Kuvaa Dhahabu Nyeupe kwa Wanaume

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvaa Dhahabu Nyeupe kwa Wanaume

Question

Je, pete zinazotengenezwa kwa dhahabu nyeupe ni haramu kwa wanaume?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Jina la Dhahabu nyeupe huitwa kwa vitu vingi, huitwa kwa jina hilo madini ya platinamu ambayo yana sifa zinazofanana na dhahabu, na huzingatiwa ni yenye thamani ya juu zaidi kuliko dhahabu, na hayo madini ni ruhusa kwa wanaume kuyatumia kwa Ijmaa ya wanazuoni, na hakuna hitilafu yeyote, Kwa sababu hakuna katazo lolote lililopokelewa kuhusu madini haya, na kwa kukosekana kwa maana za kiburi na majivuno kwa kuyatumia hayo madini, na vile vile hukumu ya kila aina za madini yenye thamani isipokuwa dhahabu.
Ama kuyaita madini ya platinamu kama dhahabu nyeupe haiyafanyi madini hayo yawe haramu, kwani madini hayo hayahusiani na dhahabu yenyewe isipokuwa kwa jina tu la kuazimwa pamoja na kuwapo tofauti ya uhalisia wake, na jambo la kuzingatia ni vinavyoitwa na wala sio majina, na iliyo haramu ni dhahabu ya njano iliyo maarufu tu.
Jina la dhahabu nyeupe hutumika pia kuiita dhahabu ya njano iliyopakwa platinamu, na aina hii ndio inayopitishiwa hukumu ya dhahabu, na wala haijuzu kwa mwanaume kujipamba nayo, kwani uhakika wake haujabadilika kwa kupakwa platinamu, kwa hiyo ina hukumu yake ile ile ya dhahabu ya njano iliyo maarufu.
Jina Dhahabu nyeupe hutumika pia kuuita mchanganyiko wa dhahabu maarufu ya njano na maada ya Palladium au mada nyingine, kwa hiyo badala ya kuichanganya dhahabu ya karenti 21 kwa fedha au Shaba, mtengenezaji huichanganya na palladium, Ni madini yanayofanana na Platinamu na rangi yake ni ya kijivu, na hutokana na madini ghafi ya Shaba na Nikol. Na Sonara kwa ujumla anachanganya ili dhahabu iwe na nguvu au aiwekee kivuli maalumu kama vile wekundu, manjano, kijani na kadhalika.
Na dhahabu maarufu ya njano inapochanganywa na madini ya platinamu huwa na rangi kama iliyopakwa platinamu, na mchanganyiko huu huzalisha kitu kiitwacho na Masonara kama ni dhahabu nyeupe. Na aina hii ya dhahabu, wenye elimu wamehitilafiana hukumu yake. Wapo walioihalalisha na miongoni mwao wapo walioiharamisha.
Na hukumu tunayoichagua sisi ni kuwa uzito wa madini ya platinamu unapouzidi wa dhahabu safi, au uzito ukawa sawa, basi matumizi yake ni halali, na iwapo uzito wa dhahabu safi utauzidi ule wa platinamu basi ni haramu. Na hukumu hiyo ni kwa kigezo cha kauli ya wanazuoni katika Hariri iliyochanganywa na nyuzi za aina nyingine.
Na Al Khatwib Asherbiniy akasema katika kitabu cha: [Mughniy Al Muhataaj 583/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah], "Ni haramu kwa mwanaume na Khunsa (jike dume) nguo ya Hariri, na Hariri inapokuwa Zaidi ya nyuzi nyingine, na kinyume chake ni halali. Nayo ni kuwa na mchanganiko uliopunguza Hariri zaidi kuliko nyuzi nyingine kama vile kifungo kushonwa kwa uzi wa hariri au kuchanganyika na sufi nyingi zaidi ya hariri, basi huwa halali, na pia huwa halali kama hariri na nyuzi nyingine zitalingana uzito wake kwa kauli iliyo sahihi zaidi kwani hiyo haiitwi nguo ya hariri na asili yake ni uhalali.
Na kwa Abi Dauwd kwa isnadi sahihi kutoka kwa Ibn Abaas alisema: "Hakika ni kwamba Mtume S.A.W, ameharamisha nguo iliyotengenezwa kwa Hariri safi."
Na pamoja na kujuzu kwa wanaume kutumia dhahabu yenye platinamu iliyoizidi dhahabu hiyo kwa uzito, au madini hayo yakilingana uzito, lakini ni vyema zaidi kujiepusha navyo, ili kujitoa katika hitilafu.Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas