Je, Utangazaji Uisalmu ni Sharti la...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je, Utangazaji Uisalmu ni Sharti la Uislamu Sahihi?

Question

Mimi ni mwanamke wa Marekani nimeingia Dini ya Uislamu kwa itikadi ya kweli mwaka wa 2005 yaani tangu miaka kadhaa iliyopita na nimeshuhudia kwamba “Hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Mohammad ni mja wake na Mtume wake”. Kisha nimeolewa na Mwislamu kutoka Jordon kwenye Msikiti wa Chicago, nchini Marekani, tangu wakati huo hadi sasa, mimi ninafanya ibada za Kiislamu zikiwemo Sala, Saumu, na Zaka; lakini sikutangaza Uislamu wangu mbele ya watu wote isipokuwa baada ya kufika Misri mwaka wa 2009. Ni nini hukumu ya Uislamu wangu katika muda huu uliotangulia? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Usilamu wako katika muda huu ni sahihi kwa mujibu wa Sheria, na utangazaji wa Uislamu siyo sharti miongoni mwa masharti ya usahihi wa Uislamu mbele ya watu; mtu mmoja Muumini, aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni alificha Imani yake kwa muda. Vile vile Mfalme Najashi alikuwa Mwislamu na hakuwafahamisha watu wake kuhusu Uislamu wake. Na Mtume S.A.W alimswalia Mfalme Najashi swala ya maiti asiyekuwepo baada ya kifo chake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote
 

Share this:

Related Fatwas