Jihadi na Kuwaua Watalii.

Egypt's Dar Al-Ifta

Jihadi na Kuwaua Watalii.

Question

 Siku hizi tunasikia maneno mengi kuhusu jihadi, na kwamba ni faradhi inayozoroteshwa, na uvumi unaenezwa kwa ajili ya kuhalalisha vitendo vikali chini ya wito wa kufufua faradhi ya jihadi ya kiislamu; kama vile kuwaua watalii wanaoingia nchi za Waislamu kwa viza, vitendo vya kulipua mabomu, shughuli za kujitoa muhanga katika nchi zisizokuwa za kiilamu, hivyo kwa sababu kwamba viza siyo usalama, kwa hivyo, inaruhusiwa kuwaua watalii walioingia nchi za Waislamu, vile vile, wanaruhusu kwa walioingia nchi za wasio Waislamu washiriki katika shughuli za kujitoa mhanga.
Je, faradhi ya Jihadi inazoroteshwa? Na Je, viza ni usalama unayohifadhi damu na mali ? Ni ipi Hukumu ya vitendo vya kulipua mabomu na shughuli za kujitoa muhanga?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuhusu wito wa kuzorotesha Jihadi : Mwanzoni tunapaswa kusisitiza kwamba Jihadi ni haki na ni faradhi ambayo hawezi yeyote kuizorotesha wala kuizuia, lakini kama ikikiukwa Sheria na kutotekelezwa nguzo na masharti yaliyotajwa na Wanazuoni wa Sheria ilikuwa siyo Jihadi iliyoruhusiwa ; mara moja inakuwa uharibifu katika ardhi, na mara nyingine inakuwa uhaini na usaliti. Siyo kila kupigana ni jihadi, wala kila kuua katika vita inaruhusiwa.
Ni lazima kupambanua kati ya dhana mbili muhimu : “Jihadi” na “Irjaf” : istilahi ya “Jihad kwa ajili ya Allah” ni istilahi ya kiislamu ina maana pana katika Uislamu ; inaitwa Jihadi ya binafsi, matamanio, na Shetani, na inaitwa kupigana na adui ambapo inatakiwa kuondosha uadui na kuzuia udhalimu, na aina hii ya Jihadi ina masharti yake ambayo haikuwa sahihi isipokuwa kwake, kuwepo kwa khalifa Mwislamu anayewahamasisha Waislamu miongoni mwa raia wake kwa ajili ya Jihadi, kuwepo kwa bendera wazi ya kiislamu, utoaji wa nguvu kwa Waislamu. Jihadi ni miongoni mwa faradhi za kutosha ambayo jambo la kuipanga linarudia Watawala na mabwana waliochukua madaraka ya nchi na waja na walikuwa na uwezo zaidi kuliko wengine kujua matokeo ya maamuzi haya, ambapo wanafikiria udharura unaoita kwa ajili yake kutoka kuzuia uadui au kuzuia udhalimu. Basi uamuzi wa Jihadi unasomwa kwa njia ya kisayansi kutoka pande zake zote na matokeo yake njia hii ina uwiano kati ya maslahi na uharibifu, pasipo na kuogopa au udhaifu, pasipo na ujuu juu au vurugu au mhemuko ambao hautawaliwa kwa uthibiti wa akili timamu. Watu hawa watalipwa thawabu kwa ajili ya jitihada zao kwa kila hali, kama wakishinda kufikia yanayotakiwa basi watalipwa thawabu mara mbili, na kama wakishindwa watalipwa thawabu mara moja tu, na kama hawakujitahidi basi watapata dhambi, na hakuna yeyote ana la kufanya kwao isipokuwa kutoa shauri kama akiwa miongoni mwa wenye shauri, lakini kama akiwa siyo miongoni mwa wenye shauri basi hasemi kuhusu jambo ambalo halijui. Na asianze Jihad kwa mwenyewe au hali hii itakuwa ukiukaji wa haki za khalifa, pengine madhara ya kutoka kwa ajili ya Jihadi yatakuwa zaidi kuliko maslahi ambapo anapata dhambi ya matokeo ya kazi yake.
Kama watu wote walilazimishwa kutoka kwa ajili ya Jihadi mmoja mmoja pasipo na kuwahamisishwa na Khalifa maslahi ya watu yatalemazwa na maisha yao hayatakuwa sawa sawa. Mwenyezi Mungu Mukufu alisema : {Wala haiwafalii Waumini kutoka wote} [ATAWBAH : 122], Ingawa hali hii inapelekea maangamizi, kutojali matokeo, inasababisha kuwashambulia mataifa juu ya Waislamu, inayaangamiza mabustani yao, na ni sababu ya kuingia katika fitna na mgogoro unaowaangamia Waislamu, sababu ya mambo haya yote ni maumizi wa kupigana mmoja mmoja yasiyosomwa vizuri. Inafahamika kwa upande wa Sheria na akili na kupitia hali ya kweli kwamba hali ya utawanyiko na kutokwepo kwa bendera hupoteza kupigana mpango wake kwa upande mmoja, inaondosha thamani yake na inachanganya heshima ya lengo lake kwa upande mwengine.
Imepokelewa kutoka kwa Imam Al-Qurtubi katika kitabu cha [Hukumu za Qur’ani 5/259]: kutoka kwa Imam Sahlu Ibn Abdullah Al-Tostari -Mweneyzi Mungu amrehemu- amesema kuwa : “Tiini kauli ya Khalifa katika mambo saba: kutengeneza pesa, vipimo na mizani, hukumu, kuhiji, kusali ijumaa, kusali edi mbili, kusimamisha jihadi”.
Imam Abu Bakr Ibn Al-Arabi Al-Malki alisema katika kitabu cha: [Hukumu za Qur’ani 1/581- Darul Kutub Al-Elmiyah] kwamba: “Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru watu kufanya Jihadi katika vita vidogo vinavyotawanyika au vinavyokusanyika kwa Mfalme, vita hivi vidogo vikitokea, basi havitokei isipokuwa kwa idhini ya Khalifa; ili awatafutie habari, nguvu, na pengine wanahitaji kumwepushia mbali”.
Imepokelewa katika kitabu cha: [Mawahibul Jaliil kwa Imam Al-Hattab Al-Malki 3/349- Dar Al Fikr] kuwa: “Ibn Arafah Al-Sheikh alisema: Je Inaruhusiwa kupigana vita pasipo na idhini ya Khalifa? akasema: Ama kuhusu Jeshi hairuhusiwi isipokuwa kwa idhini ya Khalifa na kuongozwa na mkuu wao”.
Vile vile, katika kitabu hicho (3/350) imepokelewa kutoka kwa Bwana wangu Ahmad Zarruuq miongoni mwa Wanazuoni wakubwa wa madhehebu ya Imam Malik na miongoni mwa watu wema sana, alisema kuwa: “Kuelekea Jihadi pasipo na idhini ya kundi la Waislamu na Khalifa wao ni ngazi ya fitna, na hakuna wengi walioshughulikia jambo hilo ila walishindwa”.
Imam wa Misikiti Miwili Mitukufu alisema katika kitabu chake cha: [Ghaithul Umam fii Al-Tiyaath Al-Dhulam 155-156] kuwa: “Inapasa kujua kuwa: faradhi nyingi za Kutoshelezeana zisizosimamishwa na Makhalifa, inapaswa wenye madaraka wote wazijali faradhi, kama vile; kuandaa wafu na kuwazisha kusali juu yao. Ama kuhusu J/ihadi, inategemewa kwa Khalifa”.
Ibn Qudamah Al-Hanbali alisema katika kitabu cha [Al-Mughni 9/166- Daru Ihyaa Al-Turaath Al-Arabi] kuwa : “Mambo ya Jihadi yanategemewa kwa Khalifa na jitihadi yake tu, watawaliwa wanabidi kumtii kuhusu anavyoona”.
Kutoka upande mwengine istilahi ya Jihadi haina maana ya kupigana tu, bali maana yake ni kutayarisha majeshi, kulinda mipaka, kuhifadhi mapengo, na mambo hayo ni miongoni mwa faradhi za kutoshelezeana [Kifaya] katika Jihadi. Kama hali hii ikifanyika kutegemea uwezo basi wakati huu haisemekani kuwa : Jihadi imelemazwa. Mabwana wa madhehebu ya Imam Al-Shafii walisema kuwa : “Faradhi ya Kifaya -yaani Jihadi- inatekelezwa na Khalifa anapokusanya idadi ya watu katika mapengo yanayo sawa na idadi ya makafiri pamoja na kulinda bima na handaki, na kuwaiga wafalme, au Jihadi inatekelezwa pia kupitia kuingia Khalifa na makamu mkuu wake nchi za makafiri pamoja na majeshi kwa ajili ya kupigana nao”. [Mughni Al-Muhtaaj 4/210 – Al-Halabi].
Vile vile kutayarisha kwa “njia za kuzuia uhalifu” ni muhimu sana zaidi kuliko vita venyewe; kwa sababu njia hizi zinasitisha umwagikaji damu, Qur’ani imeashiria hali hii katika kauli yake: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu} [AL ANFAAL : 60].
Imam Al-Shafii -Mwenyezi Mungu amradhi naye- alisisitiza kwamba kulinda mapengo na mipaka ya Uislamu ni muhimu zaidi kuliko kupigana vita na nchi za makafiri, kupigana vita nao wakati ule kuna masharti ya kutodanganya Waisalmu, na inatarajiwa kushinda. Kutokana na hivyo, inafahamika kwamba shughuli za kujitoa mhanga zinazosababisha maangamizi ya Waislamu zaidi kuliko wasio Wasilamu haziruhusiwi kamwe, kwa sababu ya maangamizi yake kwa Waislamu pasipo na kushinda juu ya maadui. Imam Al-Shafii alisema katika kitabu cha [Al-Um 4/91-92] kuwa : “Mwanzoni ni wajibu kulinda mipaka ya Waislamu, vile vile, handaki na kuwazuia maadui, na kabla ya kurudi kwa maadui nchi zao waislamu wote wapigane vita na Washirikina … kama ikifanya hivyo, ni wajibu juu ya Khalifa kuwaingiza Waislamu nchi za Washirikina katika wakati wa kutodanganya Waislamu, na anatarajia kushinda”. Halafu Imam huyo anasisitiza kuwa hairuhusiwi kuhamasisha Waislamu kupigana vita kwa maangamizi yao akisema katika kitabu cha [Al-Um 4/91-92] kuwa : “Haipaswi Khalifa kumwamuru yeyote kupigana vita ila mwenye imani, jasiri, mwenye akili katika vita, siyo mwenye haraka, na Khalifa amwambie yule aliyemwamuru asipigane na Waislamu kamwe”
Al-Qaadhi Abdulwahab Al-Malki alisema katika kitabu cha [Al-Maunah 1/393] kuwa: “Nayo -Jihadi- ni miongoni mwa faradhi za Kifaya siyo faradhi za lazima, anayeifanya inaondoshwa kwa waliobakia, na lengo lake ni kulinda mapengo na kuyahifadhi kwa nguvu na idadi ya watu”.
Imam Ibn Jazi Al-Malki alisema katika kitabu cha [Al-Qawaniin Al-Fiqhiyah, uk. 126] kuwa : “Kuhusu hukumu ya Jihadi, ni faradhi Kifaya kwa mujibu wa Wanazuoni wengi ..., kama mipaka ya nchi ikilindwa, na mapengo yakihifadhiwa, faradhi ya Jihadi iliondoshwa na ilikuwa sunna tu”.
Ktokana na matini hizi zilizotangulia inafahamika kwamba faradhi ya Kifaya katika Jihadi kwa kuilinda mipaka inatofauti katika nchi nyingi za Waislamu kwa jumla, na Jihadi haikulemazwa kama wanvyodai wale.
Jihadi ni faradhi ya lazima katika nchi zinazodhalilishwa ndani yake utukufu wa Waislamu na wapiganaji vita ambao ni wadhalimu, wenye nchi hizi ni lazima wazilinda, katika wakati huu Jihadi ni faradhi ya Kifaya kwa wanaokaa nje ya nchi hizi kwa mujibu wa kauli ya Wanazuoni wa Fiqhi.
Mwanachuoni Al-Shirbini Al-Khatib alisema katika kitabu cha Al-Iqnaa nacho ni miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Shafii [4/254, 255, na Hashiat Al-Bijermi, Darul Fikr] kuwa : “Na hali nyingine ya Makafiri ni kuingia nchi yetu, wenye nchi hii ni lazima kuilinda kwa kadiri wanavyoweza. Jihadi katika hali hii ni faradhi ya lazima, na hukumu yake ile ile kwa wanaokaa mbali kidogo lakini ndani ya nchi hii, ama wanaokaa nje ya nchi hii wanalazimishwa kurudi nchi yao kama wakihitajiwa, kwa ajili ya kuilinda, basi ni faradhi ya lazima kwa wanaokaa ndani, na ni faradhi ya Kifaya kwa wanaokaa nje”.
Kutokana na hivyo, inafahamika kwamba Jihadi inategemea haja kwa wanaokaa ndani ya nchi iliyoshambuliwa, na kama wanaokaa ndani ya nchi hii wakihitajiwa kwa ajili ya kuilinda ni lazima waende huko, kama hawakutosha, basi wanaokaa mbali zaidi waongezwe nk. Lakini kutekeleza hukumu ya Kisheria kwa njia hii ni lazima iwe na njia sahihi inayohusishwa na pande zinazojua ukweli wa mambo ya vita, siasa, pande zinazokadiri haja, zinazoangalia hisabu za matokeo, maslahi, ufisadi unaohusiana na hali ya kitaifa, mikataba ya kimataifa, kujua mizani ya nguvu za kidunia, na kila kinachohitaji bajeti maalum, mafunzo ya kina ya vita, ya kisiasa, yanayoangalia chaguo la amani lililoashiriwa na Mwenyezi Mungukufu Mkatika aya hii : {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua} [AL ANFAAL : 61], na kulinda usalama wa nchi za Kiislamu, raia wao, maslahi zao kwa upande mwengine, uwezo wao wa kupambana na kuvumilia chaguo la vita kwa upande wa tatu, ili jambo hili linafanyika kwa njia rasmi na inayoainishwa umbo lake inaaminiwa watakao Jihadi ili wasiwe mateka kwa pande zinazotiliwa shaka, zinazowatumia hisi zao, na hamasa zao kwa kuhudumia malengo yao ya nje kwa jina la Jihadi kwa upande wa nne. Hayo yote ni masuala yanayohusiana na fiqhi ya umma, ambayo yanaangaliwa na mifumo, majeshi, taasisi kubwa tu. Na hayahusiani na fiqhi ya watu, na hawawezi kuamua kuhusu hatima ya mataifa. Wanaotawala Waislamu tu ni wenye mamlaka juu ya masuala hayo, hata kama hawakujitihadi, basi hali hii haifanyi Jihadi ikalemazwa pamoja na kulinda mapengo na mipaka. Na hakuna sababu yoyote kwa kukiuka mipaka ya mfumo wa ujumla wa kundi la Waislamu ili maumizi ya vita yawe kupitia watu ovyo, hali ambayo inasababisha kuangamia nchi kavu na ya kijani, licha ya vitendo hivi vya mabomu ambavyo havihusiani na Jihadi ya Kiislamu wala vita heshima.
Kisha Jihadi ambayo ina maana ya kupigana haikusudiwi yenyewe, kupigana na wasio Waislamu hakukusudiwi pia kinyume na wanaofikiri wenye mitazamo mikali inayofanya asili kwa wasio Waislamu kuwa damu yao ni halali, wakati ambapo wanazuoni wa Sheria wamebainisha kwamba Waislamu wanapofanya faradhi ya Kifaya kupitia kulinda mapengo na mipaka ya nchi za Kiislamu, basi ulinganiaji unatosha badala ya kupigana na wasio Waislamu, na ulinganiaji unapokuwa sahihi, basi hakuna haja ya Jihadi, na kwamba kumwua kafiri hakukusudiwi kamwe, na jihadi ni chombo tu haikusudiwi yenyewe, Wanazuoni walisema : “Umuhimu wa Jihadi ni umuhimu wa vyombo tu, kwani inayokusudiwa kupitia kupigana ni kuongoza, lakini hali ya kupigana na makafiri haikusudiwi hata kama ikiwezekani kutoa uongofu kupitia dalili pasipo na Jihadi itakuwa ni bora zaidi kuliko Jihadi”. [Mughni Al-Muhtaj 4/210].
Ama kuhusu wanayoyasema wale ni “Irjaf” siyo Jihadi, nayo ni istilahi inayotajwa katika Qur’ani katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu (60) Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa (61) Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.(62)} [AL AHZAAB : 60-62], nalo ni neno linalo na maana mbaya, maana yake ni kueneza fitna kupitia kuhalilisha kumwaga damu na kushambulia mali kati ya wanajamii chini ya madai tofauti, miongoni mwao ni: kudai kuwa mtawala akatoka katika Uislamu, au serikali ya nchi, au makundi maalum ya watu, na miongoni mwa madai hayo ni kuhalilisha kumwaga damu za wasio Waislamu chini ya dali la kuamrisha mema na kukataza maovu, au kuhalilisha kumwaga damu za wasio Waislamu katika nchi zao, au wale walioingia nchi za Kiislamu kwa kudai kuwa nchi zao zinapigana na Uislamu…n.k kuhusu madai ya kueneza fitna zinazoshawishwa na Shetani kwa waenezao fitna, na ambazo baadhi yake zilikuwa sababu ya kujitokeza kwa Khawarij katika wakati wa Masahaba na wanaokuja baada yao wakatoa sababu za ufisadi wao katika ardhi na kumwaga damu ambazo ni haramu.
Katika wakati huu utawala unatofauti kufuatana na dhana ; wanavyofanya wenye mitazamo mikali katika nchi za Kiislamu kuhusu kuwaua watalii, au katika nchi zisizo za Kiislamu miongoni mwa shughuli za kujitoa mhanga, au vitendo vengine vya ufisadi vinavyotokea mbinu za “Irjaf”, vitendo vyote hivi ni haramu, navyo ni aina ya udhalimu iliyoharimishwa kwa Sheria, na kuwapigana na wenye mitazamo hii kama hawajiepushi na kuwadhuru Waislamu na wasio Waislamu wakiwa wananchi waliopewa amani, na kuitoa jina la Jihadi ni uwongo ili wenye akili dhaifu wasadiki ufisadi wao na kueneza fitna zao, na hali hii ni jeuri katika nchi bila ya haki, wenye jeuri hii ni wadhalimu wanapiganwe kama wakiwa na nguvu mpaka waepushe udhalimu wao na kueneza fitna.
Hivyo vinabainishwa kwa hukumu ya aliyepewa amani, kueleza viza na athari yake kwa mujibu wa Sheria :
Siku hizi watalii ni wasafiri waliokuja kwetu miongoni mwa wanaume na wanawake wakaingia nchi zetu kwa usalama, na hukumu yao katika hali hii ni kama (Musta’man) kafiri aliyepewa amani. Maana ya (Musta’man) katika lugha : Ni yule aliyepewa amani. Na maana yake katika istilahi : “Ni yule aliyeingia nchi nyingine kwa amani akiwa ni Mwislamu au adui wa kivita”. [Al-Darul Mukhtar kwa Imam Al-Haskafi Al-Hanafi pamoja na Hashiyat Ibn Abdiin 4/166].
Amani ni ahadi ya Kisheria na mkataba unaolazimisha uharamu wa kumwua mtu yule na uharamu wa kuiba mali yake. Sheria imeamuru kutimiza ahadi, na dalili za Kisheria zimesisitiza kutimiza ahadi zote.
Imam Al-Shafii -R.A- alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/106, Darul Shaab] kuwa : “Kutimiza ahadi katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} [AL MAIDAH :1], na kauli yake pia {Wanatimiza ahadi} [AL INSAAN: 7], vile vile Mwenyezi Mungu ametaja maudhui ya kutimiza ahadi katika aya nyingi za Qur’ani, nayo ni pamoja na ahadi zote…”
Hukumu ya kafiri aliyepewa amani ni: kuthibitishwa kwa amani kwake na inalazimishwa kuhifadhi nafsi yake, mali yake, na heshima yake kama walivyo wananchi. Kama Khalifa au mwengine akimpa yeyote amani, Waislamu wote wanalazimishwa kutimiza ahadi hii na hairuhusiwi kumwua wala kumteka, wala kuchukua chochote kutoka mali yake, wala kumwudhu.
Imam Al-Shafiy -R.A- alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/107] kuwa : “Kama ikiwa hivyo -yaani kama Khalifa akiwapa watu ahadi au akichukua Jizyah kutoka kwao – hairuhusiwi kwa Mwislamu yeyote kuchukua mali zao au kumwaga damu zao”.
Imam Al-Nawawi katika Kitabu cha [Rawdhatul Talibiin 7/474]: “Kama Kafiri akipewa amani, basi hairuhusiwi kumwua wala kumteka”.
Amani inafanyika kwa mujibu wa Sheria kwa vyovyote; ikiwa ni neno, maandishi, ishara, desturi, na kwa njia yoyote ikiwa kwa uwazi au kwa ishara, au kwa lugha yoyote. Pia amani inapewa kwa yeyote aliyedhani hata kwa makosa kwamba amepewa amani, basi hairuhusiwi kumsaliti, iwapo Wanazuoni wa Sheria wamesema kwamba kufahamu kuwa asiye Mwislamu ana amani kwa hali yoyote, hali hii inalazimisha kuihifadhi damu yake na mali yake.
Ibn Al-Hajib alisema katika kitabu chake [Jami’ul Umahaat] kutoka vitabu vya maimam wa madhehebu ya Imam Malik [246-247, Darul Yamamah] kuwa : “Kama adui wa kivita akidhani kuwa ana amani, na Khalifa akiwakataza watu wakaasi au wakasahau au hawakujua hivyo, adui huyo arudishwe kwa amani yake”.
Imam Ibn Juzayya Al-Maliki alisema katika kitabu chake [Al-Qawaniin Al-Fiqhiyyah, uk. 134, Darul Fikr] kuwa: “Kama kafiri akidhani kuwa Mwislamu alitaka kumpa amani, lakini Mwislamu huyo hakutaka hivyo, basi hairuhusiwi kumwua. Na kama akihitaji amani kwa jamaa zake na mali yake, inalazimishwa kutimiza ahadi yake hii… na aliyeingia ubalozi wowote hakukosea amani, lakini makusudi yake haya ni amani kwake tu”.
Sheikh Al-Khatib Al-Sherbiniy alisema katika kitabu chake “Mughni Al-Muhtaj” kutoka vitabu vya [Maimam wa Madhehebu ya Shafii 6/52, Al-Halabi] kuwa : “Inaruhusiwa kumpa amani kupitia neno lolote lina maana hiyo kwa uwazi ; kama vile kumwambia nimekupa ulinzi na amani, au usiogope wewe utakuwa kama unavyopenda, au uwe kama unavyotaka, na inaruhusiwa kwa kuandika hivyo pia”.
Wanazuoni wa Fiqhi walisema kwamba ikiwa mtu yeyote asiye Mwislamu atapewa idhini ya kuingia nchi za Kiislamu, hali hii ina maana ya kumpa amani pia, basi hairuhusiwi kuivunja ahadi hiyo:
Al-Hafidh Abu Umar Ibn Abdulbar Al-Malkiy alisema katika kitabu chake [Al-Istidhkar fi Sharh Madhab Ulamaa Al-Amswaar 5/35] kuwa : “Kila kinachofahamika kwa adui wa kivita kuhusu amani ikiwa kupitia maneno au ishara au idhini, basi ni amani na inapaswa kwa Waislamu wote kutimiza ahadi hiyo”.
Siku hizi kuingia nchi kwa njia rasmi kupitia viza ya kuingia au ya kupita, na viza hii ni kibali cha kuingia nchi kwa amani kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na desturi za ubinadamu. Kuruhusiwa kwa kuingia nchi tu kuna maana ya kupa amani, na imetajwa kwamba amani inapewa kupitia chochote kinachomaanisha hivyo. Kwa hivyo, imethibitishwa kuwa viza ina maana ya kupewa amani, na ahadi zote zinazofanyika kupitia viza zitimizwe. Ahadi inafanyika kwa chochote kinachomaanisha hivyo, yaani asiye Mwislamu yeyote akiingia nchi za Kiislamu kwa haja yeyote - ikiwa kwa ajili ya utalii au haja nyingine- akapewa amani, basi hairuhusiwi kumwaga damu yake wala kuiba mali yake. Na hivyo ndivyo Wanazuoni walivyosema kuhusu kudhani amani kunailazimisha kwa asiye Mwislamu hata akiwa ni adui wa kivita, hata akidhani kwa kosa kuwa akipewa amani.
Mkataba wa amani kwa jumla unafanyika kwa Makhalifa, lakini mkataba wa amani kwa idadi maalum ya ujumbe wa watalii au wa kibiashara, mkataba huu unafanyika kwa Mwislamu muungwana, mwenye akili timamu, na aliyebaleghe kwa mujibu wa maafikiano ya Wanazuoni. Amani hii haimtegemei Khalifa pekee yake, lakini kama Mwislamu yeyote alimpa amani mtu asiye Mwislamu, ni lazima Waislamu wote watimize ahadi hii na hairuhusiwi kumsaliti asiye Mwislamu huyo kufuatana na kauli ya Mtume S.A.W, kuwa : “Dhima ya Waislamu ni moja; hata aliyechukua dhima hiyo ni Mwislamu aliye chini kabisa, basi Mwislamu anayevunja dhima aliyechukua Muislam mwengine juu ya kafiri, atalaaniwa na Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote. Haitapokelewa ibada yake ya faradhi wala ya sunna siku ya Kiama.”. Hadithi hii imeafikiwa na Wanazuoni kutoka katika Hadithi ya Ali Ibn Abi Talib rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie.
Kauli yake Mtume S.A.W – “dhima ya Waislamu” ni: ahadi yao, na kauli yake: “aliyechukua dhima hiyo ni Mwislamu aliye chini kabisa” yaani: aliyehusika na dhima yao ni aliye chini kabisa miongoni mwao katika hali na idadi. Basi kama Mwislamu mmoja – au Khalifa – atampa mtu mwengine ahadi, hairuhusiwi kuivunja. Na kauli yake “Haitapokelewa ibada yake ya faradhi wala ya sunna” yaani: haitapokelewa kazi yoyote.
Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalani katika kitabu chake [Fathul Bari 4/86, Al-Slafiyyah] kuwa : “Na maana ya kwamba : dhima ya Waislamu ni ikiwa imepewa na Mwislamu mmoja au Waislamu wengi, mheshimiwa au mwenye hali ya chini. Kama Mwislamu mmoja akampa kafiri amani, hairuhusiwi kwa yeyote kuivunja ahadi hiyo, wote ni sawa katika jambo hili mwanamke, mwanamume, muungwana, na mtumwa, kwa sababu Waislamu wote ni kama nafsi moja”.
Kufuatana na hivyo, matini za Wanazuoni wa Fiqhi zimetajwa kama zifuatazo :
Imam Al-Shafii – Mwenyezi Mungu awe radhi naye – alisema katika kitabu chake [Al-Um 4/196] kuwa : “Kama Mwislamu balighe akampa amani kwa muungwana au mtumwa anayepigana au asiyepigana au mwanamke, basi amani inaruhusiwa.. kama Mwislamu akiwaashiria watu hawa kwa kinachomaanisha amani akisema : Nimewapa amani kwa ishara, basi hii ni amani”.
Al-Qaadhi Abdulwahab Al-Malkiy alisema katika kitabu cha [Al-Maunah ala Madhhab Alam Al-Madinah 1/408, Darul Kutub Al-Ilmiyyah] kuwa: “Amani iliyopewa na Mwislamu muungwana aliyebaleghe hairuhusiwi kuivunja awe Mwislamu huyo ni mwanamume au mwanamke”.
Imam Ibn Juzayya Al-Maliki alisema katika kitabu chake [Al-Qawaniin Al-Fiqhiyyah, uk. 134, Dar AL Fikr] kuwa: “amani ni aina tatu : Ya kwanza na ya pili ni amani ya kijumla nayo inahusiana na Khalifa tu, nazo ni mapatano na dhima, ya tatu ni : Inahusiana na kafiri mmoja au idadi maalum, anapewa na Mwislamu yeyote mwenye akili, akiwa ni mwanamke kwa mujibu wa madhehebu manne, na pia mtumwa kwa mujibu wa madhehebu tatu tu (yaani madhehebu yote isipokuwa madhehebu ya Imam Ahmad Ibn Hanbal )”.
Ibn Al-Hajib alisema katika kitabu chake [Jami’ul Umahaat 247-246] : “Inaruhusiwa amani inapewa na mkuu wa jeshi kwa ujumla na kwa sharti.. Vile vile kila Mwislamu, muungwana, balighe, anaweza kupa amani… Pia mwanamke, mtumwa na mtoto akiwa na akili timamu wanaweza kupa amani kwa mujibu wa mtazamu mashuhuri wa Wanazuoni”.
Watalii hawa wasio Waislamu walipewa amani na Khalifa kupitia viza, pia hawa waliofanya mkataba pamoja na jumbe hizi za kiutalii na walipanga safari zao na waliwakaribisha katika nchi zao pia waliwapa amani, waliowafikisha miongoni mwa Waislamu mpaka nchi zao waliwapa amani, na waliowapokea katika uwanja wa ndege, wakawaingiza nchini wakawapa amani, hali hizi zote zina hukumu ya amani iliyohifadhi damu zao na mali zao.
Kama mtu asiye balighe au asiye na akili timamu akiwapa amani, wakadhani kwamba hii ni amani, hairuhusiwi kuwaua, lakini ni lazima kuwapa amani na ulinzi wao, kwa sababu ya kutopambanua baina aliyeruhusiwa kupa amani na asiyeruhusiwa.
Imam Al-Shafii -R.A- alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/196] kuwa : “Kama kafiri moja akipewa amani na wasio balighe au mwenye wazimu hairuhusiwi kuivunja ahadi yake kabisa, vile vile mwenye dhima akipewa amani hairuhusiwi kuivunja ahadi yake kabisa. Kama yeyote miononi mwa hawa akitoka kwa amani ni lazima kuihifadhi amani yao wala hairuhusiwi kuiba mali zao au kumwaga damu zao”.
Vitendo vya uharibifu vya makundi dhalimu dhidi ya watalii na kuwaua ni ukiukaji wa watawala Waislamu na ukiukaji wa umma wote na kuivunja ahadi zao.
Dalili zao kuhusu kuruhusiwa kwa vitendo vya mabomu kama ilivyothibitika katika Sunna Tukufu kuhusu kuwashambulia washirikina dalili hizi ni kosa kubwa na upimaji mbovu ; kwa sababu kushambulia hakuruhusiwi isipokuwa kwa kuivunja ahadi na amani au inayofahamika siku hizi kwa azimio la vita, na hairuhusiwi kabisa kushambulia pamoja na kutimiza ahadi na amani.
Imam Al-Shafii -R.A- alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/107] kuwa : “Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema : {Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini} [AL ANFAAL : 58], Imam Al-Shafiy alisema : Kama ikitajwa dalili zenye maana ya kutotimiza watu ahadi yao ya kusitisha uadui, basi dalili hizi zinarudishwa kwao, [4/108] “Kama wenye kusitisha uadui walikuwa miongoni mwa wanaoruhusiwa kuchukuliwa Jizya hairuhusiwi kuwadanganya. Baada ya kuivunja ahadi na azimio la vita, Khalifa anaruhusiwa kuwashambulia waliovunja ahadi katika wakati wowote na kuwachukua mateka kama wakimdanganya”.
Upimaji wa kudanganya katika vita ni upimaji mbovu ; kwa sababu ni upimaji tofauti ; kwani ipo tofauti kubwa kati ya kuivunja ahadi na uhaini unaoruhusiwa katika vita, kuhusu jambo hili Imam Ibn Jazi alisema katika katika kitabu cha [Al-Qawaniin Al-Fiqhiyah, uk. 135] akisisitiza tofauti hii kuwa: “Tofauti kati ya kuivunja amani na uhaini unaoruhusiwa katika vita ni kwamba amani inaitua nafsi ya kafiri, udanganya ni utaratibu wa mafumbo ya vita kwa njia iliyowadanganya adui kugeuka kutoka kwake hivyo kuna nafasi, basi kudanganya na tauria inaruhusiwa, na hairuhusiwi kuwafahamisha makafiri kwamba yeye amekuja kwa ajili ya kuwashauri, hali hii ni uhaini nayo hairuhusiwi”.
Imam Al-Nawawi alisema kuwa : “Wanazuoni wameafikiana juu ya kuruhusiwa kwa kuwadanganya makafiri katika vita kwa kadiri inavyoweza, ila kwa kuivunja ahadi au amani, hali hii hairuhusiwi”.
Yaliyotangulia yanathibitisha utukufu wa damu, mali, na heshima ya wasio Waislamu wakati wa kuingia nchi za Waislamu kwa amani. Hairuhusiwi wakati huu kuwashambulia kabisa. Hali ile ile kuhusu kuingia kwa Mwislamu nchi za wasio Waislamu kwa viza : kama kwamba hairuhusiwi kuwadanganya wasio Waislamu wakati wa kuingia nchi za Waislamu kwa amani, hali ile ile kuhusu Mwislamu akiingia nchi za wasio Wasilamu kwa viza, basi ana haki ya kupewa amani, na hairuhusiwi katika wakatu huu kukiukwa utukufu wake au kumshambuliwa. Damu zao, mali zao, na heshima yao ni haramu, hali kumshambulia ni uhaini kwa mujibu wa yaliyotajwa na Wanazuoni ; kwani tumetaja kwamba viza ya kuingia nchi za Waslamu ni amani kwa wasio Waislamu, hali ile ile kwa Mwislamu wakati wa kuingia nchi za wasio Waislamu, kwa sababu wasio Wasilamu hawakumpa Mwislamu viza ila kwa sharti ya kuacha kuwadanganya na kuhifadhi nafsi zao, ingawa sharti hii haikutajwa kwa uwazi, lakini inafahamika katika maana kama alivyosema Imam Ibn Qudamah Al-Hanbali katika kitabu chake [Al-Mughni], maneno yake yatatajwa baadaye. Mkataba wa amani una maana ya kuwa na haki ya kupewa amani pande zote mbili, na kwamba kila upande umeupa upande mwengine amani, kwa hivyo, Mwislamu wakati huu haruhusiwi kumdanganya mwengine asiye Mwislamu kabisa.
Imam Al-Shafii -R.A- alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/164-165, 188] kuwa : “Kama wasio Wasilamu wakimpa Mwislamu amani, wakamruhusishia kuingia nchi zao kwa wema, nao wana uwezo juu yake, ni lazima kwake kuwapa amani pia, yaani kumpa amani kwake ni amani kwao, Mwislamu katika wakati huu haruhusiwi kuwaua au kuwadanganya.. Kama watu miongoni mwa Wasilamu wakiingia nchi za kivita kwa amani, basi adui ni lazima kupewa amani mpaka watoke au kufikia muda ya amani, na hairuhusiwi kwao kuwadhulumu maadui au kuwadanganya.. na hatujui mtazamo mwengine unaopinga mtazamo huu”.
Imam Mohammad Ibn Al-Hassan Al-Shibani alisema katika kitabu chake [Al-Sair Al-Kabiir maa Sharhul Sarkhasi 2/66-67, Dar Al Kutub Al-Ilmiyyah] kuwa : “Kama baadhi ya Waislamu wakija mahali pa adui wa kivita wakiwaambia kuwa : sisi ni wajumbe wa Khalifa, wakitoa barua inayofanana na barua ya Khalifa au hawaitoi, na jambo hili lilikuwa hila kutoka wao kwa washirikina, maadui wakawaambia : ingieni, Waislamu wakaingia nchi ya kivita, basi Waislamu hawaruhusishwi kumwua yeyote miongoni mwa maadui wa kivita wala hawaruhusishwi kuchukua mali zao kama wakiwepo katika nchi zao”.
Aliyeeleza mtazamo huu alisema : “Kwani makafiri hawajui nia ya Waislamu wanaoingia nchi, basi hukumu inategemea wanaoonesha; kwa sababu ni lazima kuepuka kudanganya, hivyo kwa sababu suala la amani ni nguvu na uchache wake unatosha”.
Imam Ibn Qudamah alisema katika kitabu chake [Al-Mughni 12/587, Dar Al Hadith] kuwa: “Suala: anayeingia nchi ya adui kwa amani haruhusishwi kuwadanganya katika mali yao, kwa sababi udanganya wao ni haramu, kwani wamempa amani kwa sharti la kuacha kuwadanganya na kuwapa amani, ingawa sharti hili halikutajwa kwa uwazi, lakini linafahamika katika maana”.
Kutokana na hivyo, inadhihirisha kosa kubwa linalofanyiwa na hawa madhalimu katika nchi za wasio Waisalmu kutoka shughuli za kujitoa mhanga zenye uhaini, madhalimu hawa wanawashtusha wanaowaamini kwa shughuli hizi na wakawaruhusisha kuingia nchi zao, na kwamba vitendo hivi haviruhusiwi kabisa, bali vinapinga mafunzo ya Kiislamu na utukufu wake ambayo yanakataza uhaini hasa kwa walioturuhusishia kuingia nchi zao kwa amani.
Na sababu zinazotajwa na hawa kwa ajili ya kuhalilisha vitendo vyao vyenye kueneza fitna, ufisadi na vya mabomu katika nchi zinazopigana vita na Waislamu au zinazopinga wananchi Waislamu wanajibiwa kuwa vitendo hivi vya uhaini havitofautisha kati ya raia na mwanajeshi, na kwa mujibu wa Sheria, hairuhusiwi kukaribia kuwaua raia wakiwa ni wanaume au wanawake, na kama ikitangazwa Jihadi ni jambo la lazima tufautishe kati ya mwanajeshi na mwengine, hasa ikijulikana kwamba mara nyingi wananchi katika nchi za demokrasia za wasio Waislamu wanapinga vita vinavyopigwa na serikali zao dhidi ya baadhi ya nchi za Kiislamu, maandamano yanayopinga vita hivi yanajitahidi kuondosha serikali hii iliyotangaza vita. Maana ya hivyo ni kwamba siyo wananchi wote ni madui wa kivita kufuatana na serikali zao, kwa hivyo, kuwaua pasipo na kutofautisha kati ya raia na mwanajeshi siyo kutoka mafunzo ya Kiislamu. Na imethibitika kwa mujibu wa nguzo za Sheria Tukufu kwamba hairuhusiwi kumwadhibu mtu kwa sababu ya kosa la mwengine, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe.} [AL ANAAM: 164].
Imam Al-Shafii alisema katika kitabu cha [Al-Um 4/108] kuwa : “Kama wakitofautiana au baadhi ya watu hawakukubaliana nao, na baadhi yao wakaonehsa ikhlasi na wengine wakaonesha kinyume na hivyo, inaruhusiwa kupigana nao lakini siyo wote, inaruhusiwa kuwaita wenye ikhlasi watoke, wakitoka wanatimizwa ahadi na waliobakia wanauawa, lakini wenye ikhlasi kama hawakuweza kutoka wanaepushwa, na hairuhusiwi kuchukua mali zao wala kumwaga damu zao”.
Kutokana na kauli yake “inaruhusiwa kupigana nao lakini siyo wote” inadhihirisha kuwa wakiwepo watu miongoni mwao hawakupigana nasi (nao ni wengi miongoni mwa wananchi wa dunia wasio Waislamu wanaokataa kushiriki katika kupigana vita pamoja na serikali zao dhidi ya nchi za Kiislamu) watu hawa hairuhusiwi kupigana nao wote kwa vitendo vya mabomu au kwa shughuli za kujitoa mhanga. Na kupitia maneno ya Al-Shafii inajulikana ubatili wa dalili za watu hawa wanaosema kuwa shughuli za kujitoa mhanga zinaruhusiwa dhidi ya wasio Waislamu katika wakati ambao hakuna vita pasipo na kupambanua kati ya adui wa kivita na mwengine.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia inadhihirika kuwa kuwadhuru watalii wageni walioingi nchi za Waislamu kwa kuwaua ni maovu mazito na ni dhambi kubwa, kwa sababu hali hii inapingana na amani waliopewa nasi kupitia viza ya kuingia nchi zetu kwa njia za kisheria. Na ni hali ile ile kwa wasio Waislamu katika nchi zao hairuhusiwi pia kuwauawa kwa njia za kujitoa muhanga au kwa vitendo vyakulipua mabomu, kwa sababu vitendo hivi ni haramu, kwani vinapingana na amani waliopewa nasi tulipowaruhusu kuingia nchi zetu kwa nija ya kisheria, Na Sheria ilituamuru kutimiza ahadi na mikataba; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} [AL MAIDAH:1]. Na imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Abdullah Ibn Umar RA. kwamba Mtume S.A.W. anasema : “Mambo manne mwenye kuwa nayo basi huwa ni mnafiki wa kweli, na mwenye kuwa na moja tu katika hayo basi huwa na sifa moja ya unafiki mpaka aiwache: Anapo zungumza husema uongo na anapoweka miadi hatekelezi, na anapotoa ahadi hatimizi na anapo gombana hupindukia mipaka”.
Sheria imewatishia kama hawa wasiotimiza ahadi ya amani pamoja na waliowapa amani na wakawaruhusu kuingia nchi zao kuwa watabeba bendera ya uhaini Siku ya Kiyama. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Amr Ibn Al-Hamq Al-Khuzai R.A. amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anasema “aliyeaminiwa na mtu kwa damu yake na akamwua, basi atabeba bendera ya uhaini Siku ya Kiyama”.
Vitendo hivi ni miongoni mwa madhambi makubwa, kwani ni kumwaga damu iliyo haramu, kuua nafsi za Waislamu wasio na hatia, na nafsi za wasio Waislamu zilizoharimishwa kuziua isipokuwa kwa haki. Sheria Tukufu imeitukuza damu ya Mwislamu na ikatishia sana kuimwaga bila ya haki. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni moto wa Jahannamu na humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.} [AL NISAA : 93]. Imepokelewa kutoka kwa Al-Nasaa’i kutoka kwa Abdullah Ibn Umar R.A. kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anasema kuwa: “kuondokwa kwa dunia ni nyepesi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kumwua Mwislamu”, vile vile Mwenyezi Mungu aliharimisha kabisa kuua nafsi bila ya haki, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki.} [AL ANAAM : 151], bali Mwenyezi Mungu amefanya kuua nafsi -ikiwa ni Mwislamu au asiye Mwislamu- ni kuua kwa watu wote, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema : {Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.} [AL MAIDAH : 32].
Pia kuna kuua kwa wasio waangalifu, imepokelewa kutoka kwa Abu Dauud na Al-Hakim katika Mustadrak kutoka kwa Abuu Hurairah R.A. alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anasema: “Muumini haui mtu mwengine, Imani ni kizuizi cha kuua”. Ibn Al-Athir alisema katika kitabu cha [Al-Nihayah]; “Kuua maana yake ni kwamba mtu anamshambulia mwenzake bila kujali na kumwua”. Maana ya Hadithi ni kwamba Imani inazuia kuua kama kizuizi kinavyomzuia mtu kutenda, kwani kuna hila na udanganyifu, na kauli ya Mtume S.A.W: “Muumini haui” hili ni katazo au maneno haya yana maana ya katazo.
Katika hukumu za Jihadi inathibitika kwamba hairuhusiwi kumwua mtu ambaye mwito haukumfikia hata kama atakuwa ni adui wa kivita asiyepewa amani, fidiya ya mauaji yake ni juu ya aliyemwua, Imam Al-Shafii alisema katika Kitabu cha [Al-Um 4/157] kuwa : “Kama Mwislamu akiua mwengine mshirikina ambaye mwito haukumfikia, akamwangamiza”, hali vipi kwa aliyemwua aliyepewa amani na akamdanganya, akaihini dhima ya Allah, Mtume wake S.A.W, dhima ya Waislamu na watawala wao.
Na kwamba vitendo hivi vinapinga makusudi ya Sheria ya kuu :
Sheria Tukufu inasisitiza kuhifadhi vitu vitano ambavyo dini zote zimekubaliana umuhimu wa kuvihifadhi, navyo ni: dini, nafsi, akili, heshima, na mali, hivyo vitu ni makusudio matano ya Kisheria.
Ni wazi kwamba vitendo vya mabomu hivyo vinabatilisha makusudi hayo, miongoni mwao ni kuhifadhi nafsi; basi aliyeuawa kama akiwa ni yule aliyejitoa muhanga na aliyetenda vitendo vya kulipua mabomu aliyejilipua n.k. basi ataingia chini ya kauli yake Mtume S.A.W: “Mwenye kujiua kwa kitu fulani katika dunia ataadhibiwa kwa kitu hicho Siku ya Kiyama” Hadithi hii imekubaliwa kutoka kwa Hadithi ya Thabit Ibn Al-Dhahak R.A.
