Kuifasiri Hotuba ya Ijumaa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuifasiri Hotuba ya Ijumaa

Question

Ni ipi hukumu ya kuitafsiri hotuba ya Ijumaa kwa mujibu wa madhehebu ya Imamu Shafi, kwa wasioijua lugha ya kiarabu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Bajuriy anasema katika maelezo ya kitabu chake cha [Sher hu Ibn Qasim A`la Mutun Abi Shuja`a, chapa ya Mustafa Al- Halabi 228]: "Na wala si sharti katika hotuba nyingine isipokuwa kusikiliza, msikilizaji, na mwenye kuhutubu awe ni mwanamme na hotuba iwe kwa kiarabu. Na imewekwa sharti ya hotuba kwamba iwe kwa kiarabu pindi watu wake watakapokuwa ni waarabu, na kama si hivyo inafaa kwa lugha nyingine isipokuwa katika kusoma aya ni lazima iwe kwa kiarabu. Na italazimu mmoja kati ya waislamu wasiojua kiarabu, ajifundishe kiarabu. na kama hatajifunza mmoja kati yao basi wote watakuwa makosani. Na wala haitasihi Ijumaa yao pamoja na kuwepo uwezo wa kujifunza Usomaji wa Quraani". Mwisho.
Na hakuna tatizo kwa mujibu wa madhehebu ya imamu Shafi kuitafsiri hotuba ya Ijumaa kwa lugha nyingine kabla ya kutolewa hotuba hiyo au baada yake, kwa ajili ya wasiojua lugha ya kiarabu wajue kinachosemwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas