Kutaja Jina la Mwenyezi Mungu Katik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutaja Jina la Mwenyezi Mungu Katika Kumchinja Mnyama.

Question

 Ni ipi rai ya wanachuoni wa Madhehebu ya Hanafi kwa Mnyama aliyechinjwa bila kutajwa jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja? Na kama wakiwa wanyama kumi wamechinjwa, lakini halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu ya wanyama watatu miongoni mwao. Halafu wakachanganywa pamoja kwa namna ambayo hawaweza kujulikana wanyama watatu waliochinjwa bila ya kutaja jina la Mwenyezi Mungu, kwa hiyo ni ipi hukumu ya wanyama hao kumi kufuatana madhehebu ya Hanafi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kinachochinjwa, kwa mujibu wa viongozi wa Madhehebu ya Hanafi ni sharti kuwe sambamba na kutaja na uwezo, na atakayechinja kwa kusahau au kwa kushindwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu basi kichinjo chake ni halali, na atakayekusudia kuacha kutaja akiwa na uwezo wa kutamka basi kichinjo chake hakitaliwa. Kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya: {Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu} [AL ANAAM 121]
Al Kassani; mwanachuoni wa Madhehebu ya Hanafi, anasema katika kitabu cha: [Badaa'i Aswanaa'i 46/5, Ch. Al Maktabah Al Elmiyah]: "Na katika masharti ya kuchinja: ni kulitaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kukukumbuka, kwetu sisi tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu}.
Na kutoa dalili ya aya hiyo ni kutoka pande mbili: Moja yake ni; kwamba hakika uwazi wa kukataza kwa ajili ya uharamu katika haki ya kufanya kazi, na ya pili: Hakika yeye aliviita vichinjo ambavyo havikutajwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa ni upotovu, kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwani huo ni upotofu}, Na hakuna uchafu isipokuwa kwa kufanya yaliyoharamishwa. Na hakuna chochote kwa watu wanaosahau. Kwa yaliyopokelewa kutoka kwa Rashed Bin Saa'd kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba akasema: "Kichinjo cha Mwislamu ni halali, iwe limetajwa jina la Mwenyezi Mungu au halijatajwa, kwa kuwa tu sio kwa makusudi" na hayo ni maandiko yaliyopo katika mlango huo".
Na Wafusasi wa Madhehebu ya Hanafi wanazingatia sharti la kuainisha kichinjo wakati wa kuchinja, kwa hiyo lazima kuainisha kinachochinjwa, na kama hakikuainishwa kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu basi nyama yake haitaliwa. Na kwa asili hii sharti la kuainisha kinachochinjwa hujengeka kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu katika uchinjaji wa hiari, na kwa njia hii hutoka iwapo kilichochinjwa ni mbuzi na jina la Mwenyezi Mungu likatajwa kisha akachinjwa mbuzi mwingine ikidhaniwa kuwa utajo wa kwanza wa jina la Mwenyezi Mungu unatosha kwa wote wawili basi nyama yake haitaliwa.
Na ni lazima katika kila kichinjo ataje upya jina la Mwenyezi Mungu, na kama mtu atamwangalia mnyama wake kisha akasema: Bismillah (kwa jina la Mwenyezi Mungu), kisha akachukua mnyama mmoja na kumlaza kisha akamchinja na kuacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa makusudi huku akidhani kuwa kutaja jina alikofanya kunatosheleza, basi mnyama huyo hataliwa. Kwa sababu yeye hakutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja na sharti ni kulitaja jina hilo kwa kinachochinjwa, nako ni kutaja jina wakati wa kukichinja na wala sio wakati wa kukiangalia, na kuainisha kichinjo ni makadirio. [Tazama: Badaa'i Aswanaa'i 48/5, Ch. Al Maktabah Al Elmiyah].
Na wafuasi wa Madhehebu ya Shafi wanaelemea rai inayoona kuwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu kunapendeza; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhalalishia vichinjo vya watu wa kitabu kwa tamko lake: {Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao.}[AL MAAIDAH 5], na wao hawavitaji, Sheikh Zakariyah Al Answari wa kishafi akasema katika kitabu cha: [Isniy Al Matwaleb 540/1, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]; "Na inasuniwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu; kwa kusema Bismillah (kwa jina la Mwenyezi Mungu) na kumswalia Mtume S.A.W. wakati wa kuchinja, kwa ajili ya tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake}[AL ANAAM 118], {Basi kuleni walichokukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu} [Al Maidah 4].
Na kwa kufuata; Maimamu wawili wakapokea Hadithi ya kutaja jina la Mwenyezi Mungu, Na ama Swala juu ya Mtume S.A.W. ni kwa kuwa hapa ni mahali panaposuniwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi inasuniwa kumtaja Mtume S.A.W. kama vile Adhana na Swala.
Lakini kutaja jina la Mwenyezi Mungu haiwajibiki kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja} [AL MAIDAH 3]. Basi aliyechinja akahalalisha, na wala jina la Mwenyezi Mungu halikutajwa kimehalalishwa. Kwa tamko la Aisha R.A.: kwamba watu fulani wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Hakika watu wapya katika zama za ujahili hutujia wakiwa na nyama na hatujui je walichinja kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu au hawakulitaja? Je tule nyama hiyo au tusile? Basi akasema tajeni jina la Mwenyezi Mungu kisha kuleni!" Imepokelewa na Al Bukhariy. Na hata kama ni wajibu kwa kujuzu kula pamoja na kuwepo shaka.
Ama tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu} [AL ANAAM 121] Na uovu katika kichinjo unatafsiriwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni kile kilichochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na jina hili limeachwa hivyo pamoja na Swala kwa makusudi ya kuchukiza; kwa ajili ya kuwa na ukakika wake.
Na kutokana na hayo, inajuzu kwa Madhehebu ya Hanafi kufuata madhehebu ya Shafi wakati wa haja ya kufanya hivyo; kwa ajili ya kulinda mali isiharibike, na haiwi hivyo nje ya misingi ya madhehebu ya Hanafi. Kwani jambo muhimu hapa katika masuala haya mbali mbali ndani yake kuna kujuzu kutumia kwa kauli ya mmoja wa Wenye kujitahidi inapokuwepo haja ya kufanya hivyo. Na hivyo hivyo ndivyo inavyokuwa katika mjumuiko wa wanyama waliochinjwa ambao baadhi yao jina la Mwenyezi Mungu lilitajwa na baadhi yao halikutajwa, inajuzu kwa Hanafi kula nyama ya wanyama hao wote kwa kufuata madhehebu ya Shafi katika jambo hili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi wa wote.

Share this:

Related Fatwas