Na kama aliyeuawa ni mwengine, basi kama aliyeuawa ni Mwislamu, kumwua kwa makusudi ni uadui mkubwa, na hakuna dhambi kubwa zaidi kuliko dhambi hiii baada ya ukafiri. Kuhusu kukubali kwa toba yake au kutoikubali ipo tofautia kati ya Masahaba na waliowatangulia. Na Kama aliyeuawa yule si Mwislamu, kama akiwepo katika nchi zetu, basi yeye amepewa ahadi ya amani, na kama akiwepo katika nchi yake, basi yeye ni mwananchi asiyemwangalia na hana dhambi yeyote. Katika hali zote hizi nafsi zao zinahifadhiwa na ni hairuhusiwi kuzivamia na ni lazima kuzihifadhi.
Vile vile vitendo hivi vyakulipua mabomu vinabatilisha makusudio ya kuhifadhi mali; ambapo matokeo ya vitendo hivi ni wazi sana, miongoni mwa matokeo hayo ni kupoteza mali, majengo, mamlaka ya umma na ya kibinafsi, kupoteza mali ni suala lililoharamishwa na Sheria, uharamu unazidi maradufu kama mali hizi zilizopotezwa si za mwenye kuzipoteza bali ni mali za mwengine – kama hali ilivyo katika suala hili – uharamu unahusiana na uhalifu wa katazo la Sheria kwa upande mmoja, na uharamu unahusiana pia na haki za viumbe kwa upande mwengine.
Pia vitendo hivi vinasababisha madhara na ufisadi mkubwa: makusudio ya Sheria Tukufu ni kuleta maslahi na kuondosha ufisadi. Ni wazi kwa mwenye akili kwamba vitendo hivi vinaleta uharibifu kwa Waislamu katika Mashariki na Magharibi mwa Dunia hii; miongoni mwa uharibifu huu ni kuvitumia kama sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Kiislamu, kuzitumia heri zake, uporaji wa rasimali zake kwa kisingizio cha kutafuta ugaidi au kwa ajili ya kuhifadhi maslahi ya kiuchomi, au kuwakomboa wananchi, mwenye kuwasaidia hawa ili kutekeleza makusudi yao na kufikia malengo yao kupitia vitendo vyao vibovu, kwa sababu ya vitendo hivi shari Waislamu wamezipata nyingi, pia vimesaidia kupungua nguvu ya Waislamu na hali hii ni uhalifu mkubwa.
Miongoni mwa ufisadi mkubwa ni vitendo hivi ambavyo viko mbali na mafunzo ya Uislamu na utukufu wake, vitendo hivi vinazidisha uvumi na shutuma za uongo ambazo maadui wa Uislamu wanazielekeza kwenye Dini ya Uislamu kwa nia ya kuivuruga sura yake, na kusisitiza kuwa ni dini ya kinyama na ya umwagaji damu, lengo lake ni kuwashinda watu na kueneza ufisadi katika ardhi, na hali hii ni miongoni mwa uzuiaji wa njia na dini ya Mwenyezi Mungu.
Miongoni mwa ufisadi mkubwa ni yale yanayotokana na vitendo hivi kama vile; kuwanyanyasa Waislamu katika baadhi ya nchi za kigeni kutoka kwa wenye mtazamo mkali. Kutokana na hivyo, Waislamu wanapata madhara makubwa katika nafsi zao, mali zao, heshima zao, na baadhi yao wanalazimishwa kuitekeleza dini yao kwa siri au kuacha baadhi ya mambo ya Ibada na ya faradhi.
Mambo hayo yote yanasababishwa na vitendo hivi vilivyofanywa na hawa wajinga wasiojua wanavyovitaka wala vinavyotakiwa, na wanaharibu rasilimali na wao kuangamia wakidhani kwamba wanatekeleza Sheria, na pia kwamba kwa vitendo hivi watapata hadhi ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri} [AL KAHF: 104].
Wanazuoni wamesema kuwa kama maslahi yakipingana na madhara, basi kuondosha madhara ni bora zaidi kuliko kuleta maslahi. Na maneno haya ya Wanazuoni yanahusisha maslahi ya kweli. Je hali inakuwaje kuhusu maslahi yanayodhaniwa kuwepo au ambayo hayapo?
Ama kuhusu yanayosemwa na wajinga hawa juu ya vitendo hivi ni miongoni mwa Sehemu ya Jihadi dhidi ya adui, na baadhi ya Wanazuoni wanaiita vita, na jina hilo ni ujinga na kosa kubwa sana; kwa sababu Jihadi iliyoruhusiwa katika Uislamu ni ile iliyo chini ya bendera ya Khalifa (Kiongozi wa Waislamu) na kwa idhini yake, au kama sio hivyo, basi itakuwa fujo na umwagaji wa mabwawa ya damu bila ya haki na kwa kisingizio cha Jihadi, lakini Jihadi kwa mujibu wa Uislamu ni kwa ajili ya kuyatekeleza malengo mawili, nayo ni:
La kwanza ni: Kutetea Waislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.} [AL BAQARAH 190].
La pili ni: Kutetea uhuru wa watu katika kuamini Uislamu au kubakia kama walivyo, nayo ni fitna tuliyoamuriwa kupigana kwa ajili ya kuiondosha; ili watu wachague dini yao kwa uhuru kamili, Mwenyezi Mungu alisema: “Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu” [AL BAARAH: 193].
Ni wazi kwamba Jihadi ya kutekeleza malengo haya mawili haiwi ila dhidi ya adui wa nje.
Ama kuhusu kuitumia kwa kuua, kutishia, kuharibu mali za jamii ya Kiislamu, kama ilivyokuwa kwa vitendo vya kulipua mabomu katika nchi za Waislamu, hali hii inaitwa “Al-Hirabah” kwa mujibu wa Wanazuoni wa Fiqhi. “Al-Hirabah” ni dhuluma na uharibifu katika dunia, mwenye kufanya hivi anastahiki adhabu kali sana, kama vile adhabu ya kuua, kuiba, na kuzini, kwani ni uharibifu unaopangwa, na mtu mwenye kuufanya uharibifu huu anaufanya dhidi ya jamii. Mwenyezi Mungu anasema:
{Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusulubiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa} [AL MAIDAH: 33].
Hairuhusiwi hivyo katika nchi na jamii zisizo za Kiislamu, kama ikiongezwa mikataba ya kimataifa kati yao na Waislamu, na kwamba wataruhusu Waislamu kulingania Waislamu wengine kama wanavyofanya hivi pamoja na wasio Waislamu, basi kufanya shughuli za uhalifu ni haramu na ni ufisadi zaidi, lakini hata pamoja na kutangaza vita vya kivitendo hairuhusiwi kuua watu kwa ujumla; ambapo hairuhusiwi kuwaua wanawake wasiohusika na vita wala watoto wala wazee wanyonge na waajiriwa wanaofanya kazi katika mambo mbali na ya kivita, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} [AL BAQARAH: 190]. Imepokelewa kutoka kwa Imam Al-Tahir Ibn Ashour katika Tafsiri yake kutoka kwa Ibn Abbas na Umar Ibn Abdulaziz na Mujahid kuwa Aya hii haikufutwa, akasema: “Kwani maana ya wale "wanaokupigeni" ni wale wanaojiandaa kupambana nanyi, yaani msipigane na wazee, wanawake na watoto”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Termidhi kutoka kwa Sulaiman Ibn Buraidah kutoka kwa baba yake alisema kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. wakati alipokuwa akimtuma mkuu wa jeshi akamwusia kuwa kumcha Mwenyezi Mungu na kufanyia wema kwa Waislamu ambao ni pamoja naye akisema: “Piganeni vita kwa jina la Mwenyezi Mungu katika njia ya Mwenyezi Mungu, piganeni na aliyekufuru, piganeni vita wala msipite kiasi, wala msifanye uhaini, wala msikate kate viungo, wala msiue mtoto yoyote”.
Imepokelewa kutoka kwa Ahmad kutoka kwa Al-Muraqa Ibn Saifi kutoka kwa babu yake Rabah Ibn Rabii ndugu yake Handhalah Al-Katib alimwambia kuwa akatoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. katika vita moja, ambapo Khalid Ibn Al-Waliid alipokuwa mbele, Rabah na Masahaba zake Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. walipitia mwanmke ambaye aliuawa, wakasimama kumwangalia, wakashangaa hali yake, mpaka Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. aliwafuata akipanda ngamia wake, Masahaba wakaepuka, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasimama karibu naye, akisema: “Namna gani mwanamke kama huyo apigane vita”, akamwambia mmoja wao: “Mfuate Khalid, mwambie: usiwapige watoto wala wafanya kazi wa mambo mbali na ya kivita”.
Imam Al-Nawawi alisema katika Sharhul Imam Muslim: “Wanazuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kuwaua wanawake na watoto kama hawakupigana”.
Tukifahamu kwamba sababu ya kupigana ni vita, basi kila asiyepigana anafuata yaliyotajwa katika Matini za Kisheria, kama vile; kipofu, mgonjwa, mwenye wazimu, mshamba, na mifano yao, hawa wote wanaoitwa “Raia” kwa istilahi ya kisasa, hairuhusiwi kuwadhuru, wala kuzipoteza mali zao, pia hairuhusiwi kuwaua, kwani kuwaua raia ni dhambi kubwa.
Miongini mwa makosa yao wanayohalilishia ufisadi wao ni: kupima suala la kuua watalii, wanawake na watoto na suala la kujikinga kwao (maadui) nyuma ya wasioruhusishwa kuuawa lililotajwa na Wanazuoni.
Upimaji huu ni mbovu; kwani tofauti ni wazi kati ya suala la kujikinga kwa maadui lilitajwa na Wanazuoni na suala ambalo watu hawa wanajitahidi kulihalilishia shughuli zao za uhalifu, wakati wa vita ambapo adui wanapojikinga nyuma ya wanawake, watoto, au Waislamu kwa ajili ya kuzuia majeshi ya Waislamu kuwashambulia hali hii ni ya dharura tu, hata hivyo, kama hakuna dharura ya kuwaua maadui wanaojikinga nyuma ya wasioruhusishwa kuuawa ni bora tuwaache kuwaua. Na dharura hii ina masharti yake yaliyoainishwa kwa uwazi na yaliyotajwa na Wanazuoni. Ama kulishambulia kundi la watalii wakiwa pamoja na wanaume, wanawake, na watoto na kuwaua kwa ujumla ni uhaini pasipo na kujikinga kwa maadui wala hakuna dharura ya kuwaua, basi kitendo hiki ni uadui mtupu. Katika suala hili hakuna kujikinga kwa maadui, wala hakuna maana yoyote ya kuzingatia, kama wakiwaacha wote wakiwemo wanawake na watoto, basi hali hii haitasababisha kuzuia Jihadi wala kuifanya ni njia ya kushindwa kwa Waislamu. Wanazuoni wa Sheria walisema kuhusu suala la kujikinga kwa maadui nyuma ya Waislamu kuwa kama kuna dharura tu, wakati wa vita, na hakuna uhusiano wowote kati ya maneno haya na yanayoenezwa na wajinga hawa.
Kwa kweli wanaofanya shughuli za kujitoa mhanga wanachezea Dini, Sheria, na misingi yake iliyoimarishwa, wanategemea makosa ya kifiqhi, kuwavurugia watu, pamoja na ujinga wazi kwa misingi ya kutoa dalili na kuchagua kati ya dalili za kisheria, kufuata matamanio katika kufahamu Sheria kwa masharti yake na pasipo na masharti kinyume na walivyofuata Wanazuoni wa Sheria. Fikra zao ni mbovu, zimepotoka na zinajitahidi kuhalilisha kumwaga damu zinazohifadhiwa kwa Sheria ya Kiislamu.
Ingawa madai mapana ya Jihadi na Usambazaji wa shutuma za jeuri juu ya wanaopinga katika maoni, matokeo ya vitendo vya wadhalimu hawa ni kuanguka kwa nchi za Kiislamu chini ya utawala wa ukoloni wa kijeshi, kujaza kwa makaburi na majela kwa Waislamu wasio na dhambi lolote, na vitendo vyao mbovu hivi vinaimarisha maslahi ya maadui wa Umma wa Kiislamu. Vitendo hivi vilileta maafa na misiba iliyosababisha vifo vya Waislamu mamia elfu. Kusema kuwa wanatetea Waislamu ni dai la uongo, bali wanawaua Waislamu na kuwahamisha kama wanavyofanya wasio Waislamu, nao hawakuzuia adui na Waislamu kwa mujibu wa dai lao la Jihadi, bali walileta uadui wa mataifa ya Waislamu na wakapata uadui wao, mpaka Umma umezidi udhaifu wake kutokana na wanavyofanya.
Ukweli ambao Waislamu hawawezi kuukanusha, ni kwamba hawa ni wazushi, wadhalimu, na wenye matamanio, na mfano wa hawa elimu kwa ujumla haichukuliwi kutoka kwao, kwani wao ni wazushi na wenye matamanio na wanafanya kinyume na itikadi za watu wa Sunna, hasa wanaitia uzushi wao, matamanio yao, wanayapigania. Ni lazima watawala Waislamu kumrudisha mjinga asiyebeba silaha kwa akili yake kwa hekima na kauli mema. Ama kuhusu aliyebeba silaha ni dhalimu mpaka ashindwe, Uislamu na Waislamu watosheka na shari zake.
Kutokana na yaliyotangulia katika swali hili: inajulikana kuwa viza ni ahadi ya amani inayolazimisha kuwepo kwa amani kwa pande mbili, hairuhusiwi kuvunja ahadi hii wala kutohaini kutoka pande mbili hizi, na kwamba Jihadi ni faradhi thabiti mpaka Siku ya Kiyama, na kwamba kulinda mipaka, kuhifadhi mapengo na kuhifadhi nguvu za kutetea kwa majeshi ni faradhi Kifaya na kufanya wanavyoona ni uwezo wao, na kwamba hivyo inaondosha sifa ya faradhi isiyokwepo kwa Jihadi. Hata kama kuna kasoro katika Jihadi kutoka kwa Watawala Waislamu, basi shughuli za uhalifu zinazoangamia nchi kavu na ya kijani hazihalilishwi kwa hali zote, na kwamba ulinganiaji wa Uislamu ukiwezeshwa na hauzuiliwa, basi hakuna haja kwa kupigana, na kwamba vitendo vya kulipua mabomu na shughuli za kujitoa mhanga zinakusudiwa wasio Waislamu wanaozuru nchi za Waislamu kwa lengo sio la kivita au katika nchi zao tulizoingia kwa viza, vitendo hivi ni haramu, kutotimiza ahadi, na uhaini ambao hauna uhusiano na Uislamu, navyo sivyo miongoni mwa Jihadi Takatifu au vita iliyoruhusiwa katika Uislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas