Ahadi ya utii kwa mtu ambaye utambulisho wake haujulikani.
Question
Je, inawezekana kuweka ahadi ya utii kwa mtu ambaye utambulisho wake haujulikani?
Answer
Imekubaliwa kuwa utiifu kwa mtu asiyejulikana si halali kisheria na haukubaliki hata kidogo, basi iweje watu wakabidhi mambo yao kwa mtu ambaye hawamjui na hawajui utambulisho wake, na hiyo ndio hali ya kiongozi wa Daishi - asiyejulikana - ambaye wafuasi wake hawamjui na hawajui chochote juu yake; Matokeo yake, ahadi hiyo inavurugika kwa sababu walikuwa hawamjui.
Hakika ahadi ya utii katika Uislamu ni jambo la halali lililoamrishwa, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) alilifanya katika ahadi ya kwanza na ya pili ya Al-Aqaba na ahadi ya Ar-Ridhwan. Na ahadi ya utii ni mapatano, nayo ni kwa kuchagua kwa wenye mamlaka, kwa kusikia na kutii bila ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
Ahadi ya utii ina umuhimu mkubwa kwa sababu ya kile kinachohusika katika kusimamia mambo ya watu na siasa za nchi, kuepusha madhara na kuleta maslahi ya kidunia na kidini. Kwa hivyo, moja ya masharti muhimu ambayo lazima yatimizwe na Imamu ni kuwa mwadilifu, anayetimiza masharti ya uadilifu kamili, na anayejulikana kwa watu kwa hali yake, uadilifu, wasifu, na yeye ni nani, mpaka kushika uongozi na kukabidhi hatamu za serikali. Ni lazima watu waweke ahadi ya utii kwake huku wakijua vyema mambo yake, asili yake, hali yake, na nasaba yake. La sivyo, ingekuwa ahadi hiyo ni ujinga ambayo ingebatilishwa, basi iweje watu waweke utii kwa mtu wasiyemjua na wasioijua hali yake?