Kula Nyama Iliyochinjwa Bila Kujua ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kula Nyama Iliyochinjwa Bila Kujua Iwapo Jina la Mwenyezi Mungu Lilitajwa.

Question

Mimi ninaishi nchini Uingereza, katika mji mdogo ambapo hakuna nyama ya halali isipokuwa katika maduka mawili ya kipakistani. Mimi nilijaribu kununua nyama katika maduka hayo lakini ni machafu kama vile maduka mengine yaliopo huko!, pia yapo maduka ya kipakistani yaliyo masafi lakini yapo mbali ni kiasi cha dakika thalathini kwa gari. Je, inajuzu kwangu kununua nyama katika duka la Super Market au katika maduka ya vyakula vilivyotayari na nikataja jina la Mwenyezi Mungu kabla ya kuila? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Asili katika vichinjo ni uharamu, isipokuwa vile vilivyotengwa kisheria, navyo ni wanyama wanaoliwa wakichinjwa na mwislamu au mtu katika watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), vilivyochinjwa na Watu wa Kitabu vinakuwa halali kiasili kwa jinsi vilivyo katika hali ya kutenganisha kutokana na asili yake.
Na hiyo inakuwa ni yakini siyoondoka kwa shaka, kwani asili ni uhalali wa vichinjo vya watu wa kitabu isipokuwa itakapojulikana uyakini wake kuwa mchinjaji hakuwa mtu wa kitabu. Au yeye hakumchinja bali alimuua kwa kumpiga au kwa kumpiga umeme kwa mfano, kama haitajulikana hivyo kwa uyakini, basi asili itaendelea kubakia kuwa halali kula vichinjo vya watu wa Kitabu kama vilivyo.
Na Mtume S.A.W. Alikula mbuzi aliyetolewa zawadi na myahudi na wala hakuuliza jinsi alivyochinjwa iwapo lilitajwa jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kumchinja au la, na si sheria kwa mtu kuuliza na kuchimba dalili kwa kuwa tu yuko katika nchi ambayo wengi wa watu wake ni Watu wa Kitabu. Kwani asili katika sheria ni kuwadhania vyema watu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewazuia waumini kumchimba mtu mambo yote kwa ujumla na kumpekua kwa namna ambayo haina faida yeyote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaweka msingi wa hayo, na akasema katika Suratu Al MAIDAH: {Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni} [AL MAIDAH 101]. Ibn Kathiir amesema katika kuielezea aya hiyo: "Haya ni mafunzo ya kimaadili kwa waja waumini na kuwakataza kuulizia vitu visivyokuwa na faida kwao katika kuulizia na kuvichimba… mpaka aliposema: Na uwazi wa aya ya katazo la kuulizia vitu ambavyo iwapo mtu atavijua basi vitamfanya aingie makosani, na ni bora kujiepusha navyo na kuviacha". Basi inachukuliwa kwa undani wa mambo, bali Atwabarani ameitoa Hadithi katika kitabu chake: [Al Kabeer] kutoka kwa Haritha Bin Anuumaan R.A. kwamba Mtume S.A.W. na jamaa zake, alisema: "Kama ulidhani basi usichunguze".
Hayo ni katika mambo ya halali na haramu; Ama kuhusu unyenyekevu huu ni mpana; na tamko la wanazuoni limekubalika juu ya unyenyekevu kuwa ni mpana kuliko uzio wa hukumu ya kifikhi, na hii ni kwa kuwa Mwislamu anaweza kuacha mambo mengi ya halali kwa sababu ya unyenyekevu.
Lakini hili halimaanishi kuwa ni wajibu kwa mwingine kufanya hivyo kwa njia ya kuwajibika kisheria na ikaingia katika mlango wa uharamishaji wa halali. Na wala sio kushughulikia kinachodhaniwa na chenye hitilafu ndani yake kwa hoja ya mkato inayokubaliwa na wote na ikaingia katika kuzusha kutokana na kubana kile alichokipanua Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake S.A.W, bali lazima ajilazimishe kwa adabu ya hitilafu kama ulivyo mfumo wa Salafu (wema waliotutangulia) katika masuala yaliyo na hitilafu na ya kijitihada.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas