Kufunga Katika Nchi Ambazo Mchana H...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufunga Katika Nchi Ambazo Mchana Hurefuka Kuliko Kawaida.

Question

 Ninawaomba mnipe fatwa kwa njia ya maandishi kuhusu kufunga nchini Swiden, kwani idadi ya masaa ya kufunga katika mwezi wa Ramadhani kwa mwaka 1432 H. sawa na mwezi wa Agosti mwaka 2011, huzidi masaa 18 kwa siku. Na kuzama kwa jua (magharibi) ni baada ya saa tatu usiku, je tufuturu hali ya kuwa jua bado linaangaza?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Nchi ambazo haziko katika hali ya kawaida mpaka ikawa ni vigumu kwa muislamu kufunga: Hali kama hiyo itarejeshwa katika makisio na kuachwa alama ambazo Mwenyezi Mungu amehukumu kuwa ni sababu za kutendeka kwa hukumu za kisheria katika swala na katika funga. Kuanzia alfajiri, mapambazuko na kuzama kwa jua na kutoweka kwa mwanga hafifu wa machweo ya jua na mfano wake.
Kwa kuwa hali ya mwenendo wa Mwenyezi Mungu kurudisha hali ya mambo katika mazingira bila ya kuelezea hukumu juu ya hayo.
Hivyo wasomi wa Usuli na wasomi wa Fiqhi wanaona kuwa, lengo la sheria ni kwa kuzingatia maandiko (Aya, Hadithi, n.k.) kwa ujumla na huwa kwa hali zilizozoeleka baina ya watu katika maisha yao na pirika zao.
Al hafidh Ibn Hajar Al-Asqalaniy anasema katika kitabu cha: [Fat-hu Al-Bariy 2/62, Ch. Dar Al-Maarifah]: “Maneno –Maelezo- yameelezwa kwa kuzingatia hali ya kawaida iliyozoeleka, ama kuhusu picha -mazingira- yasiyo ya kawaida huwa hayazingatiwi.” Mwisho.
Na Al-Hafidh katika kitabu cha [Al fat-h 2/199] kutoka kwa Abi Al-Fat-hi bin Sayyid Annas Al-Yaamariy anasema: "Hukumu huzingatiwa kwa hali iliyozoweleka na si kwa mazingira yasiyo ya kawaida -nadra-" Mwisho.
Imamu Shihab Addin Al-Qurafiy anasema katika kitabu cha: [Al furuuq 1/359, Ch. dar al kutub al ilmiyyah]: "Msingi wa sheria unasema ni kuwa kitu kilichopo kikawaida na kilichopo kwa nadra basi kuwekwa -kitu cha nadra- katika vitu vya kawaida huwa ni afadhali zaidi". Mwisho. Na akasema [3/225]: "Kuzingatia neno kwa mambo ya nadra kutokea huwa ni kinyume cha ilivyokubalika, hivyo huwekwa katika hukumu ya mambo ya kawaida" Mwisho. Na akasema [4/223]: "Sheria imetengeneza hukumu zake kwa mambo ya kawaida" Mwisho.
Ibn Shat Al-Malik amesema katika kitabu chake cha: [Id-Raru Shuruuq A`la Anwari Al Furuuq 4/460]: "Hukumu za kisheria zimepokewa katika mambo ya kawaida na siyo ya nadra" mwisho.
Na mwanachuoni Abdul-Hamid As sharwaniy anasema katika kitabu chake juu ya [Tuhfatul muhtaj cha Ibn Hajar 4/273, Ch. Al maktabatul atujariyaah al kubra]: "Yakiwepo maneno ya kisheria basi huzingatiwa kwa yaliyo ya kawaida ama yaliyo nadra huwa hayazingatiwi" Mwisho.
Na mwanachuoni Ibn Abidin Al-Hanafy anasema katika kitabu cha: [Radu al muhtar a`la duri al mukhtar 2/123, Ch. Dar Al Fikr]: "Upunguzaji mbaya hauzingatiwi kama ilivyo katika urefushaji mbaya, na maneno kama yalivyo huzingatiwa kwa yale ya kawaida na sio yale yaliyofichikana na yaliyo ya nadra" Mwisho.
Hivyo, wasomi wengi wa misingi ya dini wamezingatia kuwa jambo la nadra na lenye kutokea mara chache haliingii katika mambo ya kawaida yaliyoenea; kwa ajili hiyo Imamu Shafi -radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie- anasema: "Jambo lisilo la kawaida hulazimika kuwa na maelezo yake maalumu, na jambo hilo haliingii katika maelezo ya mambo ya kawaida" Mwisho. Imepokewa kutoka kwa Imamu wa Makka na Madina katika [Al Burhanu katika Usuli Al Fiqhi 1/520-521, Ch. Kulliyatu Asharia Qatar].
Na Imamu Abu Fat-hi Bin Barhan anasema katika kitabu cha:[Al awswat]: "Mambo yasiyo ya kawaida yaliyo mbali kufikirika kiakili wakati wa kuyazungumzia na ambayo huchelewa kuingia katika ufahamu; basi haitafaa kwa maelezo yaliyokusanya (maelezo ya ujumla) kuyahusisha katika mambo hayo ya nadra kutokea; kwani sisi tumeweka ufahamu kuwa jambo kama hilo lisilo la kawaida silo linalokusudiwa katika sheria, kwa sababu ya kutoingia akilini" Mwisho.
Na imepokewa kutoka kwa Imamu Az Zarkashiy katika kitabu cha: [Al-Bahrul Muhit 3/56, Ch. Wizara wa Al Awqaf na Mambo ya Kiislamu, Kuwait).
Na waliosema katika wasomi wa misingi ya dini, kuwa maswala ya nadra huingia katika maswala ya kawaida, hawa huwa hawapingi uwepo wa dalili yake -kama itakuwepo; na hapo maswala huwa yana tafauti; kwani itakuwa:Je ni swala la ujumla lililo na dalili maalumu au swala la ujumla lakini lakusudiwa jambo maalumu? Hii ni tafauti ya kimatamshi ambayo haina matunda yeyote baada ya kukubaliana kuwa haiwezekani swala la ujumla likaingia katika swala maalumu.
Na jambo lililo karibu na hilo lililotangulia kuijaalia hukumu ya kisheria kwa mtindo wa mafumbo wakati inaposhindikana kuijaalia katika uhalisia wake, hapo itakuwa kwa mafumbo yenye kutumika kikawaida na sio yenye kutumika kwa nadra – mara chache:
Imamu ibn Al-Arabiy Al Maliki anasema katika kitabu cha: [Al Mahsuul katika Usuli Al Fiq-hi, uk. 99, Ch. Dar Al Bayariq]: "Hukumu ya Mtume –rehma na amani zimshukie- ni kama hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kuwa huzingatiwa ipo katika uhalisia wake, na wala haizingatiwi kuwa na mafumbo isipokuwa kwa kuwepo dalili yake. Na mafumbo yapo ya aina mbili: Yenye kutumika sana na yaliyo mageni na nadra kutumika. Ama yale yenye kutumika sana ni yale ambayo hutumika aya za hukumu za kisheria na maelezo yake. Na ama mageni na nadra: Ni yale yenye kutumia aya za mawaidha, ukumbusho, uogopeshaji na vitisho. Na hili linahitaji ujuzi katika kuelewa maana yake" Mwisho.
Na Sheikh Ibn Taimiyyah Al-Hanbaliy anarudia kusema, kuwa nyakati zilizotajwa katika sheria hizo huwa zimetajwa kwa kuzingatia masiku ya kawaida; anasema katika kitabu cha: [Mukhtaswar Al Fataway Al Misriyyah 1/37, Ch. Dar Ibnu El Qayyim): "Na nyakati ambazo Jibril –rehma na amani zimshukie- alizomfundisha Mtume –rehma na amani zimshukie – kwa umma wake wakati alipomuwekea wazi nyakati za sala, ndizo hizo ambazo walizozitaja wasomi katika vitabu vyao: Nazo ni katika masiku ya kawaida – yaliyozoeleka-, lakini ile siku ambayo Mtume –rehma na amani zimshukie ameisema kuwa “Siku moja ni kama mwaka” aliposema: "Ikadirieni kwa vipimo vyake, siku hii ina hukumu nyingine – ya pekee."
Kisha akasema: "Kinachokusudiwa ni kuwa siku hiyo haitakuwa na wakati wa alasiri: Kwa kuwa inatakiwa kivuli cha kila kitu kiwe mfano wake au mara mbili yake, lakini itakuwa siku ya kwanza kabla ya siku hii wakati wake ni mrefu sana, na kama itakavyo kuwa wakati wa Adhuhuri na Alasiri kwa siku hiyo ni kabla ya jua kuzidi nusu ya pili, na hivyo hivyo sala ya magharibi na isha –itakuwa- kabla ya kuzama kwa jua. Na hivyo hivyo sala ya alfajiri –asubuhi- itakuwa kwa makadirio ya wakati wa masiku ya kawaida. Na mwenendo wa jua hautaangaliwa; si kwa kuzidi nusu ya pili (wakati wa Adhuhuri) wala kwa kuzama (wakati wa magharibi) na wala kuondoka mawingu mekundu (kuingia wakati wa isha) na mfano wake" Mwisho.
Na kwa kufuatisha maelezo hayo katika maswala ya nyakati za sala na funga katika miji ambayo nyakati sio za kawaida, imamu Muhammad Abdo, Mufti wa Misri aliyetangulia –Mwenyezi Mungu amrehemu- anasema, kama alivyopokea mwanafunzi wake Muhammad Rashid Ridha katika kitabu cha: [Tafsirul manar 2/163, Ch. Al Manar]: (Mteremshaji wa Qur`ani –naye ni Mjuzi wa siri na Muumbaji wa ardhi na sayari– amewazungumzia watu wote kwa kile wawezacho kukifanya, akawaamrisha kusali, na Mtume –rehma na amani zimshukie akaweka wazi nyakati zake kwa mujibu wa miji ya kawaida; ambayo ndiyo iliopo katika eneo kubwa la Dunia hii. Mpaka uislamu ulipofika katika nchi za watu ambao mchana wake na usiku wake hurefuka kwa hali isiyo ya kawaida, hawa inawezekana kukadiria –kukisia- sala kwa kujitahidi na kupima kama alivyoeleza Mtume –rehma na amani zimshukie – hivyo hivyo kwa upande wa funga. Mwezi wa Ramadhani hautawajibika isipokuwa kwa aliyeuona mwezi.
Na kwa wale wasio kuwa na mwezi kama huo itakuwa ni wepesi kwao kukisia kwa makisio yake. Na wasomi wa Fiqhi wameeleza (maswala ya makisio) baada ya kuelewa kuwa kuna baadhi ya nchi zinakuwa na usiku mrefu na mchana mfupi, na nchi ambazo mchana huwa mrefu na usiku huwa mfupi, na wakatafautiana katika makadirio hayo, je wafuate nchi gani? Ikasemwa: "Katika nchi zenye hali ya kawaida ambazo sheria imeshuka, kama Makka na Madina. Inasemwa pia, kwa nchi iliyo karibu nayo ambayo ina nyakati za kawaida, na hayo yote yanafaa, kwani jambo la kujitahidi huwa halina maandiko (Aya, Hadithi). Mwisho.
Imamu Mahmud Shaltut sheikh wa Al Azhar aliyetangulia mbele ya haki –Mwenyezi Mungu amrehemu- anasema katika kitabu cha: [Al-Fatawa uk. 125, Ch. Dar As Shuruq]: "Hapana shaka kuwa nyakati za swala za usiku na mchana na kueleza kuhusu mwezi katika mwaka –kwa namna iliyozoeleka na kufahamika kutoka kizazi hadi kizazi- imekuwa hivi kutokana na kuwafikiana katika mazingira ya nchi zenye hali ya kawaida ambazo nyakati zake za usiku na mchana huwa maalumu, na Ramadhani huwa katika miezi maalum katika mwaka, na maeneo haya ni makubwa katika ardhi, -nchi hizi zipo nyingi duniani- na watu hawakuwa wakijua wakati wa kuteremka kwa sheria kuwa ardhi ina pande ambazo huwa mwaka wake ni kwa mchana na usiku (uliokamilika) na kuna pande ambazo mwaka wake huwa kwa mchana nusu na usiku nusu, na pande nyingine mchana wake huwa mrefu na hauwi usiku wake isipokuwa kwa muda mdogo sana, na pande nyengine usiku wake huwa mrefu na mchana wake ni mfupi sana" Mwisho.
Na Sheikh Imamu Jad Al-Haq Ali Jad Al-haq anakariri kwa kusema kuwa, sheria ya kuanza kufunga kuanzia asubuhi mpaka magharibi: "Imewekwa kwa kuzingatia mazingira ya kawaida, ikiwa na maana kuwa katika miji ya kawaida na sio kwa hali zisizo za kawaida au zilizopo katika ncha mbili za dunia au zilizo karibu na hizo Kama ilivyokuja kujulikana baada ya kuteremka kwa sheria." Mwisho.
Na mwanchuoni mwingine Sheikh, Mustafa Al-Zarqa anasema katika kitabu chake [Al Aqlu na Al Fiqhu katika Fahmi Al Hadithi An Nabawiyi Uk. 124, Ch. Dar Al Qalam): "Hadithi za mtume zilizopokewa inapaswa kuchukuliwa kuwa zimeelezea kuhusu mazingira ya kijiografia na kisayari katika bara arabu na sio kwa dunia nzima ambayo sehemu kubwa ilikuwa ni bara au bahari isiyojulikana kwa kuwa haikuwa ikijulikana kwa kitu chochote wakati huo, lakini kwa maeneo haya yasiyojulikana -kaskazini na kusini- ambayo yamegunduliwa baadae -itabidi yazingatiwe kuwa ni maeneo yaliyonyamaziwa kwa hukumu za nyakati za swala na funga, maeneo hayo yatalazimika kutumika juhudi inayoambatana na malengo ya sheria" Mwisho. Ingawa kuna ziada ya maelezo kidogo.
Na kufanya makadirio na kuacha dalili hapa kuna ishara za kisheria: nayo ni Hadithi iliyopokelewa kuhusu habari za Dajjal, ambazo amepokea Imamu Muslim katika kitabu chake na wapokezi wengine kutoka katika Hadithi ya Nawas bin Sam`an -radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie- wakati Mtume – rehma na amani zimshukie- alipokuwa akihadithia kuhusu habari za Dajjal, tukamwambia: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, huyo kiumbe atakaa kwa muda gani katika ardhi? Akasema: “Siku arobaini, siku moja ni kama mwaka mmoja, na siku nyingine ni kama mwezi, na siku nyingine ni kama Ijumaa, na baki ya masiku ni kama masiku yenu mengine ya kawaida.” Tukamwambia: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hiyo siku itakayokuwa kama mwaka, je itatutosheleza kuswali? Akasema: “Hapana, ikisieni kwa makadirio yake”.
Na hali ya masiku ya kutokezea Dajjal ni hali ya kufichika kwa nyakati, na hali hii ndio inayodhihirika katika ncha mbili za Dunia Hii ambazo usiku huendelea kwa miezi sita na mchana vile vile. Na wasomi wakaliona hili la kuwepo kwa utafauti wa nyakati katika maeneo yaliyo karibu na ncha mbili za Dunia ambazo mchana huwa mrefu na usiku huwa mfupi. Kwa kuwa sababu hizo zipo, nazo ni kutofanana kwa nyakati za kawaida ambazo zimeelezwa na Sheria yenye kuhusu maswala ya ibada; na kila inapokuwapo hali ya kufichika –kwa wakati- basi hali ya kuparaganyika –nyakati – pia hujitokezea.
Mwanachuoni Ibn Abidin Al-Hanafiy anasema katika kitabu chake [Rudu l muhtar a`la duri l mukhtar 1/366, Ch. dar fikri]: "Inaendelea: Sikumwona aliyefikwa katika sisi na hukumu ya funga zao iwapo alfajiri inachomozea kwa upande wao kama linavyozama jua au baada yake kwa muda ambao aliyefunga hawezi kukadiria kufuturu kwa mujibu wa nia yake, na haiwezekani kusemwa kuwa ni lazima kuendeleza kufunga kwa upande wao, kufanya hivyo ni kujidhuru –kutokana na muda mrefu wa kufunga- na iwapo tutasema ni lazima wafunge basi itatulazimu kukisia. Na je hukisiwa kwa nchi iliyo karibu nao kama walivyosema kina Shafi au hukisiwa kwa muda wa –makadirio ya – kuvumilika kwa kutokula chakula na kuwa na kiu au itawalazimu kuzilipa funga hizo na si kufunga kwa wakati wake? Yote haya yanawezekana. Na wala haiwezekani kusema kuwa funga kwao sio lazima. Kwa kuwa sababu ya kufunga imepatikana nayo ni kuonekana kwa sehemu ya mwezi na kuchomoza kwa alfajiri. Hili ndilo naliona liko wazi sana kwa upande wangu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi" Mwisho.
Na Imamu Hafidh Asuyut Ashafi anasema kwa njia ya ushairi katika kitabu cha: [Al Hawiyu Lil Fatawi 2/304, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah] ni jawabu juu ya muulizaji:
Kwa wale lisilozama jua kwao wakati wa mchana ** watakisia swala na Alfajiri hivyo hivyo
Na watatekeleza funga, na sala walizoziacha ** kama sala inaisha kwa kuwa faradhi
Watafuturu na kulipa sala ya faradhi ya Magharibi? ** na hukumu ya sala ya Isha itakuwaje? Nipeni jawabu
Ama kuhusu swali la hamsini na tisa na la sitini: Jawabu lake: Burhani Al Fazaziy ametoa jibu kwa kuwajibika sala ya Isha katika hali kama hii, na waliokuwa nae kwa zama hizo wakasema kuwa hailazimiki kwao; kwa sababu ya kutokuwepo kile chenye kulazimisha haki yao nao ni wakati. Na hali ya kwanza inatiliwa mkazo na Hadithi iliyopokewa kuhusu masiku ya dajjal aliposema “kisieni kwa makadirio yake”. Na Azzarkashi anasema katika kitabu cha: [Al Khadim] na juu ya hili: Watapewa hukumu ya Ramadhani kwa kuwa watakula usiku mpaka kuchomoza kwa alfajiri kwa kuzingatia nchi ya karibu nao, kisha watajizuia na kufuturu mchana kabla ya kuzama kwa jua pindi kama litakuwa lishazama kwa nchi ya jirani –ya karibu – nao, kama watakavyokula waisilamu siku za Dajjal na kufunga" Mwisho.
Na makadirio haya ya kutokuwa kikawaida kwa masiku yamechukuliwa katika majaribio halisi: Nayo ni masaa kumi na nane na ziada, nayo ni nusu siku na nusu nyingine. Na ni vigumu kwa mtu kufunga masaa kumi na nane na ziada kwa mfululizo. Nayo ni kwa maneno ya wenye fani zao ambao wamekiri kuwa kujizuia kutokana na chakula na kinywaji kwa muda huu wote bila ya shaka unasababisha matatizo katika mwili wa kiumbe. Kwa kuzingatia hali halisi ya kiumbe na uwezo wake wa kimwili, na ilivyokuwa ni hivyo basi haitasihi sheria kumkalifisha mtu –kwa asiloliweza.
Na katika makadirio ya nyakati kutokuwa za kikawaida Sheikh mwanachuoni Mustafa Az Zarqa anasema katika kitabu chake [Al Aqlu Wa Al Fiqhu Fiy Fahmi Al Hadithi An Nabawiy, Uk. 124]: “Ikisemwa, iweje iruhusiwe watu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa jua bado lingalipo hata kama halizami isipokuwa kwa nusu saa au saa?”
Tutasema: Hali hii ni kwa nchi ambazo usiku wake ni miezi sita na mchana wake ni miezi sita. Kwani nyie mumekubaliana kuwa watafurutu mchana wake uliokuwa mrefu wakati ambapo mmewawekea mipaka hata kama jua lingalipo, je hili haliwadhuru. Kwa sababu ya dharura. Na jambo lililo muhimu hapa ni; kuchunga malengo ya sheria katika kuziweka sala katika nyakati zake, na kwa kukadiria muda wa kufunga kwa namna ambayo haitakuwa kwa kumkalifisha mtu asiloliweza, na hapo makusudio ya kisheria yatapatikana bila ya kupungua.” Mwisho
Na haisemwi: Atakayeshindwa na kufunga wakati huo basi na afuturu, na atalipa katika masiku mengine ambayo ataweza kufunga, hekima yake juu ya jambo hili -la kufunga- ni kama ilivyo katika hekima ya mambo mengine na kwa kuwa sheria ya kufunga ni kuanzia alfajiri mpaka kuzama kwa jua na hili ni kwa miji yote na sio kwa miji maalumu na kwa watu maalumu.
Sisi tunasema hivi kwa kuzingatia amri ya kukalifishwa ambayo watu wengi huiweza kisha kwa wengine hutokezea hali ambazo wanashindwa kuzimudu. Kwa jambo ambalo linaeleweka na ikawa mwili wa mtu hauwezi kulimudu hata kidogo na wataalamu wakathibitisha kuwa jambo hilo lina madhara kwa mtu aliyekalifishwa awapo katika hali yake ya kawaida, hapo sheria haitamlazimu kulifanya jambo hilo. Na wala haisemwi: Atakaeshindwa basi atafuturu na kulipa; kwa kuwa hivi itapelekea kutokuwepo kwa kulazimishwa kwa funga yenyewe au kumletea madhara mtu aliyekalifishwa na sheria kwa kumuingiza katika matatizo kwa kumharibia kazi zake na masilahi yake, na kumchanganya katika maisha yake na mambo yake iwapo hali ni hiyo hivyo hata katika miaka mingine. Au kufunga katika miezi mengine –badala ya mwezi wa Ramadhani- ambao umekaribia na miezi ya kawaida iwapo utakuwa ndani ya mwaka huohuo au wakati wa kuondoka kwa hali isiyo ya kawaida –katika mwezi huo- yote hayo hayamo katika hekima ya sheria ya kufunga.
Hivyo marehemu Mahmod shaltut –Mwenyezi Mungu amrehemu - akaona jambo hilo lisiwepo; akasema katika kitabu cha: [Al Fatawa Uk, 126]: "Hapana shaka kwa yanayojiri katika maeneo hayo kwa kubainisha nyakati ambazo hujulikana kwa sala na kufunga itapelekea kwa muislamu kusali usiku wake na mchana wake -nayo ni kwa mwaka kamili- sala tano pekee zitakazogaiwa katika nyakati tano kwa mwaka mzima. Na hiyo itapelekea kwa baadhi ya maeneo kuwa sala za lazima –za faradhi- ziwe ni nne au chini ya hapo, kwa mujibu wa urefu wa mchana na ufupi wake. Hivyo hivyo itapelekea kumkalifisha muislamu katika maeneo hayo kuhusu kufunga Ramadhani ambapo -katika maeneo hayo- hakuna Ramadhani. Na baadhi ya maeneo itapelekea kufunga kwa masaa ishirini na tatu katika masaa ishirini na nne, na yote haya ni ukalifishaji ambao hekima itokayo kwa Mwingi wa Rehema inakataa. Hivyo inapasa kuondoshwa namna hii ya kukalifisha –ulazima- wa faradhi hii."
Na mwanachuoni Mustafa Az Zarqa anasema katika kitabu chake: [Al Aqlu Wa Al Fiqhu Fiy Fahmi Al Hadithi An Nabawiy Uk, 124] "Na kuenea kwa jambo hili ni kwa kutokea kwa tofauti baina ya usiku na mchana bila ya kuangalia tafauti kubwa iliyopo kati ya kila wakati -mcha na usiku-: Hili itatofautiana sana kwa malengo ya makusudio ya sheria na kauli ya “Kuondoa matatizo”. Kwani haiingia akilini kuzigawa sala za mchana au za usiku kwa nusu saa kwa mfano, na wala haiingi akilini kufunga kwa saa moja na kufuturu masaa ishirini na tatu." mwisho, pamoja na mabadiliko madogo.
Pendekezo kwa watu wa miji hiyo: Wakisie funga kwa nyakati za Makka; kwani Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni mama wa Miji, na mama ni asili, naye ndie anayekusudiwa siku zote na si kwa kuelekea kibla pekee lakini pia kwa makisio ya nyakati pindi kama hazitokuwa sawa.
Ama kukisia makadirio kwa nchi iliyo karibu ni makadirio ya hali ya utata sana, na wasemao kuwa inafaa basi wameweka masharti ya; urahisi wa kujua makadirio ya uhakika ya nchi iliyo karibu nayo sana bila ya matatizo au utata. Na hali hizo zote zinahitaji majaribio na utendaji, si hivyo tu lakini pia humuweka muislamu katika hali ya kutojielewa. Na jambo hili ndilo lililompelekea Imamu Jad Al Haq Sheikh wa Al-Azhar aliyetangulia kuona kuwa ni vigumu kulifuata na kupendelea wazo la pili, kwa kuwataka watu wa nchi ambayo mchana wake unarefuka kuwa waende sambamba na nyakati za Makka au Madina Munawara. Akasema -Mwenyezi Mungu amrehemu- "Inawezekana isieleweke ujuzi wa makadirio ya uhakika kwa nchi iliyo karibu na Norway, hivyo nahisi kuwataka waislamu wanaoishi katika nchi hizi kufunga kwa idadi ya saa ambazo hufunga waislamu wa Makka au Madina, kwa kuanza kufunga inapochomoza Alfajiri ya kweli kwa mujibu wa maeneo yao, bila ya kuangalia au kuchunga makadirio ya saa za usiku na mchana, na kuendelea kufunga mpaka jua litazame au kutoweka mwanga wake kwa kuingia usiku. Na hivi ni kwa kufuata rai za wasomi katika makadirio ya nyakati za sala na kufunga, na kwa kutoa hoja kupitia Hadithi ya Dajjal iliyotangulia kutajwa, na kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu na muongozo wa Kurani Tukufu ambayo ni rehema kwa walimwengu." Mwisho
Na kwa waliosema inafaa kwenda kwa makadirio ya Makkah katika kufunga kwa watu ambao mchana wao huwa mrefu na usiku huwa mfupi, rai hii wameikubali wasomi wakubwa wa kisasa, kwa kuanzia na kiongozi wa mwanzo wa cheo cha [Muf-ti wa Misri] Profesa Imamu Muhammad Abdo -Mwenyezi Mungu amrehemu- na rai hii imetolewa kwa kuwakumbusha wengine na kunasibishwa kwa wasomi wengine katika maswala kama haya –yaliyotangulia– Na rai hii ndio inayotumika na ndiyo inayotegemewa na Baraza la Fat-wa la Misri. Kwa kuanzia Sheikh Imamu Jad Al Haq Ali Jad Al Haq [Fat-wa nambari 214 mwaka 1981]. Kwenda kwa sheikh Abdullatif Hamza [Fat-wa nambari 160 mwaka 1984.]. na Prof. Imamu Muhammad Sayyid Tantawi [Fat-wa nambari 171 mwaka 1993. na nambari 579 mwaka 1995]. na sheikh Prof. Nasri Farid Wasil [Fat-wa nambari 437 mwaka 1998]. na kumalizia na Mufti wa Misri aliyepo Prof. Ali Juma –Mwenyezi Mungu amhifadhi. Wote hawa wametoa Fat-wa hiyo hiyo iliyotajwa. Nayo pia ni rai ya Mhe. Prof Muhammad Al-Ahmadiy Abu Nur Waziri wa Mambo ya Wakfu aliyetangulia na ni mjumbe wa Jopo la Wanazuoni wa Utafiti wa Kiislamu katika Kamati ya Al-Azhar iliyotolewa tarehe 24/4/1983. Na Mhe. Sheikh na mwanachuoni Mustafa Az Zarqa. Na Prof. Muhammad Hamid Allah katika kitabu chake (Al islamu). Na Mhe. Mahmod Ashur Wakili wa Azhar wa zamani na Mjumbe wa Jopo la Wanazuoni wa Utafiti wa Kiislamu, na wengineo katika wasomi wa elimu ya kisasa. Na rai hii ndiyo inayotumika kwa taasisi za utoaji wa fat-wa za kisheria Ulimwenguni. Mfano jopo la wanazuoni la utoaji wa fat-wa la Aman – Jordan, kwa kuwekwa saini na Mufti Mkuu Sheikh Muhammad Abdo Hashim mnamo tarehe 19/9/1399 H. na hili ndilo tulionalo na linaloendana na makusudio ya sheria na lililo jepesi zaidi kwa uchungaji wa masilahi ya viumbe.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas