Mwanamke Aliyeachika Kupata Nusu ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanamke Aliyeachika Kupata Nusu ya Mali ya Mtalaka Wake.

Question

 Mume wangu aliniacha tukiwa Marekani ya Kaskazini. Je, nina haki ya kugawana nae utajiri wake na kuchukua mali iliyo sawa na thamani ya nusu ya nyumba yake kama wanavyofanya watu hapa tulipo?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Katika baadhi ya nchi za kigeni sheria inampa haki mume au mke kuchukua nusu ya mali ya mwengine kwa mujibu wa mkataba wa ndoa ikitokea talaka ya kwanza.
Na hukumu hii katika mali ya upande mmoja wa wanandoa kwa manufaa ya mwingine haitambuliki katika sheria yetu ya Kiislamu, kwani kinachotambulika ni kwamba haki za ndoa kwa mke anapoachika na kupata talaka zinakuwa ni kama matumizi ya eda, na ya mutaa (Muda wa kujiliwaza)’. Ama mume basi kimsingi hachukui chochote kutoka upande wa mwanamke aliyeachana nae isipokuwa katika hali ya mke kuamua kuvunja ndoa.
Na hukumu katika suala la kuchukua mali katika hali iliyotajwa ni kuwa anaweza kuchukua mali, pale mahakama inapoamua kwa mujibu wa kanuni zake za kutungwa zitumikazo katika nchi hizo.
Dalili ya hayo ni kwamba kulipana mali ni haki za kiraia zinazopangwa na kila nchi, na wakazi wake wanazingatiwa kama kwamba wamekubali kanuni zinazozipangilia hali hizo, ni sawa na kujiwekea sharti la kulipa baadhi ya fedha kwa upande mwingine wakati wa kutokea talaka, basi kwa mazingira kama hayo, mtu anapaswa kutekeleza kwa mujibu wa jinsi alivyojiwekea sharti; kwani Waumini huwa wanatekeleza masharti waliojiwekea kama ilivyokuja katika Hadithi.
Hitimisho: Tunavyoona sisi ni kwamba hali hiyo ni miongoni mwa haki za kiraia ambazo hakuna kizuizi chochote kuzipata; kwani wakazi katika nchi hizo wanalazimika kuzifuata kanuni zake kama hazipingani na sheria ya Kiislamu, na inajulikana kwamba kutochukua mali katika hali hiyo ni bora zaidi ili kutokwenda kinyume na Wanazuoni wanaolipinga jambo hili.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas