Kushirikiana na Ndugu Wasio Waislamu Katika Sikukuu Zao.
Question
Mimi natoka katika kizazi cha familia ya Kikristo, kesho ni Krismasi nayo ni sikukuu ya kijamii, licha ya kuwa ni Sikukuu ya kidini, jamaa zangu hukutana katika siku hii na kupeana zawadi, tangu niliposilimu ninahisi kuwa nina dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya familia yangu isiokubali kusilimu kwangu kwa kiasi fulani, na sijui nifanyeje katika hali hii? Nimefikia mpaka kuogopa hata kupiga simu na kuwapongeza kwa kusema “Nakutakieni Sikukuu njema ya kuzaliwa” au “Sikukuu njema” ingawa nafahamu kwamba familia yangu hawazingatii mambo ya dini, mbali ya hivyo mimi nimeacha kula chakula cha usiku.
Msimamo huu unanisikitisha sana, mnaweza kuniambia nifanyaje? pamoja na kujua kwamba familia yangu hawasherehekei sikukuu hii kwa nia ya kuwa ni ya kidini, isipokuwa huenda Fatwa hii itageuza hali hii kidogo.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu ni dini ya amani, rehema, mema na kuunga udugu. Miongoni mwa wajibu juu ya Waislamu katika siku hizi ni kubainisha uzuri huu ulio ndani ya Uislamu ili wawe wanaobeba dini hii wawe na tabia na matendo mazuri. Uislamu haukuamuru kutengana na familia yako na kuwachukia wao, lakini Uislamu umekuamuru kuwafanyia wema, ipo tofauti kubwa kati ya kuchukia ukafiri kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru, ambapo ni bora mtu atupwe ndani ya moto kuliko kuacha Uislamu, na kati ya kuwachukia watu na jamaa zao kwa sababu wao ni makafiri bali anachukia kila kitu hata anachukia ardhi iliyoumbwa na Mwenyezi Mungu kwa ajilia yao. Hii ni maana potofu ya chuki iliyo mbaya sana na haina uhusiano na Uislamu wala Mtume S.A.W. wala ustaarabu wa Uislamu ulioeneza amani Ulimwenguni. Uislamu haukutuamuru kuwachukia watu, bali ulituamuru kuwapenda kwa sababu wao ni viumbe wa Mwenyezi Mungu, na kwa sababu mtu ni mjengo wa Mwenyezi Mungu na amelaaniwa mwenye kuuharibu, kwani Mwenyezi Mungu alimwumba kwa mikono yake, akampulizia roho yake, na akawafanya Malaika wake wasujudu kwake. Basi ni kumheshimu mwanadamu kwani ana sifa ya Malaika. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ametuamuru kuwapenda watu wenye kuunga undugu, kufanya mema, kuwa na tabia nzuri, kusema maneno mazuri, kucheka kwa njia nzuri, na kukaa na watu kwa njia nzuri, kwa mambo hayo Uislamu umeenezwa katika Mashariki na Magharibi, umejaza nyoyo za watu upendo kabla ya kuingia nchi zao.
Kwa hivyo, tunasema: Ewe ndugu tenda kwa huruma yako na tabia yako njema, kwani Uislamu unapenda tabia nzuri inayosababisha furaha na upendo kwa watu, utendeane na jamaa zako kwa tabia nzuri, isitoshe kwa kuwapigia simu ili kuwapongeza tu, lakini ushiriki pamoja nao furaha yao na sherehe yao kama hakuna mambo yanayopinga Uislamu. Uislamu ni dini ambayo wafuasi wake wanawaamini Nabii wote, Mitume wote, wanawapenda wao, wanawatukuza, na wanafanya mema pamoja na wafuasi wao kufuatana na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa} [AL ANKABUT: 46].
Issa Ibn Maryamu ni miongoni mwa Mitume walio vumilia tabu kubwa, Mtume S.A.W. alisema katika Hadithi yake kuwa: “Mimi ni bora zaidi kwa Bwana wetu Isa Ibn Maryamu kuliko watu wote katika Dunia na Akhera, hakuna Nabii yeyote kati ya mimi na yeye”. Basi kila Mwislamu anamwamini Bwana wetu Issa kuwa ni miongoni mwa wanadamu na ana miujiza mikubwa kama vile kufufua maiti na kuwaponesha wagonjwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, siyo kwa sababau ni Mungu au mwana wa Mungu kwa maana ya kwamba alizaliwa na Mungu na jambo hilo Mwenyezi Mungu ametukuka.
Kwa hivyo, kuifurahai siku ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Issa ni miongoni mwa Imani, mbali na itikadi za Manasara. Basi ushiriki pamoja na jamaa zako katika sherehe zao na kula pamoja nao chakula, lakini usile nguruwe, na usinywe pombe kwa upole, na jihadhari na watu wanaotaka kuharibu uhusiano wako na jamaa zako baina ya watu kwa jina la Uislamu, Uislamu hauna hatia yeyote kuhusu jambo hilo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote