Mwanamke Kuwajibika Kuvaa Hijabu Iwapo Itamsababishia Matatizo Kazini kwake
Question
Mimi ni mwanamke mwislamu na nimemeolewa, ninafanya kazi ya uprofesa katika chuo kikuu maalumu na katika nchi isiyo ya Kiislamu, na nilipoanza kazi yangu, nilishitukia kuwa wanafunzi wanapinga mimi kuvaa hijabu na wanajaribu kusababisha zogo ili wanizuie kufanya kazi zangu, ukiongezea na maneno ya kejeli wanayoyatoa na ari yao ya kutaka kuzua matatizo. Je, niendelee kuivaa hijabu au ninaruhusiwa kuivua ili niepuke matatizo hayo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hijabu ni vazi lenye hukumu ya Faradhi kwa mwanamke wa kiislamu aliyebaleghe, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao} [AN NUUR 31].
Na Abu Dawud, Al Baihaqiy na Atwabaraniy wameitoa Hadithi kutoka kwa Aisha R.A, kwamba Asmaa Bint Abi Bakr R.A. aliingia kwa Mtume S.A.W, na alikuwa amevaa nguo nyepesi na Mtume S.A.W, akamkwepa, na akasema: "Ewe Asmaa, Hakika mwanamke anapobaleghe na kutokwa na hedhi haifai kwake kuonekana sehemu za mwili wake isipokuwa hapa na hapa, akaashiria Mtume usoni na katika viganja viwili vya mikono.
Na jambo likiwa kama hivyo: Haijuzu kuivua na kufichua kile kinachositiriwa katika mwili mbele ya watu wasio kuwa ndugu isipokuwa katika hali ya dharura tu au haja ambayo inaingia katika nafasi ya dharura kama vile matibabu au utoaji wa ushahidi; kwani mambo ya dharura huhalalisha vilivyokatazwa. Na haja huwa inakuwa katika nafasi ya dharura kwa ujumla au kwa sifa maalumu. Na wamesema: Hakika huu ni uchungaji katika kila dini. [Al Ashbaah Na Anadhair kwa Asyutwe K. 85-88, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na Mambo ya Dharura kwa ujumla ni matano; kuhifadhi Dini, roho, kizazi, mali, na akili. Na wamesema kwamba yanaangaliwa katika kila mila. Ama kwa upande wa mahitaji mbali mbali: Maana yake kuwa yeye anayahitaji kwa mapana Zaidi, na kuondosha uzito ambao mara nyingi hupelekea ugumu na matatizo hapo baadae kwa kukosa kinachohitajika, na kama kipato hakitaangaliwa.
Ama kuhusu hali iliyoulizwa: Na ikiwa jambo hili linaishia kwa baadhi ya manyanyaso ya wanafunzi kwa namna ambayo unaweza kuishinda kwa maadili yako na njia nzuri pamoja na tabia nzuri basi haifai kwako kuivua hijabu yako. Ama ikiwa hali hiyo itaendelea kuwa hivyo hadi ikafikia kushambuliwa ambako huwezi kujiepusha nako, au kukosa kazi na ukawa huna njia nyingine ya kujipatia fedha ili uweze kujikimu kimaisha na pia kwa ajili ya mambo mengine, na katika sehemu hisi haswa, unalazimika uivue hiyo hijabu kwa kiasi finyu iwezekanavyo, na kwa wakati mchache iwezekanavyo, pamoja na kuwajibika kwako kujisitiri mwili wako uwezavyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.