Hotuba ya Ijumaa kwa Lugha Isiyo ya Kiarabu.
Question
Kuna hukumu gani katika kutoa Hotuba ya Ijumaa kwa lugha ya Kiiengereza kwa Waislamu wa Lugha hiyo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuna waislamu wengi ambao hawajui Kiarabu katika nchi za Magharibi, wawe ni wakazi wake wa asili au wageni ambao wameenda katika nchi hizo. Na wakati wa Swala ya Ijumaa kunakuwa na uzito wa watu kufahamu je, Hotuba ya Ijumaa itatimia kwa lugha ya Kiarabu pamoja na kuwa waisilamu wengi hawaielewi lugha hiyo au Hotuba hiyo ya Ijumaa itasomwa kwa lugha wanayoifahamu wengi wa Waislamu hao.
Suala hili, wanazuoni wamelizungumzia katika Mlango wa “Swala ya Ijumaa”, na baadhi yao katika Mlango wa “kisomo ndani ya Swala” je inafaa kwa lugha ya Kifursi au hapana?
Kauli yenye nguvu ni kuwa; inafaa Hotuba ya Ijumaa ya Ijumaa kwa lugha isiyo ya kiarabu bila ya wasiwasi na Swala ya Ijumaa huwa sahihi. Na ni bora kuzileta nguzo kwa kiarabu ili kuepukana na hitilafu iliyopo kwa upande wa wanazuoni.
Na dalili ya hayo, ni kwamba, makusudio ya Hotuba ya Ijumaa ni kuwabainishia mawaidha na hukumu za kisheria ambazo huwa katika siku ya mfano wa siku za Hijja ambazo imamu husimama na kuelezea yanayohusu Hijja, kwani haiingii akilini imamu atoe Hotuba ya Ijumaa kwa watu wengi ambao hawafahamu anachokisema naye ana uwezo wa kuwafahamisha na kwa lugha wanayoifahamu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} (IBRAHIM: 4) na maana ya {Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi} kwa lugha {ili apate kuwabainishia} ili awafahamishe yule aliokuja nayo, kama ilivyo katika tafsiri ya Jalalein.
Na tuliyoyataja ndiyo yenye kuzingatiwa katika madhehebu ya Abu Hanifa kwa kufuata tafauti na wenzake, kwa mujibu wa maelezo ya masharti ya Hotuba ya Ijumaa Atwahtwawiy anasema katika kitabu chake: [Muraq Al falah, ukurasa 277, chapa, Mustafa Al halabi]: (na) nguzo ya nne (ya Hotuba ya Ijumaa) hata kama kwa kifursi kwa mwenye kuweza kusema (hata) kiarabu. Mwisho.
Na Ibn Abidin anasema katika kitabu cha: [Radul muhtar ala Ad Dar Ilmukhtar, 1/543, chapa, Ihyau Turath]: Na wala Hotuba ya Ijumaa haikuwekwa kuwa ni lazima iwe kwa Kiarabu kwa kutosheka na yale aliyoyaelezea katika “Mlango wa sifa za Swala” kwa kuwa kwake si sharti hata kama pana uwezekano wa kusema kwa Kiarabu. Tafauti na wenzake wawili ambao wameshurutisha Kiarabu isipokuwa itakaposhindikana. Mwisho.
Na wengine wameruhusu (wamekubali) kama imamu Hanbal itakaposhindikana kwa Kiarabu. Na mwanazuoni Al Bahuti Al Hanbaliy anasema katika kitabu cha: [Kushafu Al Quna`a 2/33, chapa, Dar Al fikr): "Na Hotuba ya Ijumaa haitasihi isipokuwa kwa Kiarabu pamoja na uwezo kwani hayo ni dalili ya kukijua Kiarabu (kwa mfano, kusoma) kwani hapo itasihi bila ya kutumia Kiarabu (na itasihi) Hotuba ya Ijumaa hata kwa lugha isiyo ya Kiarabu (pamoja na kushindwa".
Kutumia kiarabu, kwani malengo ni kutoa mawaidha na kukumbusha na kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumsalia Mtume – rehma na amani zimshukie-. Tofauti na matamshi ya aya za Quraanikwani hayo ni dalili ya Utume na ni ishara ya ujumbe na wala haifai kuutoa kwa lugha isiyo ya Kiarabu (isipokuwa kisomo), na wala haitafaa isipokuwa kwa kiarabu kama ilivyotangulia kuelezwa (na iwapo atashindwa) kusoma (itamlazimu kuleta utajo wa Mungu) kama ilivyo katika Swala. Mwisho.
Na kama imamu anaweza kuleta utangulizi na Aya na Hadithi kwa lugha ya Kiarabu kisha baadae akatafsiri, basi itakuwa ni bora zaidi. Imekuja katika maamuzi ya Jamhuri ya wanazuoni wa Fiqhi ya Kiislamu: “Rai iliyo sawa ni kuwa, lugha ya Kiarabu katika kuisoma Hotuba ya Ijumaa na ya Sikukuu mbili za Eid katika nchi zisizozungumza Kiarabu si sharti (la kusihi ibada hizo), lakini ni bora kuleta utangulizi wa Hotuba ya Ijumaa na kila lenye kuhusiana nayo kwa mfano Aya za Quraani kwa lugha ya Kiarabu, ili kumzowesha asiye kuwa mwarabu kusikia Kiarabu na Quraani, jambo ambalo litamrahisishia kujifunza na kuisoma Quraani ambayo imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu, kisha baada ya hayo, Imamu ataendeleza Hotuba ya Ijumaa kwa lugha yao wanayoitumia na kuielewa.” Mwisho.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.