Mazungumzo ni Bora Zaidi Kuliko Map...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mazungumzo ni Bora Zaidi Kuliko Mapambano ya Kimaoni

Question

Ni nini mwelekeo sahihi kuhusu suala la mapambano ya kistaarabu? Na vipi kuhusu kauli isemayo kwamba Uislamu haujui mazungumzo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1. Katika njia ya kusahihisha sura ya Uislamu na Waislamu, ujumbe wa ngazi ya juu wa Maulamaa uliwahi kwenda Uingereza kujaribu kufungua milango ya mazungumzo kuhusu mambo yanayoambatana na Mashariki na Magharibi ili iwe hatua ya kwanza katika kupunguza tatizo la mapambano, pamoja na kuweka mikakati ya ushirikiano wenye faida.Mapambano hayana manufaa kwa waarabu na wala kwa Waislamu bali hata kwa viumbe wote kwa ujumla. Na wale wanaotoa wito wa mapambano, hakika wanatoa wito wauharibifu katika ardhi, na baadhi yao wanadhani au wanakuwa na itikadi isiyo legalega kwamba mapambano lazima yawepo kwa hivyo wanakwenda na hali ilivyo bila ya kutoa witowa kueneza. Jambo hilo kwetu sisi waislamu halipo hivyo, mapambano ya kimaoni yapo lakini si jambo muhimu na sio msingi wa uhusiano kati ya mwanadamu na ulimwengu, wala kati ya mwanadamu na mwenzake, bali uhusiano ni ushirikiano, kusaidiana na kufahamiana.Mufti wa Misri Prof. Aliy Jumaa alikuwa mmojawapo wa wajumbe wa ujumbe huo ambapo Waziri wa Wakfu alifanya juhudi kubwa kuuandaa kwa kushirikiana na Wizara ya mambo ya nje ya Misri.
2. Huko,ujumbe huo ulijaribu kuangalia zaidi akili ya kimagharibi na kwa nini ina khofu na matatizo katika mawasiliano yake na Uislamu na Waislamu kwa uwazi licha ya kuyaainisha matatizo hayo katika nukta maalumu ili kujaribu kutambua mgogoro uliopo pamoja na kuweka misingi ya ushirikiano kutokana na yafuatayo:
a. Umuhimu wa kuweka masuala ya kilahuti – kwa istilahi yao – mbali na masuala ya ushirikiano wa pamoja na kujenga mustakabali juu ya msingi wa ufahamu ulio na faida yake pamoja na kuhifadhi mfumo wa utambulishowa wote kwa pande zote mbili.
b. Umuhimu wa kuainisha taasisi ya kidini kwa upande wa nchi za Waislamu na kusisitizia suala la kutotenga baina ya Waislamu wanaoishi nchi za kimagharibi na wanaoishi katika nchi iliyoshukia Wahyi na ardhi ya risala na kwamba inapendekezwa nafasi hii iwe ni ya Al Azhar kwa kuwepo wasomi wengi wanaojiunga nayo pamoja na uwastani wake wa kiislamu, na historia yake ya kina, namna ya fikra zake za kielimu kuhusu Uislamu, mwelekeo wake wa kuwa mbali na mapambano ya kimaoni na kuepusha vurugu (mapigano) na kuwepo Maulamaa wake wanaosifika kwa hekima n.k.
3. Kuainisha nukta muhimu zinazozishughulisha akili za kimagharibi nazo ni:
• Msimamo wetu kuhusu vitendo vya kufa shahidi kule Palestina na msimamo wetukuhusiana na jambo hilo na inaonekana kuwa haikutolewa fatwa ya kidini kutoka taasisi yetu kama inavyodhaniwa au kama inavyotakikana kudhaniwa ambapo ukweli wa suala hilo upo katika namna ya ukandamizaji wa kiyahudi pamoja na kufikia Wapalestina kukata tamaa, licha ya kuwa mtu wa kwanza kwa kufanya kitendo cha kufa shahidi alikuwa Mkristo na sasa wasichana wameanza kufanya vitendo hivyo ingawa zamani vijana ndio waliokuwa wanafanya hivyo peke yao kwani Uislamu uliwatolea bishara ya kupata Mahurul-Aini (wanawake wa Peponi) sabini, licha ya kuwa fatwa zilizoharamisha vitendo hivyo hazikusema kuacha kuvitenda wala kuhamasisha watu wavitende.Kwani sababu ya kimsingi ni kukata tamaa siyo dini na kwamba dai la kuwa dini ni sababu ya kufanya vitendo hivyo silo sahihi.Kwa hivyo lazima kutambua sababu ya kweli ya tatizo hilo na kuiondosha.Na sababu ya kweli kabisa ni namna ya Waisraili wanavyoshughulikia masuala ya kisiasa na kibinadamu.
• Ushoga kwa kuuzingatia kuwa ni haki miongoni mwa haki za binadamu,jibu lake litakuwa ni kwamba kitendo hichi hawajakubaliana kama haki miongoni mwa haki za binadamu, na kuwa dini zote zinakiharamisha kitendo hicho, na haki za binadamu zinazozingatiwa ni zile walizokubaliana binadamu na sio zile wanazozitangaza baadhi yao.
• Je taifa katika uislamu ni la kidini? Na msimamo wetu ni kwamba ni taifa la kiraia na wala si la kisekyula ambao unaufanya utawala ni wa mwanadamu bila ya Mwenyezi Mungu katika ardhi. Wala taifa la kidini ambalo linazifanya taasisi za kidini ndizo zinazohukumu, bali ni taifa la kiraia linalolinda mambo ya watu kwa kutoa fursa za ibada na kuimarisha ardhi na kuitakasa nafsi pamoja na imani ya kutokuwepo matabaka ya kijamii na ubaguzi wa rangi, na kuamini uhuru na shura, wingi wa dini kifikra na kisiasa.
• Kuritadi na adhabu yake. Na msimamo wetu unazungukia juu ya kuwa uislamu hauwataki wanafiki, na kwa ajili hiyo ukaacha uhuru wa kuamini.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi naatakaye, aamini. Na atakaye, akatae} [AL KAHF: 29]. Na akasema tena: {Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu} [AL KAFIRUN: 6]. Akasema tena: {Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu} [AL BAQARAH: 256]. Na kwamba kutoruhusu kubadilisha taarifa marejeo yake ni kwenye katiba na sheria na utaratibu wa umma ambao daima huwa ni katika mambo ya ndani na hutofautina kwa tofauti ya takwimu za watu na utamaduni uliopo.Atakapo kuwa mwenye kuritadi nimwenye kutangaza wakati ambapo atakuwa anatoka katika mfumo wa umma, hakika mifumo yote ulimwenguni hulichukulia hilo kama uhaini na mara nyingi adhabu yake huwa ni kunyongwa, isipokuwa adhabu hii kwa sifa hii haijawahi kutekelezwa- nchini Misri kwa mfano- zaidi ya miaka elfu moja.
• Mazungumzo nawengine. Na msimamo wetu ni kufungua mlango wa mazungumzo kati ya staarabu, jamii, tamaduni na dini mbali mbali, na kwamba fikra ya ugomvi haipo katika uislamu ambapo umesisitiza juu ya ushirikiano kati ya mwanadamu na ulimwengu, na kati ya mtawala na mtawaliwa, na kati ya mwanamke na mwanaume, na kati ya mwajiri na waajiriwa, na kwamba mazungumzo yanaondoa vikwazo vingi na kuboresha uendashaji wa mambo.
• Maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika miji ya waislamu; na msimamo wetu ni kuwa sisi daima tunafanya juhudi za kuweka mikakati ya maendeleo endelevu, na kutoa nafasi kubwa ya uhuru unaokwenda sambamba na uwezo wa wananchi, na pia kuna maendeleo ya mara kwa mara ya mitaala ya elimu jambo linalotoa nafasi ya uelewa wa habari za sasa na kumjenga mwanadamu chini ya urithi wake wa kitamaduni na chini ya mahitaji yake ya kisasa.
• Masuala ya muislamu kumnyang’anya mke wake mmagharibi watoto wake, na kuwatorosha kwa kuwapeleka nchini mwake.Msimamo wetu ni kwamba hatuhamasishi kuwaowa wasiokuwa waislamu ikiwa kama jambo lenyewe linapelekea kuwepo kwa magomvi, na kwamba haifai kisheria kumtenganisha mtoto na mama yake, isipokuwa baba ana haki sawa kwa sawa ya ulezi na usimamizi pamoja na mama.
• Swala la muislamu kushirikiana na jamii yake, na kufanya kazi katika idara za kijajusi na jeshi katika mataifa hayo; msimamo wetu ni kwamba muislamu anawajibu wa kufanya hivyo na niwajibu kwake kwa mujibu wa sheria za nchi zenye demokrasia aombe udhuru katika kila ambacho kitakuwa hakiendani na imani yake katika yale anayoyaona kuwa ni dhulma au kwenda kinyume, na hivi ndivyo ilivyoainishwa kwenye sheria ya Marekani.
• Msimamo kwa watu wachache wasio waislamu; vyanzo vya Uislamu na Historia yake vinathibithisa usamehevu wa Uislamu kwa walio wachache, hakika wao bado wapo hadi leo hii katika miji ya waislamu na wanapata haki yao kamili ya uraia chini ya katiba huru za kidemokrasia.
4- Yaliyopitayalikuwa ni msimamo wa ujumbe katika mambo wanayodhaniwa kuwa ni uzembe katika Uislamu au waWaislamu, na baada ya hayo ujumbe ulitoa maombi ya Waislamu ambayo ikiwa yataitikiwa basi usalama na utulivu vitapatikana katika mahusiano ya Muislamu na Ulimwengu wa kimagharibi sawa sawa akiwa Muislamu huyu jamii yake niya kimagharibu, au ni katika jamii za kiarabu, wakaombwa yafuatayo:
• Wasimamie kusahihisha mitaala ya elimu kutokana na makosa ya kihistoria na kielimu ambayo yamesababisha kuchafua sura ya Uislamu na Waislamu katika nchi za Magaharibi.
• Wakatakiwa kufanya kazi ya kupunguza mashambulizi ya vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na Waislamu ikiwa kama haikuwezekana kusitisha kabisa, na kutoa fursa kwa vyombo vya habari kujibu mashambulizi hayo na kubainisha ukweli.
• Kama walivyotakiwa kubadilisha sheria ambazo zimewekwa kwa misingi ya kuwabagua Waislamu, na kutopitisha sheria kama hizo hapo baadae jambo linalowabana Waislamu katika jamii za kimagharibi, inakuwa ni sababu ya vitendo visivyokuwa na uwajibikaji ambavyo vinavuruga amani na utulivu katika jamii hizo.
• Wakatakiwa pia kusaidia katika maendeleo ya binadamu, na kusaidia katika kupambana na ugaidi, na tukasema: Hakika Misri ilitoa wito kabla ya matukio hayo kwenye mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi; na kuwa Misri kwa kuwa kwake nchi kubwa ya kiarabu na kiislamu imesumbuliwa sana na ugaidi, na ilikuwa katika mataifa yaliyokuwa mbele katika kupambana na ugaidi, na kwamba Misri iliomba kuwasalimisha magaidi kwa kuwazingatia kuwa ni watu wenye misimamo mikali ambao hawauwakilishi Uislamu wala Waislamu.Lakini Uingereza ilikataa, wakati ambapo hivi sasa inadurusu ombi la Marekani kwa kuwasalimisha baadhi yao.
• Tukawataka kufanya itifaki kati ya waislamu na mataifa ya magharibi kwa ajili ya ushiriki wa waislamu katika mataifa yao ya magharibi, zinayoelezea kupanga marejeo na kutambulika serikalini, na Al Azhar ndiyo iliyopendekezwa kufanya hivyo, na itifaki hizi zifanye marejeleo ya mitaala ya elimu yenye kupingana naUislamu na Waislamu, na kurejea sheria ambazo zinawabana au kuwa kali dhidi yao, na tukawabainishia maandalizi ya Al Azhar kuchangia katika kuweka itifaki hizo. Ilidhihiri hali ya maelewano, na kumalizika mazungumzo kwa ahadi kutoka kwa waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya mashariki ya kati, kwa kulipeleka jambo hilo kwa waziri wa mambo ya nje ili kulichukulia hatua muhimu.
5- Mwisho kabisa tunapenda kuweka wazi: Ni mambo gani ya wajibu kwa taasisi zetu ambayo zinatakiwa kuyasamimia na kutufanya kuwa katika kiwango cha matukio, na kuelekeza ukweli ambao tumewataka wenzetu, ni wajibu kwetu kutilia umuhimu mambo yafuatayo:
• Kutilia umuhimu lugha za kigeni, na istilahi za kisasa na kutorudia yale yanayotudhuru miongoni mwake, na kutilia umuhimu kujenga shughuli za kiasisi ili kuelekeza shughuli zinazo nasibiana na lugha za Ulaya. Na kwamba si kila kitabu kinafaa kufasiriwa au kina kuwa na manufaa hata kama kitatafsiriwa kwa uhodari na umakini, bali hakuna budi kuzingatia mawazo ya kimagharibi.
• Kama ambayvo ni wajibu kwa taasisi zetu za kidini kutoa fatwa za kuelewekwa kuhusu masuala yenye kuzua mjadala kwa mfano (Ushahidi wa mwanamke – mirathi yake – kuowa wake wengi – mipaka – jihadi), kubainisha uhakika waUislamu na kuwa hizi ni katika hukumu zake ambazo hazifai kuguswa.Vinginevyo itakuwa ni kuchanganya kati ya masualaya kithiolojia –kwa mujibu wa muono wao – na masuala ya kushirikiana kwa pamoja.
• Ni wajibu kwa taasisi zetu ziwe na uwezo wa kujifunza dini zingine na kuzilinganisha kwa upana na usahihi katika chuo kikuu cha Al azhar, mpaka tuwe na uwezo wa kuzifuatilia kielimu, na uwezo pia wa majadiliano ya kielimu yaliyosahihi kutokana na umuhimu wake katika mustakbali bali hata kwa muda tulionao.
• Ni lazima pia kwetu sisi kuifanya Al azhar kuwa taasisi ya marejeo kwa mataifa ya Magharibi, na hatua ya kwanza katika hilo ni kuiboresha kwa kuwaingiza wasiokuwa wamisri ili kuifanya kuwa ya kimataifa, kama inavyoeleza sheria namba 103 ya mwaka 61 kuhusiana na swala hili.
• Ni lazima kwetu sisi katika Nyanja za kuihudumikia Quraani, kutunga kitabu kitakacho kuwa mlango wa kusoma Quraani usomaji uliosahihi ambao hautamfanya msomaji atosheke na baadhi ya Aya na kuacha baadhi yake, na kuandika katika maudhui za Quraani kila moja katika sura ya fasihi na kutumika kama mbadala wa tafsiri ya maneno au maana ya Quraani.
• Tuna haja pia ya kuanzisha pendekezo pamoja na vikundi vya kimataifa vyenye misimamo mikali vinavyojinasibisha na Uislamu na kushiriki mataifa mbali mbali pendekezo litakalo anzia kwenye njia ya vyombo vya habari na kuwaita katika neno la pamoja ili kuwa katika kiwango cha matukio yanayotokea pembezoni mwetu, huenda tukauzuwia ufisadi aridhini/duniani. Amesema Allah Mtukufu: {Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia maji mara unaiona inachangamka na kuumuka} [FUSSILAT: 39].
Chanzo: kitabu, Simat Al- Asri. Dk. Ali Juma, mufti wa zamani wa Misri.

Share this:

Related Fatwas