Uchi wa Mwanamke wa Kiislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Uchi wa Mwanamke wa Kiislamu

Question

Je, inajuzu kwa mwanamke wa kiislamu mwenye hijabu anajionesha mbele ya mwanamke asiyekuwa mwislamu bila ya hijabu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Inajuzu kwa mwanamke wa kiislamu kumuonesha mwanamke asiyekuwa mwislamu sehemu zinazojuzu kwake kuzionesha kwa mwanamke wa kiislamu, kwa usawa bila kutofautisha. Na dalili juu ya hayo ni kwamba yale yalikuwa yakitokea katika zama za Mtume S.A.W., kama ilivyotajwa katika Hadithi nyingi, kutoka kuingia kwa wanawake wasio waislamu kwa akina mama wa waumini bila ya kusemwa kuwa walikuwa wakivaa hijabu, kama ambavyo inakadiriwa hivyo kwa mwanaume asiye muislamu kumwangalia mwanaume mwislamu kwa mkusanyiko wa jinsia moja.
Tofauti ya Dini haina athari yeyote katika jambo hili, kwani kuwaangalia wanawake kumezuiliwa kwa wanaume kwa lengo la kuzuia fitna, na jambo hili halipatikani kati ya mwanamke na mwanamke mwenziye. Ama suala la mwanamke kumzungumzia mume wake, mwanamke mwislamu, hakuna wasifu wowote tenganishi kwa jambo hili, isipokuwa ni wingi, na wasifu huo pia unaweza kuwa ni kutoka kwa mwanamke mwislamu kutokana na ujinga au uovu, na njia zote mbili zinapatikana katika uhalisia.
Kama ambavyo mwanamke mwislamu katika nchi za Ulaya au ambazo zina idadi kubwa ya wanawake wasio waislamu kwa namna ambayo kuna ugumu na uzito mkubwa wa kuepukana nao kwa namna ambayo sheria ya Kiislamu imeondosha uzito huo.
Na kama tulivyosema lilitaja kundi la watu wa elimu na miongoni mwao wanazuoni wa Kihanbaliy; Ibn Qudamah wa Kihanbaliy akasema katika kitabu cha: [Al Mughniy 105/7, Ch. Maktabat Al Qahirah]: "Na hukumu ya mwanamke na mwanamke mwenziye ni kama hukumu ya mwanaume na mwanaume mwenzake, na hakuna tofauti baina ya waislamu wala baina ya mwanamke wa kiislamu na asiyekuwa wa kiislamu (dhimiyu), pia hakuna tofauti baina ya wanaume wawili waislamu wala baina ya mwislamu na asiye mwislamu (dhimiyu)."
Na katika kuangalia Ahmad amesema: "Baadhi ya watu wamefika kusema kuwa mtu asivue kilemba chake mbele ya mwanamke wa kiyahudi au wa kikristo, ama kwa upande wangu mimi ninaona kuwa hataangalia uchi au hata kuwa mkunga wake wakati anajifungua. Na kutoka na Ahmad katika simulizi nyingine: Ni kwamba mwanamke wa kiislamu haoneshi uchi wake mbele ya mwanamke asiyekuwa mwislamu, na wala haingii naye chooni. Na kauli hiyo ni kauli ya Makhul na Sulaiman Bin Musa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Au wanawake wao}[AN NUR 31]. Na la kwanza ni bora Zaidi, kwani wanawake wa kikafiri miongoni mwa mayahudi na wengine wao, walikuwa wakiingia kwa wakeze Mtume S.A.W, na wala hawakuwa wakijigubika nguo, na wala Mtume hakuwaamrisha wafanye hivyo.
Na Aisha R.A. amesema: "Mwanamke myahudi alikuja ili kumwuliza, basi akasema: Mwenyezi Mungu akukinge na adhabu ya kaburini, basi Aisha R.A. Akamwuliza Mtume S.A.W. na akataja hii Hadithi. Na Asmaa akasema: " Mama yangu alinijia akikataa kusilimu, basi akamwuliza Mtume S.A.W.: je niwe nirejeshe undugu na mama yangu? Mtume S.A.W. akasema: Naam.
Na kwa kuwa hijabu baina ya wanawake na wanaume kuna maana ambayo haipatikani kati ya mwanamke wa kiislamu na asiye mwislamu, na kwa ajili hiyo imewajibika kutokuwapo hijabu baina ya mwanamke wa kiislamu na asie mwislamu.
Na kwa kuwa hijabu inakuwa wajibu kwa maandiko au kwa Kipimo, na haijawahi kuwapo moja kati ya njia mbili hizi, na ama kauli yake {au wanawake wao} (AN NUR 31) ina uwezekano wa kuwa na maana wanawake wote.
Ama kwa yule atakayeleta hoja ya kuzuia kwa tamko la Mwenyezi Mungu (au wanawake wao) basi jawabu lake: kinachokusudiwa kwa tamko hili ni wanawake wote, na zuio la wema waliotangulia lina lengo la kupendezesha, kama ambavyo baadhi yao wamezuia kuwaoa wanawake wa kikristo na kiyahudi, wakati ni halali kwa Matini ya Quraani.
Ibn Al Arabiy amesema katika kitabu cha: [Ahkaamu Al Quraani 385/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah}, "Kauli yake "Au wanawake wao" ina kauli mbili; moja yao ni wanawake wote, na ya pili ni wanawake wa waumini, Na kilicho sahihi kwangu ni kwamba inajuzu kwa wanawake wote, na imekuja kwa dhamiri kwa lengo la ufuasi kwani dhamiri (kiwakilishi jina) hiyo ni alama, kwani ndani yake kuna dhamiri (viwakilishi jina) ishirini na tano"
Na ufupisho ni kwamba: Hakuna zuio lolote la kuitumia kauli ya kujuzu jambo hili, kama mwanamke atakuwa na Amani ndani ya nafsi yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas