Kutoka Katika Chumba cha Mtihani k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoka Katika Chumba cha Mtihani kwa Ajili ya Kusali

Question

Chuo kikuu kimoja Mojawapo miongoni mwa vyuo vikuu vya Kairo kimefanya mitihani ya shahada ya uzamili katika Idara za Kazi za Kimataifa, mitihani ambayo inahitajika kufanyika kila itimiapo nusu ya msimu na mwisho wake.
Na wafanyaji wa mitihani hiyo ni katika wafanyakazi na mitihani yenyewe hufanyika kuanzia saa saba (mchana) mpaka saa tisa (jioni), na baadhi ya wanafunzi huwa wanataka kutoka wakati wa mtihani ili kwenda chooni kutia udhu; jambo ambalo wanafunzi wengine ndani ya chumba cha mtihani na walio nje hupata shaka, na wengine hupiga simu au kughushi katika mtihani.
Hivyo ninaomba nipate jibu iwapo kuna ulazima wa kutoka kwenye chumba cha mtihani kwa ajili ya Swala au hapana. Na pia ninaomba iwapo mtindo kama huu je, upo katika Chuo Kikuu cha Al Azhar au haupo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Swala ni nguzo ya dini nayo ni nguzo ya pili baada ya shahada mbili, na Mwenyezi Mungu ameiwekea wakati maalumu ili itekelezwe na kuwalazimisha waumini kuitekelezaa katika nyakati hizo, nayo ni lazima na haina budi isipokuwa kusaliwa tu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {kwani hakika Swala kwa waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu} [AN NISAA: 103].
Na Mwenyezi Mungu hakuiondosha kwa yeyote na kwa hali yoyote ilivyokuwa mtu ni mwenye akili timamu na anaekalifishwa na sheria, hata katika hali ya ugonjwa ambayo mtu huwa hawezi hata kuinua kitu, na hata katika hali ya vita baina ya makundi mawili yanayozozana, haya yote ni kwa sababu ya umuhimu wa Swala katika maisha ya muislamu.
Na sheria imeruhusu kupunguza Swala (idadi ya rakaa za Swala) na kuzikutanisha kwa baadhi ya mazingira, kwa mfano safari, na imeruhusu kuzikutanisha katika mazingira mengine kwa mfano kuwa na hofu kuwa ya mvua na wasiwasi (hali ya kuogopa) mkubwa. Na baadhi ya wanazuoni wakaliweka jambo hili kwa upana zaidi, wakasema kuwa inafaa kukusanya Swala mbili (kwa wakati mmoja) iwapo kuna usumbufu kwa mtu, kwa kuitendea Hadithi ya Mtume – rehma na amani zimshukie- iliyopokewa na Ibn Abbas– radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie- katika kitabu cha Muslim: "Mtume -rehma na amani zimshukie– amekusanya pamoja (amezisali kwa wakati mmoja) baina ya adhuhuri, alasiri, magharibi na isha alipokuwa Madina pasi na hofu wala mvua." Ibn Abbas akailizwa: “Kwa nini kafanya hivyo?” "Akajibu: “amefanya hivi ili asimweke mtu yeyote katika usumbufu (matatizo) katika watu wa umma wake.”
Imamu An Nawawiy anasema katika kitabu cha: [Sharhu Muslim 5/219, chapa, Dar Ihyau At Turath Al Arabiy]: "Baadhi ya kundi la maimamu wamekubaliana kukusanya Swala kwa mkazi (asiye msafiri) kwa dharura isiyo ya kawaida, nayo pia ni kauli ya Ibn Sayriyn na Ash bah katika wanazuoni wa madhehebu ya Malik.
Na Al khatwabiy ameeleza kutoka kwa Al qafali na Sha shiy Al kabiyr katika wanazuoni wa madhehebu ya imam Shafi kutoka kwa Is haq Al Maruziy kutoka kwa kundi la wanazuoni wa Hadithi, na ameichagua Ibn Al Mundhir na kutilia nguvu maneno ya Ibn Abbas: “Amefanya hivi ili asimweke mtu yeyote katika usumbufu (matatizo) katika watu wa umma wake.” Hapa hakuna tatizo la ugonjwa au kitu chengine chochote, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ajuaye zaidi. "
Na madhehebu haya ingawa ndiyo yatumikayo na inafaa kuyafanyia kazi wakati wa matatizo lakini kwa sharti la kwamba hatakiwi muislamu kufanya kuwa ndio kawaida –kama ilivyoelezwa katika maneno ya imamu An Nawawiy– na haifai kuendelea na kitendo hicho isipokuwa wakati wa udhuru mkubwa wa kipindi cha Swala na mtu akalazimika kuichelewesha Swala ya Adhuhuri na kuisali wakati wa Alasiri, Magharibi au Isha, namna ambayo atasali Swala zake ndani ya wakati wake kwa mfano iwapo mtu huyo anahofia Swala isije ikatoka katika wakati wake na akawa anahofia pia asije akapoteza kitu ambacho hataweza kukipata tena.
Na kwa hayo na kwa mujibu wa swali: Chuo kilichotajwa ni lazima kipange wakati maalumu wa mitihani wa nusu ya muhula na mwisho, kwa kutopingana na nyakati za Swala, kwa kufanya mwisho wa kumaliza mtihani iwe kabla ya kuingia kwa Swala nyingine kwa muda unaotosha ambao utamwezesha mwanafunzi kutia udhu na kusali.
Kwa mfano utatangulizwa mtihani kabla ya kuingia wakati wa Swala ya magharibi ili waweze kuiwahi magharibi na kabla ya kuingia Swala ya Isha. Au mtihani utacheleweshwa kidogo kwa ajili ya Swala ya magharibi (wataswali, kisha wataingia katika chumba cha mtihani) ili waiswali Swala kwa wakati wake, na ikiwa haiwezekani kufanya mabadiliko ya wakati wa mtihani kwa kuchelewesha au kutanguliza na Chuo Kikuu kikawa hakiwezi kuwapa wanafunzi muda wa kufanya ibada ya Swala pamoja na kutoweza kuwazuia wasifanye kughushi basi kwa hali kama hiyo itafaa –kwa kuzingatia haja ya dharura iliopo– kufanyika mtihani kwa wakati wake na wala asiruhusiwe mwanafunzi kutoka, na wanafunzi wanaweza kukusanya kati ya Swala mbili –kwa kutanguliza au kuchelewesha.
Kwa kuifanyia kazi Hadithi ya Ibn Abbas –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie yeye na Baba yake– iliyokwishatajwa. Na kwa kuzingatia kuwa mitihani katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar inachunga nyakati za Swala pamoja na nyakati za kufanyia mitihani.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas