Vitendo vya Ulipuaji wa Mabomu

Egypt's Dar Al-Ifta

Vitendo vya Ulipuaji wa Mabomu

Question

Hivi karibuni tumetizama na tumesikiliza katika vyombo vya habari kuhusu vitendo vya ulipuaji wa mabomu vilivyotokea nchini Pakistani. Vile vile vitendo hivi vimetokea London, na Madrid siku zilizopita. Vitendo hivi vilihusishwa na makundi yaliyohusishwa na Uislamu. Baadhi ya wanaoyaunga mkono makundi hayo walisema kuwa ni halali vitendo hivi kufanyika ingawa vimewalenga watu wasio na hatia. Hukumu ya vitendo hivi vilivyotajwa ni nini, na je, hukumu ya vitendo hivi inatofautiana kati ya nchi za Magharibi na nchi za Waislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Vitendo hivi vya ulipuaji wa mabomu vilivyoulizwa na vilivyotokea hivi karibuni ni aina mbili: Aina inayotokea katika nchi zisizo za Waislamu kama vile; London na Madrid, na aina nyingine iliyotokea katika nchi za Waislamu kama Bakistan, Saudia, Misri, Morocco, na nyinginezo, aina hizi mbili hazina shaka yeyote kuhusu uharamu wao kwa mujibu wa Sheria.
Ama kuhusu mabomu vilivyotokea katika nchi za Waislamu uharamu wake ni wazi kwa sababu:
Kwanza: Ukiukaji wa maandiko ya Sheria:
Na ukiukaji wa maandiko ya Sheria kutoka pande nyingi zikiwemo; vitendo hivi viliwaua Waislamu wasio na hatia, nao si wenye kufanya makosa, Sheria iliitukuza damu ya Mwislamu, na ilitoasha vitisho vikali kuhusu kumwaga damu bila ya haki; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa} [AN-NISAA 93], Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema pia: {Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote} [AL-MAIDAH 32].
Imepokelewa kutoka kwa An-Nasaai katika Sunan yake kutoka kwa Abdullahi Ibn Omar R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: “Kwa hakika kuondoka kwa dunia yote, ni jambo dogo zaidi kwa Allah kuliko kumuuwa muislamu”, pia imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Ibn Omar R.A alisema: Nimemwona Mtume S.A.W. wakati alipotufu Kaabah akisema: “Namna gani wewe ni mzuri, na harufu yako ni nzuri, namna gani wewe ni mtukufu na namna gani utukufu wako, naapa kwa Mwenyezi Mungu ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake kwamba utukufu wa muumini kwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi kuliko utukufu wako, mali yake na damu yake, na kumdhani kwake kwa kheri tu”
Vitendo hivi vililenga kuwaua na kuwadharau baadhi ya wageni wanaokuwepo nchini, hali hii ina uhaini na kuvunja agano. Asiye Mwislamu wakati anapoingia nchi za Waislamu kwa njia ya Kisheria, basi yeye yupo katika amani, inapaswa Waislamu kuilinda damu yake, mali yake, na heshima yake. Amani ni mkataba miongoni mwa mikataba na ahadi pia. Mwenye kuigusa damu ya Muumini au mali yake au heshima yake ni mwenye kuvunja ahadi, hali hii iliyopigwa marufuku kwa matini kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi}[AL-MAIDAH 1].
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Abdullah Ibn Omar R.A kuwa Mtume S.A.W alisema: “Mambo manne mwenye kuwa nayo basi huwa ni mnafiki halisi, na mwenye kuwa na moja tu katika hayo basi huwa na sifa moja ya unafiki mpaka aiache: Anapozungumza husema uongo na anapochukua miadi hatekelezi, na anapotoa ahadi hukhini na anapogombana hupindukia mipaka”. Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Omar Ibn Al-Hamiq Al-Khuzai alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mwenye kumpa mtu amani kwa damu yake akamwua, atabeba bendera ya uhaini siku ya Kiama”. Na katika mapokezi ya Al-Bayhaqi na Al-Tiyasi kwamba: “Mwenye kumpa mtu amani kwa nafsi yake, kisha akamwua, basi mimi si pamoja na muuaji hata kama aliyeuawa ni mkafiri”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kwa Ali R.A kuwa Mtume S.A.W alisema: “Dhima ya Waislam ni moja, hata aliyechukua dhima hiyo ni Muislam aliye chini kabisa, basi Muislam anayevunja dhima aliyechukua Muislam mwingine juu ya kafiri atalaaniwa na Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote na haitapokelewa ibada yake ya faradhi wala ya Sunna”
Kauli yake “Dhima ya Waislam” yaani: Ahadi yao. Na kauli yake: “Aliyechukua dhima hiyo ni Muislam aliye chini kabisa” yaani: Wachache wao, kama Muislamu mmoja akimpa ahadi hairuhusiwi kwa yeyote kuivunja, tunadhani nini kuhusu Khalifa.
Pia vitendo hivi vinasababisha kuwaua wasiokuwa waangalifu, imepokelewa kutoka kwa Abu Daud na Al-Hakim katika Mustadrak yake kutoka kwa Abu Hurairah R.A kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Hairuhusiwi kwa Muumini kuua kwa siri, Imani imefunga kuua kwa siri”
Ibn Al-Athiir katika kitabu cha Al-Nihayah alisema: “Kuua kwa siri maana yake ni kwamba mtu mmoja anakuja kwa mwenzake wakati anapokuwa si mwangalifu akamwua”.
Maana ya Hadithi hii ni kwamba Imani inazuia kuua kwa siri kama kamba inavyozuia kucheza.
Wakati Waislamu wa kwanza walipojua maana za juu hizi na walizifuata wakapiga mfano mzuri katika historia, na miongoni mwa mifano hii kisa cha Khubaib Al-Ansari R.A kilichopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake na katika kisa hichi Washirikina Wakamchukua Khubaib na wakamwuza katika Makkah. Khubaib akanunuliwa na watoto wa Al-Haarith Ibn A`amir Ibn Nawfal Ibn Abdi Manaaf. Na Khubaib ndiye aliye muuwa Al-Haarith bin A`amir siku ya vita vya Badr, na akabaki kwao hali ni mateka. Siku moja Khubaib alimtaka binti wa Al-Haarith amuazime wembe ili ajisafishe sehemu zake za chini, na yeye akamuazima, na alimchukua mtoto wake mwanamme naye binti wa Al-Haarith ameghafilika alipomjia kumchukua. Akasema: Nikamkuta amempakata pajani pake na wembe mkononi mwake. Nikafazaika mfazaiko wenyewe hata Khubaib akaujua usoni mwangu. Akasema: Unakhofu kuwa nitamuuwa? Mimi sitakuwa wa kufanya hayo. Wallahi katu sikupata kumwona mateka mtu wa kheri kuliko Khubaib… n.k. Mtu huyo ni mateka Mwislamu yupo kwa maadui zake wanaopanga kumwua ambapo yeye yupo karibu na kuuwa, pamoja na hayo, alipokuwa na nafasi ya kuwahuzunisha Washirikina kwa kumwua mtoto wao anatoa msamaha kwao; kwa sababu tabia ya Mwislamu haina udanganifu wala haina kuwashangaza wanaoghafilika.
Pili: Vitendo hivi ni kinyume cha makusudio ya Sheria:
Sheria tukufu ilisisitiza kwamba ni lazima kudumisha mambo matano yaliyoafikiwa kwa dini zote nayo ni lazima kudumisha: dini, nafsi, akili, heshima, na mali, nayo yanaitwa makusudio matano ya Sheria.
Ni wazi kwamba vitendo vya ulipuaji wa mabomu vinasababisha ubatili wa baadhi ya makasudio yanayotakiwa kudumishwa, miongoni mwao ni kuhifadhi nafsi; basi aliyeuawa akiwa ni mwenye kufanya kitendo cha mlipuko aliyejiingiza mwenyewe katika kuua anaingia katika jumla ya kauli yake Mtume S.A.W iliyopokelewa kutoka kwa Abu Awanah kutoka kwa Hadithi ya Thabit Ibn Al-Dhahaak R.A. kuwa: “Mwenye kujiua katika dunia ataadhibiwa katika Siku ya Kiama” Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Hadithi ya Abu Hurairah R.A. kuwa Mtume S.A.W. alisema: “Mwenye kujiua kwa kipande cha chuma, atatiwa motoni akiwa na kipande hicho cha chuma akijitwanga nacho tumboni kwake humo motoni milele. Atakayekunywa sumu na kujiua, basi atatupwa motoni na huko atakuwa akiinywa hiyo sumu milele, na atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua, atatupwa ndani ya moto milele”,
Imam Al-Nawawi aliweka mlango kuhusu kuieleza Hadithi hii katika Sahihi ya Muslim, akasema: “Mlango wa kutoruhusiwa kabisa kujiua na kwamba mwenye kujiua kwa kitu chochote ataadhibiwa kwake motoni”.
Kama akiua mwengine, kama aliyeuawa ni Mwislamu basi kumwua kwa makusudi ni uadui mkubwa hakuna dhambi baada ya ukafiri ni mkubwa zaidi kuliko ile. Kuhusu hali ya kukubali toba yake au la masahaba na waliokuja baada yao wametofautiana. Kama aliyeuawa asiye Mwislamu basi akiwepo nchini mwetu basi ana Amani, kama akiwepo nje ya nchi yetu basi yeye ni mzalendo aliyeghafilika na hana hatia yeyote, kwa hali zote, nafsi zao zinahifadhiwa na haziruhusiwi kuzikiuka na ni lazima kuzidumisha.
Pia vitendo hivi vya mabomu vinasababisha ubatili wa kulinda mali; vinaharibu mali, majengo, mali ya umma na ya binafsi, vinaharibu mali na vinazipoteza hali isiyoruhusiwa kwa Sheria, uharamu unazidi na kuwa maradufu ikiwa mali hizi hazimilikiwi na mwenye kuzipotea bali zinamilikiwa na mwengine -kama iliyokuwa katika suala hili- basi uharamu unahusiana na kukiuka Sheria kwa upande mmoja, na pia unahusiana na haki za watu kwa upande mwengine.
Tatu: Ufisadi na madhara yaliyosababishwa kwa vitendo hivyo:
Sheria tukufu inalenga kuleta maslahi tena kuyatimiza, na kuondosha ufisadi na kuizuia. Yeyote mwenye akili anafahamu sana kwamba vitendi hivi vya mabomu vinaleta ufisadi kwa Waislamu katika Mashariki na magharibi, pia vinatumika kama sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Kiislamu, kuzitawala, kutumia kheri zake, kuiba rasimali yake kwa kisingizio cha kuwashtaki kwa ugaidi au kudumisha maslahi ya kiuchumi au kuwaachia huru watu, basi atakayewasaidia hawa ili wafikie malengo yao kwa vitendo hivi atawadhuru Waislamu na hali hii ni miongoni mwa uhalifu mkubwa.
Miongoni mwa ufisadi mkubwa kwamba vitendo hivi vinasisitiza uvumi na shutuma za uongo kwa wasio Waislamu ambazo maadui wa Waislamu wanazipandikiza katika dini ya Uislamu kuwa ni dini ya kishenzi na ya umwagaji wa damu lengo lake ni kushindwa watu na ufisadi ardhini, na hayo yote miongoni mwa kuzuia Mwenyezi Mungu na dini yake.
Na miongoni mwa ufisadi mkubwa pia ni yanayofuatana na hayo miongoni mwa kusababishia mashambulizi na matumizi mabaya kwa Waislamu wanaokuwepo katika baadhi ya nchi za kigeni wale shupavu kaatika dini – nao ni wengi – hivyo Waislamu hawa wanakabiliwa na matumizi mabaya zaidi katika nafsi zao, jamaa zao, mali zao, heshima zao, na baadhi yao pengine wanalazimishwa kufanya ibada kwa siri au kuacha baadhi ya ibada.
Hayo yote kwa sababu ya vitendo vibaya ambavyo walivyovifanya watu wanaoghafilika wakidhani kuwa ni kufikia maslahi ya Kiislamu, na ukweli ni kwamba wanafanya maslahi kwa Shetani tu.
Wanazuoni walisema kuwa kama maslahi ni kinyume na ufisadi, basi kuondoshwa kwa ufisadi hupewa kipaumbele dhidi ya kuleta maslahi, na maneno ya Wanazuoni wetu kuhusu maslahi yapatiwayo, hali gani ikiwa maslahi hayo ni ya mawazo au hayapo?
Ama kuhusu wanavyosema miongoni mwa vitendo hivi kutoka mlango wa jihadi na hasira dhidi ya adui, na baadhi yao labda wanaita hivyo vita, hali hii ni ujinga mtupu na kosa; basi jihadi iliyoruhusiwa katika Uislamu ni ile iliyo chini ya bendera ya Uislamu na kwa idhini ya Khalifa, au jambo hilo litakuwa fujo na kumwaga damu ya watu ambao hawana hatia yeyote kwa singizo cha jihadi, nayo jihadi katika Uislamu ina malengo mawili:
La kwanza: ni kutetea Uislamu, kama Mwenyezi Mungu alivyosema: “Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui” [Al-Baqarah: 190].
La pili: kutetea uhuru wa watu katika kuamini Uislamu au kubakia kama walivyo, na hali hii ni (Fitna) tuliyoamuriwa kupigania mpaka tuiondoshe na watu, ili wachague dini yao kwa uhuru kamili, Mwenyezi Mungu amesema: “Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu” [Al-Baqarah: 193].
Ni wazi kwamba Jihadi iliruhusiwa kwa ajili ya kufikia malengo hayo mawili, kufuatana na hali hii jihadi inakuwa dhidi ya maadui wa nje.
Ama kuhusu kutumia vitendo vya kuua, vitisho, uharibifu wa mali ndani ya jamii ya Kiislamu, kama ilivyokuwa kuhusu vitendo vya ulipuaji wa mabomu katika nchi za Waislamu suala hili linaitwa “Al-Hirabah” nayo ni ufisadi katika ardhi, na anayeifanya anastahiki adhabu kubwa ziadi kuliko adhabu ya anayeua, anayeiba, na anayezini; kwa sababu mwenye uhalifu huu anachukua hatua dhidi ya jamii. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa} [AL-MAIDAH 33].
Ama kuhusu vitendo vya ulipuaji wa mabomu yaliyotokea katika nchi za magharibi pia haviruhusiwi – hata kama tukiwa katika hali ya vita kweli pamoja nao – basi maana zilizotajwa kuhusu ukiukaji wa matini na makusudi ya Sheria na lazima ya ufisadi ipo katika vitendo hivi, pia hairuhusiwi kuwaua wanawake wasiopiga vita, watoto, wazee wanyonge, na walioajiriwa kwa kufanya kazi mbali na mambo ya kupiga vita. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} [AL-BAQARAH 190].
Imepokelewa kutoka kwa Imam Al-Tahir Ibn ‘Ashuur katika tafsiri yake kutoka kwa Ibn Abbas na Omar Ibn Abdul Aziz na Mujahid kuwa aya hii haikufutwa, akasema: “Kwa sababu maana ya wale wanaokupigeni ni wanaojiandaa kukupigeni yaani msipige vita wazee, wanawake, na watoto”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmithi kutoka kwa Sulaiman Ibn Buraidah kutoka kwa Baba yake alisema kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akimtuma mkuu wa jeshi alikuwa akimwusia kumcha Mwenyezi Mungu na kufanya mema kwa Waislamu ambao ni pamoja naye, akisema: “Piganeni kwa jina la Mwenyezi Mungu na katika njia na wale makafiri, piganeni lakini msipite kiasi, wala msiwakilishe kwa miili, wala msiue mtoto”.
Imepokelewa kutoka kwa Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Al-Murqaa Ibn Saifi kutoka kwa babu yake Rabaah Ibn Al-Rabii kaka yake Handhalah Alkatib kuwa alimwambia kwamba alitoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. katika vita na Khalid Ibn Al-Waliid alikuwa mbele ya jeshi, Rabah na maswahaba zake Mtume walipitia mwanamke aliyeuawa wakasimama wakimwangalia wakishangaa kutokana na umbile lake mpaka akawakuta Mtume S.A.W., akasimama mbele ya mwanamke yule, akisema: “Yule haruhusiwi kupiga vita”, akasema kumwambia mmoja: “Mfuate Khalid na mwambie msipige vita watoto wala walioajiriwa”.
Imam Al-Nawawiy amesema katika maelezo ya Muslim: “Wanazuoni waliafikiana kuhusu uharamu wa kuua wanawake, na watoto wakiwa hawakupigana vita”.
Kama tukifahamu kwamba sababu ya kupigana vita, basi wote wasiopigana vita wanaingia katika maandiko ya Kisheria yaliotajwa kama vile; vipofu, wagonjwa ambao hawana matumaini ya kupona, mwendawazimu, mtu wa mashambani, na mifano yao, na hawa wanaoitwa katika istilahi ya kisasa ni “raia”, basi hairuhusiwi kuwadhuru na kupoteza mali zao tena kuwaua, kwa sababu kuwaua raia ni miongoni mwa madhambi makubwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas