Kuitusi Dini

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuitusi Dini

Question

Mtu fulani aliitusi dini wakati wa ugomvi mmoja, na alikuwa na hasira nyingi sana, basi je kwa kufanya hivyo, mtu huyo anazingatiwa kuwa ni kafiri?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika kwamba Kuitusi dini ni moja kati ya madhambi makubwa, kwani hupelekea kumpuuzia Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mitume wake na aya zake, na kunakwenda kinyume na utukuzaji ambao ndio imani yenyewe. Na mwislamu hazingatiwi kuwakatoka Uislamu, na hahukumiwi kuwa ametoka katika dini isipokuwa kifua chake kitakapoupokea ukafiri na moyo wake ukatulizana kwa ukafiri huo, na akawa tayari ameishauingia ukafiri huo, kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa -basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabukubwa.} [AN NAHL 106]
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.: "Hakika vitendo hutokana na nia, na kwamba kila mtu hupata alichokinuia" [Wanaafikiana nayo].
Na kwani yaliyo moyoni na ghaibuni miongoni mwa mambo ya ghaibu ambayo hayajua isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ni lazima pawepo dalili ya wazi ya ukafiri wake, dalili ambayo haitegemei ufafanuzi, hadi linasabishwe na baadhi ya wanachuoni tamko lao: "Ikiwa ukafirishaji una aina tisini na tisa na kutokufurisha kuna aina moja, basi zitolewe na wala pasitolewe fatwa ya ukafiri unaolazimu kifo na kuondosha kinga na kutorithi na nyinginezo miongoni mwa hukumu nzito." [Fath Al Aliy Al Malik kwa Sheikh Eliesh, 358/2, Ch. Dar Al Maarifah].
Na kuna tofauti baina ya ukafiri na kafiri, kwani labda tamko linakuwa na ukafiri lakini anayelisema si kafiri kwa kuwepo kizuizi, kama vile ulimi wake kuponyoka, au akawa amepoteza uwezo, au akpoteza akili kwa sababu ya ulevi au uwendawazimu, au usingizi, au ghadhabu kali au kama hayo.
Hasira nyingindizo zinazomkosesha mtu hali ya utulivu na upambanuzi, na hivyo kuepushwahukumu dhidi yake.
Na kuitusi dini tu kunaitengua imani na kunapelekea ukafiri, pindipo mwislamu mwenye akili na aliyebaleghe na huru anapoitamkia, akiamini jambo hilo naye ana uwezo kamili.
Kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipigaporojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyiamaskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake?. Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuaminikwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibukundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu.} [AT TAWBAH 65-66].
Iwapo utani hupelekea ukafiri, basi kumtusi Mwenyezi Mungu, Mtume au Dini ni hatari zaidi.
Na utani katika dini ni kama anavyosema Imamu Ar Raaziy katika kitabu chake cha tafsiri: [95/16, Ch. Dar Ihyaa Al Turaath Al Arabiy]: "Unazingatiwa miongoni mwa ukafiri na hao ni kwa kuwa utani katika Dini unamaanisha udogeshaji, na nguzo kuu katika imani ni kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kiasi kikubwa kiwezekanacho, na kukusanyika kwa mambo haya mawili ni muhali.
Na Ibn Qudamah anasema katika kitabu chake: [Al Mughniy 28/9, Ch. Maktabat Al Qahira] "Na atakaemtusi Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa amekufuru, iwe anafanya utani au anafanya kweli. Na atakaemfanyia utani Mwenyezi Mungu Mtukufu au akazifanyia utani aya za Quraani au Mitume wake au vitabu vyake".
Na Ibn Al Qayim anasema: "Na moyo wa ibada ni utukuzaji na upendo, na iwapo kimoja kati ya viwili hivi kitatelekezwa, basi ibada hiyo itaharibika, na iwapo sifa hizi mbili zitakutanishwa kwa mpenzi mtukufu basi huo utakuwa ni ukweli wa kusifia kwa sifa njema". [Madarej Al Salkeen 464/2, Ch. Dar Al Kitaab Al Arabiy]
Na baadhi ya wanachuoni wa kisasa walitaja baadhi ya mifano inayoashiria ukafiri, na wanaizingatia kuwa miongoni mwake kuitusi dini na hiyo ni kama ifuatavyo:
1- Ukanushaji wayale yaliyojulikana katika Dini kwa ulazima wake/dharua, kama kukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na uumbaji wake wa ulimwengu, na ukanushaji wa kuwepo Malaika, na ukanushaji wa unabii wa Muhammad S.A.W., na kwamba Quraani ni wahiy kutoka Mwenyezi Mungu, na ukanushaji wa kufufuliwa na thawabu, na ukanushaji wa ufaradhi wa Sala, Zaka, Saumu na Hija.
2- Kuhalalisha kilicho haramishwa ambacho waislamu wamekubaliana juu ya uharamu wake,kama vile kuhalilisha Mvinyo, Uzinifu, na Riba, na kula nyama ya nguruwe, na kuhalalisha mauaji ya wale wanaolindwa na sheria pamoja na mali zao.
3- Kuharamisha kile walichokubaliana waislamu wote juu ya uhalali wake, kama vile kuharamisha vyakula halali.
4- Kumtusi Nabii au kumpuuzia, na kadhalika kumtusi Nabii yeyote miongoni mwa manabii wa Mwenyezi Mungu.
5- Kuitusi dini,na kukosoa Quraani na Hadithi, na kuacha kutoa maamuzi kwa kuvitumia viwili hivi, na kutanguliza sheria za kutungwa juu ya vitabu hivi.
6- Mtu yeyote kudai kuwa wahyi unamteremkia.
7- Kuutupa Msahafu kwenye uchafu, na vile vile vitabu vya Hadithi, kuvidharau na kuyapuuza yaliyomo ndani yake.
8- Kulidharau jina moja miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu, au amri miongoni mwa amri zake, au katazo kati ya makatazo yake, au ahadi kati ya ahadi zake, isipokuwa awe mtu mgeni katika uislamu, na hajui hukumu zake, na hana maarifa ya mipaka yake, basi akikanusha kwa ujinga wake, basi huyo hatakuwa ni mwenye kukufuru.
Na kuna mambo ambayo waislamu wamekubaliana juu yake, lakini hawayajui mambo hayo isipokuwa watu maalumu.Kwa hakika mwenye kuyakanusha hatakufuru, bali anakuwa ni mwenye kuudhurika kwa ujinga wake, na kwa kutoenea elimu ya mambo hayo kwa watu wote, kama vile kuharamisha ndoa ya pamoja na shangazi yake.Na auaye kwa makusudi harithi, na kwa nyanya sudusi ya urithi na kadhalika. [Fiqh Al Sunna kwa As Sayed Sabiq 454/2, Ch. Dar Al Kitaab Al Arabiy].
Al Sheikh Elyesh anasema: "Na katika Al Barazliy: Na niliyonayo katika jambo hili ni kuwa haya hayatahesabika kwa aliyetukana, au aliyedai au kudharau isipokuwa kwa masharti mawili: la kwanza ni kuchukulia tamko kwa kinachomaanishwa na kueleweka hivyo. Na la pili ni kuwa kusudio la kulitumia neno husika, na iwapo maana hizi mbili zitakosekana au mojawapo, basi niliyonayokatika jambo hilo ni kwamba atatiwa adabu kali yenye kutia uchungu na afungwe kwa muda mrefu. Na katika hili pia kuna suala ambalo nalo ni kuwa mtu alikuwa anaidharau (anaibeza) swala na pengine pia anawadharau wanaoswali, na watu wengi wakamuona miongoni mwao yuko aliyezidisha na yuko asiyezidisha, na iwapo atakutwa akiwafanyia dharau wanaoswali kutokana na uchache wa imani yake kwao basi hii itakuwa ni kuwatusi waislamu na italazimika aadabishwe kwa kiasi akionacho kiongozi, na atakayemchukulia kuwa ameidharau ibada yenyewe basi kwa uhakika jambo hili ni kuritadi, kwa kuonesha kwake wazi jambo hili kama lilivyo suala hili lililotajwa na wala si uzindiki na atapitishiwa hukumu za mwenye kuritadi.
Nimesema: Ilichukuliwa kutoka katika hukumu hiyo kwa aliyeitusi dini, mila, au madhehebu, na hayo yote yanatokea mengi na baadhi ya wenyeji wajinga kama vile; wenye punda, wenye ngamia na watumishi, na pengine yalitokea kwa watu wengine, na hayo kwamba iwapo atakusudia sheria iliyotwaharika na hukumu alizoziweka Mwenyezi Mungu kwa waja wake kupitia ulimi wa Mtume wake S.A.W, basi mtu huyo ni kafiri bila pingamizi, kisha iwapo atadhihirisha hivyo basi yeye ni mwenye kuritadi na atatubishwa, akitubu S.A.W., na kama hakutubu basi atauawa, na kama hajadhihirisha basi yeye ni mzindiki na atauawa hata kama akitubu, na ikiwa atakusudia hali ya mtu na ufuasi wake wa dini basi huko ni kumtukana mwislamu na hapa kuna kutiwa adabu kwa muhibu wa aonavyo kiongozi, na atofautishe baina ya hali mbili kwa mtu kukubali au kwa kuwapo vielelezo.
Na baadhi yaowanafanya kusudio la pili kama la kwanza katika hukumu, basi katika kitabu cha [Al Badr] kutoka kwa Behraam katika utatafiti wa kuritadi: kwamba aliyeacha Sala kama alisema kwa alimwambia: Fanya Sala! Ukiingia Peponi basi funga mlango nyuma yako! Na ikiwa atakusudia kusema kuwa swala haina athari yoyote katika dini atakuwa ameritadi kwa makubaliano ya wanazuoni, na iwapo atakusudia kuwa swala ya aliyesema haina athari kwa kuwa kwake haikumzuia na machafu na yanayokatazwa, basi katika kuritadi kwake kuna kauli mbili. [Fateh Al Aliy Al Malik 346-347/2]
Na kutokana na yaliyotangulia inajulikana kwamba iwapo hasira inatawala mpaka mwenye nayo akawa hajui anachokisema, basi hatakufurishwa kwa jambo hili, isipokuwa atakuwa ni mtendaji wa dhambi kubwa, na atatakiwa auzoeshe ulimi wake maneno mazuri, na aitawale hasira yake kama tulivyofundishwa na Uislamu, na aharakishe kutubia madhambi yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na akiwa anajua na anafahamu anachokisema kwa makusudi kwa kutamka matusi haya ya kuidharau dini na anakusudia dharau hiyo hakika mtu huyu anakufuru kwa ukafiri unaomtoa katika dini na atatubishwa na kuamrishwa atamke shahada mbili tena, na kutokirejea kitendo chake hicho.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas