Hatua za kuchukua katika deni ambalo mdai hajulikani
Question
Baba yangu aliniambia kabla ya kifo chake kwamba yeye anadaiwa na mtu mmoja, na nimetafuta huyo mtu sikumpata, je kunajuzu kwangu kutumia mali hii?
Answer
Asili ya deni hili linalipwa kwa mali aliyoiacha mzazi wako, litalipwa deni kabla ya kugawa mirathi, na mnawajibika kujitahidi ili kumpata mdai au warithi wake, kama hamkuwapata basi mali hiyo ni warithi mpaka atakapopatikana mdai watamlipa kila mtu kwa fungu alilolichukua, kwa sababu gharama na hasara kwa anayemiliki, wala haizuiliwi kisharia warithi wa deni hili kuliingiza katika fungu lako la urithi, kwa maana utalilipa peke yako atakapopatikana mdai na kutaka mali yake, ikiwa hakupatikana na ukapita muda mrefu kwa namna hakuna anayedhania kuwa atapatikana mdai, basi bora zaidi mali hiyo kuitoa sadaka.