Kukopa Benki Kwa Riba

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukopa Benki Kwa Riba

Question

 Sisi ni wanachama wa Jumuiya ya kiislamu hapa mjini Muelheim, Ujerumani. Idara ya serikali mjini hapa ilituambia kuwa mahali pa Jumuiya yetu pataingia katika mpango mpya wa mtaa, na tunalazimika kutafuta mahali pengine, na tumekwisa afikiana na kiasi cha fedha kama fidia, nacho ni karibu Yuro nusu milioni.
Baada ya kutafuta tumekuta jingo linalofaa kwa upande wa vifaa na ukubwa wa maeneo ndani na nje ya jingo hilo. Jengo hili bei yake ni Yuro milioni moja, laki tatu na hamsini, na hii ina maana ya kwamba sisi tutahitaji kiasi cha Yuro karibu laki saba, baada ya kuongeza kiasi cha michango iliyopo hivi sasa.
Kwa hiyo tumefungua mlango wa michango na mikopo mizuri, na tukawaomba ndugu zetu wote pamoja na wafanyabiashara kuchangia katika mradi huu, ili tusije kulazimika kukopa katika benki zenye riba, lakini kwa masikitiko makubwa hatukuweza kupata kiasi kinachotakiwa kwa ajili ya kununua jingo hilo. Hivi sasa tuna pendekezo kutoka kwa benki ya Ujerumani ya ugharamiaji wa ujenzi wa majengo kutukopesha kwa riba inayokaribia kiasi asilimia tano utakaolipwa kwa muda wa miaka kumi. Je inajuzu kisheria kukopa benki hii ili tuweze kulinunua jingo hili jipya?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy wanajuzisha kutendeana na wasio waislamu katika nchi zisizo za waislamu kwa mujibu wa mikataba isiyo sahihi, ikiwa kwa maridhiano yao kama vile kuuza mvinyo, nguruwe na riba n.k., miongoni mwa matendeano yasiyo sahihi kwa waislamu. Na haya yanalingana na hali ya mwenye swali, kwa sababu asili ya wale ambao waislamu hununua kwao si waislamu..
Wafuasi wa madhehebu ya hanafiy walitoa dalili nyingi kuhusu swala hili, miongoni mwake Hadithi Mursal ya Makuhuul iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W kuwa amesema: “Hakuna riba kati ya waislamu na watu wa vita katika nyumba ya vita”nayo imetajwa na Al-Shafiy katika kitabu cha Al-Umm, 7/359; Al-zailai’y katika kitabu cha Nasbu-rayah, 4/44; Ibn Hajar katika kitabu cha Al-Dirayah Fi Takhriij Ahadith Al-hidayah, 2/158; Ibn Qudamah katika kitabu cha Al-Mughniy, 4/47, lakini aliielezea kuwa: Hadithi hiyo ni Mursal na usahihi wake haujulikani, na huenda alikusudia kuzuia jambo hilo. [mwisho].
Miongoni mwa dalili zao kuwa Mtume S.A.W alipowahamisha Bani Qainuqaa’ walisema: Tuna madeni kwa watu na bado haujafikia wakati wa sisi kulipwa, akasema Mtume: “Zichukueni upesi au ziacheni”, na alipowahamisha Bani-Nadhiir walisema: Tuna madeni kwa watu akasema: “ziacheni au zichukueni upesi”, na inajulikana kuwa matendeano kama hayo kati ya waislamu ni miongoni mwa riba, basi nayo siyo sahihi.
Pia walitoa dalili ya Mtume S.A.W kupigana mieleka na Rukanah alipokuwa Makkah,ambaye alikuwa kafiri, na Mtume S.A.W alimshinda, kila mara kwa theluthi ya kondoo wake, na Makkah katika wakati huo ilikuwa nyumba ya ukafiri, lakini Mtume S.A.W kwa fadhila yake na ukarimu alimrudishia kondoo wake. Asili ya kisa hiki alikipokea Abu-Dawuud na Al-Tirmidhiy pasipo na kutaja kondoo, lakini kondoo wametajwa katika Hadithi Mursal za Abi-Dawuud na wengineo.
Hivyo walitoa dalili ya Hadithi iliyopokelewa na Ibn Abbas R..A na wengineo kuwa Mtume S.A.W alisema katika hotuba ya kuaga: “Kila riba iliyokuwa katika wakati wa ujahili sasa imetenguliwa, na riba ya kwanza kutenguliwa ni riba ya Al-Abbas ibn Abdel-Muttalib”, Na upande wa dalili hapa kuwa Al-Abbas alisilimu katika Badr baada ya kufungwa kwake, akarejea Makkah alikuwa anakula riba, na tendo lake hili halifichikikwa Mtume S.A.W,na Mtume S.A.W hakumkataza, na hii ni dalili ya kujuzu.Kuhusu riba iliyotenguliwa nayo ni riba ambayo haikukabidhiwa hadi wakati wa kufungua Makkah na ikawa nyumba/mji wa Uislamu.
Hivyo walitoa dalili kuwa As-Siddiq Aba-Bakr R.A alijadiliana na washirikina wa Quraish kabla ya Al-Hijrah, wakati alipoiteremsha Mwenyezi Mungu kauli yake: {Alif Lam Mym. Warumi wameshindwa}. [AR RUM: 1-2], Quraish walimwambia kuwa: Wao na kuwa warumi watashinda? Akajibu naam, wakasema: Unakubali kuwekea na rehani nasi? Akasema naam. Hapo wakawekea na rehani kisha akamwambia Mtume S.A.W, na Mtume S.A.W akasema: “Waendee ninamzidishe rehani”, akafanya hivi, na baadaye Warumi wakawashinda Waajemi, hapo Abu-Bakr R.A akashinda rehani, na Mtume S.A.W alikiri hiyo. Na hii ni aina ya kamari ambayo wanatendeana nayo huko Makkah wakati ilikuwa mji wa ukafiri. [Rejea: Al-Mabsuut, 14/57; Fathul-qadiir, 6/178].
Kwa mujibu wa dalili hizi na nyinginezo Imamu Muhammad bin Al-Hasan anasema: Mwislamu akiingia nyumba /mji wa vita kwa ahadi ya amani hakuna kosa kuchukua malizao kwa maridhiano ya nafsi zao kwa vyovyote. [Rejea; Sharh As-Siyar Al-Kabiir, 4/141.]
Al-Sarkhasiy anasema: “Hakuna riba kati ya waislamu na watu wa nyumba / mji wa vita katika nyumba / wa vita, na kuhusu Hadithi Mursal ya Makuhuul ni dalili kwa Abi-Hanifana Muhammad, Mwenyezi Mungu awarehemu, kuwa inajuzu kwa mwislamu kumwuza kafiri dirham moja kwa dirham mbili katika nyumba / mji wa vita…, vile vile akiwauzia nyamafu au akacheza kamari nao, na akachukua mali zao kwa njia hiyo, na mali hii ni halali, kwa mtazamo wa Abi-Hanifana Muhammad, Mwenyezi Mungu awarehemu”, [Rejea; Al-Mabsuut14/56]. Na kauli za maimamu wawili Abi-Hanifana Muhammad ndiyo inayotegemewa na kuchaguliwa na wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy.
Kwa muhtasari Abu-Hanifana Muhammad, kinyume cha Abi-Yusuf, wanaona kuwa inajuzu kutendeana kwa mikataba isiyo sahihi katika nyumba / mji wa wasio waislamu kati ya mwislamu na wasio waislamu, na rai hii inapingana na madhehebu mengine ambayo yanaona uharamu wa matendeano haya yakiwa katika nyumba / mji wa vita au nyumba / mji wa Uislamu.
Kwa mujibu wa hayo Jumuiya iliyouliza swali ina hiari ya kufuata rai ya Abi-Hanifana Muhammad, Mwenyezi Mungu awarehemu, na misingi ya kisheria inayojuzisha hivi nao, kwa sababu wanachuoni wanasema kuwa mtumzi maana hiari ya kufuata rai ya aliyejuzisha kitu miongoni mwa vitu vyenye hitilafu, hasa ikiwa kufuata rai ya aliyekataza na kuharamisha kutamsababishia shida na ugumu. Kwa hiyo wanasema: Anayetahiniwa kitu kama hiki yaani vitu vyenye hitilafu kati ya uhalali na uharamu ana haki ya kumfuata aliyejuzisha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas