Maana ya Kunusuriwa kwa Kuingizwa K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Kunusuriwa kwa Kuingizwa Khofu Katika Nyoyo za Maadui.

Question

 Nilisoma Hadithi moja ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: “Mimi nimeletwa na kuteremshiwa Qur’ani iliyo kusanya habari zote, na nimenusuriwa kwa kuingizwa khofu nyoyo za makafiri. Na nilipo kuwa nimelala nilijiwa na funguo za hazina za ardhi yote zikatiwa mkononi mwangu”.
Je, Hadithi hii ina maana ya kwamba Uislamu ni dini ya ugaidi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Masheikh wawili (Al-Bukhari na Muslim) kwa maneno yale yale, pia imepokelwa kwa maneno mengine. Maana ya Hadithi hii haina uhusiano wowote na ugaidi, lakini ni miongoni mwa bishara ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake S.A.W. wakati anapowapiga vita maadui wake, Mwenyezi Mungu anaingiza khofu nyoyoni mwa maadui wake wanaopiga vita ili washindwe kisaikolojia kabla ya kushindwa kijeshi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote” [AAL IMRAAN: 151]. Wanazuoni wa Tafsiri walisema: “Maana yake ni yale yaliyoingizwa nyoyoni katika siku ya Uhud mpaka Washirikina waliacha kupigana vita wakarudi pasipo na sababu yoyote na walikuwa na nguvu” [Tafsiri ya Abi Al-Saud 2/98, Dar Ihyaa Al-Turath].
Halafu Mtume S.A.W. aliwabashiria Masahaba waliokuwa masikini wakati ule na hawana mali yeyote kwamba Mwenyezi Mungu atawafungulia hazina za ardhi. Waarabu walikuwa na mali chache kuliko wengine, Mtume S.A.W. aliwabashiri kwamba mali ya Kisra na Kaisari zitakuwa mikononi mwao na watamiliki hazina zake, na jambo hili ni miujiza ya unabii wake S.A.W; ambapo yalitokea yaliyosemwa na Mtume S.A.W. na Mwenyezi Mungu akawafungulia hazina za dunia kupitia baraka ya biashara na aliwafungulia nyoyo za walimwengu wote kabla ya kuzifungua nchi zao.
Mtume wa Mwenyezi Mungu alifariki na hakupata chochote kutoka katika hazina hizo, lakini alizigawa kati ya Waislamu na akawapenedelea wao, baada ya kufa kwake Waislamu walipata ushindi kama Mtume S.A.W. alivyowaahidi Masahaba wake.
Historia ya heshima ya Waislamu haina dosari yeyote, yaani haikuwa na Baraza la Ukaguzi wala haikuwa na kumwaga damu, wala kuwafukuza wenyeji wa asili. Na hakuna uhusiano wowote kati ya Hadithi tukufu hii na kuiba mali za wengine. Hairuhusiwi kwa Mwarabu yeyote anayefahamu Kiarabu afikiri hivyo, lakini hali hii inawezekana kufahamika kupitia kutafsiri neno kwa neno kwa nia ya udanganyifu na uongo na kugeuza fadhila na miujiza kwa mambo mabaya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas