Nuksi za siku na idadi

Egypt's Dar Al-Ifta

Nuksi za siku na idadi

Question

Nini hukumu ya kutarajia mabaya wakati wa kuona idadi maalumu au ujio wa siku maalumu au tukio katika kile kinachoitwa “nuksi”?

Answer

Nuksi za nambari, siku, n.k zimekatazwa katika Sharia. Kwa sababu mambo hutokea kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na mambo haya hayahusiani na mema anayopata mtu au mabaya yanayompata. Kisheria nuksi na uchuro zimekatazwa kwa ujumla, kwani ni tabia ya kijahiliya. Katazo la nuksi limepokelewa kutoka kwa  Mtume pia liliripotiwa kutoka nyakati na miezi fulani kuhusu hilo. Kama ilivyopokelewa katika “Al-Sahihayn” kutoka kwa Abu Hurairah, (R.A), kutoka kwa Mtume, (S.A.W), ambaye amesema: “Hakuna maambukizo, wala Mfungo Tano, wala bundi (hata zama zetu ‎zinaamini nuksi kumuona au kumsikia bundi, au kumuona paka mweusi).” Sababu ya makatazo haya ni yale yaliyo katika nuksi na uchuro kutokana na  dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu, na kuchelewesha nia ya mtu katika kutenda, kama vile inavyovuruga moyo kwa wasiwasi na udanganyifu.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas