Matumizi ya Maneno Yasiyo ya Kiarab...

Egypt's Dar Al-Ifta

Matumizi ya Maneno Yasiyo ya Kiarabu Katika Talaka

Question

Ugomvi mkali ulitokea kati yetu, mimi na mke wangu, nilikuwa na ghadhabu iliyonipelekea kutamka neno la talaka moja tu, na mimi ninakiri hivyo. Baada ya tukio hilo, niliwasiliana na baba yake ili aje na kumtuliza mke wangu, alipokuja nikapagawa kwa wingi wa hasira, nikasema: (mwisho) mara mbili, na sikukusudia talaka. Baba mkwe akasema: Uhusiano umekwisha kwa talaka, yaani hii ni talaka ya tatu, kisha akaanza kuandika hivyo, akaniambia nitie saini alichokiandika, kwa shinikizo nilitia saini ili niweze kuchukua paspoti yangu, baada ya mke wangu kusema: Tia saini ili uchukue paspoti yako.
Muulizaji anauliza: Je talaka hii ni sahihi niliposema: FINISH (mwisho), wakati nilipokuwa na ghadhabu kali? Na hali ya kutia saini waraka kwa ajili ya kuchukua paspoti yangu? Mwenye swali anaomba kubainishiwa hukumu ya kisheria.
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenye swali akitamka kwa mara ya kwanza, tamko la wazi kuhusu talaka kama vile (Wewe umeachika), basi hii ni talaka ndogo ya kwanza, isipokuwa ikitanguliwa kwa talaka nyingine, na kusema kwake (Mimi ninakiri hivyo), ni kuwepo talaka moja.
Na kauli yake ya mara ya pili: FINISH (mwisho) mara mbili, kauli hii ni kinaya ya talaka yaani haiathiri isipokuwa kuna kusudio la talaka kwa upande wa mume, na kama imetajwa kuwa mume hakukusudia talaka, basi kauli hii haidhuru kamwe na hakuna talaka.
Kuhusu kutia saini waraka wa talaka, ni kukiri kilichoandikwa katika waraka huo, na akiwa mwenye kukusudia na mwenye uhuru, basi talaka itatokea kwa kutia tu saini katika waraka huu.
Haifai kupinga waraka huu ila mbele ya mahakama inayohusika ili kuthibitisha iwapo alilazimishwa kutia saini au la. Na kwa mujibu wa yaliyozungumzwa, jawabu la swali limeeleweka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas