Matibabu Kwa Njia ya Kiitikio Cha Kiroho
Question
Nilijifunza mtindo wa matibabu unaoitwa “Matibabu Kwa njia ya Kiitikio Cha Kiroho” (spiritual response therapy), kisha nikaamua kujizuia kuutumia mtindo huo kwa kuhofia kwamba ni jambo linalokwenda kinyume na Sheria.
Mimi nautumia ubao wa kupigia ramli na ninauuliza maswali yangu, kisha ubao huo una pande mbili na huwa unaniambia kwamba jibu ni sahihi au sio. Kwa mfano: Ninauuliza je, mume wa rafiki yangu anamfanyia hiyana mke wake au la? Na je, nitasafiri mwaka huu? Na kadhalika. Je? utumiaji wa tiba ya aina hii ni halali?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sheria takatifu haiweki vikwazo juu ya utafiti wa kielimu, bali imehamasisha utafiti na suala la kujitahidi kupata elimu; Mwenyezi Mungu anasema: {Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?}[ADH-DHARIYATt, 21], na anasema: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?}[AZ-ZUMAR, 9].
Lakini sheria imeuwekea vikwazo utumiaji unaoleta ufisadi au madhara, au unaohitilafiana na mila na desturi kwa ujumla.
Na matibabu kwa njia ya kiitikio cha kiroho – ambayo ni matibabu yanayolenga kutibu magonjwa ya kisaikolojia kwa njia ya kuondosha kumbukumbu za zamani zinazosababisha maudhi ambayo yanaweza kuleta ugonjwa wa kisaikolojia – yangekuwa elimu iliyozingatiwa katika vyuo maalum au vituo vya utafiti wa kisayansi basi unaweza kutumia matibabu haya pamoja na umuhimu wa kushikamana na maadili ya kazi, na kuzuia pale yanapokuwa ni sababu ya ufisadi.
Linabaki suala la njia ya kutabiri ghaibu kwa kutegemea ramli kama ilivyotajwa katika swali, basi suala hili halina nafasi katika matibabu ya kisaikolojia, bali hili ni aina mojawapo tu ya namna ya kuagua kwa ramli; vibao vya kupigia ramli vilivyotumiwa katika enzi za ujahilia viliandikwa juu yake: baadhi ya nyakati "fanya" na mara nyingine "usifanye", na mwishoni: Hamna kitu, na mtu huwa anachagua kimojawapo bila ya kujua kilichoandikwa ndani yake, basi akikuta: "fanya" huanza kufanya analolitaka, na akikuta: "usifanye", anaacha pamoja na kudhani kwamba hilo lengo baya, na anautoa nje ubao ambao haukuandikwa kitu na anaendelea kulikariri jaribio hilo mpaka ukatokea ule ubao ulioandikwa, na huku yeye akitaka apate bahati yake kutokana na kisichojulikana, kwa kutumia vibao hivyo. Na hii ni haramu kisheria; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyechinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliyekufa kwa kunyongeka koo, na aliyekufa kwa kupigwa, na aliyekufa kwa kuanguka, na aliyekufa kwa kupigwa pembe, aliyeliwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama ya aliyechinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu} [AL-MAIDAH, 3], na anasema pia: {Enyi mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa} [AL-MAIDAH, 90].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi ya wote.