Kutumia Viwakilishi vya Kiume
Question
Nini hukumu ya kutumia viwakilishi (he), (his) katika lugha ya Kiingereza; kwa maana ya (yeye) na kiwakilishi cha kumiliki badala ya kutaja jina la Mwenyezi Mungu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Majina mazuri ya Mwenyezi Mungu na sifa zake za juu hazijulikani isipokuwa kwa mujibu wa sheria; imesemwa katika maelezo ya Al Mahaliy juu ya Jaamiu’ Al Jawami’: “Iliyo sahihi zaidi ni kuwa majina ya Mwenyezi Mungu ni Tawqifiya (hakuna yeyote anayeweza kusifika kwa majina hayo isipokuwa Mwenyezi Mungu); maana Mwenyezi Mungu Amesifika kwa majina hayo kwa mujibu wa sheria” [vol. 2, uk. 496, chapa ya Dar Al Fikr].
Sheikh Al Baijuriy amesema katika kubainisha maana ya Tawqifiya ni: “Kitendo cha kujuzu kutumia kwake majina hayo kwa ajili ya kumsifu Mwenyezi Mungu kinachotegemea kupatikana kwake katika Quraani Tukufu au Sunna iliyo sahihi au iliyo nzuri au makubaliano ya Maulamaa (Ijmai)” [Sharh Al Baijuriy juu ya Al Jawahr, uk. 155, chapa ya Dar es Salaam].
Kuhusu maana ya majina: Viwakilishi vikiwezekana kutumika kumsifu Mwenyezi Mungu ambapo Mwenyezi Mungu Amejisifu katika Quraani Tukufu kwa kutaja kiwakilishi “yeye”, Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Yeye ambaye ni Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo; (zote mnemeshaji ni Yeye)}[AL BAQARAH, 163], kadhalika Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu Ameshuhudia ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye tu. Na Malaika na wenye ilimu, (wote wameshuhudia hayo); (Yeye) ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu}[AALI IMRAN, 18].
Haya hayamaanishi kwamba Mwenyezi Mungu Amejisifu kwa sifa ya kiume (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu), bali kiwakilishi hicho kina matumizi mawili; kwanza: kinatumika kwa ajili ya wanaume. Pili: kinatumika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo tunaweza kutumia kiwakilishi hiki kwa kumtaja Mwenyezi Mungu kama Alivyovitumia viwakilishi hivi yeye Mwenyewe, na kwa kuwa Mwenyezi Mungu hajatumia kiwakilishi cha kike “yeye”, basi hatuwezi sisi kukitumia kiwaakilishi hicho cha kike kwa mujibu wa Maandiko ya Quraani Tukufu.
Na kwa kuwa jambo hilo haliambatani na Qiyasi, basi linalostahika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu haliwezi kamwe kulinganishwa na viumbe vyake. Tena Mwenyezi Mungu hasifiki kwa sifa za kiume wala za kike; kwani Yeye ni Muumbaji wa sifa za kiume na za kike, na hiyo ndiyo siri ya kutumia kiwakilishi cha kiume “yeye” kwa ajili Yake badala ya Kiwakilishi cha kike.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.