudia kuepuka tofauti ya wanaosema ni la lazima kuisoma. [Rejea: Hashiat Al-Dusuqi ala Al-Sharhi Al-Kabiir 1/ 251-252, Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabia]
Na kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Al-Shaafi'i inapendezwa kufuta kichwa kizima katika udhu kwa ajili ya kuepuka tofauti ya waliosema kuwa ni la lazima kukifutwa. [Rejea: Mughni Al-Muhtaj kwa Al-Khatib Al-Sherbini 1/189, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.].
Na kwa mujibu wa Imam Ahmad Ibn Hanbal inapendezwa kwa ambaye hawezi kusoma Al-Fatiha vizuri kusali nyuma ya mtu mwengine anayeweza kuisoma vizuri ili kusoma kwa imam kuwe kusoma kwa mtu yule, kwa ajili ya kuepuka tofauti ya wanavyuoni wengine. [Rejea: Kashaf Al-Qinaa kwa Al-Bahoti 1/342, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.].
Pia jambo la kuchukua tahadhari linawezekana ni baya kama mtu yeyote akipita kiasi na akifanya uzushi ambao siyo miongoni mwa dini; basi jambo hili ni la haramu kwa kufuatana na maovu na madhara yanayotukana nalo, na mfano wake kwa mujibu wa Imam Muhamad Al-Juweni, ni kwamba kama mtu yeyote akiwa na wasiwasi kuhusu idadi ya kunawa katika udhu ni mara mbili au tatu, basi inachukizwa achukue tahadhari katika hali hii, ili asinawe mara nne amabyo ni uzushi, yeye ana wasiwasi kati ya kunawa mara nne ambayo ni uzushi na mara tatu amabyo ni sunna, na kuacha sunna ni nzuri zaidi kuliko kuanguka katika uzushi, hali hiyo ni kinyume cha hali ya mtu anayesali na ana wasiwasi katika idadi ya rakaa za sala, ni la lazima achukue idadi ya uchache ili asiwe na wasiwasi katika faradhi. [Rejea: Majmuu Sharhu Al-Muhadhab kwa Imam Al-Nawawiya 1/440, Dar Al-Fikr].
Kwa sababu ya kuchukua tahadhari kwa njia ya kupita kiasi labda mwislamu afike mpaka upeo wa wasiwasi na kubatili kwa ibada yake, katika hali hii ni bora zaidi aache kuchukua tahadhari, kwa mfano, mtu ambaye amepiga takbira ya ihram katika sala ya Adhuhuri halafu amekata sala kwa sababu ya wasiwasi, kisha alipiga takbira, halafu ameikata, kwa kudai kwamba anachukua tahadhari katika kupiga takbira ya ihram vizuri sana kwa utulivu. Basi ameanguka katika jambo la haramu kwa sababu ya kuchukua tahadhari kwa njia ya kupita kiasi, na jambo hili ni kuikata sala pasipo na udhuru, na kuikata sala pasipo na kuhakikisha kwamba imeharibika hali hii ni kinyume cha aya iliyotajwa katika Quraani tukufu isemayo: {wala msiviharibu vitendo vyenu} [MUHAMMAD: 33], na katika hadithi iliyopokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Abaad Ibn Tamim, kutoka kwa mjomba wake alisema, alilalamika kwa Mtume S.A.W., Mtu anayekuwa na wasiwasi katika sala yake, anaweza kuikata sala hii? Alisema: “Hapana mpaka kusikia sauti au kunusa harufu”. Katika hadithi hii ni haramu kwa mtu kuikata sala yake isipokuwa akihakikisha kwamba udhu wake umeharibika kutokana na mambo yanayoharibu udhu.
Imamu Al-Zarkashi anasema katika kitabu cha [Al-Manthuur, 3/38, Wizarat Al-Awqaf Al-Kuwaitiya.]: “Faradhi ain (inayomlazimu kila mtu binafsi) ni jambo la alzima kwa kila mwislamu isipokuwepo udhuru.”
Na Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Ansari anasema katika [Asna Al-Mataalib, 1/430, Hashiyat Al-Ramliy Al-Kabiir, Dar Al-kitabu Al-Islami.]: “(Na hairuhusiwi kukata kufunga saumu ambayo imelazimishwa moja kwa moja) kuifunga (au pole pole) kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: {wala msiviharibu vitendo vyenu} na kwa sababu imefanana na wajibu wala hakuna udhuru kama akiendelea katika sala mwanzoni mwa wakati wake.”
Kutokana na yaliyotangulia ni wazi kwamba dhana ya kuchukua tahadhari ni kubwa zaidi kuliko dhana ya kutia mazito katika dini, kwa sababu jambo la kuchukua tahadhari katika baadhi ya wakati ni zuri na wakati mwengine ni baya, na miongoni mwa tahadhari ambayo ni nzuri ni kuchukua mitazamo ya wanavyuoni ambayo ni mbali na uwezekano kuanguka katika makosa, na miongoni mwake pia ni kuepuka na tofauti kwa kadiri iwezekanavyo, jambo hili linapendezwa kwa makubaliano ya wanavyuoni wote kama hakuna uvunjaji wa makusudi wa sheria, na hali ya kuchukua tahadhari ni msingi ambao ni mzuri katika dini, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., ameufanya msingi huu na ameuhukumia katika matukio mengi, na kwa hivyo wanavyuoni wote wameuchukua msingi huu, hali hiyo ni kinyume cha kutia mazito katika dini, hali ambayo ni aina ya kuchukua tahadhari kwa njia iliyo mbaya na hukumu yake ni kati ya uharamu na ukaraha. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas