Kubadilisha Maumbile kwa Lengo la K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadilisha Maumbile kwa Lengo la Kutibu Maradhi ya Utambulisho wa Kijinsia

Question

Majadiliano yamekuwa mengi katika vyombo vya habari mbali mbali kuhusu maradhi yanayoitwa (Maradhi ya utambulisho wa maumbile) na watu wengi wamejitokeza wakidai kuwa wapo katika mateso na maisha yenye tabu kwa sababu ya maradhi haya, na kuwa ufumbuzi wa kimsingi wa tatizo lao ni kufanya upasuwaji ili kubadilisha na kuwa na maumbile mengine, wakidai kuwa akili zao na roho zao zina muelekeo wa maumbile mengine lakini yalijitengeneza katika mwili kimakosa, wanauelezea upasuawaji kuwa ndiyo njia ya kusahihisha maumbile na si kubadilisha maumbile ili kuepuka tuhuma ya kuwa wamefanya kitu kisichokuwa na faida na kubadilisha aliyoyaumba Allah, wakitoa ushahidi kutumia maelezo ya baadhi ya madaktari yanayothibitisha kuwa haya maradhi hayakubali matibabu ya homoni wala hata matibabu ya kisaikolojia, bali pia hakuna tiba hadi sasa iliyopatikana isipokuwa kubadilisha maumbile. Je, yanazingatiwa maradhi haya kuwa ni udhuru wa kisheria unaomruhusu mtu kufanyiwa upasuwaji wa kubadilisha?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya utangulizi huu:

Maradhi ya utambulisho wa jinsia au kama yanavyoitwa kwa lugha ya kiingereza: (Gender identity disorder) na hufahamika pia kwa kifupi kama (GID) ambao ni uchunguzi unaofanywa na madaktari na wataalamu wa saikolojia juu watu ambao wanasumbuliwa na hali ya kutoridhishwa au wasiwasi juu ya aina ya maumbile waliyozaliwa nayo, na hutambulika kama vipipo vya kisaikolojia, vinavyoelezea matatizo yanayohusiana na mabadiliko ya kimaumbile na utambulisho wa mabadiliko ya kimaumbile na kufanana na maumbile mengine, na haya maradhi ya kisaikolojia kwa kifupi yanamaanisha kuwa akute mgonjwa katika nafsi yake hisia bila yeye kukusudia kuwa yeye anamuelekeo wa maumbile mengine pamoja na kuwa yeye kakamilika umbile la kimwili na usalama wa viungo vyake vya uzazi.

Na neno (Gender): Ni neno la kiingereza linatokana na asili ya kilatini, na maana yake kilugha ni: Jinsi/Jinsia kwa mwanaume na mwanamke, na hutumika katika kuainisha majina, viwakilishi na sifa.
Na Shirika la Afya Duniani (W.H.O) linauelezea msamiati huu kuwa: Ni sifa anazozibeba mwanaume na mwanamke kama sifa za kijamii zilizounganishwa hazina mahusiano ya tofauti za kimaumbile. Na Ensaiklopedia ya Uingereza ina uelezea kuwa: Ni hisia za binadamu yeye mwenyewe kama mwanaume au mwanamke, na kisha ikiwa kama mwanaume atafanya kazi za mwanamke, au mwanamke akafanya kazi za mwanaume, hakika hapatakuwepo mwanamke au mwanaume, bali patakuwepo na (aina) yaani (Gender), na hii inamaanisha kwamba tofauti ya mwanamke na mwanaume kibaiolojia haina mahusiano ya kuchagua harakati za kinjisia anazozifanya kila mmoja wao, na hapa panakuwa na wito wa wazi wa kuwepo ushoga, ikimaanisha pia mwanaume kufanya kazi za mwanamke, na mwanamke kufanya kazi za mwanaume; Kwa kuwa kazi hizi ni maalumu kwa kila mmoja zimepangwa na jamii, na wala hazikupangwa na asili ya kiume au ya kike kama wanavyodai, na hii inamaanisha pia ni kuvunja familia ambayo ndiyo kiini cha jamii zote na bila hivyo jamii huharibika.

Ukweli ni kwamba mwanadamu ni kiumbe maskini na dhaifu, muda wote anategemea kuwepo kwake na mambo ya maisha yake kutoka kwa Muumba wake ambaye amemleta katika hii dunia, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (S.A.W) wameamrisha kudhihirisha ukweli wa mwanadamu na ukweli wa yale anayoyamiliki akisema: {Na mwanadamu ameumbwa ni dhaifu}[AN-NISAAI: 28], {Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu} [YUNUS:49]. Akasema tena Mwenyezi Mungu: {Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa. Akitaka atakuondoeni na alete viumbe vipya. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu} [FAAT'IR:15-17], mwanadamu anaweza yeye mwenyewe kuwa na miliki ya kweli akitoa tuhuma za wajinga waliopumbazwa tofauti na ukweli wa mambo, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na dhara inapo mgusa mtu hutuomba. Kisha tunapo mpa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu. Sio! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui!}[AZZUMAR: 49]. Na amepokea Al Tirmidhiy katika kitabu chake kutoka kwa Abi Barzat Al aslamiy (R.A) alisema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W): “Hauta nyanyuka unyayo wa mwanadamu siku ya Qiyamah mpaka aulizwe kuhusu umri wake ni vipi kaumaliza, na elimu yake kaifanyia nini, na kuhusu mali yake ni wapi kaipata na vipi kaitumia na mwili wake ni vipi kautumia”. Na katika Sahihi Bukhari na Muslim kutoka kwa Abdillahi Bin Amru (R.A) kuwa Mtume (S.A.W) alisema kumwambia: “Hakika mwili wako una haki juu yako, na jicho lako lina haki juu yako, na mke wako anahaki juu yako”.

Matini hizi za kisheria zikajulisha kuwa mwanadamu hamiliki kiwiliwili chake umiliki wa kweli, kwa kuwa ataulizwa kuhusu kiwiliwili hicho mbele ya Allah Mtukufu, na analipwa kwa vitendo vyake na yale aliyoyachuma au kuyafanya katika kudhulumu haki zake mwenyewe na mwili wake, wakati ambapo Mmiliki wa kweli haulizwi na wala halipwi kwa aliyoyafanya kwenye milki yake, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu} {AL I’MRAAN: 26}. Akasema tena: {Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo}[ANBIYAA: 23]. Kama inavyofahamika kuhesabiwa mwanadamu katika mali zake –Kazipata wapi na kazitumia katika nini- Ni kuwa inajulisha kwamba hazimiliki milki ya kweli inakuwa ruhusa kwake kuwa na uhuru wa matumizi ya moja kwa moja, na hivyo hivyo inajulisha kuhesabiwa kwake katika mwili wake kautumia katika mambo gani.

Anasema Ibn Al Haj Al Maalikiy katika [Elmadkhal, 1/132, chapa, Dar- Elturath]: “Ikiwa kwa mwanadamu anaweza kuitumia mali yake lakini matumizi haya siyo kamili kwa kuwa kazuwiwa au kukatazwa katika mali hiyo; Kwa sababu haimiliki miliki kamili; Na kwa kuwa kahalalishiwa kuzitumia katika sehemu na kuzuwiwa kuzitumia katika sehemu zingine, mali kiukweli sio yake, lakini ipo mikononi mwake kwa njia ya kuazima ikiwa ni wajibu kwake aitumie katika jambo fulani na asiitumie katika jambo fulani, na haya ndiyo yaliyobainishwa na matini za Quraani na Hadithi”.

Kwa msingi huu mwanadamu hana haki ya kufanya kitu katika viungo vya mwili wake isipokuwa ndani ya mipaka iliyobainishwa na sheria ya kiislamu na kuhalalisha kwa matini maaluumu au matini yeyote ile. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu} [MUUMINUN: 115-116]. Mwanadamu hakuumbwa kwa mchezo na wala hataachwa burebure bila maamrisho, makatazo wala bila kuhesabiwa, hakika yeye ni mja aliyepewa majukumu katika maisha kwa kufanya kazi maalumu atakazozifanya na atalipwa au kuadhibiwa kwa mujibu wa alichokifanya, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda}[TAWBA :105].

Kuhusu swala la kuingilia upasuaji katika viungo vya uzazi vya mwanadamu, asili yake ni kuzuwiwa isipokuwa kwa dharura au shida itakayokuwa katika kiwango cha dharura, kwa kuwa sheria ya kiislamu imeharamisha kuhasiwa na iliyoko katika maana yake kwa kuwa ni kubadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Allah Mtukufu: {Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shet'ani aliye asi. Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako. Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amepata hasara ya wazi} [ANNISAA: 117-119].

Quraani tukufu inabainisha kuwa kubadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni haramu; kwa kuwa ni kutekeleza amri ya shetani na wafuasi wake kinyume na Allah na ni hasara kubwa. Na kuhasiwa na mfano wake ni kubadilisha uumbaji wa Allah, na kukiuka maumbile yake aliyowaumbia watu juu yake nayo ni haramu, na imekuja katika tafsiri ya Ibn Abbas na Anas Bin Maalik (R.A) na pia kwa wengineo miongoni mwa watu wema, kuwa makusidio ya kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu uliopokelewa katika aya tukufu: Ni “Kuhasiwa”. [tazama: tafsiri ya Imam Tabary, Jaamii El bayaan, 9/215-216, chapa, Muassasatu Al Risalah], lakini ikiwa katika upasuaji kuna kukata au patakatwa baadhi ya viungo vya mwili kwa lengo la kumbakisha katika uhai kwa mfano au kwa ajili ya manufaa ya viungo vingine, kanuni inasema “Dharura huhalalisha makatazo/haramu, yatakapopingana mambo mabaya mawili litaangaliwa lenye madhara makubwa kwa kufanya jepesi lake kimadhara [Tazama: Al-Ashbaah wannadhaair lil –Suyutiy, uk. 84,87, chapa, Dar-Al kutub al -Almiyah].

Na maradhi ya utambulisho wa maumbile kwa baadhi ya watu ni tatizo linalofahamika tokea zama za kale zilizoutangulia uislamu, lakini maana ni kukusanyika kwa mtu mmoja alama na viashirio vya kimaumbile na tabia za kiume na za kike pamoja na kutofautiana uwiano wa hayo kati ya mgonjwa mmoja na mwingine, isipokuwa tatizo hili lina hali mbili: Linaweza kuwa kweli ni tatizo hakuna mwingiliano wa mapenzi ya mtu ndani yake, na linaweza kuwa la kutengenezwa kwa hiari yake, na kila hali moja katika hizo ina hukumu na tiba. Huitwa aliyepewa mtihani wa maradhi haya kuwa ni (Huntha kama maradhi ni ya kimwili na maumbile akawa na kiungo cha uzazi cha kike au cha kiume, basi kama patakuwepo na utata na jambo likawa ni lenye kuchanganya hakuweza kufahamu ni ipi asili na ni kipi kilichozidi huitwa: (Uhuntha usiobainisha yuko katika jinsia gani) na pia akiwa hana kiungo kabisa.

Na wanachuoni wameeleza kwamba kuwa na nguvu jinsia ya Huntha isiyofahamika aina yake kwa muelekeo wa kindani hauzingatiwi isipokuwa katika hali mbili; Ya kwanza: Kushindwa kuonekana alama zilizo wazi, na ya pili: Atakapokuwa hana utupu wa kiume kwa mwanaume au hana utupu wa kike kwa mwanamke, na tofauti na hali mbili hizo haifai kumpatia jinsia yeyote ile kwa mujibu wa muelekeo wa ndani au kwa yale yanayoelezewa siku hizi kama hisia za ndani kuwa roho yake inamuelekeo wa jinsia au maumbile mengine [Tazama: Raudat Al -Taalibiyna linnawawiy, 1/79, chapa, Al-Maktab Al-Islamiy].

Imekuja katika (Al-Ashabah wa Al-Nadhair) ya Assuyuti (uk. 241-242): Imam Nawawiy amesema: Huntha ana aina mbili: Mwenye utupu wa mwanamke, na utupu wa mwanaume. Na aina nyingine hana moja kati ya hivyo. Bali ana tundu analotolea vitu vinavyotoka nje, na wala halifanani na tupu moja kati ya hizo, aina ya kwanza: Atafahamika kwa jambo moja: Mkojo, akikojoa kwa utupu wa kiume tu: Basi ni mwanaume, au kwa utupu wa mwanamke: Basi ni mwanamke, au (Akikojoa) kwa vyote viwili itazingatiwa kwa yaliyopita, (Katika hukumu) ikiwa kama zikakata (Mkojo) kwa pamoja. Na kwa kuchelewa, ikiwa kama zitaanza kwa pamoja, ikitangulia moja, na kuchelewa ya pili: yanazingatiwa yaliyopita (Katika hukumu, vikikubaliana vyote viwili basi kwa usahihi hakuna dalili, na wala haitazamwi kwa kuzidi mkojo kwa njia moja wapo.

Aina ya pili na ya tatu: Kutoka manii na hedhi wakati ufikapo wa kuweza kutoa. Ikiwa atatoka manii kwa uume, basi ni mwanaume, au kwa uke au hedhi, basi ni mwanamke. Kwa sharti la kujirudia kutoka kwake ili kuhakikisha dhana yake kwayo, wala asidhanie kuwa kwake ni makubaliano. Hivyo ndivyo walivyojuzisha Masheikh wawili. Anasema Al-Asnawiy: Na kunyamaza kwao kwa hilo katika mkojo yahitaji kutoshurutisha ndani yake. Na mwelekeo: Ni kulingana yote katika hayo, akasema: Ama idadi inayozingatiwa katika kujirudia basi mwelekeo wenye kukubalika, ni kukutanisha (Hukumu) katika yale yaliyosemwa katika mbwa muwindaji: Iwe ndiyo ada yake. Akitokwa manii kwa vyote viwili, sahihi ni kuwa itatolewa dalili kwayo, akitokwa na manii nusu yakawa ni ya mwanaume, basi ni mwanaume au nusu yake ikawa ni ya mwanamke, basi ni mwanamke, akitokwa na manii katika utupu wa kiume nusu yake ikawa ni manii yao na katika utupu wa kike nusu yake ni manii yao, au katika utupu wa kike nusu yake yakawa ni manii ya kiume, au kinyume chake, hakuna dalili, na hivyo hivyo vitakapopingana mkojo na hedhi, au manii kwa mfano akakojoa kwa utupu wa kiume, na akatokwa na hedhi au akatokwa na manii kwa utupu wa kike. Na pia katika usahihi vitakapopingana au kutofautiana manii na hedhi. Ya nne: Kuzaa. Na hilo moja kwa moja hujulisha uwanamke wake, na hutangulizwa mbele ya alama zote zenye kupingana nayo. Katika sherehe Al-Muhadhab amesema: Laiti akitoa pande la nyama Al-Qawabil akasema: Kuwa ndiyo mwanzo wa kuumbwa mwanadamu: Itahukumiwa kwalo. Na kama watatilia mashaka basi shaka hiyo itadumu. Akasema laiti litavimba tumbo lake, na zikadhihiri alama za ujauzito: Haitahukumiwa kuwa kwake ni mwanamke, mpaka pale itakapothibiti mimba. Amesema Al-Asnawiy: Na sahihi ni kutosheka kwa kudhihiri dalili amejuzisha hivyo Al Raafiiy mwisho wa maneno ya Huntha. Na akamfuata katika (Hukumu hiyo) Al- Raudhwah. Na hivyo hivyo katika Sherehe ya Al-Muhadhab katika maudhui nyingine nayo inakubaliana na maudhi inayoendelea kupitia kanuni iliyotajwa katika kujibu yanayohusiana na kasoro, na kuharamisha talaka, na mtalikiwa kustahiki matumizi na mengineyo.

Ya tano: Kukosekana hedhi katika muda wake ni alama ya uwanamume, hutumiwa kama dalili inapokwenda sawa au kulingana katika mkojo, ameinukuu Al-Asnawiy kutoka kwa Al-Mawridiy, alisema: Nayo ni mambo mazuri na marachache kutokea mtu kupatwa na hayo.

Ya saba: kumili, na hutolewa dalili ya kushindwa kwa alama zilizopita, kumili huko hutangulizwa, akimili kwa mwanaume basi ni mwanamke, au akimili kwa mwanamke basi ni mwanaume, ikiwa atasema: Hizo mbili ni kumili kwa namna moja, na wala simili kwa moja kati ya hizo, basi atakuwa Khuntha wa kuchanganya (asiyekuwa na dalili ya wazi). Ya Nane: kuonekana ushujaa, ushujaa wa kupanda farasi, kuvumilia katika kupambana na adui, kama alivyoeleza Al-Asnawiy akimfuata Ibn Al- Musallam. Ya Tisa hadi kumi na mbili: Kuota ndevu, kutoka matiti, kushuka maziwa na kutofautina katika uso. Na sahihi ni kwamba hakuna dalili katika hayo. Na ama aina ya pili – Ambaye hana utupu wa mwaume wala utupu wa kike- katika sherehe ya Al- Muhadhab kutoka kwa Albaghawiy: Kuwa haibainiki isipokuwa kwa kumili. Al-Asnawiy amesema: Hubainika pia kwa manii yenye kusifika kwa moja ya aina mbili, kuwa hakuna kizuwizi. Ama hedhi akasema: "Huelekea kuzingatiwa kwake pia, na kunauwezekano wa kutofautina pia; kwa kuwa damu hailazimu kuwa ni hedhi, na ikiwa ni kwa sifa ya hedhi, kwa kujuzu kuwa inawezekana ikawa ni damu ya ugonjwa au iliyoharibika tofauti na manii" mwisho.

Ama ukiwa ugonjwa wa kuja wenyewe na wenye kufanana hivyo, na wenye kupingana na tabia, maneno na harakati, mwenye kupatwa na maradhi hayo huitwa Mukhanatha (mwenye kufanana na mwanamke) akiwa ni mwanaume, na dume akiwa ni mwanamke, mgonjwa huyu hana adhabu wala kulaumiwa isipokuwa atakapokuwa na uwezo wa kuuondoa ugonjwa huo na hakufanya hivyo.

Ama mwenye kujifanya kuwa na maradhi haya na kuwa afanane na jinsia au maumbile mengine, akiwa ni mwanaume huitwa (mwenye kujifananisha na mwanamke), na imesemwa pia (kwa kasra chini ya nuni), na akiwa ni mwanamke huitwa ni dume (mwenye kujifananisha na wanaume), na katika Hadidhi tukufu iliyotolewa na Imamu Al Bukhariy katika kitabu chake kutoka kwa Ibn Abbas, alisema: Mtume (S.A.W) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume, akasema: (Watoweni ndani ya majumba yenu), akasema: Mtume (S.A.W) akamtoa fulani na Umar (R.A) akamtoa fulani. (Al Bukhariy). Katika riwaya nyingine au mapokezi mengine katika Hadithi yanabainisha kuwa makusudio ya (wanaojifananisha na wanawake au wanaume) ni wanaojifananisha na maumbile ya jinsia nyingine kwa kujifanya na kujitengeneza na kwa kutaka, imekuja ndani yake: “Mtume (S.A.W) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume”.

Anasema Al- Hafidh Ibn Hajar katika [Fat-hi Al- Baary, 10/332, chapa, Dar Al-Ma’rifah]: “Amesema Al- Tabariy: Maana yake haifai kwa mwanaume kujifananisha na mwanamke kimavazi na mapambo yanayomuhusu mwanamke wala kinyume chake. Nikasema: Na hivyo hivyo katika maneno na kutembea ama muundo wa mavazi hutofautina kutokana na kutofautiana desturi za kila mji huenda watu hawatofautishi vazi la wanawake wao kutokana na vazi la wanaume wao lakini mwanamke akawa anasifika kwa kujisitiri, ama kukemea kujifananisha katika maneno na kutembea huhusiana na anayefanya hivyo kwa makusudi, ama atakayekuwa hivyo kutokana na asili ya maumbile yake basi huamrishwa kujilazimisha kuacha na kudumu kujifundisha kwa hatua na ikiwa hakufanya hivyo na akang’ang’ania basi kemeo hili humuhusu na hasa pale itakapo onekana kwake yanayojulisha kuridhika kwake, na imechukuliwa(Hukumu) hii kutoka na tamko la “Wenye kujifananisha” Ama kuacha huru kama walivyoacha huru (jambo hili) mfano wa Al-Nawawiy ya kuwa mwenye kujifananisha kimaumbile (mwenye kupenda jinsia mbili) halaumiwi ni kwamba imechukuliwa ikiwa kama hataweza kuacha maringo katika kutembea na kuongea baada ya kumpa dawa ya kuacha hayo na kama si hivyo pale itakapokuwa kuacha ni jambo lenye kuwezekana hata kwa awamu kuacha kwake bila udhuru kutamfanya alaumiwe” mwisho.

Magonjwa ya kujitakia ni kupotoka kitabia yanahitaji kukemewa na kuonywa na kurejea kumuandaa upya aliyekengeuka, ugonjwa utakapopindukia katika hali ya kujitakia na kufanana na jinsia nyingine hadi kufikia kufanya upasuwaji kwa ajili ya kufanana na jinsia ya maumbile mengine, kitendo hiki ni uhalifu na wala haifai kutaka kufanya hivyo na ni kitendo kinachostahiki adhabu; kwa kuwa ni kubadili uumbaji wa Allah na kupinga neema zake na kuichafua na kuidhuru nafsi jambo ambalo halijuzu kisheria, na husemwa kwa hili mfano wa yale waliyoyasema wanachuoni katika upasuwaji wa kujihasi na mfano wa hayo.

Anasema Al Hafidh Ibn Hajar katika [Fat-Hi Al-Bariy, 9/119]: “kauli yake: (Akatukataza hayo) - Yaani kuhusu kujihasi- Ni katazo la kuharamisha bila tofauti yoyote kwa mwanadamu kwa mujibu wa yaliyopita, na ndani yake pia kuna maovu ya kuadhibu nafsi na kuichafua pamoja na kuiingizia madhara ambayo hupelekea kuangamia, na ndani yake pia kuna kubatilisha maana ya uanaume na kubadilisha uumbaji wa Allah na kukufuru neema; kwa kuwa mtu kuumbwa mwanaume ni katika neema kubwa atakapoiondoa neema hiyo atakuwa kajifananisha na mwanamke na kuchagua upungufu badala ya ukamilifu” mwisho.

Na Al-Imam Al Qurtubiyanasema katika tafsiri yake [Al-Jaamiu Liahkaam Al Quraani, 5/391, chapa. Dar el shaab]: “Ama kujihasi kwa mwanadamu ni msiba mkubwa akiwa atajihasi basi moyo wake utabatilika pamoja na nguvu zake kinyume cha wanyama na kizazi na kukatika kizazi chake alichoamrishwa katika kauli yake Mtume: “Owaneni mzaliane hakika mimi nitajigamba kwenu nyinyi kwa kuwa na umma wenye watu wengi”, na pia ndani yake kuna maumivu makali huenda yakampelekea kuangamia, kuna kuwa ndani yake kupoteza mali na kuipoteza nafsi na yote hayo yamekatazwa, kisha kukata viungo Mtume kakataza, na ni katika (Hadithi) sahihi, na kundi kubwa la wanachuoni wa Hijazi na Kufah wametaja hiyo kuwa ni Mtume S.A.W. amekataza kununua mtu anayehasiwa kutoka Al Swaqaliyah na wengineo wakasema: Ikiwa kama hawatanunua kwao hawatajifanya makhuntha, na hawakutofautiana kuwa kuhasiwa kwa mwanadamu si halal na wala haifai kwa kuwa ni kukata viungo na kubadilisha uumbaji wa Allah na pia kukata viungo vyao vingine, Abu Umar aliyasema” Mwisho.

Ama matatizo ya kutojitakia ni mtihani wa kimaradhi unaohitaji kutibiwa na kuchunga katika kuutibu kwake kufuatilia kwa makini alama za kiume na za kike kiviungo linaamulika umbile la mgonjwa kwa mujibu wa hayo, wakati huo sasa inafaa kufanya upasuwaji na yale yanayohitajika katika matibabu baada ya kupanga utambulisho wa kimaumbile ili kudhihirisha utambulisho halisi au wa kweli, na kuondoa sehemu za viungo na athari za kisaiokolojia zilizosababisha ugonjwa wa utambulisho wa jinsia kwa mgonjwa; kwa kuwa kanuni ya kisheria inasema (Tatizo huondolewa), na hakuna shaka kwamba huku kufanana na mkanganyiko ni madhara, kuondolewa kwake ni wajibu kwa kiasi iwezekanavyo, kwa kuwa kuliacha pamoja na uwezekano wa kuliondoa humuingiza muhusika katika dhambi ya kujifananisha na jinsia nyingie inayomuwajibisha kupata laana.

Kwa mujibu wa yaliyopita, haifai kufanya upasuwaji unaoitwa: kugeuza au kubadili au kusahihisha jinsia isipokuwa kwa huntha ambaye vimekusanyika kwake viungo vya mwili vinavyomuhusu mwanaume na mwanamke (kama viungo vya uzazi kwa mfano), kama ambavyo imefahamika kuwa haifai kisheria kumtegemea (Huntha asiyebainika yuko katika jinsia gani) katika kupanga utambulisho wa jinsia kwa kutegemea tabia zake na muonekano wake au mwelekeo wake isipokuwa katika hali mbili:

Ya kwanza: Inaposhindikana kupanga kulingana na ishara za kimwili zilizo tajwa.
Pili: Atakapokuwa hana utupu wa kiume na wala hana utupu wa kike, na tofauti na hali hizo mbili haifai kumuingiza au kumpa jinsia yeyote ile kati ya jinsia mbili kulingana na mwelekeo wake wa moyoni au kwa kile kinachoitwa leo hii kama hisia za ndani kuwa roho yake inamili kwenye jinsia nyingine. Pamoja na hayo, hakika kushindwa kwa madaktari wa kimagharibi na wafuasi wao katika mataifa ya mashariki katika kuwatibu wale wanaowaita wagonjwa wa (maradhi ya utambulisho wa kimaumbilie) haihitaji kukiri moja kwa moja kuwa hawana matibabu isipokuwa kuwafanyia upasuwaji na kubadili ubinadamu wao, vipi laiti ingalikuwa kuufahamu Uislamu na kufuata sheria zake na adabu zake inazingatiwa ndiyo nguzo kuu katika kuwatibu wagonjwa wanaohitaji matibabu ya kweli, na sio wale wanaofuata matamanio ya shetani yasiyokuwa ya kawaida, na wanataka kukiri usheria au uhalali wa uhalifu wao dhidi ya haki za nafsi zao na uanadamu wao na katika haki za Muumbaji mtukufu, na vyovyote atakavyofanya mwenye kujibadilisha kwa kufanya upasuwaji kisura kwenda jinsia nyingine hawezi kubadilika kisheria, na wala hawezi kupewa haki za kimaadili na kihisia isipokuwa zile zinazonasibiana na uhalisia wake kabla ya kufanya mabadiliko na uharibifu alioufanya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kujua zaidi.

Share this:

Related Fatwas