Kudhihiri mguu wa Mwanamke
Question
Ni ipi hukumu ya kudhihiri mguu wa Mwanamke katika Swala na nje ya Swala?
Answer
Kisharia ni wajibu kwa mwanamke kusitiri mwili wake wote, isipokuwa uso na viganja viwili, kwa Rai ya Jamhuri ya wanazuoni wa Fiqhi, na wengine wameeleza kuwa si wajibu kusitiri miguu yake; sawasawa katika Swala au nje ya Swala.