Kuwachoma Maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwachoma Maiti

Question

Kwa nini Uislamu unaharamisha kumchoma maiti?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kumchoma maiti ni jambo linalokatazwa kisheria kwa ajili ya kulinda heshima ya binadamu na kumwepushia maudhi ya aina yeyote; kwani maiti anahisi kama anavyohisi mtu alie hai, kama alivyotuamrisha Mtume S.A.W, tumfanyie maiti, kwani kuwa maiti haimaanishi hali ya kutokuwepo, bali ina maana ya kutoka katika maisha ya hapa duniani na kupelekwa katika maisha mengine. Vilevile heshima ya binadamu akiwa mfu ni sawa na heshima yake wakati anapokuwa hai. Mtume S.A.W, amesema: “Kuvunja mifupa ya maiti ni sawa na kuvunja mifupa yake akiwa hai”
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas