Kumpiga Picha Maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumpiga Picha Maiti

Question

Ni ipi hukumu ya kumpiga picha maiti?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya utangulizi huu:

Maana ya kilugha ya kupiga picha: Ni kutengeneza picha. Na picha ya kitu ni umbile maalumu la kitu hicho ambacho kinatofautiana na vitu vingine. Na katika majina yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni: Almuswawiru. Na maana yake: Ni yule aliyevipa sura viumbe vyote na kuviweka katika daraja zake, na akakipa kila kitu sura yake maalumu na umbile lake la kipekee, kwa utofauti wake na wingi wake. [Lisanu Al- Arab 473/4, kidahizo cha Swawara, Ch. Dar Swader]

Na picha ama inakuwa na umbile au haina, inakuwa na kivuli au haina, na kusudio la picha yenye umbile ni ile yenye kivuli au ya aina ya mwonekano wa pande tatu (3D), kwa maana kwamba ina umbile kwa jinsi ambavyo inakuwa na viungo vyake mbali mbali vinavyoweza kutofautika kwa kuvigusa, ukiongezea na upekee wake kwa kuitazama. Ama kwa picha isiyokuwa na umbile au kivuli ni ile iliyo bapa, au ile ambayoina mwonekano wa pande mbili tu, na viungo vyake vina upekee kwa kuitazama tu, bila ya kuigusa, kwani yenyewe haina muonekano, kama ilivyo picha iliyo katika karatasi au kitambaa au juu ya kitu chochote kinachoshikika.

Picha ya aina photograph ni uzuiaji wa kivuli tu, na inajuzu kwa kipimo cha picha ya mbele ya kioo. Picha ya mbele ya kioo na picha ya photograph ni mrejesho wa kivuli na wala hayakusudiwi kufananisha na viumbe vya Mwenyezi Mungu, bali hilo ni uhamishaji picha kama alivyoumba Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ama hadithi zilizotajwa katika kukataza kupiga picha, ni zile zinazofananishwa na viumbe wa Mwenyezi Mungu, au ni kisingizio cha kumtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kwa upande wa upigaji picha huo ni uhamishaji wa picha ambayo ameiumba Mwenyezi Mungu kwa sifa zilizoitengenezea, na kukizuia kivuli chake kwa njia za kiteknolojia. Na kwa hivyokitendo hicho hakiwi kupiga picha kwa maana iliyotajwa katika Hadithi zinazokataza kupiga picha, na hayo ni nje ya mzunguko wa uharamisho katika Hadithi hizo, na asili katika vitu ni uhalali.

Na inapendeza kwa mwoshaji kuzitaja alama nzuri na tukufuzilizojitokeza kwa maiti; kwani mambo kama hayo yanawaliwaza zaidi ndugu wa marehemu na kutaka kuiga vitendo vyake vizuri, na kumrehemu pamoja na kumwombea dua iwapo mema yake yatatajwa na vile vile kwa ajili ya kuwaidhika kwa mambo hayo. Na ni haramu kuzitaja alama mbaya alizoziona ili asijekuwaudhi ndugu wa marehemu, na ili isipelekee watu kumseng'enya maiti na kuyataja mabaya yake. Basi Al Bukhariy alipokea kutoka kwa Abi Hurairah (R.A) kutoka kwa Mtume (S.A.W)amesema kwamba: "Yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho basi na aseme mazuri au anyamaze."

Na Muslim ameitoa Hadithi kutoka kwa Abdullah Bin Omar (R.A) alisema: Mtume (S.A.W)amesema: "Na yeyote atakayemsitiri mwislamu mwenzake na Mwenyezi Mungu atamsitiri".

Na Ibn Abi Al-Dunia alipokea kutoka kwa Al Hassan (R.A) kwamba amesema: "Kwamba ni miongoni mwa uhaini kuzungumza siri ya ndugu yako"

Abu Hamid Al- Ghazaliy (Hoja ya Uislamu) alisema katika kitabu chake cha: [Ihiyaa Uluum Al-Diin132/3, Ch. Dar Al- Maarifah] "Kufichua siri ni jambo lililokatazwa kutokana na kuwa na maudhi na udhalilishaji jamaa kwa marafiki"[Ihiyaa Uluum Al-Diin 132/3, Ch. Dar Al Maarifah]

Na Al Khatwib Al-Sherbiniy alisema: "Na mwoshaji anapaswa kuwa mwaminifu, na hili ni jambo linalopendeza ili aweze kuaminika katika kukamilisha uoshaji na mambo mengine ya kisheria, na vile vile msaidizi wa mwoshaji anapaswa kuwa na sifa hizo hizo. Na iwapo maiti itaoshwa na mtu mwovu au kafiri litatokea la kutokea, na ni lazima awe na elimu kwa yale ambayo yanatakiwa kuyajua katika uoshaji wa maiti, (na iwapo ataona) mwoshaji katika mwili wa maiti (kheri) kama vile uso wa maiti kuwa mng'avu, na mwili kuwa na harufu nzuri, (basi anaweza kuyasema hayo) kwa kuwa inapendeza kufanya hivyo, ili uwe ni ulinganiaji wa kuongeza idadi ya watu wanaomswalia na kumwombea (au nyingineo), kama mfano akaona weusi au mabadiliko ya harufu au sura kugeuka (ni haramu kuyasema hayo) kwani huko ni kusengenya kwa yule ambaye hakuna uhalali unaopatikana kwa kitendo hicho. Na katika kitabu cha [Sahihi ya Muslim]: "Na yeyote atakayemsitiri mwislamu mwenzake na Mwenyezi Mungu atamsitiri". Na katika kitabu cha [Sunnan Abi Dawud na Atarmiziy]: "Yatajeni mazuri ya wafu wenu na yaacheni mabaya yao". Na katika kitabu cha [Al- Mustadrik]: "Yeyote atakaemkosha maiti na akamfichia siri zake basi Mwenyezi Mungu atamsamehe makosa yake mara arubaini". [Mughniy Al- Muhtaaj Al-Maarifat Al-Faadh Al- Minhaaj 46/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]

Al-Twahtwawiy Al-Hanafiy amesema"Wanachuoni wamesema: Muoshaji akiona kwa maiti mambo mazuri kama kugh`ara uso wake, harufu nzuri na wepesi wa kumgeuza kwenye maosheo ya maiti,inapendeza kuyasema. Na ikiwa ataona mambo ambayo yanachukiza kama harufu mbaya,uso na mwili wake kuwa mweusi au kugeuka sura yake, ni haramu kusema hayo. Pia haya yameelezwa katika sherehe ya Al-Mushkat"

Ibnu Al- Haaj Al -Malikiy alisema: "Mwoshaji wa maiti na msaidizi wake lazima wawe wafuasi wa Dini na waaminifu kwani sehemu hii inailazimu hali hiyo kwani hali ya maiti inaweza kubadilika, na jambo hili hutokea mara nyingi, na iwapo mtu yeyote atamwona anaweza kudhani kuwa mabadiliko hayo yanatokana na uovu wake, na mwoshaji akiona jambo la kheri anaweza kulitaja au kutolitaja, na akiona jambo lisilo la kheri basi lazima asitaje hata kidogo" [Al- Madkhal kwa Ibn Al- Haaj 273/3, Ch. Dar Aturaath]

Ibnu Muflih Al-Hanbaliy alisema: "Na mwoshaji analazimishwa kusitiri maovu, na siyo kudhihirisha heri, basi kutoka kwa Abu l-Aswad kutoka kwa Omar (Hadithi ina hukumu ya Marfua): Mwislamu yeyote ambaye watu wanne wamemshuhudia kuwa mtu wa kheri Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi, akasema: Tukasema: Na ikiwa watamwona watu watatu au wawili je? Akasema: Hata wakimwona wawili. Kisha sisi hatukumuuliza kuhusu mtu mmoja." Ilipokelewa na Al Bukhariy, [Al Fruu' kwa Ibn Muflih Al- Hanbaliy]

Ibnu Batwaal alisema katika Sharhu Al Bukhariy: [64/9, Ch. Dar Arushd] Wakisemacho wanazuoni ni kwamba siri yeyote haitolewi ikiwa ina madhara kwa mtu huyo, na wengi wao wamesema, kwamba mtu anapokufa hakuna uwajibu wa kuficha yale yaliyomlazimu maishani mwake isipokuwa pakiwepo juu yake madhara katika dini yake"

Ibnu Hajar alisema katika kitabu cha: [Al Fatihu 82/11, Ch. Dar Al Maarifah], "Kinachodhihirika, kugawanyika huko baada ya kifo kwa yaliyo halali, na inawezekana ikapendeza kuyataja hata kama mwenye siri atachukizwa, kwa mfano iwe ndani yake kuna kumsafisha kwa utukufu au karama na mfano wa hayo, hadi kufikia yale yanayochukiza moja kwa moja, na inaweza kuwa haramu, na hilo ndilo lililoashiriwa na Ibnu Batwaal"

Na kwamba siri za maiti ni amana lazima zihifadhiwe, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao}[AL MUUMINOON 8] Na Al- Haakim ameitoa Hadithi katika kitabu cha: [Al-Mustadrak] na akaisahihisha kutoka kwa Abi Rafi' As-Lam mtumwa wa Mtume (S.A.W) kwamba Mtume (S.A.W) alisema: "Yeyote atakayemkosha maiti na akamfichia siri zake basi Mwenyezi Mungu atamsamehe makosa yake mara arubaini". Al- Haakim aliipokea na akasema kuwa ni sahihi juu ya sharti la Muslim.

IbnuMajah, Ahmad na Atwabaraniy wamepokea katika kitabu cha: [Al Mu'jam Al Kabeer], kutoka kwa Ali, alisema: Mtume (S.A.W) amesema: "Yoyote atakaemwosha maiti, akamkafini, akamtia katika jeneza na kumbeba kisha akamtakia rehma za Mwenyezi Mungu na wala hakufichua chochote alichokiona, basi madhambi yake yatamtoka na kuwa kama siku aliyozaliwa na mama yake." Imepokewa na Ibn Majah na Ahmad katika kitabu chake: [Al -Musnad],

Na inapokuwa Sunna kukitaja alichokiona katika kheri, inakuwa Sunna pia kuzuia kivuli na picha yake kuonekana wakati wa kuwa kwake Sunna; kwa ajili ya kuleta mema kutokana wa kuwaidhika, na kheri aliyokuwa nayo hutajwa pamoja na kumrehemu na kuyazungumzia mazuri yake, kwa hiyo kuona nyuso za Mashahidi wa Jihadi walio mashujaa na wenye kubashiriwa pepo kunazifanya nafsi zetu zitamani jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Inapoharamishwa kutaja aliyoyaona ya shari, inakuwa haramu piakuweka kivuli chake na picha yake kuonekana kwa sababu ya kuepusha madhara yanayotokea kwa kuwabebesha makosa wahusika wake, au kutuka katika usengenyaji wa maiti kulikoharamishwa, au mengine kama hayo miongoni mwa madhara mengi; kwani njia hizi zina hukumu za Makusudio kama walivyoamua wanazuoni wa Fiqhi.

Al -Iz Bin Abusalam alisema: "Mazuri na mabaya yana sababu na njia zake, na njia hizo zina hukumu za makusudio kama vile Kupendeza, Uwajibu, Uharamu, Kuchukiza na Uhalali. Na ni mara chache sana njia ikawa bora zaidi kuliko Makusudio yake, kama vile yaliyozoeleka katika mema na hali mbali mbali na baadhi ya aina mbali mbali za utiifu, hizi ni bora kuliko thawabu zake, na kusaidia jambo la halali ni bora kuliko Uhalali wake; kwani usaidizi huo unawajibisha thawabu siku ya mwisho, nao ni bora na endelevu kuliko manufaa ya Uhalali. Thawabu, adhabu na makemeo ya haraka au ya kukawia hutofautiana kwa kutofautiana mara nyingi mazuri na mabaya. Na yafaa utambue kuwa ubora wa njia unategemeana na ubora wa Makusudio, na uamrishaji mema ni njia ya kuufikia wema huo, na ukatazaji wa jambo baya ni njia ya kuondosha maovu hayo, kwa hiyo amri ya kuamini ni bora kuliko amri zote, na zuio la ukafiri ni bora kuliko zuio la aina yeyote". [Qawaid Al- Ahkaam kwa Al-Iz Bin Abdusalam 43/3, Ch. Maktabat Al- Kuliat Al- Azhari]

Kisha akasema: "Malipo ya njia za utiifu yanatofautiana kwa kutofautiana ubora wa Makusudio na Mema yake, kwani njia inayopelekea Makusudio ni bora zaidi ya njia nyingine, kwa hivyo kufikia kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuijua dhati yake ni bora zaidi kuliko kuufikia ujuzi wa hukumu zake. Na kila njia inapokuwa na nguvu zaidi katika kupelekea maslahi malipo yake huwa ni makubwa zaidi kuliko ujira wa kilichopungua kutokana nacho, kwa hiyo ufikishaji wa maagizo ya Mwenyezi Mungu ni katika njia zilizo bora zaidi, kwa ajili ya kupelekea kwake katika kuleta kila jambo zuri lililolinganiwa na Mitume. Na kutoa onyo ni njia ya kuzuia maovu ya ukafiri na uasi, na utoaji wa habari njema ni njia ya kuleta maslahi ya utiifu na Imani, na pia kufundisha yale yanayolazimika kufundishwa, na kuelekeza kile kilicho wajibu kuelekezwa, hutofautiana kwa mujibu wa tofauti ya ngazi yake.

Na Aya inayoashiria kuendeleza Jihadi ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili yaNjia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendochema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema} [ATAWBAH 120].

Ukweli ni kwamba walipata thawabu kwa kiu chake na machovuna wala sio kwa kitendo chao; kwani wao ndio waliowasababishia wawili hao safari yao na juhudi zao na juu ya ukweli huo, kujiandaa kwa ajili ya Jihadi kwa kusafiri kuielekea Jihadi hiyo, na kuandaa mahitaji, silaha na farasi, ni njia ya kuelekea kwenye Jihadi ambayo pia ni njia ya kuelekea kwenye kuitukuza Dini ya Mwenyezi Mungu, na Makusudio mengine kama hayo ya Jihadi.

Kwa hiyo kusudio la kuwekwa Jihadi kwa ajili yake, njia ya kuielekea Jihadi hiyo, na sababu za Jihadi hiyo, vyote hivyo ni njia ya kuelekea katika Jihadi ambayo ndiyo njia ya kuelekea katika Makusudio hayo. Kwa hiyo maandalizi yake ni katika njia miongoni mwa njia zake. Na hii inamaanisha ubora wa kuzifikia Swala za Ijumaa na Swala za Jamaa, kauli ya Mtume (S.A.W) "Na atakayejitwaharisha nyumbani kwake kisha akaenda katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu (Msikiti wowote) kwa ajili ya kutekeleza ibada ya faradhi katika ibada za faradhi za Mwenyezi Mungu basi kila hatua zake mbili zitakuwa: Moja inafuta madhambi na nyingine inamnyanyua cheo chake" Muslim ameitoa kutokaHadithi ya Abi Hurairah. [[Qawaid Al-Ahkaam kwa Al-Iz Bin Abdusalam 124-126/1, Ch. Maktabat Al Kuliaat Al- Azhari]

Al Qarafiy Al- Malikiy alisema: " Na utambue kuwa kama ilivyo kuwa wajibu kuzuia kisingizio ni wajibu pia kukifungua, na inachukiza, inapendeza, inakuwa halali, kwani kisingizio ni njia, kama ambavyo njia ya kuelekea kilicho haramu ni haramu, kwa hiyo njia ya kuelekea jambo la wajibu ni wajibu kama vile kuharakisha kwenda msikitini kwa ajili ya swala ya Ijumaa au Hija. Na vyanzo vya hukumu vimegawanyika migawanyiko miwili: Makusudio: Nayo yanakusanya ndani yake mazuri na mabaya, na njia zake ni: Zile zinazopelekea kuyafikia, na hukumu yake ni kama hukumu ya yale yaliyofikiwa iwe ni katika kuharamisha au kuhalalisha, isipokuwa daraja lake ni la chini zaidi kuliko Makusudio kihukumu. Kwa hivyo njia ya kuelekea katika makusudio yaliyo bora zaidi ni njia zilizo bora, na kuelekea katika makusudio mabaya ni kwa njia mbaya, na katika kuelekea katika hali ya kati kwa njia ya kati, na inasisitizia juu ya kuzingatia njia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendochema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema} [ATAWBAH 120]. Na Mwenyezi Mungu akawapa thawabu kwa kiu na uchovu hata kama hawakuyafanya mawili haya, kwani yamewatokea kwa sababu ya kufikia Jihadi ambayo ni njia ya kuitukuza Dini na kuwalinda waislamu, na kwa hiyo maandalizi ni njia ya njia yenyewe. [Sharhu Tanqih Al -Fusul 506/2, Ch. Sharikat Al Twabah Al- Faniyah]

Ibn Al -Qaim alisema: "Kwa kuwa makusudio hayafikiwi kwa sababu na kwa njia zinazopelekea kuyafikia, njia na sababu zake zinayafuata nyuma na zinapata kuzingatiwa kwayo; kwani njia za yaliyoharamishwa pamoja na maasi ni katika kuyachukia kwake na kujizuia nayo kwa kiasi cha kupelekea kwake katika upeo wake na mifungamano yake kwayo. Na njia mbali mbali za utiifu na kujikurubisha kwa mapenzi yake na kupata idhini ndani yake kwa mujibu wa kupelekea kwake katika upeo wake. Kwa hiyo njia ya kinachokusudiwa hukifuata hicho kinachokusudiwa, na zote mbili zimekusudiwa kwa lengo la peo zake, nazo ni kukusudiwa kwa lengo la njia zake, na msingi wa kisheria: Kuwajibika kwa njia mbali mbali kunafuata uwajibu wa makusudio yake" [I'laam Al Muwaqaiin An Rabi Al- Alameen 108/3, Ch. Dar Al Kutub Al-Ilmiyah]

Na kumpiga picha maiti hakupingani na kumkirimu maiti kunakotakiwa kisheria, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu.} [AL ISRAA 70], Na Muslim ameitoa Hadithi katika kitabu chake: [Swahih Muslim] kutoka kwa Abi Hurairah (R.A) alisema: Mtume (S.A.W) akasema kwa mtu aliyekanyaga kaburi kwa mguu wake: "Mtu kukanya jiwe la moto likaziunguza nguo zake ni bora kwake kuliko kulikanyaga kaburi la mwislamu", Hadithi hii imetolewa na Muslim.

Na Abu Dawud alipokea kutoka kwa Aisha (R.A) alisema: Mtume (S.A.W) akasema: "Kuivunja vunja mifupa ya maiti ni kama kuivunja akiwa hai". NaMtume (S.A.W) alikataza kuketi juu ya kaburi, kukidhi haja ya mwanadamu juu yake, basi Muslim alipokea kutoka kwa Abi Marad Al-Ghunawiy (R.A) alisema: Mtume (S.A.W) akasema: "Msiketi juu ya makaburi wala msiswali juu yake".

Kwa hiyo lengo la kumkirimu maiti ni kutomdhalilisha, na jambo tunalotaka kulifanya halikusudiwi udhalilishaji wa aina yeyote, bali linakusudiwa kumkirimu, kudumisha utajo wake na kumwonea huruma pamoja na kupata mawaidha na kufuata nyayo zake kwa vitendo alivyokuwa akivifanya, hapana shaka kwamba kusudio linabeba maana ya kumheshimu mwanadamu na sio kumdhalilisha.

Yanayosemwa kuwa takwa la kumsitiri haraka maiti linaweza kupelekea zuio lisilo na mipaka la kumpiga picha, jambo hili kamwe halikubaliki, kwani sababu ya kuharakisha kumsitiri marehemu ni kuchelea kuharibika kwa mwili wake. Ambapo Abu Dawud alitoa Hadithi kutoka kwa - Huswain Bin Wahawah (R.A) kwamba Twalha Bin Al -Baraa' alipatwa na maradhi, basi Mtume (S.A.W) akaja nyumbanikwake kumsaidia, basi akasema: "Hakika mimi simuoni Twalha isipokuwa atakuwa kapatwa na umauti, niombeeni nimpate, na muharakishe, kwani haifai kwa mwili wa muislamu kufungiwa ndani kwa watu wake". Na sababu katika kupiga picha ni kumkumbuka marehemu, na kuwaidhika kwa picha hiyo, na kuona heri aliyokuwa nayo marehemu, kwa hiyo sababu katika jambo hili ni nyingine katika hilo. Hakuna kizuizi chochote cha kumpiga picha kwa kuwa kufanya hivyo hakupingani na kasi ya kumzika na kumtukuza kwa kumzika huko.

Na kutokana na hayo yaliyotangulia, Hakika kumpiga picha maiti ni jambo linalopendeza iwapo kuna heri na panahitajika kuoneshwa watu kwa ajili ya mazingatio, na kuwatia shauku katika nafsi zao kwa kuwa na mwisho mzuri kama huo. Na ni haramu kumpiga picha maiti iwapo kuna shari kwa kufanya hivyo, ili kuepuka kufichua sitara ya Mwenyezi Mungu kwa maiti huyo, kama ambavyo tunapaswa kuzingatia juu ya kuzuia kupiga picha maiti ikiwa katika kufanya hivyo kunaweza kurejesha upya huzuni. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas