Kusilimu Mke na Kubakia Mume wake k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusilimu Mke na Kubakia Mume wake katika Dini yake

Question

Kusilimu Mke na Kubakia Mume wake katika Dini yake

Answer

Utangulizi:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Na miongoni mwa masuala muhimu na yenye kutatanisha ambayo yanaulizwa sana katika zama zetu, na ambayo maoni ya Wanachuoni wa zamani na wa sasa wametofautiana juu ya kusilimu mke bila ya mumewe, na kusilimu mke bila ya mume wake hata kama inamhakikishia maslahi katika dini yake, lakini hii inaweza kupingana na maisha yake ya kibinafsi, na inaweza kumuweka katika matatizo hasa katika maisha yake ya utulivu pamoja na mume wake.

Mambo hayo yote na mengine yalilazimu utafiti mpya wa suala ambalo linachunguza maoni, Madhehebu na dalili nyepesi, na kuangalia mtazamo unazingatia uhalisi na kuchagua yale yanayohakikisha maslahi kutokana na maneno ya Wanavyuoni wenye kujitahidi wa umma, na wakati huo huo anazingatia kutotoka kwenye mwavuli wa Sharia au mambo thabiti ambayo yanaelezea umbulisho wa Waislamu.

Na uchaguzi wetu kwa anwani hiyo ni kuandika kutokana na umuhimu wake mkubwa kama ilivyopita, na kwa sababu ya haja ya watu kujua hukumu ya kisheria katika suala hilo, na ambalo linajengeka juu yake mambo yanayoathiri katika kuendelea maisha ya kinyumba baina ya mke na mume wake, na kadhalika kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na suala la kuwahamasisha wasio Waislamu kuingia katika Uislamu.

Na tumegawanya utafiti huu katika Utangulizi; pamoja na umuhimu wa mada hii na sababu ya kuchagua utafiti na mfumo wa kuandika, kisha dibaji; katika dibaji hiyo, tulieleza asili ya mjadala na kueleza rai iliyochaguliwa, halafu sura tatu: sura ya kwanza katika madhehebu iliyochaguliwa na dalili zake.

Na sura ya pili katika madhehebu ya wenye kutofautiana na dalili zao na mjadala wao, kisha kuchagua rai sahihi. Na sura ya tatu inahusu kuharamisha tendo la ndoa baada tu ya kusilimu. Na mwisho ni hitimisho ambalo linajumuisha matokeo muhimu zaidi, kisha orodha ya marejeo muhimu zaidi. Na tumetegemea katika utafiti wetu huo katika kunukulu Madhehebu, maoni na nasaba zao kwa watu waq juu ya vitabu sahihi vinavyotegemewa na pia tafiti za kisasa kuhusu suala lenyewe.

Tukifuata mfumo wa kielimu katika kutaja dalili na sura zake, na kuzijadilia, Pamoja na kurejea katika Aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi tukufu za Mtume Mohamad S.A.W. kuzithibitisha kielimu na kutegemea usahihi na udhaifu juu ya hukumu za wahifadhi wake wa zamani. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu mwingi wa ukarimu, Atuongoze kwenye yaliyo sawa na Abariki utafiti huu na kuunufaisha, hakika Yeye ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema. Na kwake Mwenyezi Mungu tunaelekea.

Dibaji:

Mwenyezi Mungu Mtukufu amehalalisha ndoa kama mapenzi na huruma baina ya mwanamume na mwanamke, na hayo ni miongoni mwa neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wanadamu wote, hakuna tofauti baina ya Waislamu na wasio Waislamu, Na Uislamu umeweka misingi ya ndoa na vidhibiti vyake ambavyo vinatimizwa navyo baina ya Waislamu, na ulikubali ndoa za wasio Waislamu. Lakini akisilimu mmoja miongoni mwa mke au mume, au walisilimu wote wawili pamoja basi hapa zinaanza sura kadhaa tofauti za hukumu zake na zinatofautiana kutokana na tofauti za sura hizo.

Sura ya Kwanza: Kama mke na mume walisilimu pamoja, na mke hakuwa miongoni mwa maharimu wa mume -kama mwanamke aliyeharimishwa kwa nasaba au kunyonya- basi mume na mke hawa wataendelea katika ndoa yao sawa iwe kabla au baada ya kuingiliana, kwani sheria imekubali ndoa ya wasio Waislamu, kwa hiyo wanabakia katika ndoa wakisilimu au ikiwa wapo katika hukumu ya Waislamu, bila ya kuangalia sifa ya mkataba wao na mfumo wake, ndoa yao haizingatiwi kwa masharti ya ndoa ya Waislamu kama vile walii, mashahidi wawili na tamko la kuitika na kukubali. Katika enzi ya Mtume S.A.W wanaume na wake zao walisilimu basi waliendelea katika ndoa zao, na Mtume S.A.W hakuwauliza masharti ya ndoa na namna yake. Na jambo hili linajulikana na wanachuoni wamelikubali [Kitabu cha Al Mughniy Libn Qudama, 7/116]

Ibn Abdulbar alisema; "Wanazuoni waliafikiana kwamba mke na mume wakisilimu pamoja katika hali moja; basi wao wataendelea katika ndoa yao isipokuwa ikiwa baina yao ni nasaba au kunyonya inawajibisha kuharamisha, na asili ya mkataba unasamehe, kwani wengi wa Maswahaba wa Mtume S.A.W., walikuwa sio Waislamu  wakasilimu na kusilimu wake zao, na waliendelea katika ndoa ya kwanza, na haikuzingatiwa masharti ya Uislamu katika asili ya ndoa zao, na hili limefahamika kwa njia isiyo na shaka".[Kitabu cha; At Tamheed 23/12]

Sura ya Pili: Na kama mume alisilimu peke yake, na mke wake ni miongoni mwa watu wa kitabu na mke huyo hakuwa miongoni mwa maharimu wake basi wanabakia katika ndoa yao ya kwanza sawa iwe kabla au baada ya kuingiliana, kwani ndoa ya wanawake wa kitabu ni halali kwa Muislamu; kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu. na chakula chenu na halali kwao. Na (mmehalalishwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu. (Ni halali kwenu kuwaoa), mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila kufanya uzinzi, wala kuwaweka (wanawake) kinyumba.} [Al MAIDAH 5]. Basi mwanamke wa kitabu ni halali kwa mwislamu kabla ya kusilimu basi ni halali baada yake.

Sura ya Tatu: Lakini kama mke alisilimu, na mume wake alibakia katika dini yake. Basi Fatwa iliyochaguliwa ni:

Wanavyuoni waliafikiana kwamba mwanamke Muislamu haijuzu kuolewa na  asiye Muislamu, na kama ikitokea ndoa hiyo ni batili. Lakini huhumu gani ya kisheria kama mke na mume wake walikuwa sio Waislamu, halafu mke akasilimu bila ya kusilimu mume wake?

Basi Fatwa iliyochaguliwa ni: Ikiwa mke kasilimu kabla ya kuingiliwa basi lazima utengano baina yao wawili uharakishwe; kwani jambo hilo ni la kiasili, na hapana masilahi hapa yanayotupelekea kukubali ndoa hiyo. Na ikiwa mke alisilimu baada ya kuingiliwa, na mume wake akasilimu kabla ya kwisha eda yake basi wataendelea katika ndoa yao, lakini kama eda yake ilitimia na mume wake hakusilimu basi mke huyu atakuwa na uhuru wa kuchagua; kama atachagua kuolewa na amtakaye basi ana haki hiyo, lakini lazima aende kwa kadhi ili autengue mkataba wa ndoa, na kama atachagua kumngojea mume wake asilimu hata kama muda utarefuka basi ni haki yake, na katika hali hiyo ndoa inazingatiwa imesimamishwa, na kama mume wake atasilimu basi wanabakia katika ndoa yao ya kwanza bila ya kuhitaji kufunga tena ndoa, pamoja na kuzingatia kutokea utengano wa kihisia na kusimama kwa tendo la ndoa baina yao tangu mwanzo wa kusilimu kwa mke. Rai hii ameisema Ibn Taimia na Ibn Al Qaim, kama itakavyofuata.

Sura ya Kwanza:

Katika Madhehebu iliyochaguliwa na Dalili zake

Ibn Taymiyyah na Ibn al-Qayyim wamesema kuwa mwanamke akiingia katika Uislamu bila ya mume wake, basi ana haki ya kumngoja asilimu muda anaotaka, maadamu amechagua hivyo. Anaposilimu, yeye ni mume wake bila ya haja yakufunga upya ndoa.

Sheikh Taqiy Edeen Ibn Taimia amesema: "Wanazuoni walitofautiana katika mke wa asiyekuwa Muislamu, je ana eda juu yake? Katika kauli mbili; Na Madhehebu ya Abi Hanifa na Malik, hayana eda, na wanayo Hadithi katika hilo la kurudishwa wanawake wa watumwa wa wenye ahadi, basi hiyo ni kama kurudisha mahari za wanawake muhajirina/waliohama kutoka kwa watu wa suluhu, na wao ni wanawake mumtahina ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika haki yao: {Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani} [AL MUMTAHINA 9]

Ilikuwa kama mume wake akihama kabla ya aliolewa basi yeye ana haki kuendelea na ndoa yao, na hilo ni moja ya matamko katika suala hilo. Na hilo kwamba mke wa asiye Muislamu kama alisilimu basi je, utengano unaharakishwa au hapana? Au wanatenganishwa baina ya mwanamke aliyeingiliwa na asiyeingiliwa? Au hilo jambo linasimamia kama hakuolewa na mume akisilimu basi yeye ni mke wake?

  Na Hadithi zinaashiria kauli hiyo, na miongoni mwao Hadithi hiyo, na miongoni mwao Hadithi ya Zainab Binti wa Mtume S.A.W., basi yanayothibiti katika Hadithi kwamba alimrudisha kwa mumewe kwa ndoa ya kwanza baada ya miaka sita. [Kitabu cha: Majmuo' Al Fatawa 209/32]

Na Imamu Ibn Al Qaim amesema: Na aliyesema kwamba kusilimu mmoja wao (mke au mume) kabla ya mwingine inawajibisha kuharakisha utengano kabla ya kuingiliwa au baada ya kuingiliwa, basi tamko hilo ni kosa, Na Mtume S.A.W. hakumwuliza mtu yeyote miongoni mwa waliosilimu; je, unamwingilia mke wako au la? Bali kila mtu akisilimu na mke wake akasilimu baada yake basi yeye ni mke wake bila ya bila ya kufunga ndoa upya. [Kitabu cha: Ahkamu Ahlu Azemah 692/2]

Na kuna dalili nyingi kuhusu Fatwa tuliyoichagua:

Kwanza: Imethibiti kwamba Mtume S.A.W alimrudisha binti yake Zainab kwa Abi Al Aas kwa ndoa ya kwanza. Kutoka kwa Ibn Abaas R.A. amesema: "Mtume S.A.W alimrudisha Zainab binti yake kwa mume wake Abi Al Aas Bin Al Rabii' kwa ndoa ya kwanza na hakijatokea kitu". [Imepokelewa katika kitabu cha Sunan Abu Dawud 217/1, na Musnad Ahmad 2240, na Mustadrak Al Haakem 219/2].

Na katika tamko: "Hakukuwa na mahari" [Imepokelewa katika Musnad Ahmad 351/1 na Mustadrak Al Haakem 50/4].

Na katika tamko lingine: "Hakukuwa na ushahidi wala mahari" [Imepokelewa katika Musnad Ahmad 261/1].

Na katika tamko: "Haijafungwa upya ndoa" [Imepokelewa katika Sunan At Tarmiziy 1143].

Na katika riwaya: "Baada ya miaka sita" [Imepokelewa katika Sunan Abu Dawud 2241, na Mustadrak Al Haakem 262/3 na Al Bihaiqiy katika Asunun Al Kubra 187/7].

Na katika riwaya: "Baada ya miaka miwili" [Imepokelewa katika Sunan Abi Dawud 2240 na Musnad Ahmad 351/1 na Mustadrak Al Haakem 50/4].

Al Khatwabiy alisema kuhusu Hadithi hiyo: hiyo ni sahihi zaidi kuliko Hadithi ya Amru Bin Shuaib, na hivyo hivyo Al Bukhariy amesema. Ibn Kathiir amesema katika kitabu cha Al Irshaad: Hiyo ni Hadithi yenye nguvu nzuri [kitabu cha Tuhfat Al Ahwaziy kwa Al Mebarkafuriy 249/4]. Na At Tarmiziy amesema katika kitabu cha [Al Elal]: Nilimwuliza Mohammad Bin Ismail Al Bukhariy kuhusu Hadithi mbili hizo – yaani Hadithi ya Ibn Abbas na Hadithi ya Amru Bin Shuaib – basi akasema: Hadithi ya Ibn Abbas ni sahihi zaidi kuliko Hadithi ya Amru Bin Shuaib kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake [Kitabu cha; Tartib Elal At Tarmiziy kwa Abi Atwaib Al Qadhi 166-167/1]. Na Ad Darqutwniy alisema katika Hadithi ya Amru Bin Shuaib: Haithibitishi, na iliyo sahihi ni Hadithi ya Ibn Abbas [Kitabu cha Aunu Al Ma'abud kwa Mohammad Shams Al Haqi Al Adhiim Abadiy 232/6]. Na Hadithi hiyo ilisahihishwa na Ibn Hazm [Kitabu cha Al Mahaliy Bil Athaar 372/5].

Kitendo cha Mtume S.A.W kumrudisha mwanamke kwa mume wake baada ya kusilimu mume kinajulisha kwamba hakuna haja ya kufunga upya ndoa hata kama muda utarefuka na eda itamalizika.

Ama yaliyopokelewa katika Hadithi ya Amru Bin Shuaib kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume S.A.W alimrudisha binti yake kwa ndoa mpya, yamekuja kwa matamko mawili:

Tamko la Kwanza: "Mtume S.A.W alimrudisha binti yake kwa Abi Al Aas kwa mahari mpya na ndoa mpya" [Imepokelewa katika Sunan At Termiziy 1142, na Sunan Ibn Majah 2010 na Musnad Ahamd 207/2].

Tamko la pili: "Zainab binti ya Mtume S.A.W alisilimu kabla ya mume wake Abi Al Aas kwa mwaka mmoja kisha mume wake alisilimu basi Mtume S.A.W alimrudisha kwa ndoa mpya". [Imepokelewa katika Mustadraku Al Haakem 741/7]

Hadithi hii kwa matamko yake mawili inarejea kwa Al Hajaaj Bin Artta'ah, ambaye amezipokea kutoka kwa Amru Bin Shuaib, na alikuwa mdanganyifu mkubwa, anawadanganya watu.

Na kutoka kwa Yahya Bin Saied Al Qatwan kwamba Hajaj hakuisikia kutoka kwa Amru, na hiyo ni kutoka Hadithi ya Mohammad Bin Abdullahi Al Arzamiy kutoka kwa Amru, Al Baihaqiy alisema: Hiyo ni sura haizingatiwi na mtu yeyote anajua maana ya Hadithi [Kitabu cha Asunan Al Kubra kwa Al Baihaqiy 188/7, na Fathu-Al Bariy kwa Ibn Hajar 423/9].

Ahmad ameseme: "Hii Hadithi dhaifu, au alisema Hadithi mbaya, na Al Hajaaj hakuisikia kutoka kwa Amru Bin Shuaib lakini aliisikia kutoka kwa Muhamad Bin Ubaid Illahi Al Arzemiy, na Al Arzemiy Hadithi yake si lolote si chochote. Bali Hadithi sahihi aliyoipokea, inasema Mtume S.A.W aliwakubalia kwa ndoa ya kwanza" [Musnad Ahmad, 2/207, Ch. Muasasat Qurtubah].

Hadithi hiyo pia Al Tarmiziy ameifanya dhaifu, na akasema: "Katika Isnadi yake makala", na Al Darqattniy alisema: " Hadithi hii haithibiti, na Al Hajaaj haitolei hoja, na sahihi ni Hadithi ya Ibn Abaas: "Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake kwa ndoa ya kwanza" [Sunnan Al Darqattniy, 3/253, Ch. Dar Al Maarifa].

Na Zainabu Binti wa mtume S.A.W. alikuwa amesilimu tangu mwanzoni mwa Ujumbe, na Ibn Hazm amesimulia Ijmaa (mkusanyiko) juu ya hayo, na Zainabu hakuhama Madina pamoja na babake S.A.W., bali alibakia katika Makka pamoja na mumewe Abi Al Aasw, na alihama baada ya vita vya Badr katika mwaka wa pili baada ya Hijra. Na haukuteremshwa uharamisho wanawake Waislamu kwa wasio waislamu isipokuwa baada ya Al Hudaibia katika mwaka wa sita kutoka Hijra, na baadhi ya wanawake Waislamu walipofika Madina wakihamia Maquraishi waliomba kuwarejesha kutokana mkataba wa Usuluhisho wa Hudaibia. Basi Aya hiyo iliteremka, {Basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini} [Al Mumtahinah 10]. Na Abu Al Aasw alisilimu baada ya Al Hudaibia kwa miaka miwili, yaani katika mwaka wa nane Hijra, kama alivyotoa Ibn Asaker kutoka kwa Az Zohariy akasema:

Na Abu Jandal na Abu Baswer na wenzake walibakia kule katika pwani ya Bahari, hadi Abu Al Aasw Bin Ar Rabee'  aliwapitia, alikuwa mume wa Zainabu Binti wa Mtume S.A.W., ni kutoka Shaam Pamoja na watu kutoka Quraish, basi Abu Jandab na wenzake waliwateka na hawakuua mtu yeyote miongoni mwao, kwa ajili ya Mtume S.A.W., aliyekuwa ni shemeji wa Abu Al Aasw, na Abu Al Aasw wakati huo alikuwa si Muislamu, na yeye alikuwa mpwa wa Khadija Bint Khowaeled, na walimwachia Abi Al Aasw basi alifikia Madina kwa mke wake aliyekuwa Madina Pamoja na Baba yake, Abu Al Aasw alikuwa akimwidhinisha alipotoka Shaam, kwenda Madina ili awe pamoja na Mtume S.A.W., Basi Abu Al Aasw alizungumza na Zainabu akiwa Abu Al Aasw na wenzake wametekwa na Jandal na Abu Basweer basi Zainabu alizungumza na Mtume S.A.W. katika jambo hilo. Basi walidai kwamba Mtume S.A.W., alisimama na kuhutubia watu akisema: Sisi tuliwaozesha watu fulani na tulimuozesha Aba Al Aasw, shemeji mwema tulimpata, na yeye ametoka Shaam Pamoja na wenzake kutoka Quraish, basi Abu Jandal na Abu Basweer wakawateka na wakachukua mizigo yao lakini hawakuua mtu yeyote miongoni mwao, na kwamba Zainabu Bint wa Mtume S.A.W., ameniomba niwasaidie, basi nyinyi pia mpo tayarikuwasaidia Abu Al Aasw na wenzake? basi watu walisema ndiyo, basi Abu Jandal na wenzake ilipowafikia kauli hiyo ya Mtume S.A.W., kuhusu Abi Al Aasw na wenzake waliotekwa aliwarudishia mizigo yao yote. [Kitabu cha: Tarehe Dimisqas kwa Ibn Asaker 15/67] na inajulikana kuwa jambo hilo lilikuwa katika mwaka wa nane Hijra.

Na Ibn Kathiir alichagua kwamba Uislamu wa Abi Al Aasw umechelewa wakati wa kuwaharamishwa wanawake waamini kwa makafiri kwa miaka miwili, na akasema Uislamu wake ulikuwa katika mwaka wa nane na siyo kama katika kauli ya Al Waqidiy kwamba Uislamu wake ulikuwa katika mwaka wa sita. [Kitabu cha: Al Bidaya wa An Nahaya kwa Ibn Katheer 178/4]

Ibn Hajar alisema katika kitabu cha Al Fateh: "Ibn Hazm akasema: Hakika kauli yake alimrudia yeye baada ya muda kadhaa inamaanisha kuwakusanya pamoja, au kusilimu kwa Abi Al Aasw ilikuwa kabla ya Suluhu ya Al Hudaibia, na hayo kabla ya kuteremka uharamisho wa wanawake Waislamu kwa mshirikina, hivyo ndivyo alivyodai, na hayo yanahitilafiana na waliyokubaliana watu wa vita kwamba kusilimu kwake kulikuwa katika Suluhu baada ya kuteremka Aya ya kuharamisha. [Kitabu cha: Fat-hu Al Bariy Sharhu Sahihi Al Bokhariy 424/9]

Mwendelezo: Huu ni mwendelezo wa Hadithi ya kurudishwa Zainabu kwa mume wake Abi Al Aasw kwa mapokezi yake mawili:

Tulizungumzia hapo juu kuhusu mapokezi mawili kwa mujibu wa kutokea kwake, na tukahitimisha kuwa mapokezi ya Ibn Abbas R.A., wote wawili kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake Zainabu kwa Abi Al Aasw kwa ndoa ya kwanza ni mapokezi sahili zaidi kuliko mapokezi ya Amru Ibn Shuaib, kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume S.A.W. alimrudhishia kwa ndoa mpya.

Hata hivyo, kuna nyongeza muhumu zenye faida kuhusiana na Hadithi hii kama ifuatavyo:

Mapokezi ya Ibn Abaas yamekuja  kwa matamko mawili: la kwanza: "baada ya miaka sita" na la pili: "baada ya miaka miwili", ikasemwa: Hakika kinachokusudiwa kwa miaka sita ni muda baina ya kuhama kwa Zainabu na kusilimu kwa mumewe, na hiyo ilibainika katika (AL Maghazi), basi alitekwa katika vita vya Badr, na Zainabu alitumwa kutoka Makka kwenda kumkomboa mume wake lakini walimwachia Al Aasw bila ya fidia, na Mtume S.A.W., aliweka sharti amtume Zainabu Madina kwa mumewe Abu Al Aasw na alitekeleza ahadi yake.

Na haya yanabainishwa  katika Hadithi sahihi kwa kauli ya Mtume S.A.W., kwa kusema kwake: "Alisema nami, na  kuniambia kweli na aliniahidi na kutekeleza ahadi yake" [Iliafikiana nayo, Sahihi ya Al Bokariy 3523 na Sahihi ya Muslim 1902] na makusudio ya miaka miwili ni muda baina ya kuteremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini} [AL MUMTAHINA 10] Na kufika kwake akiwa Muislamu basi ilikuwa baina yao miaka miwili na miezi kadhaa. [Kitabu cha: Fat-hu Al Bariy sharhu sahihi Al Bokhari kwa Ibn Hajar 232/9]

Matamko mawili ya mapokezo ya Ibn Abbas: "baada ya miaka sita" na "baada ya miaka miwili" yana tatizo- kwa mujibu ya wale wanaoona kwamba kuvunjika ndoa kwa kumalizika eda- yaani kuweka mbali kwamba eda inabakia katika muda huo.

Al-Hafidh Ibn Hajar amesema: “Al-Khattabi alijibu tatizo hilo kwa kusema kwamba inawezekana kubakia eda katika kipindi hicho, hata kama si kawaida yake, hasa ikiwa muda huo ni miaka miwili na miezi kadhaa, kwani hedhi inaweza kuchelewa kwa wanawake kutokana na sababu fulani wakati fulani, na kwa ajili hiyo, Al-Bayhaqi akajibu. Na yeye ana haki ya kutegemewa  katika jambo hili.”                                                                   

Na Ibn Al Qayyim alilijibu hili, aliposema: Ama kuwa kwake hakuwa na hedhi  katika miaka sita isipokuwa hedhi tatu, basi igawa hiyo ni mbali sana na kinyume na yale aliyoyafaradhisha Mwenyezi Mungu kwa wanawake, basi ingetokea hiyo ingenukuliwa, lakini hiyo haiyakunukuliwa na mtu yeyote, na Mtume S.A.W. hakuainisha kubakia ndoa kwa muda wa eda hadi inasemekana labda eda yake imechelewa, basi jambo halikuthibitika kwa hedhi tatu na wala kuchelewa kwake miaka sita. [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Azemah 677/2]

Kuna waliosema: Kwamba riwaya ya Ibn Abbas haikusaimika kutoka na upinzani, na upinzani ni Hadithi ya Amru Bin Shuaib kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, na walipokubali upinzani huo walielekea kujaribu kuweka  uwiano baina ya riwaya zote mbili, basi wakasema kama tukikubali kuthibitisha riwaya ya Ibn Abbas, basi hiyo ni kusema kwamba ilikuwa habari juu ya hali ya dhahiri, akinyamazia kutaja kurudi kwa Zainabu kwa ndoa mpya, na riwaya ya Amru Bin Shuib kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake ni habari kuhusu maana ya tukio, akithibitisha kwamba Mtume S.A.W. kamrudisha kwa ndoa mpya basi hiyo ina haki ya kutangulizwa zaidi. [Tazama: kitabu cha: Ahkaam Al Qura'ni kwa Aj Jaswas 657/3, kitabu cha: Fat-hu Al Qadeer kwa Ibn Al Hamaam 425/3]

Jibu: Hii ni njia yenye kutegemewa na mtu asiache kitu kinachofanana kinapokuwepo ili kupatanisha maandiko mawili yaliyothibitika na yanayoonekana kupingana. Hata hivyo, hali iliyopo hapa ni kwamba riwaya hizo mbili hazilingani kwa nguvu hadi kufikia hatua ya kupingana. na tumeelezea hapo juu sababu ya udhaifu wa riwaya ya Amru Ibn Shuaib, na hakuna faida kutumia juhudi katika kujaribu kuunga baina riwaya mbili; moja ni thabiti na yingine ni dhaifu.

Na miongoni mwa kauli dhaifu zaidi kuliko zote iliyosemwa katika kukusanya baina ya riwaya hizo mbili, ni iliyosimuliwa na At Twahawiy kutoka kwa Mohammad Bin Al Hussain -rafiki wa Abi Hanifa- na aliiridhia: Basi kutoka kwa Abi Tawbah Ar-Rabie' Bin Nafi' alisema: Nilimwambia Mohammad Bin Al Hassan kutokukubaliana kwao kuhusu Zainabu kumetoka wapi? Basi alisema baadhi yao wamesema kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha kwa Al Aasw juu ya ndoa ya kwanza.

Na baadhi yao walisema: Alimrudisha kwa ndoa mpya. Je, kila mtu miongoni mwao alisikiliza aliyosema Mtume S.A.W.? Basi Mohammad Bin Al Hassan alisema kwamba tofauti yao haikuja kutoka upande huo, bali tofauti yao ilikuja kutokana na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliharamisha kuwarudisha wanawake waumini kwa makafiri katika Sura ya Mumtahina baada ya kwamba hiyo ilikuwa ikijuzu na halali.

Basi Abdullhai Bin Amru alijua hayo, kisha akaona kwamba Mtume S.A.W. amemrudisha Zainabu kwa Abi Al Aasw baada ya kujua uharamisho wake kwa kuharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu wanawake waumini kwa makafiri, basi haikuwa hayo kwake ila kwa ndoa mpya, basi akasema: alimrudishia Mtume S.A.W., kwa ndoa mpya, na Abdullahi Bin Abbas hakujua kuharamisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu wanawake waumini kwa makafiri mpaka alijua kwamba Mtume S.A.W., alimrudisha Zainabu kwa Abi Al Aasw. Basi alisema: alimrudishia kwa ndoa ya kwanza; kwani Mtume S.A.W. hakuwa na dalili ya kuvunja ndoa baina ya kusilimu Zainabu na kusilimu mumewe, Mohammad -Mola amrehemu- alisema: basi kutoka hapa ilikuja tofauti yao, siyo kutokana na tofauti waliyasikiliza kutoka Mtume S.A.W. katika kutaja kwake sababu ya kumrudisha Zainabu kwa Abi Al Aasw, kwamba ni ndoa ya kwanza au ndoa mpya. [Kitabu cha Sharhu Maani Al Athaar 256/3]

Baadhi yao walijaribu kufafanua maana ya baadhi ya maneno ya riwaya ya Ibn Abbas, na wakasema: “Wakasema kusema kwake: “Hakuna kilichotokea kwenye ndoa ya kwanza”, kama mahari ya kwanza, Ibn Abdul-Bar amesema hayo, [kKitabu cha Al Istzkaar 521/5] na Ibn Al Hamam akataja kauli yenye maana hiyohiyo: Haikutokea ziada katika mahari, na akasema huo ni ufafanuzi mzuri. [Kitabu cha Fat-hu Al Qadeer kwa Ibn Al Hammam 425/3]

Na Ibn Al Qayyim akajibu kauli hiyo na akasema: Ama kauli yake kwamba alimrudisha juu ya ndoa ya kwanza yaani kwa mahari kama mahari ya kwanza; basi kauli hiyo haikufichwa udhaifu wake na ufisadi wake, na hiyo ni kiyume cha yanayofahamika kutokana na lafdhi ya Hadithi, na kauli yake (halikutokea lolote) inakataa. [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Adhimah 683/2]

Kisha maneno mengine ya riwaya hiyo hayaungi mkono tafsiri hii, ikiwa ni pamoja na sharti la (hakutoa ushahidi wala mahari) na kauli hiyo inatosha kubatilisha ufafanuzi huo.

Wapo waliyosema kwamba Hadithi ya Ibn Abbas imefutwa, lakini wao walihitilafiana katika inayofuta…

Imesemwa kwamba ilifutwa kwa Aya ya Mumtahina nayo ni kwanjia mbili:

Ya Kwanza: kwamba kisa cha Zainab na Abi Al Aasw kilitokea baada ya vita vya Badr, na kuteremka kwa Aya ya Al Mumtahina ilikuwa baada ya Suluhu ya Al Hudaybiyyah.

At Twahawiy alisema akichukua dahili yake kwa habari mbili: ya kwanza: kutoka kwa Az Zuhzriy, kwamba Aba Al Aasw Bin Rabiah alitekwa siku ya Badr basi Mtume S.A.W. alimleta na alimrudishia Binti yake, Az Zuhariy akasema: Hayo yalikuwa kabla ya kuteremshwa faradhi.

Na ya Pili: kutoka kwa Qetadah, kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake kwa Abi Al Aasw, Qetadah akasema: hayo yalikuwa kabla ya kuteremshwa Surat Bara'ah. [Sharhu Maani Al Aathaar 260/3]

Al Hafidh Ibn Haja ametaja hayo, na alijibu aliposema: At Twahawiy alidai kwamba Hadithi ya Ibn Abbas imefutwa, na kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake kwa Abi Al Aasw baada ya kurudia kutoka Badr alipotekwa huku, kisha alifidiwa na aliachwa, na alinasibisha hayo kutoka kwa Az Zohariy, na hayo yana maoni.

Na ikithibika kutoka kwake basi inafasiriwa; kwa sababu Zainabu alikuwa pamoja naye huko Makka, na ndiye aliyetumwa kumkomboa, kama inavyojulika katika katika vita, basi ilikuwa maana ya kauli yake alimrudisha yaani alimridhia, na hayo yalikuwa kabla ya kuharamishwa, na inayothibitika ni kwamba alipoachwa aliweka sharti amtume Zainabu basi alitekeleza ahadi yake kama iliyotangulia hapo juu, lakini alimrudisha kwa hakika baada ya kusilimu kwake. [Fat-hu Al Bariy Sharhu Sahihi Al Bokhariy 424/9]

Na Ibn Al Qayyim amesema: "Na kauli ya mwisho inayosemekana kwamba kumrudisha Zainabu kwa Abi Al Aasw na kuteremka Aya ya kuharamisha ilikuwa katika wakati wa Suluhu, basi mtu atajuaje kumteremka Aya ni kutokana na kwa kisa cha mume na mke ili iwe inaifutia? Wala haijuzu kudai ufutaji kwa njia ya uwezekano" basi hiyo ni kujibu kwa yaliyosimulia kutoka kwa Az Zohariy. [Ahkaam Ahlu Adhimah 679 /2]

Ama kauli ya Qatadah: "Hiyo ilikuwa kabla ya kuteremka Suratu Bara'ah" hakuna shaka kwamba ilikuwa kabla ya kuteremka Bara'ah, lakini Ipo wapi katika Surat Bara'ah yanayothibbitisha kubatilisha yaliyopitia katika Sunna ya Mtume S.A.W., kutokana na Ujumbe wake hadi kifo chake kwa kutotengana baina ya mwanamume na mwanamke kama mmoja wao alisilimu kabla ya mwingine?

Na ahadi ambazo Mtume S.A.W. alizitoa mbali kwa Washirikina ni ahadi za Suluhu ambazo zilikuwa baina yake na baina yao, basi hizo ni kujitoa kutokana na mkataba na ahadi ambayo ilikuwa baina yake na baina yao, na wala haikutaja ndoa kwa maana yoyote, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikazia kujitoa baina ya Waislamu na makafiri kabla ya hayo katika Suratu Al Mumtahina na nyinginezo, lakini hayo hayapingani na kungojea mwanamke kwa ndoa yake mpaka kusilimu kwa mume wake. Basi kama alisilimu alikuwa ni mke wake, na kama hakusilimu basi yeye hana dhambi naye. [Ahkaam Ahlu Adhimah 679-680/2]

Na Ya pili: Na sura wa pili: kwamba Aba Al Aasw alikuwa kafiri, mwanamke Mislamu haijuzu kuwa mke kwa mkafiri Ibn Abdulbar alisema: ambayo yanadalilisha kwamba kisa cha Abi Al Aasw kinafutwa kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlichokitoa, na wao watake walicho kitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayo kuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.} [AL MUMTAHINAH 10]. Wanavyuoni walijumaisha kuwa Aba Al Aasw Bin Ar Rabi'I alikuwa mkafiri, na kwamba mwanamke mwislamu hahalalishi kuwa mke wa mkafiri, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema; {Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini} [AN NISAA 141].

Na Mtume S.A.W., amesema: kwa njia ya kiapo cha laana hukuna njia juu yake. [kitabu cha: At Tamheed 21/12]

Na jibu kwa hili ni kwamba Ibn Abdulbar alijengea maneno yake hayo kwamba Aba Al Aasw alikuwa kafiri aliporudishiwa Zainabu, na hayo yanapingana na mapokezo yote.

Ilisemwa: kwamba ujumaisho wa kukataza urejesho baada ya kumaliza eda ni dalili ya kufuta hukumu hiyo.

Ibn Abdulbar alisema: "Na habari hiyo hata ikiwa sahihi basi hiyo inaachwa inafutwa kwa wanavyuoni wote; kwani wao hawahalalishi urejesho wake kwake baada ya kutoka kwake kwenye eda yake", [kitabu cha: At Tamheed 20/12]

Kisha kwamba yeye alisisitiza hayo kwa kauli yake "Hukumu imefutwa kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nawaume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu} [AL BAQARAH 228], yaani katika eda yao, na hiyo haina tofauti baina ya wanavyuoni kwamba alikusudia eda. [Kitabu cha: Al Estzkaar kwa Ibn Abdulbar 520/5, na Aya namba ya 228 Suratu Al Baqarah]

Na Aj Jaswas alisema akiashiria kurudisha Hadithi kutokana na upande huo: "Hakuna tofauti baina ya Wanavyuoni wa kifiqhi kwamba harudishwi kwao kwa ndoa ya kwanza baada ya kumaliza hedhi tatu, na inajulikana kwamba siyo katika kawaida kwamba yeye hapati hedhi tatu ndani ya miaka sita". [Kitabu cha: Ahkaam Al Qura'an 657/3]

Na jibu la hili ni kwamba madai ya maafikiano yanakataliwa kutokana na tuliyoyasimulia kutoka kwa Amiri wa Waumnini Omar R.A.

Ama kutoana na dalili kwa Ibn Abdulbar kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nawaume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu} [AL BAQARAH 228], na kwamba ni kuifuta Hadithi, basi Ibn Taimia alistaajabu nayo na akasema: "Ninastaajabishwa kutokana na kudai kwamba inayofuta ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nawaume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu} [AL BAQARAH 228], kwani hiyo ni katika hali ya talaka ya kurejea ya wanawake kwa matini ya Qur'ani na makubaliano ya Umma.

Hamna yeyote aliyesema kuwa kusilimu mwanamke ni talaka ya kurejea, mume wake ana haki ya kumrudisha katika eda yake, na wanayohukumu kwa utengano baada ya kumaliza eda hawaitokei kutoka kusilimu, siyo kama talaka, hiyo inatokea kutokana na kumtalaki, na mume ana haki kumrudisha katika wakati wa eda yake. [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Adhimah 678/2].

Na jambo la msingi la madai ya kufutwa ni kwamba ni dhaifu mno, kiasi kwamba Ibn Al Qayyim amesema: Ama madai ya kufutwa kwa Hadithi ni mbali kabisa, kwani masharti ya kufuta hayapo, na hiyo ni uwepo wa upnzani, na mabisho yake (makatazo), na kuchelewa kwake, basi ni wapi moja  ya mambo matatu hayo? [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Adhimah 678/2].

Na Dalili ya Pili: Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abaas alisema: "Mwanamke mmoja alisilimu katika zama ya Mtume S.A.W basi akaolewa. Mume wake wa kwanza alikuja kwa Mtume S.A.W na akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa nimesilimu na mke wangu alijua kusilimu kwangu, basi Mtume S.A.W akamng'oa kutoka mume wake wa pili na akamrudisha kwa mume wake wa kwanza".

Na katika tamko: "Mwanamume alikuja hali ya kuwa ni Muislamu katika zama ya Mtume S.A.W kisha mke wake akaja hali ya kuwa ni Muislamu, basi mwanamume akasema: "Ewe Mtume wa Allah! Mke wangu alikuwa amesilimu nami basi mrudishe kwangu, Mtume S.A.W akamrudisha kwake". [Imepokelewa na Ahmad, Abu Dawud, Al Tarmiziy na Al Haakem].

Na ushahidi: kutouliza Mtume S.A.W je, mke wake alijua kusilimu kwake kabla ya kumalizika eda yake au la? Hii ni dalili kwamba eda haizingatiwi, na hayo kutokana na kutouliza katika hali hiyo, licha ya kuwepo uwezekano wa kuuliza, [Al Bahr Al Muheett, 4/201, Ch. Dar Al Kutubiy], na uwezekano hapa upo, je, mke alijua kusilimu mume wake kabla ya kumalizika eda au baada yake? pamoja na hayo Mtume S.A.W hakumwuliza, basi hiyo inaashiria ujumla wa hukumu ya hali mbili, na kuwa hakuna tofauti kati ya kurudisha mke kabla ya kutimia eda au baada yake.

Tatu: Kutoka kwa Ibn Abbas R.A alisema: "Washirikina walikuwa katika nafasi mbili kwa Mtume S.A.W na waumini; walikuwa washirikina ni watu wa vita wanapigana na Mtume S.A.W na anapigana nao, na washirikina wa watu wa ahadi hapingani nao wala hawapigani nao, na ilikuwa mwanamke wa watu wa vita anapohama haposwi hadi apate hedhi na ajitwaharishe, basi akitwaharika ndoa ni halali kwake, na kama mume wake alihama kabla ya mke wake kuolewa basi atarudishwa kwake, na kama mtumwa au kijakazi wao alihama basi wako huru, na wana haki kama haki ya Muhajirina" [Imepokelewa na Al Bukhariy].

Na maana ya hayo: Ndoa yake ya kwanza inaendelea lakini inasimamishwa -kwa maana kutojamiiana- hata kama aliolewa na mwingine basi ndoa ya kwanza itakuwa imevunjika, na kama mume wake alisilimu kabla ya kuolewa na mwingine basi atarejeshewa.

Dalili ya Nne: Yaliyosimulizwa kutoka kwa Abdulhai Bin Yazeed Al Khatwamiy akasema: "Mwanamke kutoka watu wa Al Hera alisilimu na mume wake hakusilimu basi Omar Bin Al Khtwaab R.A. aliandika kwamba mfanye kuchagua kama alitaka kutengana na mumwe na akitaka kuendelea naye basi aendelee. Na maana ya hayo: ndoa yake ya kwanza inaendelea lakini inasimamishwa -kwa maana kutojamiiana na mumewe asiye Muislamu. Bali hiyo inaashiria kwamba mwanamke anangojea kusilimu kwa mume wake, na anaposilimu basi yeye ni mke wake, hata akingojea miaka mingi, kwani yeye ambaye alichagua jambo hilio.

Basi akipinga hayo kwani labda oni hilo lilikuwa jitihadi kutoka Omar Bin Al Khatwab R.A. jibu lilikuwa kwamba alifanya hayo mbele ya jamaa ya wasahaba na hawakukataa oni hilo.

Na Dalili ya Tano: Mwanamke akisilimu kisha mume wake akasilimu baada yake basi ndoa inaendelea katika hali yake, kama vile Ummu Al Fadhl mke wa Al Abaas Bin Abdulmuttalib aliyesilimu kabla ya Al Abaas kwa muda, Abdulahi Bin Abaas alisema: "Mimi na mama yangu tulikuwa miongoni mwa waliopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: {Isipokuwa wale waliokuwa madhaifu kweli katika wanaume na wanawake na watoto} [AN NISAA 98] [Imepokelewa na Al Bukhariy].

Na siri ya swala hili ni kama anavyoona Ibn Al Qayyim kuwa mndoa katika muda huu inajuzu lakini sio lazima, na wala haukatazwi na wala hakuna madhara kwa mke, na haipingani na misingi ya sheria. Ama mwanamume akisilimu na chini yake kuna mke kafiri –inakusudiwa mwanamke asiyekuwa wa watu wa kitabu- na akakataa Uislamu basi mume kumshikilia mke kuna madhara na hakuna masilahi kwa mke huyo katika hali hiyo, kwani kama hakumtendea haki yake basi anakuwa dhalimu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu} [AL MUMTAHINAH 10], Allah S.W. amewakataza wanaume kudumu katika ndoa ya mwanamke asiyekuwa wa watu wa kitabu-, [Ahkaam Ahlu Al Dhima kwa Ibn Al Qaim, 2/662-663].

Basi mwanamume akisilimu, mke wake anaombwa kuingia katika Uislamu, basi akikataa kusilimu utengano unatokea baina yao wawili.

Sura ya Pili:

Katika matamko ya wanaotofautiana na dalili zao na kuzijadilia.

Wanavyuoni wa Kifiqhi walitofautiana tangu zamani katika suala hilo, na wana maoni kadhaa, na sisi tutaanza kuonesha maoni hayo na Madhehebu, na kutaja dalili zao na kuzijadilia.

Madhehebu ya Kwanza: Madhehbu ya Jamhuri:-

Wanavyuoni wa Malik, wa Shafi na wa Hanbali wanaelekea kwamba Uislamu wa mke ukiwa kabla ya kuingilia basi utengano unatokea moja kwa moja, na ukiwa baada ya kuingilia utengano unangojea kumaliza Eda, basi kama mumewe alisilimu kabla ya kumaliza Eda ndoa yao inaendelea, na kama hakusilimu mpaka Eda ilimaliza, utengano utatokea baina yao. Al Waza'I, Al laith, Az Zohariy na Is-haq walisema hayo.

An Nafrawiy Maliky amesema: "Na ama kama mke alisilimu kwanza, basi Uislamu ukiwa kabla ya ubainifu (kumaliza eda) ndoa yake imevunjaka moja kwa moja, na kama ulikuwa baada ya ubainifu, ndoa itaendelea kama mume wake atasilimu katika eda yake, lakini akichelewa katika Uislamu wake kutokana na eda yake basi haiendelei kwani eda yake imemaliza. [Kitabu cha: Al Fawakeh Ad Dawaniy Ala Resalet Ibn Abi Zaid Al Qairawaniy kwa Al Maqrizi 26/2]

Na katika kitabu cha: Al Minhaj na Sharhu yake kwa Ar Ramliy miongoni mwa vitabu vya kishafiy: "Na kama mke wa kafiri alisilimu na mume wake alibakia katika ukafiri wake na yeye alikuwa kutokana na watu wa kitabu au wasio watu wa kitabu, basi Uislamu wake ulikuwa kabla ya kuingilia utengano utatokea, na ikiwa baada ya kuingiliana na mume alisilimu katika eda yake basi ndoa itaendelea, na kama mumewe hakusilimu basi eda yake inaanza kutokana na kusilimu kwake, na utengano hapa unazingatiwa utengano wa kuvunja ndoa na siyo utengano wa talaka kwani utengano umetokea bila ya uchaguzi wake. [Kitabu cha: Nehayat Al Muhtaaj Ila SharhiAl Minhaaj 295/6]

Na katika kitabu cha: [Al Iqnaa' na Sharhu] kwa Al Bahuitiy, miongoni mwa vitabu vya Kihambaliy: (Na mwanamke wa watu wa Kitabu akisilimu) chini ya mwanamume wa watu wa kitabu au asiye miongoni mwa watu wa kitabu, (au) alisilimu (mmoja wa mke na mume asiye wa watu wa kitabu) kama vile majusi na wapagani (kabla ya kuingiliana basi mkataba wa ndoa umebatilika) kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu} [Al Mumtahinah 10]

Na (kama mmoja wao alisilimu) yaani mke au mume, (baada ya kuingiliana basi hali inasimamia kumaliza eda, basi kama mwingine alisilimu katika eda basi ndoa itaendelea) na mwingine kama hakusilimu katika eda (basi kuvunja ndoa ilibainika tangu kusilimu mtu wa kwanza), kwani sababu ya utengano ni utofauti wa dini basi iliwajibika kuhesabu utengano kama talaka" [Kitabu cha: Kashaafu Al Qenaa' An Matn Al Iqnaa 119-120/5]

Wameitolea dalili ifuatayo:

Ya kwanza: Ni yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Shubrumah kwamba alisema: "Watu katika enzi ya Mtume S.A.W mwanamume alikuwa anasilimu kabla ya mwanamke, na mwanamke anasilimu kabla ya mwanamume basi yeyote kati yao anasilimu kabla ya kumalizika eda basi ni mke wake, na kama alisilimu baada ya kumalizika eda basi hakuna ndoa baina yao". [" [Kitabu cha: Kashaafu Al Qenaa' An Matn Al Iqnaa 119-/5]

Na ya pili: Yalitolewa kutoka kwa Az Zahriy: kwamba mke wa Swafwan Bin Umaiah alisilimu halafu Swafwan akasilimu na Mtume S.A.W. hakuwatenganishia, Ibn Shihab alisema: Na ilikuwa muda baina yao mwezi mmoja takriban, Ibn Abdulbar akasema: Ujulikano wa Hadithi hiyo una nguvu zaidi kuliko Isnaadi yake, na Ibn Shihab amesema: Umu Hakiim alisilimu na mumewe Ikrimah alitoroka kwenda Yaman, basi Umu Hakiim alihama kwake na akamwombea Uislamu basi akasilimu, na Mtume S.A.W. alijua hayo basi walibakia katika ndoa yao [Kitabu cha Al Modawana 213/2, Mughniy Al Muhataj 320/4, Kashaafu Al Qinaa' kutoka Matni ya Al Iqnaa' 119-120/5]

Na ya Tatu: Ni yaliyopokelewa kutoka kwa Al Zahriy: "Hatukuambiwa kwamba mwanamke alihama hali ya kuwa mume wake anaishi katika nchi ya kikafiri ila kuhama kwake kunatenganisha baina yake na baina ya mume wake, isipokuwa kwamba mume wake akiwa muhajiri kabla ya kutimia eda ya mtalaka wake" [Kitabu cha Al Mudawana 214/2, na Kashaafu Al Qinaa' kutoka Matni ya Al Iqnaa' +120/5]

Lakini dalili hizo majibu ni kama ifuatavyo:

Ya Kwanza: Kwani yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Shubrumah ni isnadi Muudhwalu; kwani Ibn Shubrumah mapokezi yake mengi ni kutoka kwa Taabiyna. [Ilipokelewa na Al Ghalil katika kutolea Hadithi za kitabu cha Manaru As Sabiil kwa Al Albaniy 338-339/6, Hadithi namba ya 1920]

Ya Pili: Habari ya Swafwan ilitolewa na Malik katika kitabu cha Al Muatw' [Muwatw" Malik (544/2), Hadithi Na. 1133]. Na Al Baihaqiy katika kitabu cha As Sunan Al Kubra (187/7) na hiyo ni Hadithi ya Mursal basi haipingana na Hadithi ya Al Marfuu'.

Na kadhalika habari ya Ikrima ilitolewa na Malik katika Al Muwatwa' na Al Baihaqiy katika As Sunan Al Kubra, na Hadithi hiyo ni Mursal kama ilivyoitangulia.

Ya Tatu: Na kauli ya Ibn Shihaab Al Zahriy ameitoa Malik katika Al Muwatta, Al Bayhaqiy katika Al Kubra, na Al Tahawiy alisema: "Ni Hadithi iliyokatika haisihi kuitolea hoja katika Al uswul kama ilivyotaja katika kitabu cha Muhtasari wa tofauti ya wanavyuoni".

Na kauli madhubuti ni Hadithi tuliyoitaja; "Kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake Zainabu kwa mume wake kwa ndoa ya kwanza".

Kisha kwamba uzingatio wa utengano kwa kumaliza eda walikanusha kundi miongoni mwa Wanazuoni; basi Ibn Al Hamam miongoni mwa wanazuni wa Hanafi amesema: "Hakika uzingatio wa kumaliza eda kabla ya utengano, hakuna mfano wake katika Sharia, na wala asili inayojuzu kupima juu yake. [Kitabu cha: Sharhu Fat-hu Al Qadiir kwa Ibn Al Hamam 419/3]

Na Ibn Hazm alisema: "Mmetoa wapi kwamba yanayozingatiwa katika hali ya Abi Al Aasw na hali ya Hindi na mke wa Swafwaan na wote waliosilimu ilikuwa eda? Na nani aliyewaambieni hayo? Na hakuna kitu miongoni mwa habari hizo kutaja eda, na wala ipo dalili moja. [Kitabu cha Al Mahaliy kwa Ibn Hazm 373/5]

 Na Ibn Al Qaim alisema: "Na ama kulinza wakati wa eda haina dalili katika matini na wala ujumuisho". [Zaadu Al Miaad katika Hadie Khairi Al Miaad 122/5]

Na pia alisema: "Na kiujumla urudishaji wa kumrudisha mwanamke kwa mumewe kwa kutimiza eda, kama ulikuwa huo ni sharia ambayo Mtume S.A.W., alikuja nayo, basi ulikuwa huo ulazima ubainishwe kwa watu kabla ya wakati huo kwani watu wana haja kuubainisha". [Ahkaamu Ahl Adhimah kwa Ibn Al Qayyim 662/2]. Na kadhalika alisema: wala uzingatio wa eda hauhifadhiwi mtu mmoja tu, na kauli nzuri kabisa katika suala hilo ni kauli ya Az Zohariy iliyopokelewa kutoka kwa Malik katika Kitabu cha Al Muwata' [[Ahkaamu Ahl Adhimah kwa Ibn Al Qaim 682/2].

Bali kwamba Ibn Miflih wa Madhehebu ya Hambali alitaja katika matawi kutoka kwa baadhi ya Wanavyuoni wa kihanbali kauli yao: "Hakika uharamisho wa mwanamke Muislamu kwa Kafiri uliteremka baada ya Suluhisho la Al Hudayibiya, na ulipoteremka kuharamisha, Abu Al Aasw alisilimu, basi alirudishiwa Zainabu, na hakuna kutajwa kwa eda katika Hadithi, na wala haipo athari ya eda katika kuendelea ndoa, na kadhalika pia Mtume S.A.W. hakufanya utengano katika Hadithi, na wala hakufungusha ndoa upya. [Kitabu cha: Al Fruuo' kwa Ibn Mefleh 247-248/5]

Madhehebu ya Pili: Madhehebu ya Hanafi:

Wanavyuoni wa Kihanafiy wanatofautisha baina ya Nchi ya Kiislamu na Nchi ya Kivita, na kwao hakuna tofauti baina ya mke aliyeingiliwa au asiyeingiliwa.

Basi hayo yalikuwa katika Nchi ya Kiislamu: kama mke akisilimu na mume wake ni miongoni mwa watu wa kitabu au si katika watu wa kitabu, katika hali hiyo anaelezewa Uislamu, basi akisilimu ndoa yao inaendelea, au si hivyo kadhi anawatenganisha,

Wameitolea dalili ifuatayo:

Kwanza: yalipokelewa kwamba Mwanamume mmoja kutoka Bani Taghlib, mke wake alisilimu, basi Omar R.A alimuelezea Uislamu, mwanamume huyo akakataa, basi Omar R.A akawatenganisha baina yao. Na tukio hili wamelishuhudia Masahaba R.A, na lau utengano ungetokea katika Uislamu wenyewe basi kusengekuwa na haja ya kuwatenganisha. [Kitabu cha: Bada'e Aswanae' Lil-Kasaniy 337/2]

Pili: Uislamu hauuzu kuwa ni wenye kubatilisha ndoa, kwani Uislamu unajulikana kwa kuhifadhi miliki, sasa utakuwaje ni wenye kuibatilishia! pia haijuzu kubatilisha kwa ukafiri, kwa sababu ukafiri walikuwa nao, na haukupinga kuanzisha ndoa, kwa hiyo kutokuzuia ni bora na rahisi zaidi, na aidha tofauti ya dini, sio sababu ya kubatilisha ndoa, mfano mume ni Muislamu na mke ni miongoni mwa watu wa kitabu, na kama ndoa tutaiacha iendelee baina yao basi makusudio hayapatikani; kwani makusudio ya ndoa hayapatikani isipokuwa kwa jimai, na kafiri haifai kujamiiana na mwanamke Muislamu, na mwanamume Muislamu si halali kujamiiana na mwanamke mshirikina au majusi kutokana na uchafu wao, kwa hivyo hakuna faida kubakia ndoa hii. Basi kadhi atawatenganisha baina yao katika hali ya kuukataa Uislamu, na hii ndio sababu inayolazimisha utengano. [Al Mabsuutt kwa As Sarkhasiy 45/2, Ch. Dar Al Maarifa, Badaai' Al Sanaai' kwa Al Kasaniy, 337/2]

Na ikiwa amesilimu katika nchi ya vita basi utengano baina yao unasita mpaka zimalizike hedhi tatu kama ni miongoni mwa wenye hedhi au ipite miezi mitatu, na kama mume alisilimu ndani ya muda huu basi ndoa inaendelea na ikiwa si hivyo utengano unatokea, [[Al Mabsuutt kwa As Sarkhasiy 56/5, Ch. Dar Al Maarifa, Badaai' Al Sanaai' kwa Al Kasaniy, 338/2] na muda huo sio eda; kwa kuwa humjumuisha mwanamke ambaye hajaingiliwa kama tulivyobainisha hapo juu.

Wameitolea dalili ifuatayo:

Kusilimu mmoja wao hakulazimishi utengano, wala ukafiri kwa aliyeshikilia ukafiri, na wala tofauti ya dini kama ilivyotajwa hapo juu, lakini katika Nchi ya Kiislamu inawezekana kuidhinisha sababu ya utengano kwa kadhi kumuelezea mmoja wao Uislamu, kama akikataa anawatenganisha. Na katika Nchi ya vita haitokei hiyo kwa kukosekana walii ambaye anamwita aingie katika Uislamu, basi hedhi tatu zitachukua nafasi ya miito mitatu ya kadhi katika Uislamu kwa ajili ya kuainisha sababu ya utengano, [Al Mabsuut, 56/5, na Badaai' Al Sanaai', 338/2].

Na kama mke na mume walikuwa ni miongoni mwa watu wa Nchi ya vita, na mmoja wao alisilimu, na akaenda Nchi ya Kiislamu utengano unatokea kwa sababu ya tofauti ya Nchi  mbili, [Badaai' Al Sanaai', 338/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiya].

Wameitolea dalili ifuatayo:

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mkiona kuwa wao ni Waislamu kweli basi msiwarudishe (kwao Makka) kwa makafiri. (wanawake) hawa si halali kwa hao (wanaume makafiri)}, Aya [AL MUMTAHINAH 10], Abu Bakr Al Jasas amesema: "Katika Aya hii kuna dalali nyingi za kutokea utengano kwa tofauti ya Nchi mbili baina ya mke na mume katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi msiwarudishe (kwao Makka) kwa makafiri}, na laiti kama ndoa inabaki basi mume ana haki zaidi ya kuwa na mke. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {(Wanawake) hawa si halali kwa hao (wanaume makafiri) wala wao (wanaume makafiri) si halali kwao}, na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na warudisheni (waume zao) mali zao (mahari) walizotoa}, kwa sababu amemwamrisha mke kurejesha mahari ya mume, na laiti kama ndoa inabaki basi mume hakustahiki kurudishwa mahari; kwani haijuzu kustahiki tendo la ndoa na badala yake, na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala kwenu si hatia kuwaoa, ikiwa mtawapa mahari yao}. Na kama ndoa ya kwanza inabaki basi haijuzu kuolewa, na dalili ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu}. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukataza kujizuia kumwoa kwa ajili ya mume wake wa kivita. [Ahkaamu Al Quraani kwa Al Jasas, 355-356/3],

Na pia wameleta dalili ya kisa cha wanawake waliotekwa wa Auttwaas. Kutoka kwa Abi Said Alkhudriy: "Kwamba  Mtume S.A.W siku ya Hunain alituma jeshi kwa Auttaas, basi walikutana na maadui, basi walipigana nao, Waislamu walishinda na wakateka wanawake, basi baadhi ya Masahaba wa Mtume S.A.W walijihisi kuwa na aibu kutokana na uasherati wa wanawake hao pamoja na wanaume wao miongoni mwa washirikina, basi Allah S.W. akateremsha Aya katika hali hiyo {Na pia (mmeharimishwa) wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kiume}, [AN NISAA 24], yaani wao ni halali kwenu ikimalizika eda yao". [Imepokelewa na Muslim katika kitabu cha: Sahih Muslim Hadithi Na. 1456].

Na Wanavyuoni waliafikiana kuwa inajuzu kumuingilia mwanawake mateka baada ya kutoharika hedhi au kutimia eda, na kama alikuwa na mume katika Nchi ya vita kama mume wake hakutekwa naye, basi kutokea utengano unaungana na kusilimu kwake au kwa tofauti ya Nchi mbili au kwa kutokea kumiliki juu yake, na wote waliafikiana kuwa kusilimu kwake hakulazimishi utengano hapo hapo, na imethibiti pia kwamba kutokea umiliki hakuondoi ndoa kwa dalili kuwa kijakazi ambaye ana mume kama ameunga mkono basi utengano hautokei, na pia kama mtu kafa hali ya kuwa kijakazi ana mume basi kuhama umiliki kwa mrithi inaondoa ndoa. Kwa hivyo hakuna sababu ya kutokea utengano isipokuwa tofauti ya Nchi mbili.

Basi ikisemwa: kwamba tofauti ya Nchi mbili haiwajibishi utengano; kwani kama Muislamu aliingia Nchi ya vita kwa amani haibatiliki ndoa ya mke, na kadhalika kama ataingia kwetu mtu wa Nchi ya vita kwa amani utengano haukutokei baina yake na mkewe, na kadhalika kama mume na mke Walisilimu katika Nchi ya vita kisha mmoja wao alitokea Nchi ya Kiislamu utengano haukutokei, basi tulikubali kwamba hakuna athari kwa tofauti  ya Nchi mbili katika kuwajibika utengano.

Ikisemwa: Siyo maana ya tofauti ya Nchi mbili ulizo kwenda, lakini maana ya maana ya Nchi mbili ni mmoja wao awe ni kutoka watu Nchi ya Uislamu kwa Uislamu au Dhima, na mwingine awe ni kutoka watu wa Nchi ya vita, basi anakuwa ni mpiganaji kafiri, Na kama wawili hawa ni Waislamu basi wao ni kutoka Nchi moja hata kama mmoja anaishi katika Nchi ya vita na mwingine katika Nchi ya Kiislamu.

Basi kama aliyetofautiana nasi atachukua dalili kutokana na yaliyosimuliwa na Yunus kutoka kwa Mohammad Bin Is-haq kutoka kwa Dauwd Bin Al Huswen kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake Zainabu kwa Abi Al Aas Ibn Ar Rabii' kwa Ndoa ya kwanza baada ya miaka sita. Na Zainabu alihama kwenda Madina na mume wake alibakia Makka na alikuwa mshirikina, halafu Mtume S.A.W. alimrudisha Zainabu kwa mume wake kwa Ndoa ya kwanza. Na hiyo ni dalili ya kwamba tofauti ya Nchi mbili haina athari katika kutokea utengano, basi inasemwa kwamba haisihi kuhojiana naye kwa aliyetofautiana kutokana na sura kadhaa: 

Ya kwanza: Kwamba amesema: "alimrudisha kwake baada ya miaka sita kwa ndoa ya kwanza"; kwani hakuna tofauti kati ya Wanachuoni kwamba yeye harudishwi kwenye ndoa ya kwanza baada ya kumaliza hedhi tatu, na iliyojulikana kwamba si kawaida yeye hahedhi hedhi tatu katika miaka sita, basi anaanguka mwenye hoja kwa sura hii.

Na Sura nyingine: Iliyopokelewa na Khaled kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn Abbas katika mwanamke myahudi alisilimu kabla ya mume wake na kwamba yeye alimiliki nafsi yake; basi Madhehebu yake kwamba utengano umetokea kwa Uislamu wake, na haijuzu kwamba Mtume S.A.W. Na haijuzu kwa Mtume itokee tofauti kwake.

Na Sura ya Tatu: Kwamba Amru Bin Shuaib imepokelewa kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake: kwamba Mtume S.A.W. alimrudisha binti yake Zainabu kwa Abi Al Aasw kwa ndoa ya pili basi hiyo inapingana na Hadithi ya Dawud Bin Al Haswen, na yeye pamoja na hayo ni ya afadhali; kwani Hadithi ya Ibn Abbas ikisihi basi hiyo ni kusema kwamba yeye na mkewe baada ya kusilimu, na hakujua kwa kutokea ndoa ya pili, na katika Hadithi ya Amru Bin Shuaib alisema kutokea ndoa ya pili baada ya Uislamu wake, basi hiyo ni ya afadhali; kwani kutoa habari kwa udhahiri wa hali, na ya pili ni kutoa habari  maana ya tukio ambalo ameshalijua. [Kitabu cha: Ahkaamu Al Qura'ni kwa Al Jaswas 656-657/3]

Na anazijibu dalili za waliosema utengano katika Nchi ya Kiislamu unatokea kwa kutenganishwa na kadhi endapo mume atakataa kama ifuatavyo:

Kwanza: Kisa cha mwanamume wa Taghalabiy ni kisa dhaifu, kwani wapokezi wake hawajulikani, na hakilingani na kisa kingine kilichopokelewa kutoka kwa Omar Bin Al Khataab R.A ambacho tulikitaja katika orodha ya dalili zetu.

Na taarifa ya hayo : Kisa hiki amekitoa Ibn Abi Shaibah katika kitabu cha [Al Musanaf, 4/105, Ch. Dar Al Rushd], na Al Bukhariy katika kitabu cha [Al Tareekh Al Kabeer, 4/212, Ch. Dar Al Fikr], kwa njia ya Aliy Bin Musher, pia amekitoa Altahawiy katika kitabu cha [Sharh Maani Al Athaar, 3/159, Ch. Dar Al Maairifa] kwa njia ya Muawia Al Dharir, kisha kwa njia ya Abi Yusuf Al Kadhi na wote watatu -Aliy, Muawia na Abi Yusuf- kutoka kwa Abi Is-haaq Al Shaibaniy kutoka kwa Al Safaah Bin Mattar kutoka kwa Dawud Bin Kardus, na isnadi yake ni dhaifu, kwani hali ya Dawud Bin Kardus haijulikani, pia Al Dhahabiy amesema katika kitabu cha [Al Mizaan, 2/19, Ch. Dar Al Maarifa], hakupokea kutoka kwake isipokuwa Al Safaah Bin Mattar na yeye hali yake pia haijulikani, hajulikana kwa elimu wala mapokezi, na hakupokea kutoka kwake isipokuwa watu wawili: Abu Is-haaq Al Shaibaniy na Al Awaam Bin Haushab, na wawili hawa ni waaminifu. Na mwenye sifa hii katika mapokezi basi haichukuliwi hoja kutoka kwake, lakini Hadithi yake inafaa katika ufuatiliaji na ushahidi.

Na alikipokea Ibn Abi Shaibah katika kitabu cha [Al Musanaf, 4/105] kutoka kwa Ebaad Bin Al Awaam, na Al Bukhariy katika kitabu cha [Al Tareekh Al Kabeer, 4/212] kutoka kwa Shua'bah Bin Al Hajaj, na wote kutoka kwa Al Shaibaniy kutoka kwa Yazeed Bin Alqamah.

Na Abdulrazaaq alipokea katika kitabu cha [Al Musanaf, 6/89, Ch. Al Maktab Al Islamiy] kutoka kwa Safiaa Al Thawriy kutoka kwa Al Shaibaniy, alisema aliniambia mtoto wa mwanamke ambaye Omar aliwatengansha alipomfahamisha Uislamu akakataa ........ mpaka mwisho.

Na asiyejulikana katika riwaya ya Sufiyan anashukiwa kuwa ni Yazed Bin Alqamah mwenyewe, lakini hali ya Yazed Bin Alqamah haijulikani zaidi kuliko Al Safaah, kwani Al Shaibaniy peke yake alipokea kutoka kwake, na wala hajulikani hata kidogo, na je aliwahi enzi ya Omar? Kuhusu hili kuna rai nyingi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi. [Rejea: Islaamu Al-mar-at Wabaqaau Zawjihaa Alaa Diynihi. Dr. Abdullah Al Judaii, Uk. 106], ambao ni utafiti kati ya tafiti za Jarida la Baraza la Kutoa Fatwa la Ulaya, toleo la pili, Januari 2003 / Dhul-qaada 14323 H.

Ya Pili: Kauli yenu kwamba haijuzu kwa Uislamu uwe ni wenye kubatilisha ndoa, pia haijuzu kubatilisha ukafiri, kwa sababu ukafiri walikuwa nao, na haukupinga kuanzisha ndoa, kwa hiyo kutokuzuia ni bora na rahisi zaidi. na kama ndoa tutaiacha iendelee baina yao basi makusudio hayapatikani; kwa hivyo hakuna faida kubakia ndoa hii. Basi kadhi atawatenganisha baina yao katika hali ya kuukataa Uislamu, na hii ndio sababu inayolazimisha utengano.

Tulisema Ndiyo: Uislamu haufai kuwa ni chanzo cha kubatilisha ndoa na kadhalika ukafiri kama walivyosema, lakini haulazimishi kutokuwa ndoa ni batili kuwa ni lazima, kwa sababu katika Uislamu ndoa inakuwa inajuzu baada ya kuwa ni lazima, basi inajuzu kwa kadhi kuharakisha utengano muda wa kuwa mwanamke ndiye aliyechagua hayo na amewasilisha jambo hilo kwa kadhi. Aidha inajuzu kwa mke kungojea mpaka kusilimu kwa mume wake muda wa kuwa yeye ndiye aliyechagua hayo.

Ndoa ina hali tatu: Lazima, Kuharamisha na kuvunja ndoa, kwa mfano mtu alisilimu ana mke haijuzu kufunga naye ndoa, na hali ya kujuzu na kusimamisha ndoa, na nafasi yake ni baina ya nafasi mbili haihukumiwi kwa kulazimisha ndoa wala kwa kuikatisha kiujumla, na katika hali hiyo mke atakuwa ameachika talaka baaina. Na hii ndio hali ya kisa cha Bi Zainab na Abi Al Aasw kama ilivyotangulia.

Na ndoa katika muda huo ambao mwanamke anachagua haihukumiwi kwa kubatilika wala kulazimika na kubakia kutoka kila upande, na ndio maana Amiri wa waumini Omar alimpa uhuru wa kuchagua mwanamke wa watu wa Hira ambaye alisilimu na mume wake hakusilimu kama ilivyotangulia katika orodha ya dalili zetu

Ama kauli yenu ya kwamba hakuna faida katika kubakia ndoa kwa kutopatikana makusudio yake basi rai hiyo haikubaliki, kwani kubakia inajuzu na si lazima bila ya uwezekano wa tendo la ndoa. Hayo ni manufaa kwa mke na mume duniani na akhera bila ya ufisadi, [Ahkamu Ahlu Al Dhima. kwa Ibn Al Qaim, 695/2].

Na anazijibu dalili za waliosema utengano unatokea katika Nchi ya vita dalili yao ni kumalizika kwa hedhi tatu kunakaa nafasi tatu za kadhi kufahamisha Uislamu kabla ya kutenganisha kwa sababu walii amekosekana kwa ifuatayo:

Ama kauli yenu: Kusilimu mmoja wao hakulazimishi utengano, wala ukafiri kwa aliyeshikilia ukafiri, na wala tofauti ya dini kama ilivyotajwa hapo juu katika Nchi ya Kiislamu.

Ama kauli yenu: Lakini katika Nchi ya Kiislamu inawezekana kuidhinisha sababu ya utengano kwa kadhi kumuelezea mmoja wao Uislamu, kama akikataa anawatenganisha.

Na katika Nchi ya vita haitokei hiyo kwa kukosekana walii ambaye anamwita aingie katika Uislamu, basi hedhi tatu zitachukua nafasi ya miito mitatu ya kadhi katika Uislamu kwa ajili ya kuainisha sababu ya utengano, basi jibu lake ni:

Hii ni kauli tu iliyokosa dalili, lakini kauli thabiti ni kinyume ya hayo, kama inavyobainika katika kisa cha Bibi Zainab kutoka riwaya ya Ibn Abbas R.A.

Na dalili za waliosema utengano unatokea kama mume na mke ni kutokana na Nchi ya vita, kisha mmoja wao akasilimu na akaelekea katika Nchi ya Kiislamu kwa tofauti ya Nchi mbili zinajibiwa kama ifuatayo:

Ya Kwanza: Katika Aya ya Suratu AL MUMTAHINAH hakuna kinachothibitisha hoja yao. Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mkiona kuwa wao ni Waislamu kweli basi msiwarudishe (kwao Makka) kwa makafiri], inaashiria kukataza kuwarejesha wanawake wahamao kwa ajili ya Allah S.W na Mtume wake kuwarejesha kwa makafiri kwa kuchelea kufitinishwa katika dini yao. Sasa katika hayo iko wapi hoja inayopelekea kutokea utengano hali ya kuwa mke anamngojea mume wake awe Muislamu anayehama kwa ajili ya Allah S.W. na Mtume wake kisha anarudi kwake?

Na aidha kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wao si (wake) halali kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halali kwao.}, Hii ni dalili ya kuharamisha ndoa baina ya Waislamu na makafiri, na kwamba mmoja wao si halali kwa mwingine, na hakuna sababu inayopelekea kutokea utengano, na mmoja wao anasubiri mpaka mwenzake asilimu, na anakuwa halali yake akisilimu. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na warudishieni (waume wao) mali zao (mahari) walizotoa} pia haina dalili ya kutokea utengano, kwani kumpa mume mali alizotoa ni kupendezesha mawazo yake, na mke ni haki yake kumsubiri mume mpaka asilimu, na endapo atasilimu anarejea kwake kwa ndoa ya kwanza, pia kuna tofauti katika kuwapa mahari waume; je, ni Wajibu au Sunna? Na je, ni kwa wenye ahadi tu au kwa wenye ahadi na wapiganaji vita?

Ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala kwenu si hatia kuwaoa, ikiwa mtawapa mahari yao}, basi huo ni ujumbe kwa Waislamu unaungana na yaliyopita, lengo lake ni kuondoa uzito juu yao kwa kuwaoa wanawake waumini wahamao kama walitalakiwa na mume wao na kuachwa, na hiyo ni baada ya kumalizika eda ya mwanamke na kuchagua kwake kwa nafsi yake, na bila shaka mwanamke kama eda yake ilitimia ana haki ya kuchagua kati ya kuolewa na amtakaye au kukaa hadi mume wake asilimu na arudi kwake, na ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu}, inakataza kudumu kwa ndoa ya mwanamke kafiri na kuendelea naye hali ya kuwa amebakia katika ushirikina na ukafiri wake, na hakuna ndani yake katazo la kungojea hadi mwanamke huyo asilimu.

Ya Pili: Uhakika katika kisa cha wanawake wanaotekwa katika Auttaas kwamba kilichobatilisha mkataba wa ndoa ni umiliki wa kutekwa na siyo tofauti ya Nchi.

Imamu Al Nawawiy alisema anapoielezea Hadithi hiyo: "Na muradi wa wanawake wenye waume wao hapo ni wanawake walioolewa. Na maana yake: wanawake walioolewa ni haramu kwa wasiokuwa wa waume zao isipokuwa mliomiliki miongoni mwa wanawake watekwao, basi mkataba wa ndoa wake pamoja na kafiri unavunjwa na atakuwa halali kwenu kama eda au tohara yake atatimia", [Sharh Sahihi Muslim Lil Imamu Al Nawawiy, 35/10]

Na vitabu vya sababu za kuteremsha vilieleza hayo pia, [Lubab Al Nuquul katika Asbaab Al Nuzuul Lil Al Suyuuttiy, Uk. 64,]. Kwa hivyo kiliyobatilisha mkataba wa ndoa katika hali hiyo ni umiliki wa kutekwa na siyo kila umiliki.

Na dalili za waliosema utengano unatokea kwa tofauti ya Nchi inajibiwa na Imamu Al Mawardiy kwa kauli yake katika kitabu cha [Al Haawiy Al Kabeer, 260/9, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiya]: "Na dalili ya kuwa tofauti ya Nchi mbili haipaswi kutokea utengano kwa kusilimu kwa mmoja mke au mume ni yale yaliyopokelewa kwamba Aba Sufyaan Bin Harb na Hakeem walisilimu katika mkoa wa Mar Al Dhahraan -mkoa huo ulikuwa miongoni mwa Nchi ya Kiislamu baada ya Mtume S.A.W kuingia na kuutawala, na wake zao wapo katika ukafiri mjini Makka -wakati huo ulikuwa miongonimwa Nchi ya Kiislamu - kisha wake hao wawili wakasilimu baada ya kufunguliwa Makka, basi Mtume S.A.W. aliwabakisha katika ndoa.

Na kama ilisemwa Mar Al Dhahraan ni miongoni mwa ardhi ya Makka, inafuata hukumu ya Nchi ya Kiislamu na kusilimu kwake hakukuwa ila katika Nchi moja, basi kuna majibu mawili:

Kwanza: Mar Al Dhahraan ni sehemu ya Khuza'ah iliyo mbali na utawala wa Makka; kwani Khuza'ah ilikuwa katika ahadi ya Mtume S.A.W. na Banu Bakr katika ahadi ya Makureysh, na kwa nusura ya Mtume S.A.W. Khuza'ah ikawa kwa Makureysh wa Makka.

Pili: Mar Al Dhahraan kama ilikuwa ni sehemu ya ardhi ya Makka basi inajuzu kuitawala kwa kuingia Uislamu, kama vile Waislamu wakiifungua ardhi ya nchi ya vita, ardhi hiyo inakuwa Nchi ya Kiislamu hata kama nchi hiyo ilikuwa Nchi ya vita. Dalili ya hayo ni yaliyopokelewa kuwa Mtume S.A.W alipoingia Makka mwaka wa kuiokomboa, Safwaan Bin Umaia alikimbilia Twaifu, na Ekrema Bin Abi Jahl alikimbilia mpaka pwani ya bahari na wawili hawa ni makafiri, basi wake zao walisilimu katika Makka na mke wa Safwaan ilikuwa ni Barzah Bint Masu'ud Bin Amro Al Thaqabiy na mke wa Ekremah ni Umm Hakeem Bint Al Haarith Bin Heshaam Bin Al Mughirah, na walichukua amani kutoka kwa Mtume S.A.W kwa waume wao basi Safwaan aliingia Makka kwa amani hiyo na alikaa na ukafiri wake hadi aliposhuhudia Hunain pamoja na Mtume S.A.W na alimwazima silaha kisha alisilimu, na Ekremah alirudi Makka basi akasilimu, na Mtume S.A.W aliwarudishia wake zao licha ya tofauti ya mbili baina yao, kwani Makka ilikuwa ni sehemu ya Nchi ya Uislamu kutokana na ukombozi (Ufunguzi), ama Twaifu na pwani zilikuwa sehemu za Nchi za vita. Ikisemwa: sehemu mbili hizi ni ardhi ya Makka na zipo katika utawala wake basi jawabu yake imetangulia. [Kitabu cha Al Hawee Al Kabeer 260/9]

Ama mliyoitaja kutokana na kisa cha kumrudisha Bibi Zainab Binti wa Mtume S.A.W., basi imetangulia kukijadili kwa simulizi zake mbili, pamoja na kubainisha tuliyoyachagua ikiimarisha kwa dalili na matamko ya wazungumzaji na watu wa ufundi, na itakuja baadaye kwa ubainifu zaidi kwa jambo hilo katika sehemu husika.

Na ambayo mliitaja kutokana na Madhehebu Ibn Abbas, basi athari imetolewa na Ibn Abi Shaibah akasema: Abad Bin Al Awaam akasema kutoka kwa Khalid kutoka kwa Ekrimah kutoka kwa Ibn Abbas akasema: Mwanamke mkristo akisilimu kabala ya mume wake kwamba yeye ni mmiliki wa nafsi yake mwenyewe. [Immetolewa na Ibn Abi Shaibah katika kitabu chake; Muswanaf 105/4] Basi ilikuwa kutokana na Madhehebu yake kwamba utengano unatokea kwa sababu ya Uislamu wake. Tumesema: lakini waliyoyataja hayakubaliki; kwani kauli yake: "yeye ni mmiliki wa nafsi yake" inajulisha kuwa ndoa umebatilisha kwa uteuzi wa mwanamke siyo kwa Uislamu wake.

Madhehebu ya Tatu: Madhehebu ya Adh Dhahiriyah:-

Hiyo na kauli ya Abi Thaur pia, na Abu Mohammad Bin Hazm aliisimulia kutoka kwa Omar Bin Al Khatwab, Jaber Bin Abdullahi, Abdullahi Bin Abbas, Hammad Bin Zaid, Al Hakam Bin Utaibah, Said Bin Jubiir, Omar Bin Abdulaziz, Al Hassan Al Basweriy, Udai Bin Udai na As Shoa'biy:- "Kwamba ndoa inabatilika kwa Uislamu kama mume alisilimu baada ya mkewe kwa kipindi kifupi au zaidi au hakusilimu, na hana njia yoyote kumuingilia mkewe isipokuwa kwa ndoa mpya baada ya Uislamu wake na kwa ridhaa ya mke mwenyewe. [Kitabu cha: Al Mahaliy Bil Athaar kwa Ibn Hazm 368/5]

Na anazijibu dalili za waliosema kwa dalili kadhaa:

Ya Kwanza: Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungundiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlicho kitoa, na wao watake walicho kitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayo kuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [AL MUMTAHINAH 10]

Ibn Hazm alisema: Hiyo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo haijuzu kwa yeyote kuitoka, na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliharamisha kurudisha mwanamke muamini kwa kafiri, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja kuwa ndoa yake ni halali kwa Muislamu. Basi hiyo ni kauli wazi katika kukatika kinga (Kifungo cha Ndoa) cha mwanamke kwa kusilimu kwake, na ilisihi kwamba anayesilimu anaamrishwa kuwa hashikii kinga ya mwanamke kafiri, basi ilisihi kwa wakati wa kutokea Uislamu au kubadili dini, basi kinga cha mwanamke Muislamu ilikatika kutokana na ukafiri, na kinga cha mwanamke kafiri kutokana na mwanamume Muislamu kama akisilimu mmoja wao na walikuwa makafiri mawili, au mmoja wao alibadili dini yao na wote wawili walikuwa Waislamu basi Aya hiyo iliunga kundi la dalili.

Na ya Pili: Kauli ya Mtume S.A.W.: "Muhajiri ni aliyehama yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu" Basi aliyesilimu alikuwa amehama ukafiri basi yeye ni muhajiri" [kitabu cha: Al Mahaliy Bil Athaar kwa Ibn Hazm 373-374/5, na Hadithi ilitolewa na Al Bukhariy katika sahihi yake (10), na (6119].

Na hayo yanajadiliwa kama yafuatayo:

Ya Kwanza: Aya haina yanayowajibika kuharakisha utengano, basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi msiwarudishe kwa makafiri} dalili ya kukataza kwa kuwarudisha wanawake muhajiri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake kwa makafiri, basi ipo wapi dalili ya kumlazimisha asingojee mume wake mpaka atasilimu na atahama kwa ajili ya Mwenyzi Mungu Mtukufu na Mtume wake kisha anamrudisha kwa mume wake?

Na kadhalika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini.} [AL MUMTAHINA 10] ina thibitisha uharamu baina ya Waislamu, na makafiri na kwamba mmoja wao si halali kwa mwingine, na haina kwamba mmoja wao hangojei kusilimu mwenzeye basi atakuwa halali wakisilimu wote wawili.

Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao [AL MUMTAHINA 10] Hiyo ni uhutubiaji kwa Waislamu na kuwainulia aibu kwamba wanawaoa wanawake waumini wanaohamia kama walitalakiwa kutoka kwawaume zao na wanaachwa, na hiyo itakuwa baada ya kumaliza eda ya mwanamke na kujichagulia

Hakuna shaka kwamba mwanamke kama alimaliza eda yake atahiarishwa baina ya kuolewa na mtu yeyote aliyemtaka au kungojea mpaka kusilimu mumewe, basi anamrejea kwa ndoa ya kwanza kama tuliyoafikiana nayo, 'au kwa ndoa mpya kutokana na kauli ya aliyeona kuvunja ndoa baada ya kumaliza eda moja kwa moja.

Na kama tukisema kwamba mwanamke anabakia kungojea mumewe hatumwezeshi kuolewa baada ya kumaliza eda akitaka au asitake basi ilikuwa katika Aya hoja juu yetu, na sisi hatukusema hayo na wala watu wengine kutoka Umma wa Uislamu, bali yeye ana kaki kwa nafsi yake, akitaka aolewe na akitaka angojee.

Na ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mutkufu: {Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu} [AL MUMTAHINA 10], basi kwamba iliambatana ukatazo wa kuendeleza ndoa ya mwanamke mshirikina na kumshikia katika hali ya ushiriki na ukafiri wake, na sio ukatazo wa kungojea mpaka atasilimu kisha mwanamume alimshikia kinga yake au kifungo cha ndoa.

Basi ikisemwa: mume katika kumngojea akishika kinga chake, tulisema: Hapana, bali mke anawezesha baada ya kumaliza eda yake kumtengana na kuolewa na mtu mwingine, na kama kifungo cha ndoa kilikuwa mkononi mwa mumewe basi mke hakuweza kufanya hayo. Na pia Aya iliashiria kwamba mwanamume akisilimu na mwanamke hakusilimu basi mwanamume hamshikii, bali anatengana naye, basi kama mwanamke alisilimu baada yake basi ana haki ya kumshika kwa kifungo cha ndoa yake kwani yeye alishikia kifungo cha ndoa ya mwanamke Muislamu siye mwanamke kafiri. [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Adhimah kwa Ibn Al Qaim 686-688/2]

Pili: Hadithi tukufu iliyotangulia, haina yaliyofaa kwamba mume akisilimu baada ya mke wake katika wakati wa eda yake au baada ya kuimalizia basi anahitajia mkataba mpya.

Kisha kwamba kauli hiyo ni kauli dhaifu kabisa; kwani inatofautiana na yanayojulikana na kufuatana kutokana na Sharia ya kiislamu, na kuwa inajulikana kwamba Waislamu walioingia Uislamu walikuwa wanatanguliana pamoja kutamka Shahada mbili, basi wakati fulani mwanamume alisilimu na mwanamke alibakia muda halafu atasilimu, na pia wanawake wengi kutoka Quraish na wengine walisilimu kabla ya wanaume, na wakati mwingine mwanamume anasilimu kabla ya mwanamke kisha mwanamke anasilimu baada yake kwa muda mfupi au mrefu.

Basi kama ikisemwa kuwa hiyo ni dalili inawezekana, na hiyo labda kwamba ni kabla ya uharamu wa ndoa ya mshirikina, tulisema: watu wamesilimu na waliingia dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi baada ya kuteremka uharamu wa wanawake washirikina na kuteremka ukatazo wa kushika vifungo vya ndoa vya wanawake makafiri. Basi watu walioachwa walisilimu katika Makka, na wao ni viumbe wengi, na watu wa At Twaif walisilimu, na wao ni watu wa mji, na Uislamu wao ulikuwa baada ya Mtume S.A.W. kuwazunguka, na alichukua silaha zao, na hakuzifungua, kisha aligawa ngawira za Hunain katika Ju'ranah, na alitekeleza Umra wa Al Ju'raanah, halafu alirejea na Waislamu Madina.

Kisha ujumbe wa At Twaif uliwasili na wakasilimu na wanawake wao nawengine hakusilimu, kisha walirejea na wanawake wao wakasilimu baadaye, basi aliyesema kwamba kusilimu mmoja wa mume na mke kabla ya mwingine inawajibisha kuharakisha utengano kabla ya kuingiliana au baada yake basi kauli yake inakatika kwa kosa lake. Na Mtume S.A.W. hakumuuliza mtu yeyote miongoni mwa waliosilimu je, ulimwingilia mkeo au la, bali kila mmoja aliyesilimu na mkewe akasilimu baada yake basi yeye ni mkewe bila ya upya wa ndoa.

Na jumbe za waarabu waliwasili na walikuwa wakisilimu kisha wanarejea kwa watu wao basi wanawake wao wanasilimu mikononi mwao baada ya kusilimu kwa waume zao, na Mtume S.A.W. aliwatuma Ali na Mua'az na Aba Musa kwa Yemen basi watu wengi sana wanaume na wanawake, walisilimu mikononi mwao.

Na inajulikana ukweli kwamba mwanamume alikuwa akija na anasilimu kabla ya mkewe na mwanamke akija na anasilimu kabla ya mwanamume, na wao hawakusema kwa yeyote lazima utamke na umtamkie mkeo Uislamu iwe katika wakati mmoja ili ndoa isivunjeke, na hawakutofautisha baina ya aliyeingiliana na mkewe na asiyeingiliana naye na wala hawakuainisha jambo hilo la hedhi tatu kisha ndoa itavunjika baadaye. [Kitabu cha: Ahkaam Ahlu Adhimah kwa Ibn Al Qaim 689-693/2]

 

Sura ya Tatu

Katika Uharamu wa kuingiliana Baada ya kusilimu

Lazima ifahamike kwamba kwa kusilimu mke kunasimama kujamiiana baina yake na mumewe muda wa kuwa yeye hajasilimu bado.

Na dalili ya hayo:

Kwanza: kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala haomakafiri hawahalalikii wanawake Waumini}, basi Aya hiyo ni wazi katika kukataa ndoa ya mwanamume mshirikina kwa mwanamke Muislamu.

Ya Pili: Yaliyopokelewa kwa njia ya Ayub kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn Abbas R.A. wote wawili kwa mwanamke mkristo na myahudi wakiwa chini ya mwanamume mkristo au myahudi, na mwanamke akasilimu, alisema: Uislamu unawatenganisha; Uislamu uko juu hakuna dini nyingine juu yake.(Uislamu ni Bora na hauna kifani) [Kitabu cha: Sharhu Maani Al Athar kwa At Twahawiy 257/3, Al Hafedh Ibn Hajar alisema katika kitabu cha: Fat-hu 421/9, Sanadi yake ni sahihi], Hiyo ni dalili ya kukatika Maisha ya unyumba baina yao baada ya kusilimu kwake, na Ibn Abbas alitoa sababu kwa msingi wa " Uislamu uko juu hakuna dini nyingine juu yake ".

Na athari hiyo ilipokelewa kutoka kwa Ibn Abbas, na kadhalika Hadithi ya kumrudisha Zainabu kwa ndoa ya kwanza inapokelewa naye pia, ambayo tulijengea oni letu juu yake katika suala hilo, na hakuna kupingana; kwani R.A. hakujaalia ndoa batili baada ya kusilimu kwake, lakini inabatilika kwa njia moja kutokana na njia mbili:

Ya Kwanza: Mwanamke hujichagulia utengano, endapo akisema: "Yeye amejimiliki" kama ilivyopita katika riwaya nyingine iliyotolewa  kutoka kwake Ibn Abi Shaibah.

Ya Pili: Kadhi, alipo sema: "anatenganisha kati yao" au kwa aliye na utawala wa kutenganisha.

Na yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A. kwa wote wawili, yalitiliwa mkazo kwa riwaya zingine kutoka kwake pia alisema kwamba: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtuma Mohammad S.A.W., kwa haki ili aidhihirishe dini yote, basi dini yetu ni heri zaidi kuliko dini zote, na mila yetu ni ipo juu ya mila zote, na wanaume wetu wapo juu ya wanawake wao, na wanaume wao hawatakuwa juu ya wanawake wetu. [Kitabu cha: As Sunan Al Kobra kwa Al Baihaqiy 172/7]

Ya Tatu: Al Qurtubiy amesema: Umma wameafikiana kwamba mshirikina hamwingilii mwanamke muumini kamwe kwa sababu ni aibu katika Uislamu. [Kitabu Aj Jame' La Ahkaam Al Qura'an 64/3].

Ya Nne: Haijapatikana kunukuliwa kutoka kwa Mwanachuoni au Mwanafiqhi au Mfasiri kwamba inajuzu kuendelea mahusiano ya ndoa baina ya mke Muislamu na mume kafiri, bali wote walimeafikiana kusimama Maisha ya ndoa na kuzuia na wala haijuzu mahusiano ya ndoa baina yao wote wawili baada tu ya kusilimu mke, na haijuzu tendo la ndoa isipokuwa kusilimu mume kwa haraka, au ndani ya muda wa eda, au baada yake kama tulivyoafikiana nayo, bali sisi – baada ya dalili tulizozitaja - tunauliza nani anayehalalisha hayo?. [Tunamkusudia Dkt. Abdullahi Aj Jadee']

Je, lipo suala moja lililonukuliwa kwamba mwanamke alisilimu na mumewe alibakia katik ukafiri na mahusiano ya ndoa yaliendelea baina yao? Jibu: Hapana, na kama lipo lingenukuliwa, kwani suala kama hilo lina sababu nyingi za kunukuliwa.

Hitimisho:

Na mwisho: Rai tuliyoichagua – ni rai ya Ibn Al Qayyim na Sheikh wake Ibn Taymiyyah- ina msingi mzuri kwa kuwa kusilimu mke bila ya mume wake kunazuia mahusiano ya ndoa baina yao, na ndoa husimamishwa.

Na ndoa inaposimamishwa hukumu yake ni tangu kufunga kwake, bali athari zake hasa na matokeo yote ya kisharia yanasimamishwa, yaani hayaendelei kizuizi kinatekelezeka na kunaendelea kisharia, kwa kuwa mkataba wa ndoa uliosimamishwa hauruhusu kustarehe naye hauthibitishi haki za ndoa mpaka kikwazo hicho kiondoke. [Kitabu cha: Al Madkhal Al Fiqhiy Al Aam kwa Asheikh Az Zarqa 452-453/2]

Na hii tulioichagua imenukuu rai ya Al-Sana`aniy –- katika kitabu cha: Subul As Salaam, na akazungumzia kwa kusema"Na hii ni kauli iliyo karibu zaidi kuliko kauli zote katika suala hilo" [kitabu cha: Subul As Salaam 148/1], kama ilivyonukuliwa na AS Shaukaniy katika kitabu cha: Nail Al Autwar, na akasema: "Maneno hayo ni mazuri na yenye nguvu kabisa" [kitabu cha: Nali Al Autwar 215/6]

Hitimisho: Mke akisilimu na mume wake akabakia na dini yake – sawa iwe katika Nchi za Kiislamu au Nchi za wasio Waislamu- basi ni haramu kufanya mahusiano ya ndoa baina ya mke na mume. Na mke mwenyewe amwelezee Uislamu au amuwakilishe mtu yeyote afanye hayo, endapo mume atasilimu basi wanaendelea na ndoa yao, na kama mume atabakia katika dini yake mpaka eda kumalizika, basi mke ana hiari baina ya kuomba kubatilisha mkataba wa ndoa kwa kuafikiana pamoja na mume wake au kuyafikisha hayo kwa Kadhi ili abatilishe ndoa yao, au angojee kusilimu mume wake, na anaposilimu wanaendelea katika ndoa yao. Na jambo hili ni jepesi katika Nchi za Kiislamu, kwani mke hakai pamoja na mume wake katika nyumba moja, na akiliwasilisha tu jambo hilo kwa kadhi anawatalakisha. Ama katika Nchi za wasio Waislamu ni ngumu, ikiwa mke anaweza kutokaa pamoja na mume wake katika nyumba moja basi afanye hivyo, na kama hawezi katika hali hiyo inajuzu kukaa na mume wake katika nyumba moja lakini lazima asijidhihirishe mbele ya mume, na huwenda kubatilisha mkataba kukachelewa kwa miaka mingi lakini lazima asubiri na asiolewe na mwingine hadi mkataba wa ndoa ubatilike rasmi, ili asikabiliwe na matatizo mengi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas