Kukodi Mfuko wa Uzazi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukodi Mfuko wa Uzazi

Question

Kutokana na maendeleo makubwa yaliyofikiwa ya kisayansi katika nyanja mbalimbali tumekuwa tukisikia kila siku kugundulika mambo mapya, na masuala ya tiba kwa ujumla ni katika nyanja ambazo ndani yake kunaonekana maendeleo haya, kitengo hasa cha uzazi wa kutengenezwa ni katika vitengo vya tiba vyenye kukua haraka, haupiti muda mrefu isipokuwa kupitia vyombo vya habari vinatueleza baadhi ya gunduzi za kitiba na sayansi mpya.

Answer

Cheche za kuanza kwa nyanja hii zilikuwa pale alipozaliwa mtoto wa kwanza wa kike kwa njia ya upandikizaji wa kutengeza mwishoni mwa miaka ya sabini ndani ya karne iliyopita, tukio hilo likawa ndilo gumzo la mjini wakati huo, tokea wakati huo ikawa tiba ya uzazi wa kutengeneza katika mapinduzi endelevu na kuendelezwa siku zote.

Miongoni mwa kukuwa kwa kitengo hiki katika vitengo vya tiba ni pamoja na kinachofahamika kama “Mfuko wa uzazi mbadala” na sura yake ni kuingiza yai la mwanamke kwenye maji ya uzazi ya mume wake kisha kuingizwa tena kwenye kifuko cha uzazi, na anapozaliwa mtoto  hukabidhiwa kwa wanandoa.

Sababu ya kutumia njia hiyo ni nyingi: Kama vile mtu kuondolewa kifuko cha uzazi kwa upasuaji na kubakia salama mayai yake, au kuwepo kosoro kubwa za kimaumbile, au ujauzito unamsababishia maradhi makali, kama kuharibika kwa ujauzito au kuhifadhi mwili na kuepukana na matatizo na shida za ujauzito na kujifungua.

Sura hizi hivi karibuni zimeenea sana nchi za Magharibi, na mwanamke amekuwa hugharamia kifuko chake cha uzazi ili kukibebesha mayai ya mwengine hufanya hivi kwa malipo yanayofahamika “Wakodishaji matumbo”, vitendo hivi vimeanza kujaribu kupenya na kuingia kwenye ulimwengu wetu wa Kiislamu, yafuatayo ni maelezo kuhusu hukumu ya jambo hili na yatokanayo miongoni mwa athari zinazotokea.  

MLANGO WA KWANZA

Maelezo ya hukumu ya Kisharia ya ukodishaji wa mfuko wa uzazi

Somo la kwanza

Dalili za uharamu

Katika mambo ambayo yamekuwa na dalili nyingi ni uharamu wa kukimbilia njia ya mfuko wa uzazi mbadala, ni sawa sawa kwa kujitolea bure au kwa malipo, na haya yameelezwa na Jamhuri ya Wanachuoni wa sasa, na dalili hizo zimefikiwa kwenye maamuzi namba “1” ya kituo cha tafiti za Kiislamu nchini Misri kwenye kikao chake kilichokaliwa siku ya Alkhamisi tarehe 29/March/ 2001, na baraza la kituo cha tafiti Sharia za Kiislamu lilitoa maamuzi yake katika mkutano wake wa nane uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya nchi za Kiislamu duniani huko Makka kuanzia siku ya Jumamosi mwezi 28/Mfungo Saba/1405H mpaka jumatatu mwezi 7/Mfungo Nane/1405H sawa na tarehe 19 – 28/January 1985.

Dalili ya Kwanza: Kauli ya Mola: {Na ambao wanazilinda tupu zao * Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa * Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka} Al-Muuminun: 5 – 7, hakuna tofauti katika ulazima wa kulinda tupu kati ya mwanamke na mwanamume, na kulinda tupu kunakusanya pia kulinda tupu ya mwingine, vilevile kulinda matamanio.

Dalili ya Pili: Asili katika tupu ni haramu, wala haihalalishwi isipokuwa kwa Andiko la Sharia, na kifuko cha uzazi ni sehemu ya tupu, kama vile tupu haihalalishwi isipokuwa kwa makubaliano sahihi ya Kisharia, vilevile kifuko cha uzazi haifai kukifanyia kazi ya mwingine kwa ujauzito wa mume, hivyo asili ya uharamu inabakia palepale ([1]).

Dalili ya Tatu: Kifuko cha uzazi si kitu kinachowezekana kutolewa na kuwezekana kuwa halali hakifai kukitoa kama zawadi kwani Sharia imeharamisha kustarehe kwa asiyekuwa mume na tupu ya mwanamke, kwa sababu kustarehe nayo kunapelekea kuufanyisha kazi mfuko wa uzazi wa huyu mwanamke ambaye ametumia tupu yake kwa kuingiza tone la manii ambapo Sharia haijaruhusu kuliweka hapo isipokuwa katika wigo wa mahusiano ya ndoa inayotambulika kisharia, hivyo mfuko wa uzazi pia unakuwa si wenye kukubali kutumika na haikubali uhalali na kwa hivyo ni bora zaidi kutofaa, na hilo ni kwa ajili ya kulinda usahihi wa nasaba([2]).

Na kisichowezekana kukitoa kuwa halali hakifai kukitoa zawadi, vilevile haifai kukikodisha, kwa sababu kukodisha: “Ni makubaliano ya kunufaika yanayofahamika yenye kukubali matumizi na uchafu kwa malipo maalumu”, Wanachuoni wa Sharia wameelezea kauli yao katika maana ya: “Kukubali matumizi na kuhalalika” ni kwa kufikiwa masilahi ya tupu, kwani yenyewe si yenye kukubali matumizi na haikubali kuhalalika([3]).

Dalili ya Nne: Uwepo wa shaka ya kuchanganyika nasaba kutokana na uwezekano wa kufeli kazi za uwekaji tone ndani ya kifuko cha uzazi kilichokodiwa, na unatokea ujauzito kwa njia ya kukutana mume na mke wake, ikadhaniwa kuwa ujauzito na mtoto wa aliyekodiwa pamoja na kuwa ukweli si wa kwake.

Vilevile shaka hii inapatikana katika kuendelea mume kukutana na mke wake akiwa amebeba mayai ya uzazi, kwa sababu kiinitete lishe yake ni maji ya uzazi ya mwanamume, kama vile kinapata lishe kutoka kwa mama mjamzito.

Limepokelewa katazo la wazi kuhusu kumuingilia mwanamke mjamzito ambaye unatokana na upande huu, kutoka kwa Ruwaifaa Ibn Thabiti Al-Ansary R.A. Mtume S.A.W. amesema: “Si halali kwa mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kumwagilizia maji yake shamba la mwingine”, kwa maana: Kuyaingiza kwa mjamzito, na katika mapokezi mengine:  “Wala asimwage maji yake kwa mtoto wa mwingine”([4]).

Ibn Qayyim amesema: “Usahihi ni kuwa ikiwa atamuingilia mwanamke mjamzito basi ujauzito unakuwa ni sehemu inayotokana na yeye, kwani kuingilia kunaongeza umbile la mtoto…..Imamu Ahmad amesema: Kuingilia kunaongeza usikivu wake na kuona kwake, na Mtume S.A.W. amesema wazi kwa maana hii katika kauli yake: “Si halali kwa mwanamume kumwagilia maji yake shamba la mwingine”, inafahamika kuwa maji ambayo humwagilia mmea huzidisha na kutengeneza mmea mwingine([5]).

Haiwezekani tukasema kumzuia mume kumuingilia mke wake kipindi cha ujauzito, kutokana na kuwepo katika hili kuzuiliwa kwake kuliko lazima kwake ikiwa hana udhuru, kama ilivyoelezwa kwenye madhehebu ya Imamu Malik([6]), na Hanbal([7]), bali inakuwa ni lazima kwake kuingilia ikiwa atahofia nafsi yake kuingia kwenye uzinifu, na kuzuia kilichowajibu ni haramu, na kinachopelekea kwenye haramu kinakuwa haramu, kama vile kuweka sharti la kumzuia mume kumuingilia mke wake ni sharti batili, kwa kwenda kinyume na makubaliano ya ndoa([8]).

Dalili ya Tano: Upandikizaji kwa njia hii unahitaji kufunua tupu ya mwanamke na kuiangalia pamoja na kuigusa, na asili ya hayo ni haramu Kisharia, haifai kufanya hayo isipokuwa katika hali ya dharura, ikiwa tutakubali kuwepo hali ya dharura au haja katika haki ya mwenye mayai, hatukubali kwa upande wa haki ya mwenye mfuko mbadala wa uzazi, kwa sababu sio huyo sio mwanamke mwenye kuhitajika kuwa mama.

Dalili ya Sita: Kukodi hakufai kupanua ulinganishi kwa sababu kumewekewa Sharia tofauti na asili, kwani asili katika kumiliki ni kumiliki vitu pamoja na manufaa, wala sio kumiliki manufaa pasi na kitu, na kukodi ni makubaliano ya kumiliki manufaa tu, hivyo ukawa uhalali wake upo kinyume na asili.

Na kilichowekewa Sharia kinyume na asili hakifai kupanua ulinganishi bali kunaishia kwenye upatikanaji wa andiko linalojuzisha tu.

Ikiwa kukodi kwa sifa jumla hakufai kupanua kwa kulinganisha, basi kukodi mwanamke kunyonyesha hakufai kupanua ulinganishi ni bora zaidi([9]).

Dalili ya Siba: Ni haramu kutumia mfuko wa uzazi wa mwanamke kwa mimba ya mtu mwingine, hii ni kutokana na madhara ambayo yatamtokea, kwani hawezi kuepukana na moja ya mambo mawili: Ima mwanamke awe ameolewa, au hajaolewa.

Ikiwa ameolewa: Shaka ya kuchanganya nasaba inakuja, na ikiwa hajaolewa: Ataingiza nafsi yake kwenye kashfa na kusemwa vibaya.

Kama kauli ya kukodi ujauzito kwa gharama za mwingine ndani yake kuna kuondoa madhara ya mwanamke asiyepata ujauzito kwa kumdhuru mwanamke mwingine ambaye ndiye atakayebeba ujauzito na kuzaa, kisha hatofurahia matunda ya ujauzito wake na kujifungua kwake na uangalizi wake, na kanuni inasema: Madhara hayaondoshwi kwa madhara([10]).

Dalili ya Nane: Kuongezeka uharibifu utokanao na upandikizaji huu, miongoni mwake:

Kuharibu maana ya mama kama ilivyowekwa na Mwenyezi Mungu na kufahamika na watu, na kuundia muundo wa biashara, jambo linalopingana na maana ya mama ambayo imewekwa na Sharia na kupewa hukumu na haki nyingi, zimeelezwa na watu wa busara na kuimbiwa na wafasihi, maana hii na huo utukuzaji haiwi kwa kutumika yai tu la uzazi lililotolewa na mwanamke mwenye yai na kupandikizwa maji ya mwanamume, bali hutengeneza kitu kingine baada ya hapo nacho ni: Uchovu, kichefuchefu na udhaifu muda wa ujauzito…nayo ni dhiki, wasiwasi wakati wa kuzaa….udhaifu kuchoka na shida baada ya kuzaa, muda huu mrefu ndio unaoleta umama.

Kama vile umama kwa kizuizi hiki unapelekea kwenye mvutano na mgongano wa utiifu na uaminifu kwa mtoto baada ya kujifungua, je uaminifu wake utakuwa kwa mwenye yai au kwa aliyebeba ujauzito na kumnyonyesha maziwa yake? Jambo ambalo linaweza kuleta mshituko mkali wa kisaikolojia, ambapo mtoto hatofahamu aelekee kwa mama yake wa kwanza au mama wa pili? Kuepuka madhara kunatangulizwa zaidi ya kuleta manufaa([11]).

Utafiti

Katika hukumu ya kubeba ujauzito kwenye mfuko wa uzazi wa mke mwingine.

Baada ya Jamhuri ya Wanachuoni kuelezea – kama ilivyotangulia – uharamu wa kutumia mfuko wa uzazi kupandikiza ujauzito wa mwingine ni sawa sawa kwa malipo au kwa kujitolea, kuna kundi la Wanachuoni wameondoa sura ya aina moja nayo: Pindi mama mbadala ambaye atabeba ujauzito wa mwingine ni mke wa pili wa mume wa mwanamke mwenye mayai yaliyorutubishwa, katika hali hii inafaa ujauzito kubebwa na mke mwenzake kwa sura ya kujitolea pale itakapohitajika, kama vile mfuko wa uzazi wa mke mwenye mayai kuwa na matatizo au umeondolewa lakini mayai bado yapo mazima.

Kufaa huku kumefikiwa kwa maamuzi ya Jopo la Wanasharia ya Kiislamu huko Makka katika kikao chao cha saba kilichokaliwa ndani ya kipindi cha kati ya mwezi 11 – 16 Mfungo Saba 1404H.([12]).

Wakatoa sababu ya hilo kuwa wanawake wawili ni wake wa mume mmoja, na mke mwingine amejitolea kubeba ujauzito wa kupandikiza wa mke mwenzake, hivyo umoja wa ubaba utafikiwa, mfungamano wa kifamilia bado utakuwepo na shaka ya kuchanganya nasaba haipo([13]).

Ambalo linaonekana - bali elimu ni ya Mwenyezi Mungu - ni kuwa sura hii pia inazingatiwa ni haramu na imezuiliwa, na hilo ni kwa kukosekana kuondolewa kwa dalili zilizopita zenye kuonesha uharamu wa kutumika mwanamke mfuko wake wa uzazi kwa ajili ya mtu mwingine.

SOMO LA PILI

Katika kujadili mtazamo uliohalalisha.

Kauli ya uharamu kukodisha mfuko wa uzazi ndio kauli iliyotolewa na Jamhuri ya watafiti wa sasa, bali imetolewa katika maneno ya baadhi yao wito wa Jamhuri ya Wanachuoni kwenye hilo, au kukosekana elimu tofauti na uharamu ([14]).

Ukweli ni kuwa imethibiti rai isiyo ya kawaida ya kujuzisha kukodi mifuko ya uzazi, baadhi wamesema, lakini rai hii au mtazamo huu hauzingatiwi wenye kujeruhi yale yaliyopitishwa na Jamhuri ya Wanachuoni, kutokana na udhaifu wake mkubwa kama utakavyokuja katika kuelezea dalili zake na mijadala yake kama ifuatavyo:

Dalili ya Kwanza: Wamechukua dalili ya kulinganisha mfuko wa uzazi na chuchu katika kuleta lishe, kama vile lishe inatimia kwa njia ya mdomo katika hali ya kunyonya, pia hutimia katika mfuko wa uzazi kwa mabaki ya chakula kilichomeng’enywa ndani ya matumbo ya mama kupitia utumbo wa kitovu, ambapo ndiyo chanzo cha lishe muhimu ili mtoto tumboni kubakia katika hali zote mbili([15]).

Baadhi yao wanasema: Hali zote ni kukodi, hali hii kukodi mfuko wake wa uzazi, na hali nyingine kukodi chuchu za maziwa ya mwanamke([16]).

Dalili hii imejadiliwa kuwa kulinganisha mfuko wa uzazi na chuchu za mwanamke kuwa vyote vinanufaisha lishe katika hali zote, ufananishaji huo haufai, kwa sababu sharti la uhalali ni kuwa sifa ya wazi iliyowekwa ([17]), na manufaa hata kama ni wasifu wa wazi isipokuwa yenyewe si yenye udhibiti, kwa sababu maana ya udhibiti au nidhamu iliyokuja katika maana ya sababu ni: Sababu kulazimika na hali moja, wala isiwe yenye kuvutana, kwa maana: Haibadiliki kwa kubadilika watu na nyakati, na manufaa ni wasifu wenye kugeuka kwa kutofautiana watu na nyakati, huenda manufaa ya mtu ni madhara kwa mtu  mwingine, na huenda manufaa ndani ya wakati huu yakawa ni madhara ndani ya wakati mwingine, wala haifai kuwa sababu ya kulinganisha.

Ikiwa itasemwa: Sababu sio manufaa tu bali ni kuhusisha lishe, tumesema: Haifai pia kugonganisha lishe na kukosekana nidhamu au udhibiti, kwani lishe ya mtoto tumboni kutoka kwa mama mlezi inaweza kuwa manufaa na masilahi ikiwa mama yupo salama bila ya kupewa dawa zozote zenye kuathiri afya ya mtoto tumboni, na inaweza kuwa madhara kwa mtoto tumboni ikiwa atapatiwa chochote katika hivyo.

Vilevile lishe kutoka kwenye chuchu za mnyonyeshaji inaweza kuwa masilahi na manufaa kwa mnyonyeshaji ikiwa mnyonyeshaji yupo salama kutokana na maradhi na wala hajapewa dawa yoyote yenye kuathiri afya ya mnyonyeshaji, na madhara ikiwa atapatiwa chochote katika hivyo ([18]).

Ama kukodisha hali zote haifai, na hilo kwa mambo mawili:

Jambo la Kwanza: Ni kuwa sababu ni wasifu wa wazi wa kinidhamu, unalazimisha uwepo wa hukumu, na kulazimisha kukosekana kwake ni kukosekana hukumu, kukodisha hakuko hivyo, ambapo kunaweza kukosekana na kutokosekana uhalali wa kunyonya kwa kuwezekana kujitolea kwa hilo mnyonyeshaji([19]).

Jambo la Pili: Kuwepo tofauti kati ya mpimaji na kinachopimwa, kwa sababu kukodi chuchu za mwanamke kunaweza kuwa halali kwa dharura nayo: Kulinda uhai wa mtoto wa kunyonya, tofauti na kukodisha mfuko wa uzazi wenyewe ni kuanzisha maisha mapya, hakuna umuhimu huo, na kinachofaa kwa hali ya dharura si kipimo cha kitu chengine([20]).

Dalili ya Pili: Kuwepo hali ya haja ya Kisharia ambapo inakimbiliwa na njia hii wakati wa kuwepo sababu za kitiba mara nyingi zinamzuia mwanamke kupata ujauzito, kama vile kuzaa bila ya mfuko wa kizazi, au kuwa amepatwa na kasoro au maradhi yanayopelekea upatikanaji wa ujauzito kuwa ni jambo lisilowezekana, au wakati wa kutaka kinga ya maambukizi ya maradhi ya kimaumbile kwa upande wa kibayolojia ya mama, na utashi wa kupata mtoto ni hitaji lisilopingwa, na haja huwekwa kwenye nafasi ya dharura([21]).

Dalili hii imejadiliwa na kutokubalika na kuwepo kwa hali ya haja ambayo inawekwa kwenye nafasi ya dharura, ikiwa haja itapelekea kwenye kunufaika mtoto kwa aliyeharamishwa naye kwa njia ya kukodi mfuko wa uzazi, hata kama kuna masilahi lakini ubaya unaotokana na njia ya kuondoa hii haja ni mbaya zaidi, kwani njia hii inapelekea mgongano kati ya watu pamoja na kuwepo shaka ya kuchanganya nasaba([22]).

Dalili ya Tatu: Wamesema: Asili ya mambo ni halali, hakuna uharamu isipokuwa kwa Andiko la moja kwa moja([23]).

Dalili hii ni ya kuangaliwa, kwa sababu usahihi ni kuwa asili ya vitu ni halali katika manufaa, na haramu katika madhara, na wala si uhalali moja kwa moja([24]). Ikiwa tutakubali, basi yenyewe inafungamana na kanuni nyingine, nayo ni kuwa asili katika tupu ni haramu.

Ama kauli kuwa yenyewe ni haramu isipokuwa kwa andiko la wazi, ikiwa inakusudiwa andiko la wazi lenye kuthibiti: Haikubaliki, kwa sababu habari moja ya kifikra iliyothibiti, na inathibiti kwa upande wa kiibada pamoja na upungufu wake na kunufaika kielimu. Ikiwa inakusudiwa dalili ya moja kwa moja: Pia haikubaliki, kwani Kitabu na Sunna za wapokezi wengi miongoni mwake ni dalili ya kufikiriwa japo kuwa zenyewe zinakuwa hoja([25]).

MLANGO WA PILI

Athari zitokanazo na mtumizi ya mfuko wa uzazi katika ujauzito wa mwingine.

Somo la Kwanza

Nasaba ya mtoto kwa upande wa baba.

Utafiti wa Kwanza.

Ikiwa mwenye mfuko wa uzazi mbadala ni mke wa pili wa mwenye tone la manii.

Ikiwa mwenye mfuko wa uzazi mbadala ni mke wa pili wa mwanamume mwenye tone la maji ya manii na kuwa ndiyo baba wa Kisharia wa mtoto atakayezaliwa, kwa sababu tone la maji lililotumika katika kupandikiza ni tone lake mume, hivyo mtoto anatokana na uti wa mgongo wake, kwa sababu yeye ndiye mwenye ndoa ambayo imeleta mtoto, na Mtume S.A.W. amesema: “Mtoto ni wa ndoa”([26]).

Utafiti wa Pili

Ikiwa mwenye mfuko wa uzazi mbadala ni mwanamke aliyeolewa.

Ikiwa mwenamke mwenye mfuko wa uzazi badala ni mwanamke mwenye mume hivyo nasaba ya mtoto inathibiti kwa mume wake, wala si kwa mwenye tone la maji ya manii.

Dalili ya hilo ni Hadithi ya Mtume S.A.W: “Mtoto ni wa ndoa na mzinifu hana haki”([27]), na hukumu za Kisharia zimejengewa kwa uwazi([28]). Baadhi ya Wanachuoni wa sasa wanaona kuwa mtoto hunasibishwa na mume wa mama mwenye mayai ambaye yamepandikizwa kwa tone lake, na huthibiti kwake haki zote zinazotokana na uthibiti wa nasaba, wala hanasibishwi kwa mume wa mama mwenye mfuko wa uzazi mbadala.

Wakachukua dalili kuwa mtoto tumboni ametengenezeka kutokana na mayai ya mwanamke na maji ya mwanamume kati yao kuna ndoa sahihi ya Kisharia, na kufanyika kwa upandikizaji huu haramu hakuathiri katika nasaba ya mtoto kwa wazazi wake, kwa sababu uharamu umefanyika baada ya kufungika ndoa kwa sababu za matumizi ya mfuko wa uzazi wa mwanamke aliyejitolea kutumika bila ya kuruhusiwa na Sharia, kutokana na hayo uharamu haukuingia katika asili ya kuundika mtoto, bali ni kwa njia ya lishe yake ambayo imepelekea makuzi yake na ukamilifu wake, hivyo mtoto anafanana na kuwa amelishwa na wazazi wake vya haramu mpaka ukubwa wake, hao wawili wanadhambi kwa hilo, lakini hili haliwakatii nasaba ya mtoto wao.

Mtazamo huu unatengeneza kuwa mume aliyetajwa hafungamani na mwanamke mwenye mfuko wa uzazi mbadala kwa maana sababu miongoni mwa sababu za uthibiti nasaba kwa upande wa baba, nayo ni tatu: Ndoa – iwe sahihi au iliyoharibika – au kuingilia, au kuchanganyika kunakotokana na umiliki wa mkono wa kulia([29]).

Utafiti wa Tatu

Ikiwa mwenye mfuko wa uzazi hana mume

Baadhi ya watafiti wa sasa wanaona kuwa ikiwa mwanamke mwenye kifuko cha uzazi hana mume kwa maana hajaolewa, mtoto atanasibishwa kwa mume wa mama mwenye yai lililorutubishwa, na huthibiti haki zote zitokanazo na uthibiti wa nasaba, na aina zote za uhusiano wa ukaribu, na yatokanayo na hayo miongoni mwa uharamu uliothibiti kwa huu undugu([30]).

Dalili walizochukua katika hilo:

Moja: Fatwa iliyotolewa na timu ya Wanachuoni ya kufaa nasaba ya mtoto wa baba mzinifu kwa baba mzinifu ikiwa mwanamke aliyeziniwa hajaolewa, wamesema: Bali kuthibiti kwake hapa ni bora zaidi, na hilo kwa kuheshimu maji ya aina mbili wakati wa kuteremka na wakati wa kurutubishwa([31]).

Pili: Yaliyosemwa na baadhi ya Wanachuoni kuwa nasaba ni sharti la uhalali wakati wa kuteremka maji ya manii, wala hakuna sharti la uhalali wakati wa kuingiza kwa mwanamke.

Imamu shamsideen Alramly anasema kuhusu mama wa mtoto – mjakazi ambaye ameingiliwa na bwana wake na kupata ujauzito na kujifungua: “Lau maji ya manii ya bwana wake yakiingizwa baada ya kufa kwake, hapo hawi mama wa mtoto, kwa sababu ya kumalizika kumilikiwa kwake, kuthibiti nasaba ya mtoto na yanayofuata baada ya hapo na akamrithi ni kutokana na manii halali, wala haizingatiwi kuwa kwake halali wakati wa kuingizwa kwake tofauti na baadhi yao, kwani baadhi yao wameeleza kuwa lau atayateremsha kwa mke wake, kisha yakamfikia binti yake na akapata ujauzito kwa maji hayo, akapata mtoto, vilevile kama atafuta uume wake kwa jiwe baada ya kushusha manii kwa mke wake, kisha mwanamke wa mbali akajipangusia lile jiwe akapata ujauzito kwa jiwe lile([32]).

Katika sura ambayo tunaizungumzia: Kuteremsha maji ya manii halali kwa sababu hiyo inakuwa ni kati ya mwanamke na mwanamume wanaunganishwa na mahusiano sahihi ya ndoa, hivyo yai la uzazi la mwanamke lenye kupandikizwa kutoka kwa mume wake, na kupandikizwa mayai kutoka kwa mume hakuzingatiwi katika jumla ya yaliyoharamishwa, bali ni kutokuwa halali kwake kutumia kifuko cha uzazi cha mwengine, kukosekana uhalali kunatokana na kuingiza mayai ya uzazi ya kupandikizwa ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke mwingine, hakuna sharti la kuthibiti nasaba halali wakati wa kuingia kama yalivyotangulia maelezo ya Ramly([33]).

SOMO LA PILI

Nasaba ya mtoto kwa upande wa mama

Ikiwa itatokea na kuthibiti sura ya kifuko cha uzazi mbadala kinachozungumziwa basi mtoto anayetokana atanasibishwa kwa mwenye kifuko cha uzazi mbadala na wala si kwa mwenye mayai yaliyorutubishwa, na zitafanya kazi hukumu zote za mtoto upande wa mama yake, na mama yake upande wa mtoto wake.

Linaonesha hilo mambo mengi:

Kwanza: Aya za Qur`ani Tukufu ambazo zimeonesha wazi kuwa mama ndiye ambaye anabeba ujauzito na kuzaa, na ambacho kinakamilika kutengenezwa ndani ya tumbo lake ni mama, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu} An-Nahlu: 78. Na kauli yake:   {Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu} Luqman: 14. Na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu} Al-Ahqaaf: 15. Mwenyezi Mungu Anabainisha katika Aya ya kwanza kuwa mwenye kuzaa na kutoka kwake mtoto ni yule ambaye anaitwa Mama, katika Aya ya pili ambaye anabeba kiinitete ndiye ambaye anaitwa Mama na kunasibishwa kwake, na katika Aya ya tatu ambaye anambeba mtoto kwa taabu na kumzaa kwa tatu ni Mama yake.

Dalili hizi zikajadiliwa kuwa mama wa kweli katika historia yote na wakati wa kuteremshwa Qur`ani ni mkusanyiko wa umbile ambalo ndilo mwenye kubeba mimba na kujifungua, naye ndiye yeye mwenyewe na wakati huo huo ndio mwenye mayai.

Watoto wote wanaozaliwa kwa mama yake kuna mahusiano mawili: Mahusiano ya kutengenezwa na kurithi na asili yake ni mayai, na uhusiano wa kuzaa na kulea, na asili yake ni kifuko cha uzazi, kuitwa mama ndiye anayebeba ujauzito na kuzaa tu pasi na kuwa mayai kutoka kwake, ni uitaji kinyume na umbile lake kamili wakati wa kuteremka([34]).

Pili: Qur`ani Tukufu imethibitisha sifa ya mama ambaye amebeba ujauzito na kuzaa kwa mfumo unaonesha umaalumu wake kwenye hilo, kama ilivyokuja katika kauli yake Mola Mtukufu: {Mama asitiwe tabuni kwa ajili ya mwanawe} Al-Baqara: 233. Mzazi wa kike kwa hakika ndiye ambaye aliyezaa, vilevile kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa} Al-Mujadala: 2. Ambapo Mola Mtukufu ameweka wazi kuwa mama ndiye ambaye amezaa, na kufuata njia fupi zaidi, nayo ni: Kukanusha na kuthibitisha, amekanusha umama kwa yule ambaye hakuzaa mtoto, na akathibitisha kwa yule aliyezaa.

Tatu: Kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakika mmoja wenu hukusanywa maumbile yake tumboni mwa mama yake ndani ya siku arobaini, kisha hutengenezwa pande la damu kisha huwekwa nyama”, Mtume S.A.W. akamuita ambaye hukusanywa kiumbe ndani ya tumbo lake Mama([35]).

Nne: Yaliyopokewa na Mama wa Waumini Bi. Aisha R.A. kuwa Saad Ibn Abi Wiqas na Abdu Ibn Zam’aa waligombana kuhusu mtoto, Saad akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu huyu ni mtoto wa ndugu yangu Ataba Ibn Abi Wiqas aliniambia kuwa ni mtoto wake angalia amefanana naye” na Abdu Ibn Zamgha akasema: “Huyu ni ndugu yangu Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni mtoto wa ndoa kwa baba yangu”. Mtume S.A.W. akaangalia na akaona mfanano wa wazi na Ataba, akasema: “Ni wako ewe Abdu Ibn Zam’aa, mtoto ni wa ndoa na mzinifu hana haki, jifunike kwake ewe Sauda, hakumuona tena”([36]).

Mtume S.A.W. amemfanya mtoto ni wa Zam’aa pamoja na kuonekana kuwa si wa Zam’aa, na akafanya hukumu ya mtoto wa ndoa, ukweli wa kielimu sio ukweli wa Kisharia, kwani Sharia inahukumu yaliyo wazi na ukweli anaujua Mwenyezi Mungu([37]).

Utafiti

Uhusiano wa mtoto kwa mwanamke mwenye mayai.

Kumekuwa na kauli ya mtoto hunasibishwa na mwenye mfuko wa uzazi mbadala tafiti za mahusiano yake na mwanamke mwenye mayai, na Wanachuoni katika hukumu yao wana kauli mbili:

Kauli ya Kwanza: Mwanamke mwenye mayai hata kama hakuwa mama Kisharia, lakini si mtu wa mbali na mtoto, bali yeye ni sehemu ya mama kutokana na kunyonya.

Na hilo ni kwa kuwa sababu ya kuharamishwa kwa kunyonya ni: Sehemu, au kufanana kwake – kama ilivyoelezewa na Imamu Abu Hanifa([38]), kwa uchache yanayosemwa ni kuwa: Huyu mtoto ni sehemu ya mwenye mayai, hulazimika uharamu wa kunyonya.

Miongoni waliosema rai hii: Ni Jopo la Wanachuoni wa Sharia za Kiislamu, katika kikao chao cha saba kilichokaliwa Makka mwaka 1404H. sawa na 1984([39]).

Kauli ya Pili: Ni kuwa hakuna mazingatio kati ya mtoto na mwanamke mwenye mayai, na kazi yake imepotea, haifungamani na hukumu.

Yanasisitizwa haya kuwa uharamu wa kuoa wanawake ni uharamu wa milele unakuwa kwa moja ya sababu tatu:

Ukaribu au nasaba au ukwe au kunyonya, kama ulivyoelezwa ndani ya Madhehebu ya Imamu Shafi([40]), na inafahamika kwenye madhehebu ya Imamu Malik([41]), mtoto ambaye hujengewa hukumu ni mtoto wa Kisharia.

Miongoni mwa walioelezea mtazamo huu: Sheikh Badru Al-Mutawaly Abdulbasit - Mungu Amrehemu – na anayoyasema katika hilo: “Hivi unaonaje mwanamke fulani akimchangia mtoto wa kunyonya damu yake kwa njia inayofahamika hivi sasa, je inathibiti kati ya mwenye damu na kati ya huyu mtoto uharamu wa kunyonya... Ambalo nalisema: Ni kuwa huyu mwanamke hawezi kuvuka kuwa ni mke wa huyu baba wa mtoto, ama yaliyopo nyuma ya hayo ikiwa pamoja na kuwepo uharamu wa kunyonya, jambo lina udanganyifu zaidi kuliko hivyo linavyodhaniwa”([42]). 

Utafiti

Mjadala wa kauli ya uthibiti wa nasaba kwa mwenye mayai yaliyorutubishwa.

Baadhi ya Wanachuoni wa sasa wamesema kuwa nasaba katika hali ya kifuko cha uzazi inathibiti kwa mwenye mayai yaliyorutubishwa, na katika hili wameelezea waliosema inafaa ujauzito kwa njia ya mfuko wa uzazi mbadala, na kukubali katika hilo waliosema kufaa katika sura ya mke wa pili ([43]).

Na yafuatayo ni dalili zao pamoja majibu na mijadala:

Dalili ya Kwanza: Wamesema: Qur`ani Tukufu imetoa umuhimu wa sababu za kibaolojia kama msingi wa kuthibiti nasaba, ambapo imetaja sehemu nyingi kuwa asili ya mwanadamu ni tone la manii na lenyewe ndilo msingi wa kutengenezwa kwake, kama ilivyokuja katika kauli ya Mola: {Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani mkubwa} An-Nahli: 4. Na kauli yake: {kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu iliyo gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo} Al-Hajj: 5. Na kaui yake:{Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii} Ghaafir: 67. Na kauli yake: {Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi mbili, dume na jike * Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa} An-Najmi: 45, 46. Na kauli yake: {Hivi hakuwa tone litokanalo na manii yanayotunga} Al-Qiyama: 37.

Aya hizi zimeonesha kuwa mwanadamu ameumbwa kutokana na tone la maji ya manii, baada ya hapo amepitia hatua mbalimbali mpaka kufikia hatua ya kuzaliwa na kukuwa jambo linaloonesha kuwa mtoto hunasibishwa kwa mwanamke mwenye mayai ambayo yamerutubishwa kwa maji ya mume wake sawa na ukweli wa kibaolojia ambao umetajwa na Qur`ani Tukufu([44]).

Dalili hii ilijadiliwa kuwa maji ni ya aina mbili kama hayatakuwa ya halali wakati wa kuingiza na kutoa au vikiwa pamoja, basi yanakuwa yamepoteza uhalali wake kabisa, sababu za kibaolojia ni zenye kuzingatiwa ikiwa katika wigo ambao umewekwa na Sharia, na wigo huu umewekwa katika kuthibiti nasaba kwa sababu zake: Kama vile ndoa, na huyu mama mbadala si mke wa ndoa kwa mume wa mwanamke mwenye mayai yaliyorutubishwa.

Kipimo chote ni kwa mazingatio ya Sharia, kwani mwanamume mzinifu hata kama atafahamika kuwa ni baba wa kibaolojia kwa mtoto lakini si baba halali Kisharia wa mtoto([45]).

Dalili ya Pili: Wamesema kuwa mwanamke aliyejitolea kubeba ujauzito mtoto hana anachonufaika nacho zaidi ya lishe, hivyo anafanana sana na mtoto anayepata lishe kutoka kwa asiyekuwa mama yake([46]).

Dalili hii imejadiliwa mtoto wa mwanamke aliyejitolea kubeba ujauzito kuwa hana anachonufaika zaidi ya lishe, kwani imethibiti kuwa mfuko wa uzazi una athiri katika tabia ya kimaumbile kwa mtoto tumboni, na wala sio tu sababu saidizi kama inavyodaiwa, wakati wa kukuza mayai ya kupandikizwa inawezekana kuongezeka baadhi ya tabia za kimaumbile kutoka kwa mama ambaye anamlisha kwa njia ya mshipa wa oksijeni kwa mtoto ndani ya mfuko wa uzazi, kwani DNA ambayo inachukua tabia za kimaumbile haipo kwenye kiini cha seli pekee bali kwenye saitoplazimu ya seli pia, na sehemu hii ya asidi huathiriwa na mazingira yanayozunguka eneo hilo wakati wa makuzi ya mtoto ndani ya mfuko wa uzazi, hivyo mama aliyekodiwa huongeza baadhi ya tabia za kimaumbile kwa mtoto tumboni([47]).

Dalili ya Tatu: Kipimo cha tunda, tunda ni binti wa mbegu na wala si binti wa ardhi, mwenye kulima kilimo cha machungwa vyovyote ardhi itakavyokuwa atavuna machungwa, na mwenye kulima kilimo cha matunda atavuna matunda, ardhi pamoja na kuwa inaiandaa mbegu na kila kinachohitajika isipokuwa yenyewe haina muingiliano na aina au jinsia ya mmea ambao utakulia kwenye ardhi hiyo.

Vilevile miche ya miti baada ya kukuwa na kuwa mikubwa, huamishiwa sehemu nyingine, mti hunasibishwa na mbegu na wala sio udongo([48]).

Dalili hizi mbili zinajadiliwa kwa sura mbili:

Sura ya Kwanza: Ni kipimo kilicho tofauti, hoja haikubaliki([49]).

Sura ya Pili: Kipimo hiki ni kipimo cha kimtazamo, na kipimo cha kimtazamo ni katika aina dhaifu zaidi za kupimia shaka kwa watu wa mambo ya asili([50]).

Tafiti hii imeandikwa na:

Ahmad Mamduh

15/05/2007.

Maelezo kwa Ufupi:

Asili ya utafiti huu ni ule utafiti mrefu uliochapishwa kwenye jarida la Muislamu wa kisasa, mwaka wa ishirini na tisa, toleo la 114 la mwaka 1425H/ 2002, chini ya jina: Jaribio la kupata muundo wa jitihadi ya kisasa, ni masuala ya mfuko wa uzazi mbadala, ameiendea na kuifupisha kwenye karatasi hizi pamoja na kujengea baadhi ya maelezo na kuweka baadhi ya nyongeza.

 

([1]) Rejea kitabu cha kukodisha kifuko cha uzazi cha Dkt. Abdilkadir Abi Al-Ulaa, uk. 20.

([2]) Angalia kitabu cha kukodisha mfuko wa uzazi cha Dkt. Raafat Uthman 1/92, 93.

([3]) Kitabu cha Mughny Al-Muhtaj: 3/438.

([4]) Imepokelewa na Abu Daud 2158. Na At-Tirmidhy 1131 na kuifanya Hadithi nzuri. Na Imamu Ahmad katika musnada yake 4/108.

([5]) Sherehe ya Sunan Abi Daud na kuweka wazi sababu yake na matatizo yake 6/136.

([6]) Kitabu cha Al-Fawakih Al-Dawany 2/22.

([7]) Kitabu cha Kashaaf Al-Qinaai 5/192.

([8]) Kitabu cha Kukodisha mfuko wa uzazi cha Abi Al-Ulaa, uk. 19.

([9]) Kitabu cha Kukodi mfuko wa uzazi cha Abi Al-Ulaa, uk. 20.

([10])  Kitabu cha Al-Ashbah wannadhwair cha Imamu Al-Suyuty, uk. 95.

([11]) Fatwa ya kisasa ya Dkt. Yusuf Al-Qardhawiy  ndani ya kitabu cha Banki ya tone na kiinitete, uk. 262: 263, kitabu cha Mama mbadala – ni kaitka utafiti wa Kisharia katika kadhia za kisasa za kitiba 2/ 808, 810, 811, kitabu cha Msimamo wa Sharia ya Kiislamu kwenye nidhamu na maadili katika nyanja za kitiba cha Dkt. Amani Abdulqadir, uk. 319.

Sheikh Mustafa Az-Zarqa – Mungu amrehemu – anaona hatari ni katika kutofahamika matokeo kwa upande wa mtoto aliyetumboni kwa upande wa uwezekano wa kuongezeka kiwango cha uharibifu kwenye njia hii ya kutengeneza kinyume a ukawaida katika ujauzito kwa njia ya asili, kwa kukosekana uwezekano wa kufahamu hilo kabla ya kujirudia kwa wingi, na kwa upande wa uwezekano kupelekea kwenye madhara ya kimaradhi yasiyowezekana kuleta amani kwenye njia hii kabla ya kupita muda mrefu wa umri wa mtoto aliyezaliwa, katika tahadhari zinazolazimisha uzuiaji. “Angalia jarid la Jopo la watafiti wa Sharia za Kiislamu, tolea la tatu, sehemu ya kwanza, uk. 260: 261.

([12]) Ambapo yaliyokuja kwenye mkutano huo ni kuwa: “Mfumo wa saba ambao huchuliwa tone la manii na yai kutoka kwa wanandoa wawili, na baada ya kupandikiza ndani ya tumbo la majaribio na kupandikizwa kifuko cha uzazi cha mke mwengine wa mume huyo huyo, ambapo mwanamke anajitolea kwa hiyari yake ujauzito huu wa mke mwenzake aliyeng’olewa kifuko cha uzazi, baraza limeonesha uwa inafaa kwa masharti makuu yaliyotajwa.

Kisha Jopo hilo hilo lilikaa tena katika kikao chake cha nane kilichokaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa nchi za Kiislamu duniani huko Makka ndani ya kipindi kuanzia siku ya Jumamosi mwezi 28/Mfungo Saba/1405H mpaka siku ya Jumatatu mwezi 7/Mfugo Nane/1405H sawa na tarehe 19 – 28 /January 1985 – na kuondoa hukumu ya kufaa kwa sura hii, na kutoa hukumu ya kuzuia. “Angalia Jarid la Jopo la Wanasharia wa Kiislamu toleo la pili, sehemu ya kwanza, uk. 323, 324.

([13]) Kitabu cha Mama mbadala – ni jumla ya tatifi za Kifiqhi katika kadhia za kisasa za kitiba 2/ 820.

([14]) Miongoni mwa watafiti ambao wametaja Jamhuri ya Wanachuoni au kukosekana elimu ya tofauti ni Dkt. Aarif Ally Aarif, na Dkt. Sabry Abdulrauf – mwalimu wa somo la Sharia Chuo Kikuu Al-Azhar – na wengineo.

Angalia kitabu cha Mama wa badala ni katika jumla tafiti za Kifiqhi katika kadhia za kisasa za kitiba 2/813, katika wigo wa uamuzi wa Al-Azhar wa kuharamisha kuuza mifuko ya uzazi ya wanawake au kukodisha, tafiti za Dkt. Mustafa Imara – uhakiki umetolewa na jarida la “Zamani” la Iraq Londo la tarehe 18 – 1- 2001.

([15]) Kitabu cha mama badala cha Dkt. Abdulhamid Uthman, uk. 83. Na Dri Abdulmuuti Bayuomy – kupitia kukodi kifuko cha uzazi kitabu cha Dkt. Abdulqadir Abi Al-Ulaa, uk. 40.

([16]) Kitabu cha Mama badala cha Dkt. Aarif Ally Aarif – jumla ya tafiti za Kifiqhi katika kadhia za kisasa za kitiba 2/814.

([17]) Kitabu cha Tahriir wa Tahbiir 3/167.

([18]) Kitabu cha Kukodi mfuko wa uzazi cha Dkt. Abdilkadir Abi Al-Ulaa, uk. 41, 43.

([19]) Kitabu cha kukodisha mfumo wa uzazi cha Abi Al-Aulaa, uk. 15.

([20]) Kitabu cha kukodisha mfumo wa uzazi cha Abi Al-Aulaa, uk. 16. Na kitabu cha Banki ya tone na kiinitete cha Imamu As-Suyutiy, uk. 260.

([21]) Rejea kitabu cha Hukumu za mama badala, uk. 85. Na kitabu cha Banki ya tone na kiinitete cha Dkt. Ataa As-Sanbaty, uk. 261.

([22]) Rejea kitabucha Banki ya tone na kiinitete, uk. 260: 261.

([23]) Dkt. Abdulmuuty Bayoumi – kuhusu kukodi mifuko ya uzazi cha Dkt. Abdulqadir Abi Al-Ulaa, uk. 30.

([24]) Kitabu cha Hashiyatul-Muuty, uk. 4/352 na kuendelea.

([25]) Kitabu cha Jaribio la kufikia muundo wa jitihada za sasa “Masuala ya mfuko wa uzazi mbadala” cha Ahmad Mamduh – ni utafiti uliotolewa kwenye jarida la Musiamu wa sasa chapa ya 114 ya mwaka 1425H/2004.

([26]) Imekubaliwa na Maimamu wote wa Hadithi: Imepokelewa na Imamu Bukhari, 2105, 2395. Na Imamu Muslim 2/1080.

([27]) Umetangulia upokezi wake.

([28]) Kitabu cha Mama mbadala – ni katika jumla tafiti katika kadhia za kisasa za kitiba 2/836 – 838, kitaabu cha Al-Hukmu Al-Iqnaai ni katika jumla ya utafiri wa Fiqhi ya Kiislamu kutano wa pili tolea pili, shemu ya kwanza, uk. 318: 320. Kitabu cha Uzazi wa kutegeneza, uk. 614, Kitabu cha mjadala wa kongamano la uzazi katika Uislamu.

([29]) Kitabu cha mama badala – ni katika jumla ya utafiti wa kifiqhi katika kadhia ya kitiba 2/839, 840. Na kitabu cha Uzaaji wa kutengeneza, uk. 614, jarida la jopo la Sharia ya Kiislamu katika kikao chake cha pili, tolea la pili, sehemu ya kwanza, uk. 262, 314.

([30]) Miongoni mwao ni Dkt. Muhammad Raafat Uthman katika kitabu chake “Kukodisha mfuko wa uzazi” na Dkt. Ataa As-Suyutiy katika kitabu chake “Banki ya tone na kiinitete”.

([31]) Kitabu kukodi mfuko wa uzazi cha Dkt. Raafat Uthman – ni katika tafiti za kadhia ya kifiqh 1/98. Na kitabu cha banki ya tone na kiinitete uk. 280, na rejea kitabu cha Al-Mughny 6/228. Kitabu cha fat’wa za Ibn Taimia 3/201.

Na maji ya heshima: Ni ambayo hayatoki kwa mwenye maji kwa njia ya uzinifu.

([32])  Kitabu cha Nihaaytul-Muhataj cha Shams Ramly 8/430, 431.

([33]) Rejea kitabu cha kukodisha kifuko cha uzazi cha Dkt. Raafat Uthman katika tafiti za kifiqhi ya kisasa 1/102.

([34]) Angalia kitabu cha Mama badala – katika utafiti wa fiqhi ya kadhia za kisasa 2/830, 831. Kitabu cha njia za uzazi katika tiba ya sasa na hukumu yake Kisharia cha Dkt. Bakri Abi Zaid – katika tafiti za jopo la Sharia za Kiislamu mkutano wa tatu, toleo tatu, sehemu ya kwanza, uk. 435: 437.

([35]) Rejea jarida la Jopo la Fiqhi ya Kiislamu toleo la pili, sehemu ya kwanza, uk. 285.

([36]) Imekubaliwa na Maimamu wote wa Hadithi: Imepokewa na Imamu Bukhari Hadithi nambari 3036, na Imamu Muslim Hadithi nambari 2643 Hadithi itakanayo na Ibn Masoud.

([37]) Kitabu cha kuzaa kwa kutengeneza cha Najimy, uk. 603: 604, jarida la jopo la Wanasharia za Kiislamu kikao cha pili toleo la pili, sehemu ya kwanza, uk. 284.

 

([38]) Rejeao kitabu Al-Mabsout 5/132, kitabu cha Al-Inaya sherehe ya Al-Hidaya 3/438.

([39]) Jarida la Jopo la Wanachuoni wa Sharia za Kiislamu mkutano wa pili, toleo la pili, sehemu ya kwanza, uk. 266, na angalia kitabu cha Mitazamo katika upandikizaji wa kutengenezwa – ni katika tafiti za kongamano la uzazi katika Uislamu, kitabu cha uzazi wa kutengeneza, uk. 610.

([40]) Kitabu cha Mughny Al-Muhataj 4/287. Na kitabu cha Asnaa Talib 3/148 na kuendelea.

([41]) Kitabu cha Taji na Maua 5/108. Kitabu cha Hashiyatu Dusuuk cha sherhe kubwa 2/269.

([42]) Mitazamo katika kupandikiza – ni katika jumla ya tafiti za kongamano la uzazi katika Uislamu, angalia kitabu cha uzazi wa kutengeneza cha Dkt. Rassy Zahara, uk. 556, kitabu cha uzazi wa kutengeneza cha An-Najimy, uk. 611: 612 fiqhi na masuala ya kitiba cha Muhsiny, uk. 93.

([43]) Kitabu cha hukumu za mama mbadala cha Dkt. Abdilhamid Uthman, uk. 103: 104. Kitabu cha uchaguzi wa hukumu za kutengenezwa – masuala ya 613.

([44]) Kitabu cha banki ya tone na kiinitete cha Suyuty,  uk. 271: 273.

([45]) Kitabu cha banki ya tone na kiinitete cha Suyuty, uk. 273: 274.

([46]) Uzazi wa kutengeneza kitabu cha An-Najimy, uk. 601.

([47]) Hayo yamethibitishwa na Dkt. Ikram Abdulsalam mwalimu wa sayansi ya tiba ya watoto na mkuu wa kitengo cha tabia za kimaumbile chuo kikuu cha Kairo, angalia kwenye tovuti ya: www.islamonline.net katika wigo wa maamuzi ya Al-Azhar kuharamisha kuuza mifuko ya uzazi ya wanawake au kuikodisha, Dkt. Mustafa Imara – utafiti uliohakikiwa kwenye jarida la “Az-Zaman” la tarehe 18-1-2002.

([48]) Kitabu cha Mama wa badala cha Aarif – ni katika tafiti za kifiqhi katika kadhia za kitiba za kisasa 2/828.

([49]) Kitabu Hukumu ya ukinaishaji katika kubatilisha upandikizaji wa kutengeneza – ni katika tafiti za jarid la Jopo la ‘Sharia za Kiislamu kwenye kikao chake cha pili toleo la pili, sehemu ya kwanza, uk. 319.

([50]) Kitabu cha Al-Bahri Al-Muhiit 7/302, hoja ya kupima shaka ni sehemu yenye tofauti kati ya watu wa msingi asili, na kauli ya kufaa kupima kimtazamo kwa lengo la kufananisha sura ambayo inadhaniwa kuwa sababu ya hukumu, hayo ni mafundisho ya viziwi na mtoto wa Aliyah, kitabu cha Ahmad Mamduh.

Share this:

Related Fatwas