Kutopingana Baina ya Malipo na Kad...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutopingana Baina ya Malipo na Kadari ya Mwenyezi Mungu

Question

 Mimi nimeingia katika Uislamu hivi karibuni, na miongoni mwa mambo yanayonitatiza ni kuwepo Aya nyingi katika Qur`ani Tukufu zinazobainisha kwamba Mwenyezi Mungu anamwongoa amtakaye na anamwachia kupotea amtakaye.
Na ikiwa Mwenyezi Mungu Ndiye aliyemwachia mtu mmoja apotee, basi vipi atampa malipo yake baada ya kumwandikia kadari?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amempa binadamu chaguo aliposema: {Na tukambainishia zote njia mbili} [AL BALAD 10], na wakati huo huo alimjulisha kwamba kila kitu kinatokea kwa mujibu wa kadari, uwezo na elimu yake Mwenyezi Mungu.
Jambo linalokusanya baina ya mambo haya mawili; chaguo na kadari ni kwamba Mwenyezi Mungu amemrahisishia binadamu vitendo vyake na njia yake katika maisha, na akamwamrisha afuate njia iliyonyooka, na kwa hivyo basi haijuzu kwa mtu yeyote kuuacha uwongofu na kuyaachilia mambo katika kadari; kwani haijulikani kadari hiyo na hukumu yake.
Vile vile mtu haruhusiwi kuacha kuomba riziki kwa kudai kwamba ilikwishaandikwa, hakika Mwenyezi Mungu amerahisisha sababu na athari pamoja na matokeo yake. Naye ni Muumba wa kila kitu; Muumba wa binadamu, chaguo, kitendo na matokeo, hali ya kuwa jambo hili halitofautiani na kuwa ni juu ya mtu kuomba haki na kuchagua upande wa kheri, pamoja na kujua kwamba kila kitu kinatawaliwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu ambao hakuna chochote kinachoweza kuuepuka.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas