Mke Humbusu Mume Wake Aliyekufa

Egypt's Dar Al-Ifta

Mke Humbusu Mume Wake Aliyekufa

Question

Je, Inajuzu kwa mwanamke kumgusa mume wake au kumbusu ili amwage anapofariki dunia?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Inajuzu kumbusu maiti kwa yule ambaye anaruhusiwa kufanya hivyo katika hali ya uhai wa aliyekufa. Hayo kwa yaliyopokelewa na At Tarmaziy na alisema (Hadithi hukumu yake) ni sahihi na nzuri: kutoka kwa Aisha R.A. Kutoka kwa Mtume S.A.W. Kwamba Mtume S.A.W Alimbusu Othmaan Bin Mazu'un alipofariki dunia na yeye alikuwa akilia.

Na Al Bukhariy amepokea kuwa Aba Bakrin Al Swadeeq R.A. Aliingia aliko kuwa Mtume S.A.W. Akiwa amefunikwa kwa kanzu basi akaufunua uso wake.

Kisha akainamia juu yake na kumbusu na kisha akalia na kusema: Naapa kwa Mola wa baba yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mola hakukujumuishii mauti mara mbili. Ama mauti aliyokuandikia umekwishaionja.

Na hukumu hiyo vile vile inawakusanya wote wawili; mke na mume, kama mmoja wao angelikuwa amefariki na kama hakusababisha kile kinachowajibisha kizuizi cha ndoa kabla ya kufa kwake kama vile talaka na mfano wake au baada yake kama vile kubadili dini, muda wa kuwa kwake ni mwenye huruma na siyo matamanio kwani maiti haitamaniwi. Na Ibn Majah alipokea kutoka kwa Aisha R.A. Akasema kwamba: Mtume S.A.W. Alirejea Bakiu basi akanikuta ninaumwa kichwa huku nikisema: "Kichwa changu kinauma". Akasema: "Bali na mimi ewe Aisha kichwa changu kinaniuma." Kisha akasema: "Je, waonaje na nini kitakachokudhuru wewe lau ungelikufa kabla yangu, na mimi nikakusimamia, na nikakuosha, na nikakuvika sanda na nikakuswalia na kisha nikakuzika"

Abu Dawud alipokea kutoka kwa Aisha R.A. Alisema: "Lau ningelikutana na jambo nisingekengeuka. Hakuoshwa Mtume S.A.W. Isipokuwa na wakeze."

Na imepokewa na Al Baihaqiy kwamba Abuu bakri (R.A) Ameusia kuwa aoshwe na mkewe Asmaa binti Umais (R.A). Basi akamwosha, na hapakuwa na tofauti yeyote miongoni mwa masahaba.

Na Malik R.A. Alipokea akatia katika kitabu chake [Al Muwata'] kutoka kwa Abdullahi Bin Abi Bakr kwamba Asmaa Bint Umais mke wa Abi Bakr R.A.Ziwe kwa wote wawili alimwosha Abi Bakr Al Swadek alipokufa.

Na ikiwa itajuzu kwa mume au mke kumuosha mwenzake na kumvika sanda pamoja na yale yanayolazimika kufanya moja kwa moja na kumwangalia maiti, hii inakuwa ni ishara ya kuidhinishwa kujuzu kumgusa maiti huyo popote katika mwili wake ikiwemo kumbusu: iwapo tu hali hiyo itaendelea kuwa kwa mujibu wa tulivyozungumza, kama vile kwa huruma n.k.

Al Imamu An Nawawiy alisema katika kitabu cha [Al Muhazab 111/5, Ch. Al Muniriyah]: "(Tawi): Inajuzu kwa watu wa karibu wa maiti kumbusu usoni mwake, hadithi zimethibitisha hivyo, na Darimiy ameweka wazi katika kitabu chake cha [Al-Istidhkaar], na Sarkhasiy ametaja katika kitabu chake cha [Al-Amaaliy].

Na imetajwa katika kitabu cha [Al Menhaaj na uelezo wake "Tuhfat Al Muhtaaj" kwa mwanazuoni mkuu Ibn Hajar Al Haitamiy 183/2, Ch. Dar Ihiyaa Al Turaath Al Arabiy]: "Inajuzu kwa watu wa maiti na mfano wake kama vile wenzake kumbusu uso wake"

Na Mwanazuoni mkuu Al Sharwaniy alisema : "Na wala hakuna ubaya wowote kumbusu maiti sehemu yoyote iwayo kama ambavyo inaonesha kuwa kwake wazi jambo hilo bila ya mpaka kwa jinsi inavyoeleweka kuwa maneno yawe kwa namna ambayo hakuna matamanio yeyote na kwamba kufanya hivyo ni kwa ajili ya kupata baraka au kwa ajili ya upole na huruma juu ya maiti"

Na imekuja katika kitabu cha [Kashaafu Al Qinaa' kwa Mwanazuoni mkubwa Al Bahutiy 85/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Si vibaya kumbusu na kumwangalia maiti kwa yule ambaye kwake ni ruhusa kufanya hivyo katika uhai wake na baada ya kumvalisha sanda"

Na juu ya hali hiyo, hakuna ubaya wowote kwa mume kumgusa mke wake aliyefariki dunia au hata kumbusu uso ni mwake kwa upole na unyenyekevu kwa lengo la kumuaga dunia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas